Love story: Tears of the soul (machozi ya rohoni)

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
111.png

TEARS OF THE SOUL (MACHOZI YA ROHONI)- 1

Mtunzi: Aziz Hashim (Hash Power)

NB: UNAWEZA KUIPATA SIMULIZI HII TAMU KUANZIA MWANZO
MPAKA MWISHO KWA MFUMO WA e-Book (PDF)
UTAKAYOISOMA KWENYE SIMU YAKO KWA SH. 5000/= TU
NICHEKI WHATSAPP 0719401968!

“Mke wangu!”

“Abee mume wangu!”

“Jiandae leo nikitoka kazini nataka tutoke ‘out’!”

“Mh! Hata sijisikii kutoka leo mume wangu.”

“Kwa nini tena jamani?”

“Basi tu! Sijisikii kutoka!”

“Kwani yale ya jana bado hayajaisha mke wangu?”

“Aah! Yameisha lakini sijisikii tu kutoka.”

“Umepika nini leo.”

“Sijapika.”

“Sasa tutakula nini?”

“Nunua chipsi!”

“Vipi ule mzigo ulienda kuufuatilia?”

“Hapana! Sijaenda.”

“Kwa nini sasa hujaenda jamani?”

“Nimechoka! Sijisikii kufanya chochote leo!”

“Sasa, kwa nini hutaki tutoke mke wangu? Huoni itasaidia...” mlio wa simu upande wa pili ulisikika kuonesha kwamba simu ilikuwa imekatwa. Ilibidi nipige tena, simu ikaita kidogo kisha ikapokelewa.

“Kwa nini unanikatia simu wakati sijamaliza kuzungumza na wewe?”

“Sijakata!”

“Kumbe ni nini sasa?”

“Labda network!”

“Mh! Haya sawa! Basi baadaye...”

Nilikata simu na kubaki nimeishikilia, nikiitazama mithili ya mtu aliyekuwa anatazama kitu asichokijua. Ilikuwa ni simu ninayoitumia siku zote lakini hata sijui nini kilitokea, nikawa naitazama tu, hisia chungu zikipita ndani ya moyo wangu.

Why are doing this to me Joanna!” (Kwa nini unanifanyia haya Joanna!) nilijiuliza huku nikiwa bado naitazama ile simu.

Mabadiliko makubwa aliyokuwa nayo mke wangu kipenzi, Joanna yalisababisha niwe na huzuni kubwa ndani ya moyo wangu! Alikuwa amebadilika, hakuwa Joanna yule ambaye nilifunga naye ndoa takatifu miaka miwili iliyopita! Hakuwa Joanna yule ninayemjua, alibadilika mno na mabadiliko hayo ndiyo yaliyonifanya niwe na huzuni kubwa kiasi hicho ndani ya moyo wangu.

“Alex!” sauti ya mfanyakazi mwenzangu ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye lindi la mawazo, nikakurupuka kutoka kwenye ile hali niliyokuwa nayo na kuanza kujifanya nipo bize kwenye kompyuta yangu.

“Machozi yanakutoka, una tatizo gani?”

“Aah! Nina matatizo ya macho Joel, nikiangalia kompyuta muda mrefu machozi yanatoka tu yenyewe,” nilimdanganya, uongo ambao aliukubali.

“Jitahidi kula karoti, zinasaidia sana na kama hali itaendelea hivi inabidi ufanye mipango ya kupata miwani.

“Sure! Hali inazidi kuwa mbaya,” nilimjibu huku nikijifuta.

“Jioni nina mtoko na shemeji yako, nilitaka kampani yako! Kama vipi mpigie shemeji tuungane, mimi na ‘wife’ na wewe na shemeji!

“Dah! Kuna wageni nyumbani, shemeji yako hawezi kutoka ila nitakupa kampani usijali!”
“Basi poa,” alisema Joel, tukagongesheana mikono ‘kishkaji’ kisha akatoka huku akiniambia kwamba nijiandae mambo yakiwa tayari atanishtua. Alipotoka nilishusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye kiti chake. Uragiki wangu na Joel ulikuwa umevika mipaka ya urafiki wa kawaida, alikuwa ni kama ndugu kwangu, nilimfahamu mkewe, alimfahamu mkewe na familia zetu zilikuwa na kawaida ya kujumuika pamoja mara kwa mara.

Mwenzangu yeye alitangulia kuingia kwenye ndoa kabla yangu na hata wakati naanza michakato ya kutaka kuingia kwenye ndoa, alikuwa ndiyo mshauri wangu mkubwa.

Nakumbuka mara kadhaa nilipomueleza kuhusu mipangoyangu ya kuingia kwenye ndoa na Joanna, alinishauri kwamba kama ni kweli nataka mwanamke wa kuishi naye, ni bora nifanye kama yeye, nikaoe mwanamke wa kijijini na kuja naye mjini lakini nilimkatalia! Nilikuwa nampenda sana Joanna na kwake nilikuwa kama kipofu! Sikuona wala sikusikia.

Hali hiyo ilisababisha sasa hata matatizo yaliyokuwa yakiendelea kunisibu kila siku ndani ya ndoa yangu, yabaki kuwa siri yangu. Nitamwambia nini wakati kuanzia mwanzo alishanishauri kwamba nikaoe kijijini lakini nikamkatalia mpaka ikafika kipindi tukataka kugombana?

Sijui ni sababu zipi zilizomfanya Joel ayapinge sana mahusiano yangu na Joanna siku za mwanzo kwani nakumbuka si mara moja au mara mbili alipokuwa akinipinga! Alishasema sana, alishanionya sana kuhusu uamuzi wangu wa kuanzisha mahusiano ‘serious’ na Joanna lakini kama unavyojua tena moyo unapopenda, unakuwa kama kipofu.

