Lowasa vua viatu (ccm)mahali ulipo ni patakatifu

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
2,184
2,451
Wakuu, kwa wale ambao ni wasomaji wa biblia tukufu kuna watu wawili nataka niwazungumzie.
Mtu wa kwanza ni Saul (Paulo) mtu huyu aliifanya kazi ya kuwauwa watumishi wa Mungu tena alifanya kwa bidii na moyo Mkuu huku akifikiri watu hao walikuwa hawako katika mstari Mungu anaotaka kuabudiwa hivyo alifikiri anafanya kazi ya Mungu.Wakati Stephano anapigwa mawe ni Sauli aliydkuwa aneshika nguo za waliomuua Stephano.
Mungu aliiona commitment ya Sauli akaamua kumuita na akamtumia kueneza neno lake katika njia sahihi na kwa nguvu ileile,na akabadilishwa jina akaitwa Paulo.
Mtu mwingine ni Musa,Musa aliwahi kuuwa,alimuua Mmisiri baada ya kukuta mmisiri huyo anampiga muisrael kule gosheni.
Baadae Musa alikimbia na akaenda kuwa mchungaji baada ya kukaa huko kwa muda Mungu alimuita na katika tukio like aliambiwa avue viatu hasingeweza kutumika na VIATU vile.

Namfananisha Lowasa na watu Hawa sasa Lowasa ameambiwa avue VIATU CCM Kwakuwa sasa anaenda kuwatumikia watanzania akiwa sehemu sahihi.
KILA LA KHERI EDWARD
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom