Low wbc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Low wbc

Discussion in 'JF Doctor' started by sikama, Aug 20, 2010.

 1. s

  sikama Member

  #1
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HISTORIA

  MDOMO WANGU KWA ASILI NI MWEKUNDU.

  MWAKA 1998 NILIANZA KUWA NA VIDONDA KWENYE ULIMI AMBAVYO KUNA WAKATI VINAKUWA VINGI SANA NA KUNA WAKATI VINAKUWA KIDOGO AU KUPOTEA (MPAKA SASA NAVYOANDIKA) ILA KWA SASA KUNA TOKEA KAMA VIDONDA NA VITU VYEUPE(UTANDO) KWENYE MAKUTNO YA MENO YA CHI NA YA JUU.

  VIDONDA HIVI WAKATI MWINGINE HUSABABISHA KUTOKA DAMU WAKATI NAPIGA MSWAKI (MPAKA SASA NAVYOANDIKA)

  MNAMO MWAKA 2004 NILIANZA KUWA NA MBA KICHWANI NA BAADA YA MIAKA MIWILI KUKANZA KUTOKEA VIJIUPELE KICHWANI AMBAVYO UKIVITUMBUA VINATOA DAMU NYINGI SANA. MARA NYINGI HIVI VIPELE NI KAMA HAVIIVI NA KUTOA USAHA(SIJUI LABDA HUWA NAWAHI KUVITUMBUA).

  VIPELE HAVIWASHI SANA ILA VINAKERA KWELI KWELI. NILIANZA KUTUMIA DAWA ZA KUPAKA (MAJINA SIYAKUMBUKI) LAKINI NAONA HAIKUSAIDIA.

  NILIAMUA KUACHA KUNYOA KAMA MIEZI MITATU, VIPELE HIVI VIKAZIDI SANA, NA VIKAWA VINAWASHA SANA. NILIVYONYOA NYWELE, KICHWA KILIKUWA KIMEHARIBIKA KABISA. KILIKUWA NA UNGA UNGA WA MBA ULIOCHANGANYIKA NA DAMU DAMU. HALI HAIKUWA SHWALI KWA KWELI.

  NILIMWONA DAKTARI AMBAYE ALICHUKUA SAMPLE KUTOKA KICHWANI (ULE UNGA UNGA NA DAMU DAMU) NA KUPELEKA MAABARA KUONA KAMA NI BAKTERIA GANI WANANISHAMBULIA. BAADA YA WIKI MBILI, MAJIBU YALIKUJA NA KUSEMA HAKUNA BAKTERIA (MMHH).

  DAKTARI HUYU ALINIPA DAYA YA KUPAKA SCALP LOTION PAMOJA NA SHAMPOO (NIMEISAHAU JINA(INA RANGI YA PINK)) LAKINI SIKUPATA NAFUU.

  DAKTARI HUYU AKANI REEFER KWA BINGWA WA NGOZI AMBAYE ALINIANDIKIA NITUMIE ANTIBIOTICS
  1.DALACIN (T) TOPICAL LOTION NA
  2.ANTIBIOTICS VIDONGE VYA KUMEZA(NIMESAHAU JINA(KIMOJA KUTWA))
  ILA AKASEMA KABLA SIJATUMIA HIVI VODONGE INABIDI INI, LIVER PROFILE IANGALIWE.

  MAJIBU YA INI YALIPORUDI YAKASEMA NI ABNOMAL KWANI INAONEKANA KUNA INFLAMMATION KWENYE INI (AKASEMA ILA SI SANA)

  AKASEMA INABIDI WAPIME WAJUE KWA NINI.
  WAKACHUKUA SAMPLE KAMA NNE ZA DAMU ZA KUPIMA, IKIWEMO KUONA KAMA KUNA hepatitis .ALITAKA KUPIMA NA HIV NIKAGOMA (LOL).

  KASEMA NIFANYE NA ULTRASOUND SCAN (US LIVER) KUONA NIMEATHIRIKA KIASI GANI KWENYE INI

  MAJIBU YALIVYOKUJA IKANOKENA KILA KITU KIKO SAFI ISIPOKUWA KUNA ANTIBODIES FLAN ZIKO CHINI.

