LOWASA KATIKA HARAKA ZA KUNUNUA URAIS 2015 ameanza na Sh billioni 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LOWASA KATIKA HARAKA ZA KUNUNUA URAIS 2015 ameanza na Sh billioni 8

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by lifeofmshaba, Apr 3, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowassa ameelezwa kuwa na mradi wa karibu Sh. 8 bilioni wa "kujisafisha" na kumwingiza ikulu.

  Lowassa alipoulizwa na gazeti hili kuhusu mradi huo, alijibu kwa mkato, "Mimi sijui."

  MwanaHALISI limeelezwa kwamba fedha za "kumsafisha" Lowassa zimeahidiwa na swahiba wake, Rostam Aziz ambaye wamesimama pamoja muda wote wa sakata la kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond iliyothibitika kuwa feki.

  Richmond ilipewa mkataba wa kufua umeme ikiwa haina fedha, wataalam wala uzoefu katika eneo hilo; huku nyaraka zilizopo juu ya kashfa hiyo zikionyesha kuwa mkataba ulipatikana kwa njia ya upendeleo – tuhuma ambazo zinamwangukia Lowassa.

  Taarifa zinasema mabilioni hayo ya shilingi yamelenga kutumika kulegeza wajumbe wa vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa kuelekea, na wakati wa mkutano mkuu ndani ya chama hicho ambao utafanyika mwaka kesho.

  Fedha hizo pia zinadaiwa kulenga kuyumbisha jumuiya za CCM – Umoja wa Wanawake (UWT), Jumuiya ya wazazi na Umoja wa Vijana (UV-CCM).

  Wengine ambao wanadaiwa kulengwa katika hatua ya kushawishi, kulegeza na kushirikisha katika mradi wa kusafisha Lowassa ni wabunge, vyombo vya habari na waandishi wa habari mmojammoja.

  "Mradi wa kumsafisha Lowassa" umeelezwa kuwa chini ya kundi la watu watano. Mbali na Lowassa mwenyewe na Rostam, wengine waliotajwa ni Andrew Chenge, Makongoro Mahanga na Peter Serukamba.

  Chenge ni mbunge wa Bariadi Magharibi; Mahanga ni mbunge wa Segerea na Serukamba ni wa Kigoma Mjini. Taarifa zinasema tayari baadhi ya wajumbe wa kundi hilo wamefanikiwa kushika nafasi za juu za Kamati za Kudumu za Bunge.

  Walioshika nafasi hizo ni Lowassa (Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama) na Serukamba (Miundombinu).

  Gazeti hili limeelezwa kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya UV-CCM, unatokana na "kasi ya mbio za Lowassa kugombea nafasi muhimu" ndani ya chama chake na baadaye urais.

  Kwa wiki mbili sasa, viongozi wa vijana wamekuwa wakisutana, kulaumiana na kutuhumiana kujenga makambi ndani ya umoja huo. Wiki iliyopita walimrukia waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wakimtuhumu kuhujumu chama "kwa kuzungumza nje ya vikao."

  "Sikiliza bwana ee, vurumai hii ya vijana ni ya kutafuta kujenga kundi la kumsafisha Lowassa. Wapo wanaofanya kazi hiyo kwa kujua na wapo wanaofanya hivyo bila kujua," ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM.

  Hatua ya baadhi ya viongozi wa vijana, kurukia kila wanayeona ana uwezekano wa kupinga Lowassa na kundi lake, inaelezwa kutokana na waliokuwa wapinzani wao wakuu kubaki serikalini na wao (akina Lowassa) kuwa nje ya utawala.

  Wanaotajwa kuwa serikalini, lakini wanadaiwa kuwa wapinzani wa Lowassa katika mgawanyiko wa wanaopinga ufisadi na wanaoutetea, ni pamoja na Samwel Sitta, ambaye hivi sasa ni waziri wa Afrika Mashariki.

  Wengine ambao akina Lowassa hawakutegemea kuwemo serikalini, ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Benard Membe; naibu waziri wa ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe na mkuu wa wilaya ya Masasi, Nape Nnauye.

  Lowassa hakuwa na simile pale alipohojiwa kwa njia ya simu kuhusu "mradi wa kujisafisha."

  Swali:
  Mheshimiwa, tumepata taarifa kuwa una mradi wa Sh. 8 bilioni kwa ajili ya "kujisafisha kisiasa." Je, hii ni kweli?
  Lowassa: Muulizeni huyo mpuuzi aliyewaambieni.
  Swali: Gazeti linakuliza wewe kwa kuwa ndiyo mwenye mradi.
  Lowassa: Mimi sijui. Sitaki kusikia mambo ya kijinga…"

  MwanaHALISI liliripoti katika toleo lake la Machi 9 – 15 mwaka huu, chini ya kichwa cha habari kisemacho, " Siri ya Edward Lowassa nje," juhudi za mbunge Beatrice Shelukindo "kumsafisha" Lowassa.

