Lowasa aishtukia Serikali ya CCM ,asema mgogoro Arusha ni mpango wa kukatisha tamaa wapinzani.

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,935
5,558
Wana JF.
Kwenye gazeti la mwananchi liripoti taarifa kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakatisha tamaa wapinzani kutekeleza wajukumu yao kwa wananchi.
Waziri Mkuu Mstaafu, ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa ameishtukia Serikali ya CCM ,asema Mgogoro wa Arusha ni mpango wa kuwakatisha tamaa wapinzani kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.
My take :
Kwanza nampongeza sana Lowasa kwa kuweza wazi kuhusu mpango huo serikali kutumia mgogoro wa Arusha kati ya madiwani na Mkuu wa Mkoa kumbe ni mkakati wa kuwakatisha tamaa madiwani kutimiza wajibu wao. Ndo maana mpaka sasa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi Simbachane ameshindwa hata kutoa tamko kuhusu mgogoro huo kumbe ni mkakati.
Madiwani wa Arusha fanyeni kazi kwa kufuata sheria na kanuni zinazowaongoza nadhani sasa nimeshatambua lengo la serikali kwenye migogoro inayoendelea na mnatakiwa kujiuliza ni kwa nini ni Arusha tu migogoro kila siku kati ya Mkuu wa Mkoa na Mkuregenzi kuhusu madiwani ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom