Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

sasa nimeamini Lowasa anataka urais kwa gharama yoyote ile na anaungwa mkono na Rais jk,lkn niwakumbushe wenzangu mwaka 1997 kikwte hakuwa amechafuka kwa jamii alichafuka kwa viongozi wenzake tena kwa mambo yao ya starehe zao lkn leo EL amechafuka kwa jamii nzima.Akimsingizia Nape leo atakuwa anamuonea tu mana amechafuka kabla nape hajakuwa mwenezi anachotakiwa aje barabarani atueleze ukweli sisi watu wa site na pia atuambie kwanini baba wa Taifa alimkataa toka mwaka 1995 pale dodoma atueleze tu jee tukimpa huo urais anaoupigania Hatutapata laana ya baba wa Taifa?otherwise sitamkubali Lowasa
 
Watanzania sasa amua wenyewe. Lowassa kwa mara nyingine amemshinda Kikwete je Bunge letu litaendelea kuchekelea kwa vile wote ni nyani wana mikia?
Haya chini ni maneno mazito aliyomwaga Lowassa akiamua kumwaga mboga baada ya Kikwete kutaka kumwaga ugali.

"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: "Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".

Hizi ni habari za nyuma ya pazia Kwa maana ya kuwa inaweza kuwa sumu nashauri unapopitia habari kama hizi weka maziwa jirani lasivyo waweza zurika
 
sasa nimeamini Lowasa anataka urais kwa gharama yoyote ile na anaungwa mkono na Rais jk,lkn niwakumbushe wenzangu mwaka 1997 kikwte hakuwa amechafuka kwa jamii alichafuka kwa viongozi wenzake tena kwa mambo yao ya starehe zao lkn leo EL amechafuka kwa jamii nzima.Akimsingizia Nape leo atakuwa anamuonea tu mana amechafuka kabla nape hajakuwa mwenezi anachotakiwa aje barabarani atueleze ukweli sisi watu wa site na pia atuambie kwanini baba wa Taifa alimkataa toka mwaka 1995 pale dodoma atueleze tu jee tukimpa huo urais anaoupigania Hatutapata laana ya baba wa Taifa?otherwise sitamkubali Lowasa

Ni mtazamo wako, lakini Lowasa hajatamka kwamba anataka urais, ila anajisafisha ilivyo hulka ya kibinadamu. Kumwandama peke yake haileti mantiki kwa vile wapo wengi na wapo walio wabaya zaidi yake, iweje leo aandamwe yeye?

Uchaguzi wa Igunga Lowasa hakuwako kule, lakini tumeshuhudia magamba yakifanya hujuma za kijasusi hadi kuangamiza roho za watu kwa ajili ya kugombea ubunge, je hayo yaliyofanyika wangefanya wapinzani nini kingetokea?

Lowasa alishatamka tangu tatizo la Arusha linaanza kuwa jambo hilo lisuluhishwe kwa kukaa pamoja na kujadili, lakini walimsakama na kumwambia anaongea mambo nje ya vikao, sasa angesubiri leo walipo Dodoma ndio awaambie wakae pamoja na Chadema kusuluhisha tatizo wakati sasa damu zimeshawagika? Wangemsiikia Lowasa yanayoendelea leo Arusha yasingetokea.
 
Hongera lowasa. Kama wewe ni gamba basi ni la kobe. ndo nyumba inayoficha kobe mwenyewe. Ukijivua gamba nshaandika humu kuwa gamba la kobe likivuliwa kobe haponi hujifia. Ulisema wakato fulani kuwa wakimwaga mboga wewe unamwaga ugali. Simama imara lujitetea, ni heri kufa kishujaa kuliko kifa kinyonge. Sema yote yoote uyajuayo ili hata ukifa uende mbinguni kuliko kuwafichia aibu na huku unabeba mizigo yao mabegani mwako.
 
wacha hasira mkuu lowasa anaonekana ana mengi ya kutueleza ila ukumbuke mwanasiasa huongea ukweli kwenye jina lake tuu na sio hoja zake na mengineyo...lowasa haitaji huruma za jk bali jk ndio anahaha atamfadhili vipi lowasa kwa kufichiana siri...ikumbukwe kama jk angejiuzulu yeye ingekuwa balaa zaidi ndio maana akamuomba lowasa abebe adhabu yake ili aweze kujilinda na kumlinda yeye siasa mchezo wa hila

inaelekea jk amshukuru mzee wa maamuzi ya kiume ben kwa kumshtua abadili mwelekeo la sivyo pangenuka..

