Lowassa adaiwa kuifadhili ACT-Tanzania; yeye, ACT wakanusha

Taarifa hiyo ni ya kupikwa na gazeti la Tanzania Daima ambalo linamilikiwa na Mbowe,huo ni mkakati endelevu wa kumchafua ZITTO KABWE na chama cha ACT, CDM wana kiwanda cha kupika uongo.
uko sahihi sana nilifikiri kuna vichwa vibovu tu kumbe vizima vipo shukran sana
 
Inashitua kuona huyo anayejita mtunza hazina wa ACT akikiri kuwa wamechangiwa zaidi ya million 74 na zote zimetumika na taarifa kutolewa. Kwa chama kichanga namna hii lazima tukuhoji pesa zote hizo zimepatikanaje na kwanini zitumike haraka hakaka? Hii kwa vyovyote inatupa ushaidi wa mazingira wa akuwepo ufadhili wa kununua watu.
 
vyama vya tanzania vilivyokuwa registered vina idadi ya wanachama, the highest ni CCM yenye wanachama wasiozidi milioni nne, tanzania ina watu zaidi ya milioni 44

Thanks

Mkuu,
Citation/ Source ni muhimu, maneno hayo bado hayajaweza kufanya rekodi yako iwe authenticated. Weka source ya takwimu ili watu wakafanye utafiti ku-verify the authenticity of your claim.
 
Mkuu,
Citation/ Source ni muhimu, maneno hayo bado hayajaweza kufanya rekodi yako iwe authenticated. Weka source ya takwimu ili watu wakafanye utafiti ku-verify the authenticity of your claim.

we dont need to be comically academic kwenye kila kitu especially in a country where data quality validation is not a NORM

usijitoe fahamu kipuuzi - hizo tafiti ndio zilizotufanya kushindwa hata kufanya simple decisions

i believe you have done some planning in your life... the concept is simple, you dont need to go to decimal points when forecasting... i would recognize lack of this concept kama uko bado kwenye bolts and nuts, na sio kwenye strategic level

the funniest part ni hiyo ya kusema weka source ya takwimu ili watu wakafanye utafiti ku-verify... so low!! you want to verify instead of wewe kufanya hiyo tafiti
 
lowassa3.jpg

IMEGUNDULIKA kwamba Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) ndiye mfadhili mkuu na mpanga mikakati mkuu wa kundi linalomfuata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambalo limeanzisha chama kipya cha siasa, Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).

Kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, makundi ya wanachama, washauri na wapanga mikakati wa Lowassa na Zitto wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam na kupeana mbinu, lengo kuu likiwa ni jinsi ya kumega Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mapande ili kidhoofike kabla ya uchaguzi mkuu 2015.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Lowassa amejiaminisha kwamba ndiye atakayekuwa mgombea urais kupitia CCM. Kazi kubwa anayoona mbele yake ni kuanza mapema kusambaratisha CHADEMA ili kupunguza upinzani wakati wa kampeni utakapofika.

Zitto naye, ambaye uanachama wake kwa CHADEMA umebaki kwenye makaratasi tu, anatajwa kuwa ndiye mwasisi mwenza wa ACT, na amekuwa na uhusiano wa “kikazi” na Lowassa, hata kabla hajaingia kwenye matata ya wazi na chama chake, ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilimvua vyeo vyake vyote vya uteuzi ndani ya CHADEMA kwa tuhuma mbalimbali.

Katika hatua mojawapo, chanzo kimoja kilicho karibu na Lowassa kimesema kwamba mapema mwaka juzi, Zitto alimwendea Lowassa na kumwambia kuwa mustakabali wake kisiasa ndani ya CHADEMA si mzuri, na kwamba alikuwa tayari kumsaidia Lowassa kufanikisha malengo yake, lakini kwa sharti kwamba iwapo mbunge huyo wa Monduli atafanikiwa kupata urais, basi amteue kuwa Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kauli hiyo kwanza ilimstua Lowassa kwa sababu ilimuonesha Zitto kama kiongozi asiye mwaminifu, ambaye yupo tayari kufanya hujuma dhidi ya chama chake, jambo ambalo lilimfanya Lowassa atilie shaka lengo la ombi hilo.

Jambo la pili lililomshtua Lowassa ni cheo kilichopendekezwa na Zitto, maana kwa mujibu wa Katiba ya sasa, Waziri Mkuu lazima atokane na wabunge wa majimbo, na awe kwenye chama chenye wabunge wengi.

Kwa kuwa hoja hiyo ilitolewa katika mazingira ya Katiba ya sasa, na kwa kuwa haikujulikana wakati ule kama Zitto alikuwa bado ni mwanachama na kiongozi wa CHADEMA, Lowassa hakuipata nafasi kauli hiyo, lakini amekuwa anaitumia kujadili sura halisi ya Zitto.

