Lowasa hana sifa ya kuwa Rais nchi hii hata kwa bahati mbaya

moody kabwe

Member
Mar 13, 2015
76
21
Hakuna shaka yoyote kuwa sasa kapteni mstaafu wa JWTZ Edward Ngoyai Lowassa ameanza kupoteza "kumbukumbu" kuhusu mbinu nzuri za kijeshi alizofundishwa alipokuwa anatumikia jeshi la wananchi wa Tanzania kabla hajajitumbukiza kwenye siasa na baadaye kupanda mpaka nafasi ya uwaziri mkuu kabla ya "kuporomoka" kwake mwanzoni mwa mwaka 2008.

Watu mbalimbali wanamtazama Lowassa kwa namna tofauti kuna wale wanaoamini kuwa ni kiongozi shupavu anayejua kusimamia analolisema na kuna baadhi wanaoamini kuwa Lowassa ni mfanyabiashara aliyejitumbukiza kwenye siasa na mwishowe "kuangukia pua". Hoja hapa si juu ya Lowassa hasa ni nani? isipokuwa Lowassa hasa anafanya nini wakati huu?

Kuhusu Lowassa ni nani? hili hata siku moja haliwezi kuwa jambo la mjadala ukizingatia kuwa bado watanzania wana kumbukumbu za hotuba ya Lowassa ya kung'atuka mnamo mwezi February 2008 kufuatia kusombwa na "kimbunga" cha kamati ya bunge chini ya uenyekiti wa Dr Harrison Mwakyembe iliyochunguza kashfa iliyohusisha kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Kuondoka kwa Lowassa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu kumekuwa na athari za wazi kwa chama chake na yeye mwenyewe, nitajadili hili.

Ikumbukwe kuwa kwa kawaida kila unapofika mwisho wa uchaguzi basi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine kwa maana nyingine ulipoisha uchaguzi wa mwaka 1995 uliomwingiza madarakani Benjamin Mkapa ndiyo ulikuwa mwanzo wa hii safari ya misukosuko iliyompeleka madarakani Jakaya Kikwete 2005 huku ikimwingiza kwenye nafasi ya uwaziri mkuu Edward Lowassa kabla ya msonge huo kusambaratika na kumfanya Lowassa afike hapa alipo leo.

Inafaa watanzania waelewe wazi kuwa Lowassa si mwanasiasa wa aina "hiyo" wanayomfikiria, nadhani ukiacha udhaifu wa shule za kata lakini ukiangalia jinsi Lowassa alivyosimamia zoezi hilo hutasita kusema kuwa walau alijitahidi kutimiza majukumu yake vizuri na hata "alipoingia" kwenye kashfa na kuamua kuachia ngazi bado alitimiza wajibu wake wa msingi wa kusimamia kanuni ya uongozi hasa wa kuwajibika unapoona "umechemsha" kama ilivyokuwa kwa upande wake.

Fumba macho kidogo rudisha kumbukumbu zako miaka minne iliyopita mwaka 2008 mjini Dodoma wakati ambapo Lowassa aliitangazia dunia kuwa "tatizo ni uwaziri mkuu" ndiyo maana analazimika kujiuzulu. Tatizo nini? Ati ni uwaziri mkuu kauli yenye utata mkubwa hii! Baadaye Mwakyembe akazidi kuivuruga dunia kwa kudai kuwa kuna mengine "wameyaficha" la sivyo nchi "ingetikiswa" kauli yenye utata sana hii! Baada ya kauli hizi watu wakakaa mkao wa kula kungoja kuona vita itakayofuata ila kwa bahati mbaya si Mwakyembe wala Lowassa aliyekuwa na ubavu wa kumtisha mwenzake. Ila lililo la msingi ni jinsi Lowassa anavyopambana kiasi cha kutoa ishara kuwa ama la hamjui adui yake wa kweli au amesahau mbinu za kijeshi.

