Lowasa Alikuwa Akitoa Tenda za Ujenzi kwa Kampuni za Kuuza Maziwa ya Nido...Hafaiiiiii!!!!

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
Sikushangaa kusikia tarifa kuwa wabunge wa CCM walimshangilia Edward Lowassa wakati akichangia hoja bungeni. Sikushangaa ndiyo kwa sababu Lowassa, Kikwete, Rostam na wenzao ni watu wa Rushwa. Pia sikushangazwa na mlolongo wa Posts zilizokuwa zinarushwa JF za kumpigia kampeni huyu mwizi(Lowassa). Lowasa ni mtu wa rushwa. Alishanunua wabunge wa kumshangilia, alishanunua members wa JF, alishajiandaa kushangiliwa ili kukonga nyoyo zetu.

But one thing you don't know about this thief is wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alikuwa akiruhusu kampuni za kusambaza maziwa ya Nido kwenye taasisi za serikali kupewa tenda za ujenzi wa barabara na ujenzi wa majengo. Kama nchi, kama tutarogwa, kwa namna yoyote ile kumpitisha Lowassa kuwa mgombea wa chama chochote cha siasa, Urais wa JMT, tutajuta. Wakati wa Lowassa baadhi ya wafanyabiashara waliiweka nchi mifukoni mwao. Kuna wakati niliwahi kumnukuu mfanyabiashara mmoja, ambaye kampuni yake hufanya kazi ya kuuza maziwa ya Nido na sukari na majani ya chai, lakini ina tenda za kutengeneza Barabara akimuagiza mmoja wa wabunge aliyekuwa mjengoni azungumze jambo fulani lenye interest na yeye.

Kama leo hii, mtu huyu Lowasa, ambaye mimi ninamuita mwizi, atatimiza ndoto zake za kuwa kiongozi wa nchi hii, basi pengo la masikini na tajiri litapanuka zaidi na litafikia deformation point. Kwa waliosoma Hooke's Law wanajua ninachomaanisha kuhusu deformation point.

Lowassa ni mtandao mmoja na kikwete. Watu hawa wameunda genge la watawala walafi wenye uchu wa madaraka wasio na huruma, ambao kwao, uongozi ni kujitajirisha kupitia madini yetu, Maziwa yetu, Bahari zetu, misitu yetu, Mbuga zetu na kila aina ya utajiri ulio katika nhi hii.

Kama Watanzania. Lazima kuwa makini. Genge la watu hawa ni kubwa. Wana fedha. Wanaweza kumnunua yeyote.

Lazima tuungane. Bunge, na hasa wabunge wa CCM ni watu wasaliti. Wanajifanya wawakilishi wa wananchi, lakini ukweli ni kuwa ni wawakilishi wa matumbo yao na mabwana zao ambao ni mafisadi.

Watanzania na hasa huko vijijini Amkeni!!!
 
Mkuu we all know that these guys are corrupt, however, would you add weight in your posts by mentioning which company were given a tender, to construct which roads or buildings? please...
 
Ninachoshangaa mimi ni kitu kimoja!
Waliokuwa wanamshangilia Lowassa Bungeni ni wabunge wa ccm!
Lakini pia wao ccm ndio wamewapa siku 90 akina Lowasa na wenzie wang'oke toka kwenye Halmashauri kuu, aka kujivua magamba.
Sasa nashindwa kuwaelewa wana uchaguzi gani katika sakata la huyu jamaa!
Mbona wanaonyesha kumweka pabaya NAPE?
 
Mkuu PJ, hii inaonyesha ni jinsi gani chama hicho kilivyogawanyika
 
Sikushangaa kusikia tarifa kuwa wabunge wa CCM walimshangilia Edward Lowassa wakati akichangia hoja bungeni. Sikushangaa ndiyo kwa sababu Lowassa, Kikwete, Rostam na wenzao ni watu wa Rushwa. Pia sikushangazwa na mlolongo wa Posts zilizokuwa zinarushwa JF za kumpigia kampeni huyu mwizi(Lowassa). Lowasa ni mtu wa rushwa. Alishanunua wabunge wa kumshangilia, alishanunua members wa JF, alishajiandaa kushangiliwa ili kukonga nyoyo zetu.But one thing you don't know about this thief is wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alikuwa akiruhusu kampuni za kusambaza maziwa ya Nido kwenye taasisi za serikali kupewa tenda za ujenzi wa barabara na ujenzi wa majengo. Kama nchi, kama tutarogwa, kwa namna yoyote ile kumpitisha Lowassa kuwa mgombea wa chama chochote cha siasa, Urais wa JMT, tutajuta. Wakati wa Lowassa baadhi ya wafanyabiashara waliiweka nchi mifukoni mwao. Kuna wakati niliwahi kumnukuu mfanyabiashara mmoja, ambaye kampuni yake hufanya kazi ya kuuza maziwa ya Nido na sukari na majani ya chai, lakini ina tenda za kutengeneza Barabara akimuagiza mmoja wa wabunge aliyekuwa mjengoni azungumze jambo fulani lenye interest na yeye. Kama leo hii, mtu huyu Lowasa, ambaye mimi ninamuita mwizi, atatimiza ndoto zake za kuwa kiongozi wa nchi hii, basi pengo la masikini na tajiri litapanuka zaidi na litafikia deformation point. Kwa waliosoma Hooke's Law wanajua ninachomaanisha kuhusu deformation point.Lowassa ni mtandao mmoja na kikwete. Watu hawa wameunda genge la watawala walafi wenye uchu wa madaraka wasio na huruma, ambao kwao, uongozi ni kujitajirisha kupitia madini yetu, Maziwa yetu, Bahari zetu, misitu yetu, Mbuga zetu na kila aina ya utajiri ulio katika nhi hii. Kama Watanzania. Lazima kuwa makini. Genge la watu hawa ni kubwa. Wana fedha. Wanaweza kumnunua yeyote. Lazima tuungane. Bunge, na hasa wabunge wa CCM ni watu wasaliti. Wanajifanya wawakilishi wa wananchi, lakini ukweli ni kuwa ni wawakilishi wa matumbo yao na mabwana zao ambao ni mafisadi.Watanzania na hasa huko vijijini Amkeni!!!
Duh, Umefika mbali sana! Kama hakuna chuki hapo kweli huyu Bwana hafai. Anatoa tenda? Nilidhani kama ni kweli basi ungesema alipata kuingilia mchakato wa utoaji Tenda, PM na utoaji Tenda wapi na wapi Mkuu?Hata hivyo, taja walau nusu jengo na robo ya bara bara ambayo ilijengwa na kampuni ya usambazaji maziwa ya Nido.
 
Instead of discussing substance, you discuss people....that's very lame for an educated person...Alichosema Mh Lowasa ni ukweli mtupu, atleast give him his due credits for that, nyu ngonjera ya ufisadi imepitwa na muda, mahakama c zipo, kama kuna ushahidi wa kutosha basi DPP na PCCB wampeleke court ili ukweli ujulikane..na sio kuchafuana tu...
 
Sikubaliki hatuwezi kukukubali kamwe Kama jina lako linavyosema. Mimi Siko upande wowote wala wa Lowasa wala wadau wengine wenye nia ya kugombea 2015 hicho kiti cha uraisi. Ila madai yako hata mtoto wa shule ya vidudu (kindergaten) anajua tu kuwa wewe ni mwongo. Hamna namna sheria ya manunuzi ya umma namba 21 ya 2004 haimpi Waziri Mkuu nafasi yeyote kutoa award ya zabuni.
 
Mkuu go back to my post.Nilichoonesha hapo ni mshangao wangu kuhusu madai ya mwanzisha thread- ndiyo maana kuna question marks kibao, huenda hukuelewa style yangu ya presentation, nilichotaka kusema kwa kifupi ni hicho ulichosema wewe kwamba sheria haimpi room mtu asiye member wa procurement committee kutoa Tenda, ila mwanzisha thread alipashwa (kama aliona ni lazima kuweka hiyo thread yake) kutushawishi kwamba PM aliingilia mchakato wa utoaji zabuni, hili nimelishuhudia katika maeneo ambako nilikuwa member wa hizo committees na lilikuwa linafanyika wakati wa evaluation, ambapo anaependelewa kupewa Tenda hupewa weak competitors, ingawa mara zote tuliamuru kutolewa kwa tangazo upya.
 
Kama Chuki binafsi vile.

i think we need to dig deep about ones past to know how reliable he/she is.... kilichosemwa hapa ni kibaya lakini kwa mfumo tulionao inawezekana kabisa

trust me
 
hamna facts hapo siwezi kukubaliana na porojo...rudia kuandika mnyonge mnyongeni laki ni haki yake mpeni.....ccm haiwezekani kusafishika hata kama mapacha watatu wataondolewa kwani uchafu ushachukua na kupenya sana ndani ya ccm.
 
