Lowasa kujaribu nguvu ya kundi lake ya kabla ya urais

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Mh. Lowasa mbunge wa Munduli atajaribisha nguvu ya kundi lake katika uchaguzi wa Arumeru unaotarajiwa kufanyika 01.04.2011. Katika siku za hivi karibuni ndani ya chama tawala CCM kumeibuka makundi ambayo yanakinzana katika kila jambo.

Hali hiyo ilijihiridhisha wazi wazi katika uteuzi wa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika jimbo la Arumeru na kupelekea mgombea anayetajwa kuwa kipenzi cha Lowasa kupita kwa mawaa mengi.

Jambo hilo limeibua sintofahamu nyingi hasa juu ya uadilifu wa kamati nzima iliyohusika na mchakato wa kumpata mgombea kama ilizingatia vigezo au nguvu ya rushwa ilitawala kwa wajumbe na kupelekea kupata mgombea ambaye hata uraia wake unatilisha mashaka.

Itakumbukwa mgombea huyo imebidi apitishwe mara mbili mara baada ya kuonekana kulikuwa na kasoro katika fomu yake ya ubunge. Kasoro zilizojatwa inaonekana hazikushughulikiwa ipasavyo na kupelekea Sioi Sumari kupita licha ya kuwa na utata ambao ungeweza kumuengua bila shida.

Nyuma ya hili tunajifunza kitu fulani ambacho ni rushwa kutawala katika uchaguzi ule hali iliyopelekea wajumbe wake kutoona mapungufu na kupiga kura kwa shukrani na si matakwa.

Mtu pekee ambaye amehusishwa na mchezo huo ni mbunge wa Monduli Mh. Lowasa ambaye inadaiwa ni mkwe wake na ndiyo maana anapigana kufa na kupona na kupona kuona Sioi Sumari haukosi ubunge huo. Naomba nitoe angalizo hoja si kuwa mkwe wa Lowasa, hoja ni kuwa Sioi ni chaguo la Lowasa kwa sababu anazozijua yeye na nguvu ya mapenzi yake imejidhihirisha wazi.

Swali la msingi, ikiwa nguvu aliyotumia Lowasa itashinda na Sioi kushinda ubunge je ni dalili za wazi nguvu ya kundi lake kuwa kubwa na kupelekea Lowasa kushinda urais endapo afya yake itamruhusu?

Ikumbukwe ni nguvu ake iliyombeba mpaka hapo alipo licha ya mizengwe toka kundi pinzani.

Nawasilisha kwenu wapembuzi yakinifu kwa majibu.
 
hakuna point hapa wewe inaonekana
weekend huna kazi ukaone ujaribu kubumba bumba thread

Ukisom kwa kukimbia kimbia unaweza usione kitu trya again to think twice, ushindani mkubwa upo kwenye upatikani wa mgombea na huko kwingine kunakuwa na external force kama system inakukubalije n.k
 
Lusambo!

Siyo kawaida yako Mkubwa wangu!

Try again thread!

Huu uzi umetulia sema haujakaa kishabiki umekaa kitafiti zaidi. Hivi LiverpoolFc hujiulizi Sioi kapitaje pitaje?
Dogo ana akashiga kibao lakini kapeta, je kupeta kwake ni kiashirio mkuu akitumia nguvu hii au zaidi ndani ya CCM anaweza akapitishwa kuwa mgombea urais na akachukua nchi?
Hilo ndilo swali langu.
 
Back
Top Bottom