Lowassa amekana rasmi kuwa yeye hahusiki na mkataba wa Richmond!

images

Nanukuu:

mwisho wa kunukuu

Hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo amedai kwamba siyo la kweli.

Chanzo: Mwananchi
OK, alitaka kuvunja mkataba huo kama walivyokuja kufanya baadaye na matokeo tunadaiwa mabilioni. Lowasa anaweza kuueleza umma wa watanzania ni nani aliyewezesha Richmond kupewa mkataba huo aliotaka kuuvunja?
 
8.jpg

Tabia hii ndiyo ninayoikataa mimi kuwa mwanaCCM maana yake unatakiwa ufanya kama huna akili timamu vile, unapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Hata kama ungekuwa na upeo gani utadumazwa tu na kuishia kufanya usanii wa maigizo kama binti kawawa anavyofanya kama si mtoto wa mzee wa Simba wa Nyika.

Badala ya kufikiria mambo muhimu ya taifa letu wao ni sherehe na ulaji wa ushindani.

Please.... (Zamaradi?) please stand up, tunakujua hv na wewe umeshamezwa na haya mambo???? siamini,
hebu rudia hali yako, kwanza wewe ni legacy ya SIMBA WA VITA, lazima ulibebe hilo,
baba yako alikuwa anasimamia haki Siku Zote wasikuteke hao, wewe toka kivyako. Sie tuko nyuma yako,
 
naona una usingizi unaota bado
Lowassa kaiba nini? achana na fitina weka data na evidence.halafu mimi nimeshanga mno watu wakiugua wanapelekwa india mnasema ni lowassa.hivi yeye kama ni kweli anawapataje hao watu na kuwapa sumu au ni wewe ndio unaumiwa aulishatumiwa kuwapa simu wengine ndio maana una imamani hiyo?
.huko india mbona zisiletwe taarifa tz kuwa wagonjwa wamepewa sumu,tatizo binadamu ukitenda ubaya unakuwa na mashaka sana
 
Ni mtazamo wako, lakini Lowasa hajatamka kwamba anataka urais, ila anajisafisha ilivyo hulka ya kibinadamu. Kumwandama peke yake haileti mantiki kwa vile wapo wengi na wapo walio wabaya zaidi yake, iweje leo aandamwe yeye?

Uchaguzi wa Igunga Lowasa hakuwako kule, lakini tumeshuhudia magamba yakifanya hujuma za kijasusi hadi kuangamiza roho za watu kwa ajili ya kugombea ubunge, je hayo yaliyofanyika wangefanya wapinzani nini kingetokea?

Lowasa alishatamka tangu tatizo la Arusha linaanza kuwa jambo hilo lisuluhishwe kwa kukaa pamoja na kujadili, lakini walimsakama na kumwambia anaongea mambo nje ya vikao, sasa angesubiri leo walipo Dodoma ndio awaambie wakae pamoja na Chadema kusuluhisha tatizo wakati sasa damu zimeshawagika? Wangemsiikia Lowasa yanayoendelea leo Arusha yasingetokea.

Candid usintie aibu hivi unasubiri Lowasa aseme ndo ujue atagombea Urais hapana mkuu,hata wakati Jk hajatangaza sisi wenye akili tulijua anautaka na hata leo sisi wenye akili Tunajua Lowasa anautaka urais na utakuja kuniambia pia Benard anataka Urais lkn hajatangaza na tupo tunaomuunga mkono na kumpigania ucku kucha kwa misimamao yake kutokuyumba.Huo mtizamo wangu
 
Maselef shukrani sana kwa kuipenda Title yangu. Hata picha yangu bomba sema mvivu mmoja ajiitaye washawasha ameikopi kiasi cha kunidhalilisha. Naye ni gamba tena la kiakili. Tuendelee kujadili CCM inavyoendelea kubaka taifa letu huku fisadi mkuu Jakaya Kikwete akijifanya atapambana na magamba wakati yeye ndiye gamba kuu.