“Yataisha tu! Hili nalo litapita, nitakuwa sawa na Joanna, tutaendelea na maisha yetu kama kawaida,” nilijipa moyo. Kwa jinsi kichwa changu kilivyokuwa kimevurugika, sikuweza tena kuendelea kufanya kazi, niliinuka na kuzima kompyuta yangu, nikafungafunga mafaili niliyokuwa nayafanyia kazi na kutoka mpaka kwenye ‘kantini’ iliyokuwa nje, jirani na kazini kwetu.

Nikiwa pale kantini, angalau kidogo nilichangamka kutokana na mazoea ya kucheka na kila mtu niliyokuwa nayo! Mara huyu kanitania hili, yule kanitania lile, ilimradi burudani. Niliagiza juisi na kujumuika na watu kadhaa waliokuwa wakitazama runinga pale nje, stori za hapa na pale zikaendelea na kiukweli, nilisahau kwa muda kero zilizokuwa zinanikabili.

Mara simu yangu ilianza kuita, nilipotazama namba ya mpigaji, alikuwa ni Joel.

“Uko wapi Alex!”

“Nipo kantini hapa nje.”

“Nimekuja ofisini kukushtua kwamba muda wa kuondoka umefika naona patupu! Nakuja basi jiandae tuondoke,” aliniambia Joel na kukata simu.

Muda mfupi baadaye, alinifuata pale kantini, nikainuka na kuwaaga marafiki zangu tuliokuwa tukipiga stori, tukaongozana na Joel mpaka kwenye gari lake, mwenzangu yeye alishafanikiwa kununua gari dogo la kutembelea, Toyota Carina.

“Twende kwanza nyumbani tukampitie shemeji yako, nataka leo twende sehemu moja nzuri sana, tukale, kunywa na kufurahi!” alisema Joel huku akiendesha gari lake. Tulitoka Kurasini na kwenda moja kwa moja mpaka Tabata, nyumbani kwa Joel.

Hatukukaa sana, mkewe alishajiandaa na kupendeza, akaja tukasalimiana naye kisha akaingia kwenye gari, safari ya kuelekea mahali Joel alikokuwa amepanga ikaanza. Sikuwa najua tunaenda wapi.

Aliendesha gari mpaka Kinondoni, tukapita jirani kabisa na mahali nilipokuwa naishi.

“Kwani si tunampitia dada?” alihoji mke wa Joel, akimaanisha mke wangu, mumewe akawahi kumjibu kwamba alikuwa na wageni kwa hiyo hatajumuika nasi. Swali lake ni kama liliutonesha moyo wangu, nikatoa simu yangu na kutafuta namba yake.

Nilitaka nimtaarifu kwamba nitachelewa kidogo maana isije ikawa fujo tena baadaye nitakaporudi kama kawaida yake.

“Natoka na rafiki zangu, nitachelewa kidogo kurudi,” nilimtumia ujumbe mfupi, kisha nikashusha pumzi ndefu na kusubiri atakachokijibu.

“Niletee chakula kwanza, wewe hata kama unataka kwenda kulala hukohuko shauri yako.”

“Siwezi kukuletea chakula sasa hivi! Nipo mbali, kama ni chipsi si uagize hapo nje kwa wagosi?”

“Kwa hiyo umeamua kunishindisha na njaa si ndiyo? Sawa, nashukuru!” ilisomeka meseji yake.

Ikabidi nimtumie nyingine: “Nakushindisha na njaa kivipi wakati ndani kuna kila kitu, isitoshe nimekuachia fedha? Si suala la kuagiza tu hapo nje? Anyway ngoja nimpigie mimi simu mgosi akuletee, unataka chipsi na nini?”

“Sina haja! We endelea na mambo yako,” ilisomeka meseji ambayo ilinikata maini kabisa. Nikaamua kuachana naye.

“Vipi?” aliuliza Joel baada ya kuniona sipo sawa, nikamjibu kwa kifupi tu, safari ikaendelea. Tulienda mpaka Mikocheni, kwenye kiwanja kimoja tulichokuwa tunapenda sana kwenda, Glitters Grill. Hakikuwa kiwanja maarufu sana lakini kiukweli palikuwa pazuri sana.

Palikuwa na huduma nzuri ya vyakula, vinywaji, muziki laini na sehemu nzuri za kupumzikia. Nilifurahi sana kugundua kwamba kumbe safari yetu ilikuwa ikija kuishia hapo, nikamshukuru Joel kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba nita-enjoy kwelikweli na kusahau shida zote zilizokuwa zinanikabili.

Baada ya kupaki gari, tuliteremka na kupokelewa na wahudumu wachangamfu, wakatuchagulia sehemu nzuri ya kukaa, kwenye bustani za maua zilizokuwa zinatunzwa vizuri.

Cha kwanza ilikuwa ni kuagiza chakula, kila mtu aliagiza anachokitaka, mimi niliagiza ugali na makange ya kuku, chakula ninachokipenda sana. Shemeji yeye aliagiza chipsi kuku na Joel aliagiza ugali na samaki mzima.

Muda mfupi baadaye vyakula vililetwa, tukaanza kula huku stori za hapa na pale zikiendelea, nikijitahidi sana kujichangamsha lakini wapi!

“Shemeji leo umepooza, siyo kawaida yako! Sisikii zile stori zako zile,” alisema mke wa Joel na kusababisha wote tucheke. Nikiwa na furaha huwa napenda sana kupiga stori za kuchangamsha genge ambazo hufanya watu wanaonizunguka muda wote wawe wanacheka lakini siku hiyo ilikuwa tofauti.

Nilijitahidi kujichangamsha lakini huzuni iliyokuwa ndani ya moyo wangu haikufichika, ikabidi nisingizie kwamba nilikuwa na maumivu ya kichwa yanayotokana na matatizo ya macho yaliyokuwa yananiandama! Wote huo ulikuwa ni uongo, Joanna ndiye aliyesababisha niwe kwenye hali hiyo.

Basi Joel aliniunga mkono, wote wakawa wananishauri kula sana karoti na mbogamboga kwani husaidia kurekebisha matatizo ya macho.

Baada ya kumaliza kula, wenzangu walianza kupiga moja moto moja baridi! Joel na mkewe wote walikuwa wanywaji lakini mimi pombe zilikuwa hazipandi kabisa! Ikabidi niagize juisi na kwa sababu walishanizoea, hakukuwa na aliyehoji.

Hata hivyo, wakati naendelea kunywa juisi, wenzangu wakianza kuchangamka kwa kilevi, akili ilinituma na mimi kujaribu mbili tatu nikiamini pengine naweza kuwa na furaha kama wenzangu.

“Hata mimi nilitaka kukushauri hivyohivyo! Itakusaidia kupunguza maumivu ya kichwa, mhudumuuu!” aliita Joel ambaye hata sauti yake sasa ilishaanza kubadilika, akaja ambapo nilimuagiza kinywaji ambacho kabla sijaachanana mambo ya ulevi nilikuwa nikikipendelea.

Muda mfupi baadaye, mhudumu alikuja akiwa na chupa kubwa ya Bacardi, akaifungua na kuiweka mezani, kazi ikaanza.

Muda mfupi tu baadaye, tayari nilishaanza kulewa, uchangamfu wangu uliokuwa umepotea, ulianza kurudi kwa kasi ya ajabu, stori zikawa zinapigwa na kusababisha wote tuwe tunacheka sana.

Huwezi kuamini, nilisahau kabisa matatizo makubwa yaliyokuwa yananisibu, ikawa ni furaha kubwa kwelikweli utafikiri hakuna kilichotokea. Ilipofika majira ya saa tatu, ilibidi nimueleze Joel kwamba sitaweza kuendelea kujumuika nao, inabidi nirudi nyumbani.

“Mbona mapema?”

“Aah! Si unajua nyumbani kuna wageni, siwezi kurudi usiku sana, tena nikiwa nimelewa! Inaweza kuleta picha mbaya,” nilisema, basi ikabidi azungumze na mkewe na kwa pamoja, walikubaliana kwamba Joel anipeleke mpaka nyumbani kwangu kisha arudi waendelee ‘kula bata’.

Tulitoka na kwenda mpaka kwenye gari la Joel, tukawa tunaendelea kupiga stori za hapa na pale huku tukicheka kwa furaha. Nilijitahidi sana kuficha kilichokuwa ndani ya moyo wangu kwa sababu siku zote huwa nina kasoro moja, ninapokunywa pombe basi uwezo wa kutunza vitu moyoni huwa mdogo sana.

Siku hiyo nilijitahidi sana, hatimaye tukawasili Kinondoni, alinipeleka mpaka nyumbani kwangu, akaniteremsha kisha tukaagana. Huku nikipepesuka nilielekea kwenye geti dogo la kuingilia, kwa kuwa nilikuwa na funguo, nilifungua na kuingia ndani lakini hapohapo nikakumbuka suala la mke wangu kuhusu chakula.

Kwa jinsi nilivyokuwa namjua, endapo ningeingia nikiwa sina chakula chochote mkononi, halafu nimelewa, ugomvi mkubwa ungeweza kuibuka! Sikuwa nataka kugombana naye, sikuzoea kabisa maisha ya purukushani kwa hiyo niliamua kumpigia simu kijana aliyekuwa na kibanda cha chipsi jirani na hapo nyumbani.

Nikamuagiza chipsi kuku na soda huku nikimsisitiza awahishe! Sikutaka kuingia ndani, kwa hiyo nilisogea pembeni na kukaa kwenye kibaraza, nikiwa namsubiri kijana huyo aniletee chipsi ndiyo niingie ndani.

Basi nikiwa nimekaa pale kibarazani, nikiendelea kubofabofya simu yangu, mlango wa ndani ulifunguliwa! Alikuwa ni mke wangu.

“Vipi mwenzetu mbona umekaa nje?”

“Nasubiri chipsi nimemuagiza dogo hapo analeta.”

“Ndiyo ukae nje? Unanidanganya si ndiyo?”

“Nakudanganya nini tena mke wangu?”

“Yaani umetoka kwa wanawake zako huko, umeona haitoshi unafika nyumbani badala ya kuingia ndani unaanza kuchati hapa nje, hivi wewe mwanaume unanichukuliaje? Nakuuliza unanichukuliaje?” alisema Joanna huku akinisogelea mwilini. Ilibidi nisimame kwa lengo la kutaka kumuelewesha vizuri.

“Nachati na nani mke wangu, mbona unanihisi mambo mabaya bila sababu!”

“Halafu umelewa si ndiyo? Nakuuliza, umeenda kulewa tena si ndiyo?” alisema huku safari hii akiwa amenikwida shati nililokuwa nimevaa shingoni.

“Nimekunywa lakini sijalewa! Nilikwambia tutoke leo ukakataa, sasa ulitaka nifanye...” kabla sijamalizia kauli yangu, kengele ya getini iligongwa kuonesha kulikuwa na mtu, Joanna akaachia ‘msonyo’ mkali na kunisukuma!

Akatembea harakaharaka kuelekea kule getini, alikuwa ni yule kijana niliyemuagiza chipsi. Kwa kuwa sikuwa nimemlipa, ilibidi na mimi nisogee huku nikifungua waleti yangu kwa lengo la kutoa fedha.

“Nani amekuagiza?”

“Broo amenipigia simu,” alisema yule kijana wa chipsi, nikawa tayari nimeshafika.

“Mimi ndiyo nimemuagiza,” nilisema huku nikitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa, akaipokea na kutoa chenji. Joanna wala hakuwa amempokea na kwa jinsi alivyokuwa amesimama na kuniziba, hata mimi nilishindwa kumpokea.

“Uliagiza kwa ajili ya nani?”

“Kwa ajili yangu na wewe, sijala na najua na wewe hujala.”

“Hapana! Mimi sitakula, sikia dogo, wewe umeshakula?”

“Hapana sista!”

“Basi hiyo moja ya kwangu utakula wewe sawa eeh!” alisema Joanna huku akisogea pembeni. Ikabidi nimpokee mfuko mmoja wa chipsi pamoja na chenji, sikutaka kuongeza neno, basi akaondoka akiwa amefurahi, nikafunga mlango huku nikiwa nimefedheheka sana ndani ya moyo wangu.

Joanna hakusema chochote, akawa ameuvuta mdomo kisawasawa na kutembea harakaharaka kuelekea ndani, na mimi nikawa namfuata. Tuliingia ndani, mimi nikakaa sebuleni, Joanna akapitiliza chumbani.

Sikuwa nimeagiza chipsi kwa ajili yangu, nilishashiba huko nilikotoka lakini sikutaka Joanna ajue kwamba nimekula ndiyo maana niliagiza sahani mbili kwa hiyo kitendo cha Joanna kukataa kuzipokea, tena mbele ya yule kijana, kilinifanya niishiwe nguvu kabisa.

Nikiwa nimekaa pale sebuleni, nikiwa hata sijui nifanye nini sasa, Joanna alitoka na kunisogelea, akionesha bado kutaka shari kwelikweli.

“Sikiliza nikwambie! Kuanzia leo kila mtu atakuwa analala chumba chake, nimechoshwa na maudhi ya kila siku.”

“Khaa! Mke wangu, kwa kosa lipi hasa mpaka ufikie uamuzi huo? Nimekufanyia nini kikubwa?”

“Ndiyo nimeshasema! Kama kuna kitu unataka kwenda kuchukua chumbani nenda, nataka nilale mimi,” alisema, nikamwambia sina cha kuchukua, basi akaelekea chumbani na kubamiza mlango kwa nguvu, nikasikia akiachia msonyo mkali.

Kwa kuwa nilikuwa nimekunywa, haukupita muda mrefu nikapitiwa na usingizi palepale kwenye sofa nilipokuwa nimekaa. Nilipokuja kuzinduka, ilikuwa ni usiku sana, majira ya kama saa nane, kwa mbali nikawa nasikia kama mtu anaongea na simu. Nilipotega masikio mazuri, niligundua kwamba alikuwa ni Joanna, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwelikweli.

Niliinuka na kuanza kusogea upande wa chumba chetu cha kulala! Kweli alikuwa ni Joanna na ilionesha kama anazungumza na mwanaume maana nilimsikia mara kwa mara akimshukuru ‘asante baba’, na maneno mengine ya aina hiyo.

Joanna alikuwa na mapungufu mengi sana ambayo kwa mwanaume kumvumilia, ilikuwa inahitaji moyo kwelikweli lakini siku zote nilikuwa naamini kwamba ipo siku atakuja kubadilika. Sikuwahi kuhisi kwamba kwenye mapungufu yake hayo, pia ana tabia ya kunisaliti, sikuwahi.

Siku zote nilikuwa naamini kwamba mke wangu ni miongoni mwa wanawake waaminifu sana kwenye ndoa lakini kumbe nilikuwa najidanganya! Mapigo ya moyo yaliendelea kunienda kwa kasi kubwa, kijasho chembamba kikawa kinanitoka nikiwa naendelea kumsikiliza.

Nadhani mwenyewe hakuwa anajua kwamba namsikiliza, aliamini nitakuwa nimelala fofofo hasa ukizingatia kwamba nilikuwa nimepasha kidogo. Pengine hata uamuzi wa kuja kuniambia kwamba tunatakiwa kutengana vyumba, alikuwa anatafuta uhuru wa kufanya upuuzi wake bila kuulizwa chochote.

“Basi tuchati baba,” alisema kisha akakata simu. Nikiwa bado katika hali hiyo, wazo lilinijia kichwani mwangu kwamba nimgongee mlango ili ajue kwamba nimemsikia. Hata hivyo, upande mwingine wa nafsi yangu ulikataa, ningeweza kusababisha matatizo makubwa zaidi usiku huo, ikabidi nirudi pale kwenye sofa, safari hii machozi yalikuwa yananitoka kwa uchungu.

Sikupata usingizi tena mpaka kulipopambazuka. Akawahi kuamka kama kawaida yake na alipotoka, alinikuta nikiwa nimekaa kwenye sofa, nikiwa nimejiinamia. Hakunisemesha chochote, hata salamu yake hakutana kunipa, akanipita kama hajaniona na kwenda kufungua mlango mkubwa wa nje.

“Siku nyingine kama unajijua huwezi kula siyo kuniletea uchafu ndani kwangu, usafi huwa unafanya wewe?”

“Joanna!” nilisema kwa jazba huku nikisimama. Alipoona nasimama, na yeye aliacha kila alichokuwa anakifanya, akanisogelea kisharishari, tukawa tunatazamana.

“Ndiyo hivyo nimeshasema! Au unatakaje?”

“Nimekusikia usiku ukiwa unazungumza na simu, unaweza kuniambia ulikuwa unaongea na nani?” nilimuuliza huku nikitetemeka, basi akacheka kwa dharau na kuanza kunitazama kuanzia juu mpaka chini.

“Simu yangu, unataka kunipangia matumizi? Mbona wewe ukienda kwa hao malaya zako mimi sikuulizi chochote? Tena ukome kunifuatafuata, kila mtu ajue ustaarabu wake,” alinijibu kwa nyodo.

Sikuwahi kupandwa na jazba kama siku hiyo. Nilitamani nimkamate na kumfinyangafinyanga kwenye mikono yangu, nilitamani kumzibua kisawasawa, nilitamani hata nikachukue kisu na kumchinja kama kuku lakini kuna sauti ndani yangu ikawa inanituliza.

Itaendelea hapo chini!
 
TEARS OF THE SOUL (MACHOZI YA ROHONI)- 2

Mtunzi: Aziz Hashim (Hash Power)

NB: UNAWEZA KUIPATA SIMULIZI HII TAMU KUANZIA MWANZO
MPAKA MWISHO KWA MFUMO WA e-Book (PDF)
UTAKAYOISOMA KWENYE SIMU YAKO KWA SH. 5000/= TU
NICHEKI WHATSAPP 0719401968!

ILIPOISHIA:

Sikuwahi kupandwa na jazba kama siku hiyo. Nilitamani nimkamate na kumfinyangafinyanga kwenye mikono yangu, nilitamani kumzibua kisawasawa, nilitamani hata nikachukue kisu na kumchinja kama kuku lakini kuna sauti ndani yangu ikawa inanituliza.

ENDELEA NAYO...

Huwezi kuamini, licha ya jazba nilizokuwa nazo, niliamua kujifanya mpumbavu, nikakaa chini na kujiinamia, mikono ikiwa kichwani, machozi yakiwa yanaendelea kunitoka kwa wingi.

“Khaa! We vipi wewe? Tusipangiane,” alisema kwa nyodo huku akielekea chumbani. Asubuhi hiyo nilikuwa natakiwa kujiandaa na kwenda kazini lakini sikuweza kufanya chochote. Nilitamani hata ardhi ipasuke na kunimeza.

Kitu pekee nilichoona kinaweza kunifariji kwa muda huo, ilikuwa ni kunywa pombe, tena pombe kali! Nilitaka kulewa ikiwezekana hata nizime kabisa! Moyo wangu haukuwa tayari kuamini kile kilichokuwa kinatokea.

Niliamka na kutoka nje, jirani na pale nilipokuwa naishi, kulikuwa na ‘supermarket’ ndogo ambayo ilikuwa na kila kitu. Nikaenda kununua mzinga mkubwa wa ‘konya’ na soda ya kuchanganyia, nikarudi ndani.

“Eeeh! Samahani baba, vyombo vyangu siyo vya kunywea pombe, tutagombana, sipendi ujinga mimi, wanaume wenzako wanajiandaa kwenda kazini wewe unawaza pombe tu, hebu mtazame,” alisema Joanna baada ya kunikuta nimechukua glasi kabatini na kumimina ile pombe na kuchanganya na soda, akaichukua ile glasi na kwenda kumwaga ile pombe kwenye karo, akaiosha glasi huku akiachia misonyo mingi, akairudisha kabatini.

Donge kubwa lilinikaba kooni, jazba nilizokuwa nazo, kama ningeamua kufanya jambo, pengine ningefanya tukio ambalo lingeushangaza ulimwengu mzima, kwa hasira nikaushika ule mzinga na kuanza kujimiminia pombe mdomoni huku nikiwa nimefumba macho kutokana na ukali wake.

Kasoro kubwa ambayo nilikuwa nayo, ambayo pengine ndiyo iliyokuwa inanifanya niichukie pombe na kuamua kuachana nayo kabisa, ni tabia yangu nikishalewa, hasa pale ninapokunywa pombe kali.

Huwa nakuwa mgomvi sana na jambo hilo huwa silipenzi ndiyo maana niliamua kuachana na unywaji wa pombe kwa sababu nilikuwa najijua akili zangu, hasa pale ninapokunywa pombe kali.

Muda mfupi tu baadaye, akili zilishabadilika, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kuliko kawaida, akili zangu zikawa zinanituma kumkabili Joanna mpaka aseme ukweli. Ule upole wangu, busara na utaratibu, vyote vilishatoweka na sasa nilikuwa tayari kwa chochote.

“Joanna!” niliita kwa ukali, kumbena yeye alishanisoma na akajua ni nini kinachoenda kutokea kwa hiyo akawahi kuchomoka, wakati namuita tayari alikuwa nje ya geti, nikatoka huku nikitembea kwa kasi kumfuata.

“Naenda kwa mama kanipigia simu,” alisema huku akibamiza geti kwa nje, nikasimama huku nikitetemeka kwa hasira! Ni kama alikuwa na Mungu kwa sababu kweli ambacho kingetokea, kingekuwa gumzo nchi nzima.

Wakati mwingine wanaume wanaonekana kuwa wakatili kutokana na baadhi ya vitendo wanavyowafanyia wake zao lakini ukichunguza kwa kina, kwenye kila tukio, kuna kisa cha kuudhi na kupandisha mno hasira nyuma yake.

Basi nilirudi ndani, nikafunga milango yote na kuendelea kunywa pombe kwa hasira, nikiwa kwenye hali hiyo, simu yangu ilianza kuita, mapigo ya moyo yakanilipuka baada ya kugundua kwamba ni bosi alikuwa ananipigia, harakaharaka nikapokea huku nikijitahidi kuvaa uhalisia wa kuumwa.

“Sijakuona mpaka muda huu ofisini na hakuna mwenye taarifa zako, una matatizo gani?”

