Lowasa akienda Makanisani CCM hawalalamiki lakini CDM wakiungwa na Makanisa , Kuna Udini??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowasa akienda Makanisani CCM hawalalamiki lakini CDM wakiungwa na Makanisa , Kuna Udini???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Nov 27, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ni jambo la Unafiki sana pale ambapo Udini unapo wanufaisha CCM halalamiki!!
  Ukweli ni kwamba Lowassa ameacha kabisa kazi ya Maendeleo kwa Taifa na sasa anatafuta urais Makanisani Jambo ambalo linapaswa kukemewa na Serikali ya Kikwete!!!
  Mwaka 2010 Maaskofu wengi waliunga mkono Chadema kwa sababu ya Sera lakini Rais Kikwete akasema kuna udini , sasa Hivi Lowassa ambaye ni CCM anachanja Mbuga makanisani na kufanya kampeni za Urais 2015 Hakuna mtu ndani ya CCM anayekemea UDINI huo!!!


  Kumbe Udini unaponufaisha CCm hakuna tatizo!!

  Nawashauri na CHADEMA muanze kualikwa Makanisani na matamko ya Maaskofu yaanze tena tuona nani zaid!!!

  CUF nao nendeni Misikitini siku za ijumaa!!!
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Afanye kazi za maendeleo ya Taifa kwa cheo au mamlaka ipi? Halafu JK, Pinda & Co. watafanya nini.

  ...Harambee anazoshiriki katika hayo makanisa si kazi za maendeleo?

  ...Udini ni agenda muflisi za watu fulani. Mtu yeyote mwenye akili hawezi kupoteza muda wake kwenye upuuzi huo.
   
 3. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,234
  Likes Received: 10,395
  Trophy Points: 280
  hivi lowassa si mbunge wa monduli.halafu nasikia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ulinzi na usalama.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kha kha hii ni hatari sana yafaa wakristu wenyewe mlikomalie hili msije mkatumika kwa manufaa yao binafsi na mnaona wanakotupeleka
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umeanza vizuri ulivyo malizia cjakuelewa kabisa kama unamsapoti kwa kampeni zake za makanisani au la
   
 6. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kwani ni lini Lowassa ametangaza uadui na Kikwete ??
  Kama bado ni Marafiki ni kwa nini Mkoa wa Arusha ndio unaongoza kwa Vurugu wakati yeye lowasa ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama??

  Kwa nini Lowasa aseme CHADEMA hawamtukani ilia CCM???
  Mbona JK anahoma kali sana na CHADEMA?? Ina maana LOWASSA na Kikwete wapo vyama tofauti??
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  All in all Lowasa wewe si ni fisadi ambae mpaka chama chako kinakugwaya iweje makanisa wakukumbalie tena? Yafaa makanisa na nyie mwangalie vitu vingine sio mnatuhubiria mafisadi mafisadi wanaimaliza nchi yetu afu huku mnawakumbatia kwenye michango ili mpate michango mikubwa
   
 8. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  lowassa ni mwizi haka kama anakwenda makanisani lakini ukweli ni kwamba toba ya lowassa ni lazima iwe wazi???

  Alipaswa kuwaomba radhi watanzania kwa kuwalea richmond/ dowans na kutuletea umasikini!!!

  Yeye kasha sema kuwa ana urafiki mkubwa na kikwete hivyo hafai kuwa rais kwasababu yupo katika mtandao wa wezi??
  Tunapinga hata hatua ya serikali kuwahamisha viongozi wezi badala ya ku
  wapeleka jela!!!

  Wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, wakiiba wanahamishwa !!!

  Leo lowassa na kikwete wanakashifa ya richmondi badala ya kuwaweka pembeni watu wanaangalia utajiri wa lowassa na kumutaka agombee urais haya ni matusi kwa watanzania!!!
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nadhani ccm wameshaharibu huko makanisani kwani Pengo keshatoa tamko kuwa cdm na wanaharakati wanachafua amani ya nchi
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Thread yako ina ujumbe wa maana sana kwa ccm, lowassa, na makanisa bravo mkuu..wajitazame
   
Loading...