Mkuu, hapa ndipo ninapokumbuka maneno ya Mzee wetu, Mwl. J.K. Nyerere kuhusu wote wawili EL & Baba Ridh. (J.M.K). Anyway worry yangu ni Uchaguzi mkuu wa 2015, huyu Maasai anakuja kwa speed kubwa (supersonic), sijuhi hatima ya nchi yetu hapo baadae; may be pigs might fly one day.
 
Waulize fisadi Rostam, Mwakyembe aliyelambishwa vya kulambishwa, Sitta anayeitwa mnafiki na baadhi ndani ya magamba kwa kutetea maslahi ya nchi dhidi ya malipo ya kifisadi, Wabunge ndani ya magamba ambao hawaridhiki na utendaji wa Kikwete na hivi karibuni walikaribia kumuomba abwage manyanga. Pia usisahau kwamba ukipenda basi chongo utaita kengeza...Kama huoni vitisho ya kutaka kumuua Sitta na Mwakyembe na wahusika kusema hadharani hivyo kwamba wamepokea vitisho vya kunyang'anywa uhai wao kwa njia za simu, basi hutaona lolote lile la kuonyesha mpasuko mkubwa ndani ya magamba. Kwenye upinzani wa kweli ndani ya chama chochote kile cha siasa kunakuwa hakuna vitisho vya kutoana roho, vitisho kama hivi vya kuchukua uhai wa baadhi ya wahusika ndani ya magamba au chama chochote kile huwa vinaashiria mpasuko mkubwa sana.

Wewe usihangaike na huyo, kama hakuna mgogoro muulize CC imekabidhiwa kazi gani na NEC, kama CCM walijua hakuna magamba kwa nini walianzisha dhana ya kuvuana walikuwa wanamvua nani ikiwa wote walikuwa wasafi, utakumbuka Wassira baada ya kutoka Arusha alitamba amemaliza mgororo wa vijana lakini jana akaanza kuwashambulia tena, kwa hiyo wengine hatutashangaa wakitoka kule na kufanya pati kuwa wamemaliza ugomvi wakati sote tumeona kabisa M/kiti kaufunika.

Migogoro CCM ndimo nyumbani mwake, huwezi amini maneno aliyotamka leo Lowassa kwamba (Kikwete kafika pale kwa neema tu) alikuwa nayo moyni zaidi ya miaka kumi ila ukiwauliza wanakuambia ni tofauti tu ya mitazamo, mitazamo gani inafikia kuwekeana sumu? (imefikia wakati hatuaminiani hata kuachiana glass ya maji, JK).

Nape ataadhibiwa si kwa kosa lake bali kwa ujinga wake, alijua wazi anatumiwa na watu walimweleza mapema kuwa wewe ni chambo tu utatupwa, leo lengo lililokusudiwa limeshindikana anageuziwa kibao afadhali basi lingefanikiwa angebaki na heshima yake lakini sasa labda atakachoambulia ni ubalozi wa nje lakini heshima na utu wake kwa watanzania na vijana umepungua kama si kwisha.
 
kwaheri CCM mipasuko na makundi ndani ya chama hayataisha kwa mtindo huu, halafu hiyo NEC na CC ya CCM utadhani ni watoto wadogo bana sasa wamekaa karibu wiki nzima kipi cha maana walichojadili zaidi ya kusutana,kudhalilishana na kuumbuana?
 
Wewe usihangaike na huyo, kama hakuna mgogoro muulize CC imekabidhiwa kazi gani na NEC, kama CCM walijua hakuna magamba kwa nini walianzisha dhana ya kuvuana walikuwa wanamvua nani ikiwa wote walikuwa wasafi, utakumbuka Wassira baada ya kutoka Arusha alitamba amemaliza mgororo wa vijana lakini jana akaanza kuwashambulia tena, kwa hiyo wengine hatutashangaa wakitoka kule na kufanya pati kuwa wamemaliza ugomvi wakati sote tumeona kabisa M/kiti kaufunika.