“Naumwa bosi, naendesha sana kila nikijaribu kutoka naishia getini,” nilidanganya. Kwa kuwa haikuwa kawaida yangu kutofika kazini wala kutoa visingizio, aliniamini, akanipa pole na kunitaka niende hospitali, nikamshukuru na kukata simu harakaharaka asije akagundua kwamba nilikuwa nimelewa.

Nilishusha pumzi ndefu na kukaa vizuri pale kwenye sofa! Kutokana na usingizi niliokuwa nao kutokana na kukesha usiku kucha, haukupita muda mrefu, nikapitiwa na usingizi mzito.

Nililala kwa muda mrefu sana, nilipokuja kushtuka, ilikuwa ni tayari saa tisa za alasiri, nikaamka na kuelekea bafuni kwani bado nilikuwa nimeamka na pombe zangu, nikafungulia bomba na kuanza kujimwagia maji. Nilikaa kwa muda wa kama dakika kumi hivi, angalau akili yangu ikawa imetulia.

Nilitoka na kuingia chumbani, angalau sasa niliweza kukaa kwa uhuru, nikajilaza kitandani huku nikitafakari mambo mengi ndani ya kichwa changu. Siku mbili zilizopita, kulitokea ugomvi kati yangu na Joanna na sababu niliwahi kurudi nyumbani kuliko siku zote na sikuwa nimemtaarifu chochote.

Kufika nyumbani, hakuwepo! Na hakuwa amenipa taarifa zozote kwamba anatoka! Na mimi sikupiga simu kumjulisha kwamba nipo nyumbani, nikawa nasubiri nione uongo wake.

Kwa kawaida, huwa narudi nyumbani saa moja jioni, siku nyingine kukiwa na foleni mpaka saa mbili lakini siku hiyo nilirudi saa tisa mchana. Huwezi kuamini, saa moja jioni ndiyo Joanna alirudi na bila kujua kwamba nipo chumbani, alipofika alitaka kukimbilia bafuni kuoga, akiwa anavua nguo zake ndiyo akagundua kwamba kumbe tayari nilisharudi.

Hata baada ya kugundua kwamba nimerudi, hakutaka kuzungumza chochote na mimi zaidi ya salamu tu, akakimbilia bafuni ambako alikaa kwa muda mrefu. Alipotoka ndiyo tukaanza kuzungumza.

Japokuwa yeye ndiyo alikuwa na makosa, cha ajabu ni kwamba alinigeuzia kibao. Akaanza kulaumu kwa nini nimerudi nyumbani bila kumpa taarifa, ina maana simuamini? Kwa nini namuwekea mitego ya aina hiyo?

Sikutaka matatizo naye, nilimtaka tu anieleze ni wapi alipokuwa ameenda na kwa nini hakunipa taarifa, akajikanyagakanyaga sana lakini kwa kuwa nilikuwa namuamini, niliamua kuyaacha mambo yapite. Hata hivyo, mwenzangu bado aliweka kinyongo na mawasiliano yakawa mabovu.

Aliniandalia chakula lakini yeye hakutaka kula, hata muda wa kulala, hakutaka stori na mimi kabisa! Asubuhi yake pia alininunia na ndiyo siku hiyo ambayo nilimuomba jioni yake tutoke lakini akanijibu mkatomkato na kukata simu. Baadaye nilipopata mwaliko wa rafiki yangu, niliona huo ndiyo wakati wa kwenda kubadilisha mawazo lakini niliporudi ndiyo yakatokea yale yaliyotokea.

Nilibaki na maswali mengi ndani ya kichwa changu, ushahidi wa kumsikia Joanna akiwa anazungumza na simu usiku uliopita, ulinifanya nipate picha kubwa kuhusu kilichokuwa kinaendelea.

Mke wangu alikuwa ananisaliti, swali ambalo sikuwa na majibu nalo, ni kwamba anatoka na nani? Amekosa nini kwangu mpaka kufikia hatua ya kunisaliti? Na nilipojaribu kuunganisha matukio, nilizidi kuchanganyikiwa zaidi kwa sababu kwa miezi kadhaa alikuwa na mabadiliko makubwa ya tabia lakini siku zote nilikuwa nikiamua kupuuzia huku nikijidanganya kwamba mke wangu hawezi kunisaliti.

Nilichoamua kukifanya, kwa sababu sasa nilikuwa peke yangu humo ndani, niliamua kuanza kupekua vitu vyake. Sikuwahi kumpekua mke wangu hata siku moja tangu nimuoe, penzi langu kwake lilinifanya niwe ni kama kipofu.

Nilishusha mikoba yake yote na kuanza kuupekua mmoja baada ya mwingine, hakukuwa na kitu chochote ambacho kingenifanya nimtilie wasiwasi zaidi. Kulikuwa na vitu vya kawaida vya mwanamke.

Hata hivyo, kwenye kabati lake, kuna droo moja alikuwa ameifunga na funguo na hata sijui funguo aliiweka wapi, nikaamua kuachana nayo huku nikijiapiza kwamba siku nitakayopata nafasi, nitafungua kuona kuna nini.

Kwa kuwa njaa ilikuwa inaniuma sana, ilibidi nimpigie simu yule kijana wa chipsi na kumpa oda yangu, nikatoka na kwenda kukaa sebuleni huku nikichezea simu yangu. Ghafla nilipata wazo.

Nimewahi kusikia kwamba kuna utaalamu fulani unaweza kuufanya na ukawa na uwezo wa kusoma meseji zote zinazoingia kwenye simu ya mtu unayetaka kufuatilia mawasiliano yake. Sikuwahi kufikiria hata mara moja kwamba hiyo ni njia nzuri lakini kwa jinsi mambo yalivyokuwa yamekorogeka, ilikuwa ni lazima nifanye kitu.

Nilikuwa najua kwamba Joanna ananisaliti lakini kumhisi kwa maneno tu, au kutumia ushahidi wa kumsikia akizungumza na mwanaume mwingine kwenye simu, kusingeweza kufanya madai yangu yawe na nguvu.