Hali ya kulumbana na Mwakyembe au Samwel Sitta ni uthibitisho wa wazi wa kufanana kimchezo au kulingana kiubavu. Mwanajeshi anayepambana pasipo kumjua adui yake ni hatari anapokuwa na bunduki iliyosheni risasi hatari iliyoje kwa mpiganaji wa aina hii anapoamua kumchakaza kamanda wake kwa kudhani ni adui.

Hata kama hajawahi kusema moja kwa moja lakini kauli za Lowassa za mara kwa mara za kusema ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka zinailenga serikali ya CCM inayoongozwa na rais Kikwete. Kurudiwa mara kwa mara kwa kauli za aina hii kunatahadharisha uwepo wa mpambano wa chini kwa chini wa mitandao na makundi hasimu ndani ya chama hiko.

Wako watu wanaojiuliza kama tabia ya CCM kukosoana kwenye vikao au ikiwa ni kweli Lowassa ana hadhi ya kuitwa "waziri mkuu mstaafu" siyo aliyejiuzulu anashindwa nini kuonana na rais Kikwete na kumwambia ajitahidi kupanua wigo wa ajira kwa vijana kuliko kuendelea kurusha maneno kwenye mikusanyiko ya watu? Kuna nini hapa? Au huu ni uthibitisho na wito wa wazi kwa "mathomaso" kuamini kuwa mstari unaotenganisha urafiki na uadui ni mwembamba mno.

Kuna hoja hapa ilitolewa na Edward Lowassa kule bungeni kuwa serikali ifanye "maamuzi magumu" bilashaka yoyote kwa mara nyingine tena Lowassa aliilenga serikali inayoongozwa na Kikwete. Hapa kuna maswali tata lukuki, hivi serikali ya Kikwete haifanyi maamuzi magumu? Kama haifanyi maamuzi magumu basi inafanya kinyume chake ? "legelege" sivyo? Iwapo kauli hiyo ya Lowassa ni kweli au si kweli si jambo la msingi lakini lililo dhahiri ni kuwa huu ulikuwa ni mwendelezo wa "mbinu za kijeshi" za kapteni Lowassa katika siasa za Tanzaniana ndani ya CCM .

Baada ya kauli hiyo kila mmoja anakumbuka kilichofuatia, ilikuwa ni kama nchi nzima imesimama kuanzia ndani ya chama mpaka serikalini, kwenye vyumba vya habari mpaka vijiweni watu walikuwa wako busy kuijibu kauli ya Lowassa hii kwa mara nyingine tena ilidhihirisha sasa ni "piga nikupige" baada ya Lowassa kutumia mbinu za " kijeshi" na wenzake wakamjibu kwa mashambulizi ya "kijeshi". Hii ilikuwa ni "vita" yenye tabia ya kipekee duniani hususani kutokuwa na uwanja maalumu wa mapambano. Baadaye ikasikika kauli ya Nape kuwa ndani ya CCM kuna "watu wameasi" kauli nzito sana hii! Alilengwa nani? haijulikani lakini kila mmoja anaelewa kilichosikika kwenye vyombo vya habari ambacho kilisababisha Lowassa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kule Monduli mkutano ambao uliripotiwa moja kwa moja na baadhi ya vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii. Katika mkutano huo kati ya mengi ila lililosikika sana kutoka kinywani mwa Lowassa ni "napenda kukariri tena kuwa rais Kikwete sikukutana naye bararani na nitakuwa mtu wa mwisho kufikiria kumhujumu"

Ukiipima kwa makini kauli hii ya Lowassa unabaini huu ulikuwa ni mwendelezo wa makonde ya tupa nikutupe ndani ya CCM kiasi cha kutishia uhai wa chama chenyewe. Watu wenye busara watakubali kuwa upendo haupimwi kwa maneno wala maneno si kipimo cha urafiki sasa hiyo kauli ya Lowassa na urafiki wake na Kikwete inatoka wapi? Na ina maanisha nini? Bilashaka kauli hii haikuashiria maji kutulia mtungini kama Lowassa alivyotaka tuamini bali half time yaani mapumziko na baadaye mechi ingeendelea. Kabla watu hawajasahau haya mara hii akaibuka tena kapteni Lowassa kwa mbinu zilezile za kijeshi mara hii ilikuwa huko mto wa mbu alipoamua kusimamia ukweli ambao si chama chake wala Kikwete wanaotaka kuusikia.

