Lowassa ajiweka mbali na kampeni Arumeru,ajikita kanisani.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa ajiweka mbali na kampeni Arumeru,ajikita kanisani..

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Independent Voter, Mar 20, 2012.

 1. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa ufisadi wa richmond,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"] Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu aliyejiuzulu.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya richmond,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
  [​IMG]
  Mke wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya richmond,Mama Regina Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.

  Na mwandishi maalum
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya richmond Mh Edward Lowassa, amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.Mh Lowassa aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi na viongozi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mtakatifu Anns iliyoko Morogoro.Aidha Mh Lowassa alitoa zawadi ya mpira kwa kila darasa katika shule hiyo, ikiwa ni katika kuhamasisha michezo mashuleni.Naye Mkuu wa shule hiyo Sister Dennis pamoja na wanafunzi na watawa wengine shuleni hapo walimtakia Mh Lowassa afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia watanzania.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Leo Tar 19 March alikuwa Ifakara, inasemekana ameondoka kuelekea Arumeru kwa Mkwewe Siyoi
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowasa ameishtaki serikali kwa maaskofu kuhusu swala la ajira kwa vijana. Gazeti la Mwananchi la leo lina taarifa za kina toka Ifakara hukoooo Morogoro..........

  Lowasa aikaanga serikali

  ASEMA IMEKWAMA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA, AWATAKA MAASKOFU WAINUSURU, RUWAICHI AIPONDA KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI

  Juma Mtanda, Ifakara

  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema anashangazwa na Serikali kuendelea kulifumbia macho tatizo la ajira kwa vijana na kuwaomba maaskofu wasaidie kulimaliza akisema hilo ni bomu linalosubiri kulipuka.

  Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akitoa salamu zake kwenye sherehe za uzinduzi wa jimbo jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara zilizofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Edward, Ifakara.

  Alisema viongozi wa juu serikalini wameshindwa kulitatua na kulifumbia macho tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo kuwaomba maaskofu waliangalie kundi hilo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi.

  “Suala la ajira kwa vijana hakuna kiongozi anayelishughulikia ipasavyo ndani ya Serikali, hivyo niwaombe maaskofu nchini walione hili. Nawaomba katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Lowassa na kuongeza:

  “Kanisa Katoliki limekuwa likisaidia sana katika sekta ya elimu na afya kwa hiyo sasa waelekeze nguvu hizo katika kusaidia ajira kwa vijana. Wengi wanaomaliza elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tunavyosema ni bomu linalosubiri kulipuka, sasa naliomba Kanisa lisaidie juhudi za Serikali kutatua tatizo hili,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

  Ruwaichi na mgomo
  Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Dadeus Ruwaichi alisema mgomo wa madaktari nchini umedhihirisha udhaifu wa Serikali katika kushughulikia migogoro na kusema ni aibu kwa Tanzania.

  “Watu wengi wamekufa katika mgomo ule na hii imeonyesha Tanzania ni taifa lisilo na dira,” alisema Askofu Ruwaichi huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki akimsikiliza.

  “Hakuna hata uharaka uliochukuliwa kushughulikia mgomo ule na hii ni kwamba nchi yetu sasa imefikia pabaya kwani inaonekana imeshindwa kushughulikia matatizo,” alisisitiza.

  Katika salamu hizo kwa Askofu mpya wa jimbo jipya la Ifakara, Salutaris Libena, Askofu Ruwaichi alisema kanisa litaendelea kupiga vita umasikini.

  Alimtaka askofu huyo kutoogopa kukemea maovu yanayofanywa na viongozi wa Serikali na kusababisha pengo kati ya wenye nacho na wasionacho.

  Mwinyi asisitiza upendo
  Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alimtaka Askofu Libena kutumia nafasi yake kuleta amani na upendo miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali.

  Mwinyi alisema uaskofu ni daraja kubwa linalofanana na nafasi ya uwaziri katika Serikali hivyo waumini wa dini ya Kikristo katika jimbo jipya la Ifakara wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kiongozi huyo aliyesimikwa kutumikia dini hiyo na Watanzania kwa ujumla.

