Sijaelewa una maana gani kusema hivyo, kama unasema kwa dhati ya moyo au umeandika kwa kebehi lakini yote kwa yote (msemo wa Maulid Kitenge) ujumbe wako umefika na mimi kwa dhati ya moyo nakuunga mkono.
Kuna jambo najiuliza kuhusu Lowasa nakosa jibu kabisa. Naomba labda kwenye kitabu hicho au hapa jamvini nitasaidiwa:
1. Tume ya Bunge ya Mwakyembe haikutamka moja kwa moja kuwa Lowasa ni culprit wa Richmond ili walisema yeye mwenyewe apime uzito aamue. Kama alivyosema mwenyewe kuwa mimi ni waziri mkuu na ndiye nayesimamia utendaji wa serikali yote na kwa kuwa makosa ya richmond yalitendwa na watendaji wa serikali walio chini yangu, na kwa kuwa inaonekana anayetafutwa sio Lowasa (hii ni kweli maana mpaka leo hajashtakiwa) bali ni uwaziri mkuu basi naachia ngazi kweli, akaachia uwaziri mkuu ndio ikiwa mwisho wa hadithi. Angekuwa anatafutwa Lowasa na sio uwaziri mkuu tungeshasikia naye kesi yake iko Kisutu siku nyiiiingi.
2. Lowasa hajashtakiwa, wala hakustaafishwa ila ni waziri mkuu mstaafu, kwa hiyo kuondoka kwake ilikuwa ni kuwajibika(Mwinyi aliwahi kuwajibika lakini baadaye akaja kuwa Raisi wa nchi hii)
3. Sijaona wala sijasikia kiongozi wa upinzani wala wanaharakati wala wapiga vita ufisadi wa CCM wakitia shime kuwa Lowasa ashtakiwe rasmi zaidi tu ya maneno ya pembeni ambayo sisi kwetu tunaita majungu
4. Mara nyingi wanasiasa au wanaharakati wakiona kuna kiongozi kafanya madhambi na dola inamlinda huwa wanaitisha maandamano au nguvu ya umma kutaka serikali imchukulie hatua huyo mwanasiasa, jambo hili sijaliona likitendeka kwa lowasa kwanini? Nafsi zao zinawaambia hana hatia yoyote
4. Dola imemuona hana hatia, Mahakamani hajafikishwa, tume ya Bunge katika taarifa yao rasmi haikumhusisha moja kwa moja Lowasa na Richmond haya mengine yanatoka wapi?
Edward Lowasa yawezekana ana mapungufu mengine kama mwanadamu yoyote lakini kwa hili la Richmond mimi namtetea hadi nipate uthibitisho mwingine tofauti na hali ilivyo sasa.
Naam, Lowasa andika kitabu ueleze ukweli wote, wapo wengi ambao tunajua kupima mambo kwa kuaangalia pande mbili zote kuliko kushabikia tu. Wewe bado ni shujaa tu.................................