Lowassa amesikika akisema kuwa kupwaya kwa viongozi kunakatisha tamaa vijana hivyo kuwafanya watimkie kambi ya upinzani mwishowe akasisitiza ati CCM ikijipanga vema hakuna mbadala wake. Wako watu wanaoamini kuwa kauli hii ni kauli ya mwana CCM wa kawaida lakini ngoja niweke kumbukumbu sawa hapa kuwa huu ni mwendelezo wa "vita moto" na "vita baridi" ndani ya CCM. Lowassa anafahamu vema uongozi wa CCM ulivyo dhaifu hata Kikwete anajua vema kulegalega kwa CCM kulikosababisha kuwapoteza makamanda kama James Ole Millya na wengine lakini pia wote wanafahamu kuwa ni utaratibu wa CCM "kumalizana" kwenye vikao vya chama lakini huu utaratibu mpya alioanzisha Lowassa wa "kukosoana" majukwaani ni mzuri sana ila ni mpya ndani ya CCM..

Kama inavyoeleweka miongoni mwa mabondia kuwa ngumi inajibiwa kwa ngumi na hata wacheza karate wanafahamu vema kuwa teke ni kwa teke ndivyo ilivyokuwa pale Willison Mukama alipoamua kutumia vyombo vya habari kumjibu Lowassa alichomjibu kinasikitisha na kufurahisha lakini kinasisimua na kupambanua waziwazi uwepo wa "vita" inayoonekana siyo tu kuziumiza "nyasi" bali imekuwa kali kiasi cha kutishia uhai wa nyasi zenyewe. Siku chache zilizopita ameibuka Edward Lowassa huko Monduli na kudai kuwa "rais Kikwete ni kiongozi shupavu mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa kijasiri".

Niliposikia kauli hii kutoka kinywani mwa Lowassa nilivuta nywele zangu na kutishia kuzing'oa nikasema ningelikuwa mkufunzi wake wa "jeshi" basi ningeshamvua nishani zote nilizomtunuku. Wanajeshi wanafundishwa kupigana vita kwa ushupavu na akili kubwa wanafundishwa kusonga mbele daima . Inatia shaka sana kwa mwanajeshi wa kiwango cha "kapteni Lowassa" kujichanganya kiasi cha kuwaita maadui zake marafiki na kinyume chake. Hii inathibitisha kuwa Lowassa sasa ameanza kusahau mbinu za kijeshi . Kapteni Lowassa anaonekana kuzoea maisha ya "uraiani" kiasi cha kujisahau yeye ni mwanajeshi anayepaswa kupambana mpaka tone la mwisho ili kuwachakaza maadui. Ni dhahiri sasa Lowassa ameanza "kutupwa" na wakati na pengine zama zake zipo ukingoni.

Ushauri wa bure kwa Lowassa ni vema akaacha kuwapotezea muda "wafuasi" wake au kuendelea kuwasumbua "wapambanaji" wake kwa "vita" ambayo yeye kamanda mkuu anaonekana kusahau mbinu za kijeshi atangaze kushindwa mara moja na kuinua mikono juu au "apakie risasi" kwenye "bunduki" yake na kurejea kwenye uwanja wa mapambano sasa!
 
Ipo Kazi mwaka huu, tatajua mengi .tupeni ukweli wote bayana ili tufanye maamuzi hasi .
 
Bado sijaona MTU Wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa mtanzania. Nje ya hapo ni upambe,kambi etc
 
Back
Top Bottom