  “Nafasi ya uaskofu haifungamani na dini wala kabila kwani daraja hilo limejaa roho ya huruma na upendo hivyo jamii ya jimbo la Ifakara ni wakati wa kutoa ushirikiano ili kumpa nafasi mhashamu Askofu Salutari Libena ya kuwahudumia katika nyanja mbalimbali za elimu, afya na tabia njema,” alisema Mwinyi.

  Kadinali Pengo
  Katika mahubiri yake, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alisema uamuzi wa kugawanya Jimbo la Mahenge ni mchakato wa muda mrefu uliotokana na ukubwa wa Jimbo la Mahenge.

  “Mchakato huo uliridhiwa na Papa Benedict wa 16 Januari 14, 2012 kwa kukubali Ifakara kuwa jimbo jipya na makao makuu katika Kanisa la St Andrew lililopo mji mdogo wa Ifakara.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na taasisi wakiwemo maaskofu wa majimbo 34.

  Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Kilombero, Francis Miti
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Lowassa aikaanga Serikali [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 19 March 2012 21:40 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa

  ASEMA IMEKWAMA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA, AWATAKA MAASKOFU WAINUSURU, RUWAICHI AIPONDA KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI
  Juma Mtanda, Ifakara
  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema anashangazwa na Serikali kuendelea kulifumbia macho tatizo la ajira kwa vijana na kuwaomba maaskofu wasaidie kulimaliza akisema hilo ni bomu linalosubiri kulipuka.

  Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akitoa salamu zake kwenye sherehe za uzinduzi wa jimbo jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara zilizofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Edward, Ifakara.

  Alisema viongozi wa juu serikalini wameshindwa kulitatua na kulifumbia macho tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo kuwaomba maaskofu waliangalie kundi hilo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi.

  “Suala la ajira kwa vijana hakuna kiongozi anayelishughulikia ipasavyo ndani ya Serikali, hivyo niwaombe maaskofu nchini walione hili. Nawaomba katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Lowassa na kuongeza:

  “Kanisa Katoliki limekuwa likisaidia sana katika sekta ya elimu na afya kwa hiyo sasa waelekeze nguvu hizo katika kusaidia ajira kwa vijana. Wengi wanaomaliza elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tunavyosema ni bomu linalosubiri kulipuka, sasa naliomba Kanisa lisaidie juhudi za Serikali kutatua tatizo hili,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

  Ruwaichi na mgomo
  Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Dadeus Ruwaichi alisema mgomo wa madaktari nchini umedhihirisha udhaifu wa Serikali katika kushughulikia migogoro na kusema ni aibu kwa Tanzania.

  “Watu wengi wamekufa katika mgomo ule na hii imeonyesha Tanzania ni taifa lisilo na dira,” alisema Askofu Ruwaichi huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki akimsikiliza.

  “Hakuna hata uharaka uliochukuliwa kushughulikia mgomo ule na hii ni kwamba nchi yetu sasa imefikia pabaya kwani inaonekana imeshindwa kushughulikia matatizo,” alisisitiza.

  Katika salamu hizo kwa Askofu mpya wa jimbo jipya la Ifakara, Salutaris Libena, Askofu Ruwaichi alisema kanisa litaendelea kupiga vita umasikini.

  Alimtaka askofu huyo kutoogopa kukemea maovu yanayofanywa na viongozi wa Serikali na kusababisha pengo kati ya wenye nacho na wasionacho.

  Mwinyi asisitiza upendo
  Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alimtaka Askofu Libena kutumia nafasi yake kuleta amani na upendo miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali.

  Mwinyi alisema uaskofu ni daraja kubwa linalofanana na nafasi ya uwaziri katika Serikali hivyo waumini wa dini ya Kikristo katika jimbo jipya la Ifakara wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kiongozi huyo aliyesimikwa kutumikia dini hiyo na Watanzania kwa ujumla.

  “Nafasi ya uaskofu haifungamani na dini wala kabila kwani daraja hilo limejaa roho ya huruma na upendo hivyo jamii ya jimbo la Ifakara ni wakati wa kutoa ushirikiano ili kumpa nafasi mhashamu Askofu Salutari Libena ya kuwahudumia katika nyanja mbalimbali za elimu, afya na tabia njema,” alisema Mwinyi.