  Katika ujumbe wake wa maandishi kwa mbunge mwenzake, Pindi Chana, Shelukindo alisema ameambiwa na Nabii Joshua wa Nigeria kuwa "rais ajaye ni Edward Lowassa" na kwamba maisha yake ya nyuma yanayomhusisha na kashfa ya ufisadi, "si kitu."

  Joto la Shelukindo katika mawasiliano haya lilitokana na kile alichoeleza kuwa, "Mungu ni wa ajabu. Lowassa ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Mungu ana njia za ajabu za kufanya mambo."

  Shelukindo alikuwa akirejea fadhila za Lowassa kumwombea kura wakati wa kugombea nafasi ya kamishena wa bunge. Alishinda.

  Naye Rostam alitafutwa kwa simu bila kupatikana. Hatimaye alipelekewa swali kwa njia ya sms.

  Swali:
  Kuna taarifa kuwa umeahidi kumwezesha Mhe. Edward Lowassa kwa Sh. 8 bilioni katika kile kinachoitwa "mradi wake wa kujisafisha kisiasa." Je, hii ni kweli? Simu yako haiitiki.

  Tofauti na Lowassa aliyesema hataki kusikia "mambo ya kijinga," Rostam alijibu kwa sms, "Sidhani Lowassa anahitaji mradi wa kumsafisha maana si mchafu," kauli ambayo haikushangaza kwa kuwa ilitoka kwa swahiba mkuu wa wakati wa jua na mvua.

  Rostam aliandika, "Isipokuwa nimetenga pesa kuwasaidia nyie MwanaHALISI mnunue mtambo wa kuchapisha gazeti bila bughdha!"

  Hata hivyo, gazeti hili lina uhakika kuwa Rostam hana mtambo wa kuchapa magazeti yake ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba. Anayachapia kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

  Majibu ya Rostam yameelezwa kuwa ya kumfariji swahiba wake kwa msingi mmoja tu; kwamba wameshiriki – kwa njia mbalimbali – katika kutafuta miradi ya kufua umeme, ambayo imeleta kashfa na kumfikisha Lowassa alipo sasa.

  Mtoa taarifa amesema kundi la watu watano limekuwa likifanya vikao; lakini ni kikao cha Dar es Salaam cha mwishoni mwa mwaka jana, ambacho kiliweka mkakati wa Lowassa kujitokeza hadharani "kila inapobidi," kushiriki mikutano na kutolea matamko hoja kadhaa zinazoibuka ili aonekane karibu na wananchi.

  Maswali yaliyotumwa kwa wajumbe wengine wa kundi hili ambao simu zao ziliita bila kujibiwa au hazikupatikana, hayakujibiwa.

  Wakati hayo yakifanyika, taarifa zinasema baadhi ya wajumbe wa NEC wamejipanga kupeleka hoja katika vikao vya juu kutaka watuhumiwa wote wa ufisadi waenguliwe kwenye nafasi zao za uongozi ndani ya chama.

  "Tunakwenda kwenye NEC tukiwa na dhamira moja ya kumuondoa Rostam, Lowassa na Chenge katika vikao vya maamuzi vya chama chetu. Huo ndio mkakati wetu na lazima tuutekeleze ili kukinusuru chama," ameeleza mmoja wa wajumbe wa NEC.

  Katika minyukano hiyo, vijana ambao wasiokubali kuingia katika mradi wa kumsafisha Lowassa wameanza kusakamwa. Tayari mjumbe wa Baraza Kuu la uongozi la UV-CCM kupitia mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesimamishwa uongozi na baraza la vijana la mkoa huo.

  Pamoja na kutuhumiwa kuhujumu kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Baltida Buriani, Gambo anatuhumiwa kumweleza mmoja wa watu walio karibu na Lowassa kuwa "hafai kabisa", akitumia maneno ambayo, kwa kuzingatia maadili, gazeti hili haliwezi kuyachapisha.

  Kauli ya Gambo ilipofikishwa kwa mtoto wa Lowassa, Frederick, mtoto huyo alimwandikia Gambo sms ifuatayo: "Gambo unayo haki ya kumchagu mtu yeyote unayemtaka na siyo kumutukana mzee wangu. Hiyo siyo siasa, lakini endelea." Ilikuwa 4 Machi 2011, saa 2:14:39 usiku. Gazeti hili limeona mawasiliano hayo.