Migogoro CCM ndimo nyumbani mwake, huwezi amini maneno aliyotamka leo Lowassa kwamba (Kikwete kafika pale kwa neema tu) alikuwa nayo moyni zaidi ya miaka kumi ila ukiwauliza wanakuambia ni tofauti tu ya mitazamo, mitazamo gani inafikia kuwekeana sumu? (imefikia wakati hatuaminiani hata kuachiana glass ya maji, JK).

Nape ataadhibiwa si kwa kosa lake bali kwa ujinga wake, alijua wazi anatumiwa na watu walimweleza mapema kuwa wewe ni chambo tu utatupwa, leo lengo lililokusudiwa limeshindikana anageuziwa kibao afadhali basi lingefanikiwa angebaki na heshima yake lakini sasa labda atakachoambulia ni ubalozi wa nje lakini heshima na utu wake kwa watanzania na vijana umepungua kama si kwisha.

Siasa za ccm unahitaji uzifahamu hakuna hata moja atakosa..kuleana..wanaboa sana

Nape hana kosa, lowassa hana kosa, Chenge hana kosa, RA hana kosa, ....

Nani mwenye kosa??
 
Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma
Thursday, 24 November 2011

Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.

Mi cjui bana, maana lishanichosha sasa....hata hivyo, ,kuna jambo moja ambalo nalifahamu kwa 100% ambalo naweza kulisimamia hata The Hague. Nakumbuka aliwahi kusema : "Mheshimiwa Spika, Nimedharirishwa sana! Nimechafuliwa sana! Nimetukanwa sana! Lakini najua, tatizo ni uwaziri mkuu!"

Leo hii:
"
tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015."

Sooner or later
"Babaz Maaskofu, nimedharirishwa sana , nimechafuliwa sana, nimetukanwa sana! lakini kubwa ninalofahamu kwa vita hii ya sasa ni Unaibu Katibu Mkuu wa UN!"
 
lowassa yuko organized sana katika mambo yake..hakuna issue tena hapo..tutafakari mambo mengine sasa
 
Nawezaje kuipata ripoti hio ya 1997 ya huyo Mzee? Ilihusu nini hasa? Content yake je? Mkapa alisaidiaje? Kwanini alimsaidia? Ilikua na athari gani? Kwahio si kweli kwamba JK ndio kiongozi mwenye mvuto? wala sio chaguo la Mungu? Mmmmh
 
We mkandara ndo haswaa unatumia masaburh kufikiri.unaita wengine wajinga basi we ni mpumbavu.unataka kufunga watu midomo huna adabu.
 
Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.

Yeye alikuwa waziri mkuu na sii katibu wa chama, hakuwahi kupendwa na Nyerere hadi leo hii wananchi hawampendi pengine huko kwenu CCM. Halafu naweza sema ni jambazi lililokubuhu yaani anatuondolea watu tu kila mwaka. Kesho sintoshangaa Nape mgonjwa anatakiwa kupelekwa India..

Mkuu, mzee wetu Nyerere si kwamba alisema kwa EL tu hata kwa J.K. Matokeo ndo tunayaona sasa; the comedy tupu!
 
Maselef shukrani sana kwa kuipenda Title yangu. Hata picha yangu bomba sema mvivu mmoja ajiitaye washawasha ameikopi kiasi cha kunidhalilisha. Naye ni gamba tena la kiakili. Tuendelee kujadili CCM inavyoendelea kubaka taifa letu huku fisadi mkuu Jakaya Kikwete akijifanya atapambana na magamba wakati yeye ndiye gamba kuu.
Washawasha ni mpuuzi mmoja tu humu JF, na nashukuru umejipambanuwa kama huna ushirika nae.
 
Hizi ngonjera za CCM zinatafsiriwa na ma-great thinker kama mimi kuwa ni mbinu mahsusi ya kupoteza watu maboya na kuanza kuijadili CCM badala ya mambo muhimu. Wanajifanya wanapigiana makelele mengi kumbe hamna chochote cha maana watakachofanyana. Badala yake wanaishia kufukuza vijittu vidogo kama Katibu wa CCM Mkoa DSM.
 
Back
Top Bottom