Lowasa tumia fursa hii kuingia ikulu achana na makanisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowasa tumia fursa hii kuingia ikulu achana na makanisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Mar 23, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kwanza napenda kuwa wazi kwamba Sikukubali Lowasa kama Mtanzania unayestahiri kuwa kiongozi wa Taifa letu kama Taifa kutokana na Historia yako isiyoridhisha.

  Lakini napenda pia kuwa wazi kwamba, nakutambua lowasa kama mmoja ya watanzania wenye moyo wa kuthubutu na kusimamia kile unachokiamini au unachokitaka, kwa mfano, ulisimamia bila kujali vikwazo vya taratibu za kazi na kuhakikisha kwamba Richmond inapata dili la Tanesco na hivi sana unasimamia mchakato wa kuhakikisha kwamba anaingia Ikulu bila hofu yeyote ile.

  Leo nataka kutoa hoja ya kukusaidia katika kujisifisha na kujijenga vizuri na uweze kutimiza ndoto zako, Fursa pekee ya msingi uliyobakiwa nayo ndugu ni nafasi yako Bungeni kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama.

  Nakushauri ufanye mambo yafuatayo kupitia nafasi hii, na hakika mioyo ya watanzania inaweza kukugeukia kama shujaa wao. Japo kwa kupiga kelele Bungeni ufanye yafuatayo
  1. lazimisha report ya uchunguzi ya Kampuni ya Meremeta ifikishwe kwenye kamati yake na kaisha aiweke wazi.
  2. itake Serikali itoe report yake juu ya milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la Moto na report juu ya mchakato wa kuwafidia wahanga wa miripuko hiyo.
  3. muombe Rais Kikwete kuweka wazi List ya wauzaji wa Madawa ya Kulevya nchini aliyolitangazia Bunge kuwa nayo mwaka 2005. Na itake serikali kulieleza Bunge mikakati yake katika kudhibiti ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinauhathiri uchumi wa nchi na afya za vijana kwa kasi sana.

  Nadhani hii ni njia mbadala ya kufikia malengo yako badala ya kupoteza muda na mambo ya ajira kwa vijana na michango ya makanisani ambayo tayari ameishaanza kupata upinzani kwayo kutoka kila pande.

  Kumbuka itakuwa Rahisi sana kukwepa mauharisho ya kina Nape sababu watanzania wote watajua kwamba unatimiza wajibu wako kama Mwenyeki wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama

  Ukinielewa sawa, ukinipuuzia sawa.
   
 2. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ushauri bomba kwa lowassa.......tehetehetehe...ila hatakuwa hana haja ya kuutafuta urais akifanya hivyo kwakuwa anautfuta akayalinde hayo yasimdhuru
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii ni kali kuliko zote. This is antithesis of Edward Lowasa
   
 4. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lowasa anapitaga huku jamani????

  Ushauri mzuri, lakini mtoa mada unafikiri Lowasa anaweza kuwa na akili za aina hiyo? halafu uchaguzi ujao, si CCM wanatoa mgombea kutoka upande wa pili wa Muungano? Sasa lowasa anahangaikia nini? au atajibadili jina na kujiita Hassan kutoka Mkoa wa mjini Magharibi?????? Kazi kweli kweli.... Au umesahau jinsi Sitta alivyotakiwa kujibadili jisnsa ndani ya masaa 24 ili agombee nafasi ya U - BIBI KIROBOTO???? ndivyo itakavyokuwa 2015, kama atatakiwa mgombea wa chama cha magamba kutoka Zenj Lowassa atafanyaje????
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Ndugu
  Kwanza, Humu ndani kuna kagroup kanajiita Friends of Lowasa.
  Pili, Hakuna Mwanasiasa wa Tanzana especially kwenye level ya ubunge ambaye haingii humu ndani, Kama utakumbuka vizuri baada ya JF kutajwa kama chanzo cha kuporomoka kwa kura za JK kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 kulitokea kundi kubwa sana la members wapya humu ndani wakiwa na mlengo wa kuitetea CCM kwa kutumia nguvu nyingi sana.

  Tatu, sio lazima aingie front, uwepo wa watu kama Hussein Bashe, DR Kigwangala n.k ni ushahidi wa kutosha kwamba Lowasa yumo humu ndani japo by proxy.
   
Loading...