Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Hoja tunayokataa sisi hapa ni kule kunyoshewa kidole watu watatu na wakati ndani ya CCM nzima ni uvundo tupu. Vijana wenyewe akina Nape na wenzake kama wana ubavu si wangetoka nje ya CCM na kuanza kuwanyooshea vidole badala ya kuanzisha chama cha CCJ wakati wako ndani ya CCM kitu ambacho ni usaliti wa hali ya juu na tabia ya ukinyoknga. Vijsent tulisimamia kwenye account ya kisiwa cha UK, lowasa Richmond.

Lakini siri ni kwamba account hizo ni za CCM wanaoiba pesa za serikali na kuzificha nje ya nchi kwa kufungua account za watu binafsi. Ndio maana unamwona vijisent katulia tuliiii, Mnadhimu wa jeshi nchini Abdalah Shimbo anapeta tu na account yake ya mabilioni nchini Afrika kusini, yote hayo ni mapesa ya CCM, vinginevyo wasingethubutu kuachwa na kufunikwa kana kwamba hakuna kinachoendelea.
Sasa mbona huwasemi Lowassa na JK walivyotishia nao kuondoka CCM au wao ni elites hawaguswi. Kutishia kila mtu anaweza kutishia hata ndoa watu hutishia kuvunja ikiwa matakwa yao hayatafikiwa.. sasa jiulize walirudi vipi na iweje JK aliwapa madaraka makubwa zaidi..
Mkuu wangu usafi unauanza ndani na hasa ukikabidhiwa ufagio sasa mlitaka afanye nini? siasa za majitaka kutukana vyama vya Upinzani wakati uchafu uko ndani mwako!..

Yes, CCM imejaa mafisadi lakini unaanza na wale waliokwisha kamatwa na ushahidi upo na wao ndio sababu ya chama kudhoofika. Popularity ya CCM imeiondolewa na watu hawa na sii JK amini maneno yangu kwa sababu Chadema wametumia tu Ufisadi na sasa hivi CCM mahtuti kisha mnafikiri kwenda Loliondo ndio dawa?.. Lowassa ana nini huyu mtu alotuaminisha mvua za kisayansi na Uganga wa Loliondo...Leo ati ni mtu wa kanisa sana kuvaa ngozi ya kondoo basi mnafikiri kesha kuwa Paulo mtakatifu..Hamjiulizi tu kwa nini kila mtu ni against yeye lakini sii wao kuwa na maadui zaidi, maana nijuavyo maadui wa Nape wanatokana na Lowassa na sii wao wenyewe - WHY?

Nakwambieni atawachafua vibaya sana na hakika kufikia mwaka 2015 sijui CCM watabakia kina nani..
 
Hukumweleza nape,maana alishaikana ID yake,we ulimweleza mwngne
Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.

Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.
 
Eti Mkapa alikua anafurahi wakati wakati Lowassa anamsema Kikwete, what does this tell us ? Inaonekana Mkapa kachoka na Kikwete.
 
"Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu"
Nimeyapenda haya maneno ya mwenyeketi. Yamejaa busara na hekima tele.
 
Hivi hapo kuna habari ya kutishwa Kikwete? Tatizo lenu kubwa huwa mnasoma muandishi anavyotaka na si uhalisia wa yaliyojiri, mtu akiogea kwenye hadhara kama ile halafu mwandishi anukuu vipande atakavyo yeye na kuvijengea hoja, ujuwe huyo mwandishi anataka wewe uyashike yake na si yaliyojiri. Hapo mmepigwa changa la macho.

Sioni mahali ambapo Kikwete ametishwa au kuna cha kumtisha sasa hivi? Kama Ukuu ndio anao, hajatishika hiyo 1997 na akasema kama urais ni Mungu mwenyewe ndiye apangae atatishika leo hii? Unanchekesha.
Kumbe kuna nyakati huwa unakuwa haupo biased?
Umenifanya nianze kukupenda.
 
Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.

Yeye alikuwa waziri mkuu na sii katibu wa chama, hakuwahi kupendwa na Nyerere hadi leo hii wananchi hawampendi pengine huko kwenu CCM. Halafu naweza sema ni jambazi lililokubuhu yaani anatuondolea watu tu kila mwaka. Kesho sintoshangaa Nape mgonjwa anatakiwa kupelekwa India..

Licha ya hii ya Richmond ambayo tunajua urafiki, unafiki na kubebana kunakoiua CCM ndio kulimbebesha Lowasa hili zigo (offcouse alipata chochote) kuna ufisadi/ wizi, kutokuwajibika kwingine anakohusishwa nako?
 
.......Anayoyaongea Nape ndiyo msimamo wa Chama.
By Jakaya.
Kwa kauli hiyo inabidi JK ajiulu nyazifa zake katika chama ili kuipisha CC ichukulie hatua stahiki watuhumiwa na katika mazingira huru.
 
Licha ya hii ya Richmond ambayo tunajua urafiki, unafiki na kubebana kunakoiua CCM ndio kulimbebesha Lowasa hili zigo (offcouse alipata chochote) kuna ufisadi/ wizi, kutokuwajibika kwingine anakohusishwa nako?
Ana kashfa ardhi, chini ya Mwinyi. Jamaa respnsibilities kubwa keshapewa sana, na ameprove tamaa yake....
Tatizo ni kuwa wale viongozi wa CCM wanaoonana na watu mitaani na vijijini, hasa ngazi za wilaya na mikoa wamegawanyika sana kutokana na hawa wapuuzi walio kwenye ngazi ya Tafa.
Njaa, tamaa, siasa na pesa ni combination mbaya sana..... almost like money and blood.
 
Lakini siri ni kwamba account hizo ni za CCM wanaoiba pesa za serikali na kuzificha nje ya nchi kwa kufungua account za watu binafsi. Ndio maana unamwona vijisent katulia tuliiii, Mnadhimu wa jeshi nchini Abdalah Shimbo anapeta tu na account yake ya mabilioni nchini Afrika kusini, yote hayo ni mapesa ya CCM, vinginevyo wasingethubutu kuachwa na kufunikwa kana kwamba hakuna kinachoendelea.

Kwa nini hizi pesa za kisiwa cha uingereza za vijisenti na mabilioni ya Abdalah Shimbo huko Afrika ya kusini zimezimwa na serikali ya Jakaya? Kuna mchezo mchafu sana hapa, hizo ni pesa zinazoibwa na CCM na kufichwa nje ya nchi, kama hamuamini ipo siku yote yatafichuliwa.
 
......... sasa jiulize walirudi vipi na iweje JK aliwapa madaraka makubwa zaidi..
Mkuu wangu usafi unauanza ndani na hasa ukikabidhiwa ufagio sasa mlitaka afanye nini? siasa za majitaka kutukana vyama vya Upinzani wakati uchafu uko ndani mwako!..

............Yes, CCM imejaa mafisadi lakini unaanza na wale waliokwisha kamatwa na ushahidi upo na wao ndio sababu ya chama kudhoofika. ............Nakwambieni atawachafua vibaya sana na hakika kufikia mwaka 2015 sijui CCM watabakia kina nani..
Nakubaliana nawe kwa hizi statemants,
CCM masikini wananyoosheana vidole wakati sasa wangetakiwa kusimama, na kurudi kwa wananchi na kutuhakikishia lengo la chama ni kutufanyia kazi, na kukubali walitetereka sasa waanze kuwa serious na kila ushahidi wa waliomo kati yao kuhusiana na wizi. Wasiogope, wawe mfano wa kwanza wa kufuata sheria.
Hapo sie wapenzi wa zamani wa chama tutarudi.
Bila wao kutuongoza kufuata sheria kwa uwazi tutabakia hewani tu.
Shares zao kwenye makampuni kama ya cementi, madini, bandari, mabenki nk kwa kutumia hela zetu wakubali tu watakaotuhumiwa wachitakiwe na wahukumiwe BASI.
 
.......Anayoyaongea Nape ndiyo msimamo wa Chama.
By Jakaya.
Kwa kauli hiyo inabidi JK ajiuzulu nyazifa zake katika chama ili kuipisha CC ichukulie hatua stahiki watuhumiwa na katika mazingira huru.

Huu mstari wako waanza kuoyesha mwanga kwa Watanzania ... In fact hiyo ni Tiba!!
 
Ana kashfa ardhi, chini ya Mwinyi. Jamaa respnsibilities kubwa keshapewa sana, na ameprove tamaa yake....
Tatizo ni kuwa wale viongozi wa CCM wanaoonana na watu mitaani na vijijini, hasa ngazi za wilaya na mikoa wamegawanyika sana kutokana na hawa wapuuzi walio kwenye ngazi ya Tafa.
Njaa, tamaa, siasa na pesa ni combination mbaya sana..... almost like money and blood.
Downhill ........hakuna kusimama, labda uwe na breki za ajabu
CCM inakwenda kwa spidi sana shimoni, inasikitisha lakini. Yani hata vijana kama kina Nape tayari wako pale kwa ajili ya maslahi ya wazee, eti vijana, masikini
 
"Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu"
Nimeyapenda haya maneno ya mwenyeketi. Yamejaa busara na hekima tele.

Ha ha ha, "tukajenge chama chetu na magamba yetu." Hakyanani gamba limegoma kuvulika.
 
Back
Top Bottom