  Kadinali Pengo
  Katika mahubiri yake, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alisema uamuzi wa kugawanya Jimbo la Mahenge ni mchakato wa muda mrefu uliotokana na ukubwa wa Jimbo la Mahenge.

  “Mchakato huo uliridhiwa na Papa Benedict wa 16 Januari 14, 2012 kwa kukubali Ifakara kuwa jimbo jipya na makao makuu katika Kanisa la St Andrew lililopo mji mdogo wa Ifakara.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na taasisi wakiwemo maaskofu wa majimbo 34.

  Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Kilombero, Francis Miti.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 5. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Alichangia sh. Ngapi huko st. Ann?
   
 6. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Naomba kujua hili jina la kanisa lilikuwapo kabla au kanisa hilo limepewa jina hilo baada ya usimikwaji na udhuru wa Waziri Mkuu Mstaafu?
   
 7. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Homa zake za vipindi zinamtesa huyu mzee,mbona hakuwahi kulizungumzia hili suala alipokuwa waziri mkuu,why now?anataka nini?
   
 8. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  alitoa zawadi ya (mipira sijui ipi) kwa kila darasa...!
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo la ajira lina muda mrefu, je, yeye alipokuwa Waziri Mkuu alifanya nini?

  Tangu lini Kanisa limekuwa wawekezaji ambao wanajishughulisha na kuongeza ajira?

  Lowassa ni Mbunge kwanini asitumie nafasi yake ya Ubunge kuishauri serikali iandae sera nzuri za uwekezaji ili kuvutia wawekezaji ambao wanaweza kutoa ajira kwa vijana?

  Kwanini asiikabe serikali Bungeni ili iweze kuweka mazingira mazuri ya vijana kujiajiri wenyewe huko waliko?

  Mkoa wa Arusha unaongoza kwa biashara ya utalii, na jimbo la Monduli liko kwenye ukanda huo huo, je Lowassa amefanya nini kuwapatia ajira vijana wa Monduli ambao wameamua kujiajiri wao wenyewe kwa kuwa walinzi wa mijini badala ya kushiriki kwenye biashara za utalii kama tour guides, kuuza vinyago, na vitu vya utamaduni wa kimasai na/au kuanzisha vikundi vya cultural tourism ambavyo huonyesha utamaduni wa kimasai?

  Ukipita barabara ya Arusha - Monduli - Mto wa Mbu utakuta wamasai/wamachinga kibao wameweka bidhaa zao chini ya miti kwanini asiishauri Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ijenge small trade centres na kuwapangisha hao wamachinga na kuboresha maboma ya maonyesho ya cultural tourism ili angalau watalii wawe wanapita na kununua bidhaa kwenye organized business premises badala ya kusimama chini ya mti halafu unakutana na bidhaa zimepigwa vumbi la kutwa nzima au wiki nzima mpaka bidhaa zinachakaa?

  Lowassa badala ya kuilaumu serikali angeanzia huko jimboni kwake kuweka mambo sawa na ndipo aigeuzie kibao serikali.

  Kwenda kulalama kwenye jukwaa ambalo halihusiki ndo udini wenyewe, alitakiwa kulalama Bungeni na kupeleka hoja binafsi za kuboresha mazingira. Yeye ni sehemu ya tatizo lililotufikisha hapa na alikuwa mstari wa mbele kumfungia Zitto Bungeni zama za Buzwagi na hakuna mahali popote alipopendekeza namna ya kuendeleza wachimbaji wadogo ambao wako kibao mkoani kwake Arusha!

  Hii ni kusaka cheap popularity kwa kutumia majukwaa ambayo hayahusiki. Akina Dr. Slaa na Zitto walianzia Bungeni na walipoona wabunge wa CCM na serikali hawawaelewi ndipo walipoamua kwenda kwa wananchi kuwashitaki na hawakupitia kwenye majukwaa ya dini kama anavyofanya yeye.
   
 10. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lowassa ni mnafiki wa kutupwa,analeta hadithi mcheza drafti ambae siku zote akiwa ndani anacheza haoni pa kucheza ila akiwa nje kwa kutoa maelekezo kwa wachezaji wapi pa kucheza ndio mwenyewe!

