Lowassa aikosoa Ripoti ya Jumuiya ya Ulaya kuhusiana na Uchaguzi Mkuu 2015

Carlos Valderrama

JF-Expert Member
Dec 27, 2014
664
240
.

Aliyekuwa Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe.Edward Lowasa ameikosoa Ripoti ya Jumuiya ya Ulaya kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa ilikuwa na dosari nyingi na imetengenezwa katika mazingira ya kukifurahisha chama tawala.

Mhe.Lowasa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani amesema Ripoti hiyo ya Jumuiya ya ulaya ilitakiwa iende mbele zaidi na kuelezea kile kilichofanyika nchini kama kilikuwa ni huru na haki kwa mustakabali wa Demokrasia nchini ambapo pia ameikosoa vikali Tume ya Uchaguzi.

Katika hotuba yake kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambao ni wanachama wa CHADEMA ,Mhe.Lowasa amesema na kila ushahidi kuwa alishinda Uchaguzi Mkuu katika kiti cha urais mwaka jana lakini ameamua kuwa kimya juu ya hilo kwa mustakabali wanchi.Baadhi ya wanafunzi hao wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu wamemweleza kuwa walikabiliana na wakati mgumu kipindi cha masomo yao hasa baada ya kuweka wazi hisia zao za kuunga mkono upinzani.

==========My Take=========

Lowassa kubali yaishe utaendelea kupinga mpaka lini mtambue Rais Magufuli kama rais wako unapingana mpaka na Umoja wa Ulaya, wewe mwenyewe ulisema kura za urais tukuachie mwenyewe leo tena hutaki kukubali matokeo.
 
Lowasa haamini kama Urais ameukosa. Huu Mwezi wa Saba Magufuli yupo Magotoni
 
Katika hotuba yake kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambao ni wanachama wa CHADEMA ,Mhe.Lowasa amesema na kila ushahidi kuwa alishinda Uchaguzi Mkuu katika kiti cha urais mwaka jana lakini ameamua kuwa kimya juu ya hilo kwa mustakabali wanchi..

Lowasa inamwuma pesa aliyomwaga.
Hela alizomwaga hazilingani na kura alizopata.Labda hili ndilo alitaka waangalizi wa kimataifa waandike.

Muulize hapo kituo gani cha kura ataje hata kimoja tu alichoibiwa kura uone atakavyojikanyaga!!!!
Vituo vyote kura zilihesabiwa vizuri na mawakala wake wote walisaini hakuna aliyesusa!!!
Huyi mzee kwa uongo hajambo ili uongo wake umefika mwisho
 
Ninachokona hapa ni Lowasa kugeuza CHADEMA kuwa mali yake. Yeye ndiye huoa matamko ya chama na yeye ndiye huamua wapi chama kielekee
 
Lowasa inamwuma pesa aliyomwaga.
Hela alizomwaga hazilingani na kura alizopata.Labda hili ndilo alitaka waangalizi wa kimataifa waandike.

Muulize hapo kituo gani cha kura ataje hata kimoja tu alichoibiwa kura uone atakavyojikanyaga!!!!
Vituo vyote kura zilihesabiwa vizuri na mawakala wake wote walisaini hakuna aliyesusa!!!
Huyi mzee kwa uongo hajambo ili uongo wake umefika mwisho
Anasema anao ushahidi kuwa alishinda uchaguzi mkuu lakini hataki kuonyesha.
 
Umoja wa ulaya ni wale wale kama marekani wanaojifanya kuuma na kupulizia wakati wana njaa ya rasilimali zetu kama madini. Nchi za jimuiya ya ulaya kama uingereza zinazofaidika sana na Tanzania.
Chezea wakanushe alafu kina fastjet watafaidika wapi. Nchi ilishabinafishwa.
 
Kama ni ushahidi anao chumbani basi tumwachie mweenyewe na mama Lowasa
Jamani Chadema wampe cheo cha Urais atulie maana kila siku ameibiwa kura zake na ushahidi anao kuutoa hatoi mara TB Joshua amesema yeye ameshinda lakini serikali imemwambia TB joshua ambembeleze akubali kushindwa sasa inaelekea TB Joshua ni Mungu kwa EL, looh, makubwa haya!!
 
Umoja wa ulaya ni wale wale kama marekani wanaojifanya kuuma na kupulizia wakati wana njaa ya rasilimali zetu kama madini. Nchi za jimuiya ya ulaya kama uingereza zinazofaidika sana na Tanzania.
Chezea wakanushe alafu kina fastjet watafaidika wapi. Nchi ilishabinafishwa.
Wewe ulitaka Umoja wa Ulaya wamtangaze Lowassa kuwa ndiyo rais bila ushahidi wowote mbona Dr.Sheni hawamtabui.
 
Mzee Mjanja sana huyu, kulalamika huku anajipanga na kuwaaminisha Wanachama wake kuwa anafaa kutetea tena nafasi ili asimame tena, Fanyeni tathmini, mkitanguliza Mahaba akaangukia tena pua Mtatoweka ktk siasa kuna dalili kwamba kila kitu kimekuwa Ndio Mzee, Kaeni vikao ambianeni ukweli, Maana makamanda Lissu,Lema,Mnyika na Wengineo hawasikiki kabisa kuna Sintofahamu hapa.
 
Chadema ndiyo mali yake kwa sasa hamna wa kumpinga kaishaanza kuweka wenyeviti wa wilaya Makongoro tayari kashinda Ilala.
 
Huyu mzee anatafuta pakutokea. Siku hizi hamna matamasha ya kuchangisha wala kitchen party. Anaona anaozea Monduli sasa amekuja na maneno kama haya.
 
Back
Top Bottom