Hata hivyo, taarifa zinasema uhusiano wao umeimarika baada ya Zitto kuchukuliwa hatua na CHADEMA, huku wapambe wa Lowassa wakipita huku na kule kusambaza propaganda kuwa CHADEMA bila Zitto inakufa.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Zitto anatarajiwa kujiunga rasmi na ACT mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, na timu ya Lowassa imedhamiria kumfadhili ili kujenga taswira ya mpasuko ndani ya CHADEMA, na kuipa CHADEMA mpinzani mpya ambaye ataifanya ishindwe kumfuatilia na kumshambulia Lowassa.

Katika kikao cha mwisho kilichofanyika kati ya timu ya Lowassa na “Vijana wa Zitto” kilijumuisha baadhi ya wapambe wakuu wa Lowassa wenye kauli ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM, watu wa karibu kifamilia na Lowassa na washauri wa karibu wa Zitto, akiwamo Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ajenda zao nje nje

Moja ya ajenda zao kuu ni kufadhili na kupandikiza watu ndani ya mfumo wa CHADEMA ambacho kinaendelea na uchaguzi wa ndani, ili wapate nafasi za uongozi, wazitumie kupata taarifa na mipango ya chama, na baadaye wajivue nafasi hizo na kukimbilia ACT, na kuleta msisimko wa kitaifa.

Gazeti hili lina taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa sasa wa CHADEMA ambao “Vijana wa Zitto” wamekuwa wakiwapigia simu na wakati mwingine kuwatembelea na kuwashawishi ahadi ya fedha na vyeo ili wajiondoe CHADEMA.

Baadhi hao ni viongozi wa majimbo na mikoa ambao katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hawana uhakika wa kuchaguliwa kutokana na upinzani mkubwa unaojitokeza baada ya chama kukua na kuvutia wasomi na wafanyabaishara wenye mvuto katika maneo yao.

Baadhi ya viongozi walioendewa au kupigwa simu wamechukua tahadhari, na wametoa taarifa panapohusika ndani na nje ya chama.

Mbinu mojawapo ambayo imekuwa inatumiwa na “Vijana wa Zitto” kujaribu kuvunja ngome za CHADEMA ni kuwatangazia viongozi hao kwamba ipo idadi kubwa ya wabunge wa CHADEMA wanaotarajia kujiunga na ACT. Wanawataja majina kama njia ya kujenga ushawishi.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi hao wameliambia gazeti hili kuwa wanajua hizo ni mbinu za kipropaganda. Na baadhi ya wabunge wanaotajwa wamesema hizo ni mbinu za Zitto kutaka kuwagombanisha na chama chao na kujitafutia njia mpya kwa kutumia majina yao.

Mmoja wao alisema, “Zitto mwenyewe ameshalikoroga. Sasa hii ni tabia ya kututaja baadhi yetu, mimi na wenzangu kadhaa tumeshasikia, ni ile ile roho mbaya ya tukose wote. Kwa kuwa yeye amekosana na chama, anatafuta watu wa kufa naye.”

Mbali na kupandikiza wagombea nafasi za uongozi na kuvizia viongozi wanaoogopa joto la uchaguzi ndani ya chama, wamekuwa pia na mbinu ya kushawishi baadhi ya “wagombea watarajiwa” katika baadhi ya majimbo, wanaotajwa kuweka nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia CHADEMA.

Makada kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamezungumza na gazeti hili na kutumia kauli zijazofanana. Kwa mfano, makada sita walioweka nia ya kugombea ubunge katika majimbo kadhaa ya kanda ya Ziwa Mashariki na Magharibi, wamekiri kwamba kila wanapojadili mkakati huu na “Vijana wa Zitto,” kila mmoja wa nafasi yake anapewa ahadi ya kupewa pesa zote za kufanyia kampeni.

Vile vile, baadhi yao wamesema kuwa wanaambiwa kwamba iwapo watakubaliana na mpango huo wa ACT, moja kwa moja watakuwa wamepitishwa, maana chama hicho hakina mpango wa kupata wagombea kwa kutumia kura za maoni.

Taarifa zinasema sehemu ya malengo ya vikao ya Zitto na Lowassa ni kutafuta pesa kwa ajili ya mradi huu.

Zipo taarifa zisizothibitishwa kwamba mwezi uliopita Lowassa aliambatana na Zitto katika ziara ya kimya kimya ya Mkoa mmoja wa kanda ya Ziwa ambako anasemekana anataka kujenga ngome nzito ya ACT.