“Haloo!”

“Nambie Alex! Umekuwa kimya sana ndugu yangu, vipi shemeji hajambo!”

“Hajambo, tupo ndugu yangu, si unajua tena majukumu ya hapa na pale. Sasa mambo yasiwe mengi, nimekupigia simu kuna jambo nataka unisaidie,” nilimwambia Clarence, mmoja kati ya marafiki zangu wakubwa tangu tukiwa chuoni.

Yeye alikuwa amesomea masuala ya teknolojia ya mawasiliano na ukiachilia mbali kusomea, pia alikuwa mtundu sana wa mambo ya kompyuta na simu, akatega sikio na kunisikiliza kwa makini.

Nilienda moja kwa moja kwenye point yangu ya msingi, nilimwambia kwamba nahisi mke wangu ananisaliti lakini sina namna ya kumnasa ‘red handed’ mpaka kupitia simu yake kwa sababu alikuwa mjanja sana.

“Daah! Ndugu yangu, mimi sikushauri kabisa kufanya hiyo kitu.”

“Kwa nini Clarence?”

“Unajua ukimchunguza sana bata huwezi kumla! Hawa wanawake karibu wote wanasaliti, ni wachache sana ambao kweli ni waaminifu kwenye ndoa zao. Unapotaka kumchunguza, unaweza kukutana na mambo ambayo yatakuumiza sana moyo wako na mwisho ukaishia kufanya tukio litakalokulostisha,” aliniambia, maelezo yake yakawa hayajaniingia kabisa.

Alinitolea mfano wa rafiki yetu mwingine ambaye pia tulisoma naye chuo. Alikuwa anaitwa Godknows Mhavile ingawa tulizoea zaidi kumuita kwa kifupi God.

“Unajua kwamba God yupo Segerea?”

“Segerea?”

“Ndiyo! Na yeye ishu ilikuwa hivihivi, alikuwa na uhusiano na dada mmoja hivi na tayari walishaanza mipango ya ndoa, sasa akawa hamuamini. Akanipigia simu kama unavyonipigia wewe na kuniambia tufanye kama unavyotaka kufanya wewe, kudukua simu ya mke wake.

“Kweli nilimsaidia lakini hakuna kitu ambacho nakijutia maishani mwangu kama kumsaidia God! Alikuja kugundua kwamba kumbe mchumba wake alikuwa na uhusiano na mtu mwingine tofauti na yeye na kila siku alikuwa akimdanganya jamaa kwamba anampenda sana, God akaenda mpaka kumtambulisha kwao, siku alipogundua, tena na ushahidi wa meseji, sauti na picha, aliamua kuchukua uamuzi mbaya sana.

“Alimchoma kisu na kumuua wakiwa gesti, akakamatwa na huu unaenda mwezi kama wa saba jamaa yupo ndani akikabiliwa na kesi ya mauaji! Sitaki kukupoteza na wewe Alex, haya mambo ni hatari sana ndugu yangu. Kama unahisi anakusaliti, ni bora ukamrudisha tu kwao, usimfuatilie,” alisema Clarence, nikashusha pumzi ndefu na kukata simu, nikimuahidi kwamba nitampigia baadaye.

Nilikuwa nikimfahamu vizuri God na hata namba yake ya simu nilikuwa nayo lakini kwa sababu ya ubize wa kazi, tulijikuta tukipotezana kwa kipindi kirefu sana, sikuwa najua chochote kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yake, Clarence ndiyo akawa amenifumbua macho.

Nilibaki nimepigwa na butwaa, nikiwa ni kama siamini ile stori niliyopewa na Clarence. Nilikuja kuzinduliwa na kengele ya getini iliyokuwa inalia, nikaamka na kwenda kufungua. Alikuwa ni yule kijana wa chipsi, basi tukasalimiana kwa uchangamfu pale, nikamlipa na yeye akanipa mzigo wangu.

“Vipi shem yupo?”

“Aah! Katoka, vipi kwani!”

“Daah! Bro, ujue kuna mambo mengine yanatokea sisi wadogo zako tunakuwa tunajisikia vibaya sana, ukizingatia tunaishi vizuri sana na wewe, unatujali wadogo zako tukiw ana shida! Mambo anayokufanyia shem siyo kabisa,” alisema kijana huyo huku akigeuka huku na kule kama anayetakakuhakikisha hakuna mtu mwingine anayetusikiliza.

“Vipi kwani!” nilimuuliza nikiwa na shauku kubwa ndani ya moyo wangu.

“Kuna gari huwa linakuja hapa kwako kila ukitoka asubuhi, linakuja mida ya kama saa nne hivi mpaka saa nane au saa tisa, huwa linapaki hapo nyuma. Unalijua?”

“Gari gari?”

“Gari dogo hivi, nafikiri ni Brevis au Crown!”

“Hapana! Silijui, nani huwa anaendesha?”

“Jamaa mmoja sharobaro hivi! Muda wa kuondoka huwa wanaondoka na shemeji na hata kama hujui kinachoendelea, ukiwatazama inaonesha wazi kwamba kuna kitu kinachoendelea.

Juzi mlipishana kidogo tu, wakati wewe unaingia walikuwa wameondoka kama nusu saa nyuma! Nafikiri hata shem alivyorudi alikukuta umesharudi,” alisema, mapigo ya moyo wangu yakanilipuka kuliko kawaida.

Siku aliyoisema ni ile niliyorudi nyumbani bila taarifa na kukuta Joanna hayupo nyumbani wakati hakuwa amenipa taarifa zozote. Aliporudi nikamhoji lakini mwisho tukaishia kugombana na akaninunia kabisa. Kumbe alitengeneza mazingira ya kufanya eti nionekane kama mimi nina makosa kwa kurudi nyumbani na kumchunga wakati ukweli ni kwamba alikuwa na mwanaume mwingine.