  WAKATI HUO NILIKUWA NIMESHANZA KUTUMIA DALACIN (T) TOPICAL LOTION NA HALI ILIKUWA NZURI SANA KAMA WIKI MBILI HIVI ILA BAHATI MBAYA NILIKATIZA DOZI KUTOKANA NA UTARATIBU WA UTOAJI DAWA HAPA KWANI NILIVYOENDA KUNUNUA TENA NIENDELEE, WALINIAMBIA MPAKA CHETI CH DAKTARI TENA NA MIMI NILIKUWA BIZ NA HATA HUYO DAKTARI INGECHUKUA KAMA WIKI MBILI NYINGINE KUMUONA.

  KWA HIYO WAKATI MAJIBU YANATOKA VILE VIUPELE KICHWANI VILIANZA KURUDI.

  NILIVYO ENDA KUCHUKUA MAJIBU KWA DR AKANIAMBIA INASHANGZA KUNONA KUWA MAJIBU YA US LIVER YAKO SAFI LAKINI KUNA ANTIBODIES FLAN ZIKO LOW.

  AKASEMA INAWEZEKANA NI MAUMBILE YANGU TU NDIVYO YALIVYO KWA ANTIBODIES KUWA LOW, LAKINI BAADAYE AKASEMA AU NI ANEMIA???????

  KWA HIYO IKABIDI IFANYIKE Full Blood Count Test NA VIPIMO VINGINE KAMA VIWILI NA HEMOGLOBIN PIA. KWA SABABU NILIMWAMBIA PIA KUWA DALACIN (T) TOPICAL LOTION ILIONEKANA KUNISAIDIA AKANIANDIKIA NIENDELEE NAYO, NA KWA KWELI KWA SASA KICHWANI KUNA MAENDELEO MAKUBWA SANA NA NINAENDELEA KUITUMIA.

  LEO MAJIBU YA VIPIMO NAYO YAMETOKA NA INAONEKANA KILA KITU KIPO SAFI ILA WBC IKO LOW
  (1.4) NA AKANIMBIA KAWAIDA NI 1.6 NA AKASEMA BAADA YA WIKI MBILI ITABIDI NIKAPIME TENA.

  SASA NDUGU ZANGUNI, NIMEKUWA MTU WA HUZUNI KUBWA NA NIKIKUMBUA ULE MPANGO WA DR KUPIMA HIV, NINAKATA TAMAA KABISA NA KAMA NAELEKEA ELEKEA (MMMMHH)

  MABINGWA, WAJUZI NA MA(DR) NAOMBENI USHAURI, HIVI INAWEZEKANA NDIO HIVO TENA.

  NDIMI SIKAMA
   
 2. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,149
  Likes Received: 23,828
  Trophy Points: 280
  Bwana Sikama pole ndugu yangu. Hiyo WBC kuwa low hasa kwa watu wenye asili ya Africa saa ingine huwa inakuwa ni normal, ila kwa hiyo ya kwako naona ipo chini sana. WBC inatakiwa iwe kwenye standard range ya 4.0-11.0 na je, na hizi component hapa chini wamekwambia zipo kwenye standard range gani?.
  1. Neutrophilis %
  2. Lymphocytes %
  3. Monocytes %
  4. Basophilis %
  5. Eosinophilis %
   
 3. s

  sikama Member

  #3
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  YEGOSHIKA, nashukuru sana kwa majibu yako mazuri, hizo components nyingine kwa kweli sijauliza,
  Actually hii ndio mara yangu ya kwanza kupima kwa sababu hawa jamaa, kila kitu lazima upime, huwezi pewa dawa, mpaka upime.

  KUSEMA kweli hata mimi nimeshangaa lakini inaonekana hizi measurement za hapa UK ni tofauti na hizo nafikiri zinhitaji kufanyiwa conversion katika hivo vipimo ulivyo toa.

  kwa sababu dr nilipomuuliza normal ni kiasi gani akaniambia 1.6 kwa hiyo nikaona kuwa labda 1.4 sio mbaya, lakin naona hata ni kigoogle, hivo vipimo vyako ndivyo vimetawala.

  kuna forum moja tu ndio nimeona mama mmoja na yeye anasema alikutwa na 1.4 na akaambiwa 1.6 ndio normal

  Mzee, wewe unaonekana mtaalamu labda jaribu kukumbuka kama ni measurement tofauti au ndio kweli imedrop kutoka 4 mpaka 1.4 lakini kwa nini aniambie 1.6 ni normal?

  NATANGULIZA shukran.
   
Loading...