  Lowassa kapumzike uangalie afya yako waachie vijana kina zitto na mwanao fredy mambo ya siasa,unafanya siasa za kizamani.
   
 11. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nadhani kiswahili kidogo kinakupiga chenga mkuu. Udhuru ni ombi la kutokuhudhuria lakini waziri mkuu 'mstaafu' aliyejiuzulu yeye alihudhuria.
  Back to the point, jina hili la kanisa ni la tangu zamani na leo ilikuwa ni kumsimika askofu tu hapakuwa na fund raising kama ilivyokuwa ikidaiwa hapo awali
   
 12. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  urais 2015..huyu jamaa kadhamiria kweli..ndani ya miaka 3 hii tutaona mengi
   
 13. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyo Mke wa waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya richimondi hana kazi ya kufanya? naona kila siku yupo nyuma anamfuata huyo waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya richmondi tu. inamaana Lowasa ameshindwa hata kumuwezesha mkewe ili asimame kama mama wa mfano?
   
 14. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Aliwahi kulizungumza mwaka jana mwanzoni au mwaka juzi mwishoni pale uwanja wa ndege wa KIA alipokutana na wanahabari na likazua mjadala sana licha ya kwamba alisema ukweli. Lakini Ukiangalia uhalisia, Lowassa ni much much better than JK katika utekelezaji na utoaji wa maamuzi, huenda hata hili la ajira kwa vijana angekuwa madarakani angeweza kulifanyia kazi WALAU! Ni maoni yangu msinishambulie!!!
   
 15. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo mambo ya fund rising na u.puuzi mwingine wa aina hiyo yamekua yakienezwa na watu wake wa humu na wa kwenye magazeti yake huko mitaani,yeye alikwenda pale kumsindikiza mkewe
   
 16. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  aahaaaaaaaaaaaaaa kumbe mwalikwa alikuwa mkewe na sio yeye???
   
 17. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kwa ugonjwa wa huyu mzee, ni bora apumzike tu, akitaka stress na kufa kabla ya 2015 aendelee na mpango wake wa urais, siasa za sasa nadhani ni zaidi anavyofikiria.
   
 18. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona hakuwahi hata kuligusia katika kipindi alichokaa madarakani wakati hili lipo toka kipindi cha mkapa na wao waliingia na gia ya ari mpya nguvu mpya kasi mpya lakini yeye kama mtendaji mkuu wa serikali akaisahau hii mara moja na hatukumsikia tena hata akiitamka akawa bize kuandaa kuwachangisha wahindi pesa za shrehe za uhuru na kupiga dili zake mpaka alipopata ajali yake ya kisiasa,kwa mshangao wa wengi baada ya kuona chadema inaungwa mkono na vijana wengi ndio mwaka jana akaibuka na hili bila haya.

  Kiufupi jamaa yenu sio kiongozi yeye ni mtu wa maagizo tu yenye lengo la kumjenga yeye binafsi na hili amekua nalo alipopita kwenye maisha yake,hana tofauti na mrema yule waziri wa mambo ya ndani wa kipindi cha mwinyi,ni misifa jazz band wote tu,bora hata ya magufuli ana afadhali.
   
 19. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Japokuwa ni mwepesi wa kutoa maamuzi lakini maamuzi yake mengi ni ya kukurupuka. Nakumbuka ni huyu aliyetuletea maamuzi ya kuleta mvua ya mabomu, ikashindikana. juu ya suala la foleni, aliletaga wazo lake la njia tatu, nilipoteza rafiki yangu pale karibu na makumbusho kwa ajali mbaya sana ya gari kutokana na implementation ya njia tatu. alisahau pia kuna wanafunzi walifundishwa na kukariri ya kwamba ukitaka kuvuka bara bara lazma kwanza uangalia kulia, then kushoto, kama hakuna gari wewe vuka. kwenye hili wanafunzi watoto wengi walipata ajali na kupoteza maisha na wengine kuwa vilema.
   
 20. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Labda anajiandaa kuwa First Lady.
   
Loading...