Duh, Umefika mbali sana! Kama hakuna chuki hapo kweli huyu Bwana hafai. Anatoa tenda? Nilidhani kama ni kweli basi ungesema alipata kuingilia mchakato wa utoaji Tenda, PM na utoaji Tenda wapi na wapi Mkuu?Hata hivyo, taja walau nusu jengo na robo ya bara bara ambayo ilijengwa na kampuni ya usambazaji maziwa ya Nido.
mkuu haya mambo ya ppra, na waheshimiwa kuingilia mchakato kwa tanzania yapo sana tu!
 
kama iliwezekana internet cafe kupewa tenda ya kuleta umeme wa dharula lipi la kushindikana?
 
mkuu haya mambo ya ppra, na waheshimiwa kuingilia mchakato kwa tanzania yapo sana tu!
Najua, na nimefafanua katika moja ya posts zangu hapo juu. Tatizo ni uelekeo wa mwanzisha thread kuwa Mheshimiwa alikuwa anatoa Tenda, nadhani alikuwa na maana hii ya kuingilia mchakato. Tuko pamoja Mkuu.
 
Inafurahisha sana kuona watu tunavyoelewa mambo kwa sasa yaani hatudanganyiki na hata tukidanyika huwa tunapotezea japo ukweli tunao. il come next time members!
 
Kwani tenda ya Richmond ilikuwaje?mbona mnasahau haraka?kuhusika kwa EL kulithibitishwa na kamati ya bunge ktk kutoa maelekezo ili wale wezi washinde,PPRA walikuwaepo na Tanesco walikuwepo
Kila kitu kinawezekana bongo
 
Jamani si huyu EL ambaye aliachiwa laana na Baba wa Taifa kwamba ni mchafu hafai uongozi? Leo tena eti anajidai na kulaumu kwamba maamuzi mazito hayafanyiki. Haya yangefanyika asingeishia kujiuzulu. Ilipashwa afikishwe mahakamni kujibu mashitaka ya abuse of office kama ilivyofanyika Uganda kwa aliyekuwa Makamu wa Raisi. Ingekuwa Uganda inajifunza kutoka kwetu, kama alivyofanya kiongozi wao, M7, tangu ujana wake.
 
Mkuu go back to my post.Nilichoonesha hapo ni mshangao wangu kuhusu madai ya mwanzisha thread- ndiyo maana kuna question marks kibao, huenda hukuelewa style yangu ya presentation, nilichotaka kusema kwa kifupi ni hicho ulichosema wewe kwamba sheria haimpi room mtu asiye member wa procurement committee kutoa Tenda, ila mwanzisha thread alipashwa (kama aliona ni lazima kuweka hiyo thread yake) kutushawishi kwamba PM aliingilia mchakato wa utoaji zabuni, hili nimelishuhudia katika maeneo ambako nilikuwa member wa hizo committees na lilikuwa linafanyika wakati wa evaluation, ambapo anaependelewa kupewa Tenda hupewa weak competitors, ingawa mara zote tuliamuru kutolewa kwa tangazo upya.

Muu uniwie radhi, nilikuwa namlenga Prophet anayeonyesha chuki za wazi kwa kuleta taarifa za majungu ambazo wala hakuzipika vizuri, ila mimi na wewe tunaongea kitu kimoja. Anyway nafikiri vilevile hakuna sheria inayoweka mipaka kwenye biashara as long long as mfanya biashara anasajili kisheria, ana capacity ya kufanya kazi fulani na ana mtaji. Inaonyesha Prophet si mtu makini ajaribu kwenda pale BRELA akachukue Memorandum and Articles of Association za kampuni yeyote aone jinsi wafanyabiashara wanvyoruhusiwa kufanya shughuli mbalimbali kadri ya sheria ya makampuni rura 212.

Aunimpe mfano wa Kampuni ya TATA ya India ambayo inaoknekana Tanzania ikijihusisha na biashara ya magari. Huko kwao wapo hadi kwenye viwanda vya madawa, stationery na ujenzi. Kwa hiyo si ajabu Muuza maziwa ya NIDO kutengeneza biashara kama tu ana vigezo
 
Back
Top Bottom