Elections 2010 Lowasa sasa autaka Uspika

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Kuna taarifa ya kuwa Edward Lowassa ameanza mikakati ya kuusaka Uspika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya muungani wa Tanzania.
 
Anafaa na anastahili.
Ana uzoefu wa kutosha sasa bungeni na serikalini.
Bado taifa letu linahitaji mchango wake.
 
Kuna taarifa ya kuwa Edward Lowassa ameanza mikakati ya kuusaka Uspika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya muungani wa Tanzania.

Kama ni kweli ngoma hiyo itanoga sana kwani atapambana na Mr. Speed na Viwango aliyetangaza mapema kuwa akirudi mjengoni atatetea kiti chake cha uspika!! Sasa sijui hiyo chama yao itampendekeza nani kati yao?
 
Jizi na fisadi mkubwa anatafuta nini pale mbele ya mjengo. Yeye aendelee kusinzia kwenye kiti chake cha kawaida. Nitawashangaa sana ccm wakimruhusu jambazi awe spika. Isitoshe ana hulka ya kujisikia na ana dharau sana.
 
Kuna taarifa ya kuwa Edward Lowassa ameanza mikakati ya kuusaka Uspika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya muungani wa Tanzania.

Siku EL anakuwa SPIKA wa bunge la 10 narudisha CARD YA CCM mbele ya vyombo vya habari na siku hiyo wana JF ndio mtanifahamu waziwazi me ni mwanamageuzi makini ndani ya CCM pasipo uoga ninae taka mabadiliko mahali nilipo ndani ya hiki chama wananijua fika kuwa nina fuata mkondo ule wa mwalimu aliutaka uwe kuwatumikia watu na sio matumbo yetu.

 
twafwaaa watz! Naamini akipata hamna hoja ya msingi itakayo jadiliwa, sijui tunaelekea mahali gani watz
 
"TULIFURAHI PAMOJA,TULISIKITIKA PAMOJA NA TUTASONGA PAMOJA NA TUTASHINDA" hiyo ni kauli mbiu ya el katika jimbo la monduli,je mnafahamu maana yake ?
 
el AKICHUKUA USPIKA BASI TUMEKWISHA LAZIMA ATALIPIZA KISASI . ok labda anangojea kwanza rafiki JK yake kama atashinda ndio achukue
 
Na hakuna anayeweza kumzuia akisimama lazima mafisadi wenzake watamchagua labda Mwakyembe nae achukue fomu halafu zipigwe kura ambazo indirect zitaamua Lowasa fisadi au sio fisadi akishinda basi sio fisadi
 
Hizi ni porojo,EL hawezi hata ku uwaza uspika.
Labda uwaziri kwa swaiba wake.
 
Hiv mnajua kikwete ninyi???? Amini msiamini mnaweza kushangaa EL anakuwa spika mpya wa bunge. bwana 'kuchekacheka' hajali chochote. Tangu lini mlisikia kikwete ametendea kazi malalamiko ya wananchi. Tena safari hii ndiyo mtalia zaidi atasafiri nchi za nje mpaka mlie.
 
Leo Alhamisi ndio mwisho wa kuchukua fomu za kuwania Uspika kwa mujibu wa makamba. Tupashane kama jamaa ana guts za kufanya hiyo. Ni vema tukazama kwenye maombi asifanye hivyo. Mungu wa Israel atatusikia tu.
 
Back
Top Bottom