“Ninachojua ni kwamba iwapo ACT itafanikiwa kupunguza makali ya CHADEMA, Mzee atapita kirahisi, maana kikwazo kikubwa alichonacho hadi sasa hakipo ndani ya CCM, bali CHADEMA,” alisema mtoa taarifa wetu aliye karibu na Lowassa, ambaye hakutaka kuthibitisha kama wawili hao walisafiri pamoja kwenda Kanda ya Ziwa

Chanzo: Tanzania Daima

===================

Lowassa akanusha:

ACT pia wakanusha:
hilo ni kweli na ndomana ma ccm ni bora wampe urais prof. anna tibaijuka kuliko hao wanaotaka utawala km lowassa
 
nani kakwambia mimi ni bavicha? fikiria kwa ubongo!,..%loi

Msamehe bure tu mvuta b.angi huyo. Wengine tumemzoea. Mkipishana mawazo kidogo basi anakuita kila jina linalomjia kichwwani mwake!
 
Kwanza nikusaidie jambo moja sio kila mtu humu anaishi Dar , so kumwambia kila mtu karibu ofisini sio sahihi kwani wengine wapo nje ya nchi, nje ya Dar nk, utawarejeshea nauli?

Pili, unasema umeshatumi milioni 74 tangu mlipoanza harakati zenu , je ? Mna watumishi wangapi na mnawalipa kiasi gani kwa mwezi , ili hesabu ziweze kufanyika .
je? Mna magari mangapi na kilamoja mlinunua bei gani ama ni sehemu ya michango na hiyo michango ipo kwenye hizi hesabu ulizotaoa?

Je? Ofisi za Makao makuu pale jengo la NHC Ubungo mnalipia kiasi gani kwa mwezi na mmelipia miezi mingapi ? Au nalo ni mchango kutoka NHC kwa kuwa ni moja ya mashirika ya umma ambayo yanakaguliwa na kamati ya PAC ?

Mwisho, viongozi wenu wakisafiri nje ya Dar huwa mnawalipa kiasi gani? Ni wangapi walishiriki zoezi la usajili na usaili na mpaka sasa umewalipa kiasi gani? Na kikao cha kuandaa mpango kazi mlifanya hoteli ghali sana Morogoro , mlilipia kiasi gani na mlikaa siku ngapi? Na wale baadhi ya viongozi wa Chadema mliowatoa tabora kuja Dar mliwalipa kiasi gani na wale waKahama , Shinyanga mliwalipa kiasi gani .

ukinipa majibu ntakuwekea nyaraka na Benki statement za ACT ........ila jua unafiki hauna Tija maana ukweli unaujua ......

Nasubiri majibu Mhasibu ........
 
vyama vyetu vya siasa havina budi kujipanga upya, kama mtu mmoja akitoka ndani ya chama na chama kinateteleka, hili siyo hali nzuri katika msitakabali wa vyama vya siasa, leo au kesho wakiruhusu mgombea binafsi basi vyama vyetu vya siasa vitakufa, nimeanza hivyo kuonyesha ni namna gani vyama vyetu vya siasa vimeshindwa kuweka misingi imara, hoja imara, na sera imara ambazo zinaweza kuwa nguzo na kivutio kikuu kwa wanachama kujiunga na chama husika badala ya wanachama wengi kujiunga na vyama siasa kwa kumufuata mtu, kwani pindi mtu huyu anapotoka ndani ya chama hukiacha chama kikiwa hali mbaya na hatimamye chama husika kinaweza kufa, mfano angalia ,adhara ya zitto kabwe ndani ya chadema, na nguvu kubwa inayotumiwa na chadema kumudhoifisha zitto, badala chama hiki kijiweka zaidi kwa wananchi.......tatu chadema wapunguze lawama bali waweke mikakati madhubuti ya kujijenga zaidi kama chama na kuweka misingi imara.
 
Mzito Kabwela

Kwa hiyo sasa una doubt CPA yangu au? Bahati mbaya mtunza hazina wenu amesomea political science na mhasibu mkuu ni cashier. Ni kwa sababu hii huwezi kuelewa maana ya CPA!! Na unadiriki ku-doubt udaktari wa mtu aliyewaandikia ilani ya mwaka 2010 iliyowafanya mseme mlishinda uchaguzi. Mmelaaniwa?

CPA sio makaratasi. Wala sio kujisifia mitandaoni. CPA ni pamoja na demonstration. Kama wingi wa initials ingekuwa ni issue, tunao kina KAPUYA wengi sana Tanzania. Mhasibu gani unaleta ripoti ya mapato na matumizi ya chama kama muuza nyanya wa Tandale?
 
Ulivyo mjinga wewe mwenye CPA umeona kuandika Ilani ni CV kuuubwa kwa huyo msaliti mwenzenu?! Nikukumbushe tu kuwa hata Lusinde, Mbunge wa Mtera ameshiriki kuandika Ilani ya mabosi na wafadhili wenu CCM. Nikwambie kingine? Hata Mrema Lyatonga na yeye ameandika Ilani ya TLP. Sasa kama kuandika ilani ni issue basi Kitila ana u dokta wa mashaka
 
Hivi chama chenu wanazotaarifa za fedha zinazofanana na za wauza maandazi. Kijana badilika utafute ukweli. Zitto mlimzushia mambo mengi ya uongo kawapuuza lakini bado mnamfuatafuata. Siku utakapojua ukweli wahafidhina watakuwa wamekuoa
 
Umeijua chadema mwaka 2010 wakati mgombea wenu wa uraisi akiinadi ilani iliyoandikwa na dr kitila. Shida yenu hamthamini potentials za watu, wakiondoka mnabaki kutukana. Hamna mnachojua zaidi ya matusi, act ni habari nyingine imejaza watu wenye uwezo. Hamuoni aibu mnawazushia wao wanasonga mbele na bado.
 
... huhitaji ujuzi wa particle physics to connect the obvious. Scenario iliyo wazi inahusu harakati za KINGMAKER kuendeleza mbinu za kuweka madarakani watu wake (wao) kwa sababu na mahitaji wanayojua wao. Its not a laughable matter. List ya Ministers waliotengenezewa nyadhifa walizo nzao sio fupi. It is significant. ZZK alinaswa siku nyingi na ni part ya long term strategy. Just connect the dots.
SOURCE: Myself
 
Yaani lowassa aache kupambana na maasimu wake ndani ya chama ccm kama akina membe, sitta, makamba,sumaye,magufuli katika kinyanganyiro cha uraisi et ajee afadhili act.....act itamsaidia nini na chadema itamsaidia nini in short mtoa mada ametumwa na kundi 209 ndani ya kumchafua mzee wetu kwenye kura za maoni

People always gotta have a plan B
 
Umeijua chadema mwaka 2010 wakati mgombea wenu wa uraisi akiinadi ilani iliyoandikwa na dr kitila. Shida yenu hamthamini potentials za watu, wakiondoka mnabaki kutukana. Hamna mnachojua zaidi ya matusi, act ni habari nyingine imejaza watu wenye uwezo. Hamuoni aibu mnawazushia wao wanasonga mbele na bado.
Ulivyofilisika kwa hoja unaanza kuandika mavi tu. Waliojiunga 2010 wana alama gani? Kama kuandika ilani ni issue hata Hashim Rungwe naye kaandika Ilani. Usiwe kama bata, rudi kwa ID yako we mwenye CPA ya kuuzia mayai ya kuku!
 
Hivi chama chenu wanazotaarifa za fedha zinazofanana na za wauza maandazi. Kijana badilika utafute ukweli. Zitto mlimzushia mambo mengi ya uongo kawapuuza lakini bado mnamfuatafuata. Siku utakapojua ukweli wahafidhina watakuwa wamekuoa
Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ameridhishwa na namna mapato na Matumizi Chadema yalivyo. Wewe mwenye CPA ya kuuzia sumu za panya unakuja hapa unamwaga uharo. CPA holder unaleta ripoti kama muuza kitimoto? Huna akili kabisa!
 
Hivi chama chenu wanazotaarifa za fedha zinazofanana na za wauza maandazi. Kijana badilika utafute ukweli. Zitto mlimzushia mambo mengi ya uongo kawapuuza lakini bado mnamfuatafuata. Siku utakapojua ukweli wahafidhina watakuwa wamekuoa

Kwaiyo wewe umeolewa na nani? Hao waliokupa CPA ya kuuzia kitimoto?
 
we dont need to be comically academic kwenye kila kitu especially in a country where data quality validation is not a NORM

usijitoe fahamu kipuuzi - hizo tafiti ndio zilizotufanya kushindwa hata kufanya simple decisions

i believe you have done some planning in your life... the concept is simple, you dont need to go to decimal points when forecasting... i would recognize lack of this concept kama uko bado kwenye bolts and nuts, na sio kwenye strategic level

the funniest part ni hiyo ya kusema weka source ya takwimu ili watu wakafanye utafiti ku-verify... so low!! you want to verify instead of wewe kufanya hiyo tafiti

The point here ni ku-verify takwimu na source yako. Una uhuru wa kusema lolote lile, I don't care kusema hivyo is too low or whatever you can call it but ukweli utabaki palepale. Verification ya source ni muhimu.
 
Back
Top Bottom