  Uhusiano wa Gambo na wafuasi wa Lowassa ulizidi kuwa mbaya kutokana na kunukuliwa akielezea wajumbe wa baraza la vijana la taifa mjini Dodoma wiki mbili zilizopita kuwa, sababu kubwa iliyofanya CCM kufanya vibaya katika uchaguzi uliopita, "ni chama kukumbatia watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini."

  "Lowassa na Rostam ndio wanakipotezea mvuto CCM. Tusitafute mchawi. Watanzania wanakerwa sana na Richmond na Dowans na lazima CCM iwashughulikie wahusika wote ili kujenga taswira mpya kwa chama chetu," alieleza.


  Source: MwanaHalisi
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,598
  Trophy Points: 280
  Tukiweza kufikia hatua kama ya kijana mrisho nchi hii itaenda tena kwa kasi...uthubutu kusema ukweli na kwa wakati muafaka!!!tukiuma maneno haitatusaidia
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kweli umenena mkuu
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  God ..
  .. which low this nation has to go .... so that we can realy wake up !?
  .. Do we realy need another bunch of tyrants to confuse us for our wake up ... !
   
 5. B

  Blessing JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :disapointed: WHO ???? LOWASA !!! Surely we Tanzanians are not serious. MFISADI SUGU !!! huyo akiwa Rais nchi kweli itauzwa kama hapa tulipo tumeuzwa ndani ya nchi yetu na MKAPA na then JK sembuse LOWASA aise ni hatari avai.

  Noma dogo aifai
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2015
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,568
  Trophy Points: 280
  Mwanahalisi katika ubora wao ....
   
 7. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2015
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,504
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaaa nasikia baada ya Lowasa kumdunga bilioni kadhaa Mbowe akatoa masharti asishindanishwe na mtu yoyote...maana alijua atakatwa tu
   
 8. d

  droidwallmail JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2015
  Joined: Aug 24, 2015
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Oneni bao la mkono lilivyoandaliwa hapa. huu uzi kila napouweka unafutwa fasta fasta wadau.
  KULINGANA NA TAKWIMU ILIYOTOLEWA NA TUME WATANZANIA 23700000 WAMEJIANDIKISHA NA SIKU YA KUPIGA KURA VITUO 72000 VITATUMIKA KUPIGIA KURA NA KILA KITUO KINATAKIWA KIWE NA WAPIGA KURA 450 JE UKIANGALIA HIYO TAKWIM NA IDADI YA WAPIGA KURA MBONA VITUO ULIVYO VITAJA NI VINGI KULIKO IDADI KAMILI YA HESABU.
  Tuhakiki
  Chukua idadi ya watanzania waliojiandikisha 23700000 gawanya kwa wapiga kura wa kila kituo ambao ni 450 jibu linalopatikana ni 526670 ambayo ndio tungetegemea iwe idadi halisi ya vituo vya kupigia kura.
  Kulingana na hesabu za jaji Lubuva vituo 72000- 52666=19333
  Kwa maana hyo kulingana na hesabu zangu kunavituo feki 19333
  Goli la mkono mwisho bafuni
  Chukua 19333 x 450 = 8700000
  Jaji lubuva kaandaa vituo feki 19333 vitakavyokua na wapiga kura mil. 8700000
  JAJI LUBUVA USITAKE KUTUHARIBIA NCHI YETU CHUNGA SANA
  ICC ITAKUHUSU
  ULIPO TUPO
   
 9. f

  fukunyungu JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2015
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 726
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Lowasa lowasa lowasa lowasa lowasaaa
   
 10. NAMKONG'O

  NAMKONG'O JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2015
  Joined: Mar 29, 2014
  Messages: 335
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii ni ya kuogopwa,
  Magufuri komboa nchi hii Mzuri ila watu wake ndio Shida.
   
 11. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2015
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Mtu aliyezunguka nchi nzima kwa kuhonga miaka yote eti ndo apite na tumwache mwenzetu aliyesimama mwenyewe bila hata kutoa mabilioni! this is satirical! ...never ever.
   
 12. b

  boyayoparuparu JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2015
  Joined: Jul 30, 2015
  Messages: 344
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama lowasa mtu mmoja tu ametoa kiasi hicho cha pesa,na anashindwa kurusha mikutano yake live kwenye tv stations,basi ccm itakuwa imetoa mara mia zaidi ya lowasa.angalia wanavyoingia gharama kubwa
   
Loading...