Nilijisikia uchungu sana ndani ya moyo wangu lakini nilijikaza nisije kuonesha udhaifu mbele ya yule kijana muuza chipsi, Muddy Mgosi kama alivyokuwa akifahamika zaidi pale mtaani.

“Enhee! Kumbe ndiyo mambo yenyewe hayo?”

“Ndiyo broo! Hata kama watu hawakwambii, mtaa mzima wanajua uchafu unaofanywa na mkeo sema kila mtu anajiuliza ataanzia kukwambia wapi. Mimi mwenyewe nimejitosa sana kukwambia maana najua haya mambo ya mapenzi,kesho mnaweza kupatana halafu nikaonekana mimi ndiyo mchonganishi! Lifanyie kazi bro utaujua ukweli,” aliniambia huku akigeuka na kutaka kuondoka, nikamrudisha.

“Kwa hiyo huyo jamaa huwa anakuja kila siku?”

“Ndiyo! Hata leo pia amekuja sema alipaki gari kule ng’ambo ya barabara, nikajua haupo. Ameondoka na shem,” alisema, kauli nyingine iliyozidi kuupasua moyo wangu, donge kubwa likazidi kunikaba kooni lakini nikajikaza kisabuni.

“Sasa sikia! Nataka unisaidie kitu mdogo wangu, shika kwanza hii,” nilisema huku nikiingiza mkono mfukoni, nikatoa noti mbili za shilingi elfu kumikumi na kumpa.

“Nataka uwe unafuatilia kila kinachoendelea na kunitaarifu, ukiona kitu tu nitumie meseji kwenye simu yangu.”

“Usije ukanichoma broo, ujue shem tunaelewana sana sema mambo yake ndiyo sisi wote pale ofisini kwetu yanatuumiza sana. Mbona unampa kila anachokitaka? AU kuna tatizo lingine broo!”

“We niachie mimi Muddy mdogo wangu, fanya kama nilivyokwambia,” nilimwambia, basi tukaagana, akarudi kwenye kazi yake ya kuuza chipsi. Nilibaki nimeganda pale mlangoni, nikiwa hata sijui nashangaa nini. Zile pombe nilizokunywa asubuhi, zote ziliyeyuka ndani ya kichwa changu, nikawa najiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.

“Joanna mke wangu, nimekukosea nini kustahili haya yote?” nilijiuliza, safari hii machozi yakianza kunibubujika kama mtoto mdogo. Nilibamiza geti na kurudi ndani, kwa kuwa sikuwa nimeumaliza ule mzinga wangu wa ‘konya’, nilianza kuugida tena! Nilikuwa ni kama nimechanganyikiwa, nilihisi kichwa chote kikivurugika kabisa.

“Joanna! Kweli? Haiwezekani,” niliendelea kujisemea mwenyewe huku nikigida pombe kwa fujo! Hicho ndiyo kitu pekee nilichoona kinaweza kuniondolea mawazo kwa wakati huo, nilikunywa mpaka ikafika mahali, nikawa sikumbuki tena mambo ya Joanna, nikawa nasikiliza muziki niliofunguliakwa sauti kubwa pale sebuleni.

Hata hivyo, kuna nyimbo zilipokuwa zinapigwa, nilikuwa nahisi kama naimbiwa mimi, uchungu ukawa unaendelea kunitesa ndani ya moyo wangu kuliko kawaida, nikaona kama pombe nilizokunywa hazitoshi.

Nilitoka na kwenda tena pale kwenye super market ndogo iliyokuwa jirani na pale kwangu, nikaenda kununua mzinga mwingine na kurudi ndani huku nikipepesuka. Watu waliokuwa wananijua wakawa wanashangaa kwa sababu ni wachache sana waliokuwa wanajua kwamba kuna kipindi nilikuwa nakunywa pombe, wakawa wanajiuliza nimepatwa na nini? Sikujali.

Nilirudi ndani na kuendelea kulewa, ikafika mahali nikawa sielewi tena kinachoendelea, nikalala usingizi wa kifo palepale sebuleni. Kibaya ni kwamba hata chipsi nilizokuwa nimeagiza, nilishindwa kabisa kuzila, ukichanganya na ukali wa pombe nilizokuwa nakunywa, basi ilikuwa balaa kubwa kwelikweli.

Nilipokuja kuzinduka, ilikuwa ni saa sita za usiku, nikashtuka sana baada ya kuangalia saa, nikawa najiuliza nimewezaje kulala kwa muda wote huo? Sijui ni akili za pombe au sababu ya usingizi, nilipozinduka, kitu cha kwanza ilikuwa ni kumuita mke wangu, Joanna.

Niliita mara mbili bila kuitikiwa, ni hapo ndipo kumbukumbu ziliponirudia kuhusu kilichokuwa kimetoka, moyo ukaanza kuniuma mno utafikiri kidonda. Kuna wakati nilitamani kila kilichotokea kiwe ndoto lakini haikuwa hivyo.

Niliamka huku nikipepesuka na kuelekea kwanza chooni, baada ya kumaliza haja zangu nilielekea chumbani kwangu kumuangalia Joanna! Hakuwepo. Nilirudia kuangalia saa nikiwa ni kama siamini, saa sita za usiku mke wa mtu hayupo ndani!

Nilizunguka vyumba vyote lakini Joanna hakuwepo, nikaenda kuangalia mlango, bado ulikuwa umefungwa vilevile kama nilivyokuwa nimeufunga. Joanna hakuwa amerudi mpaka muda huo, nikakumbuka maneno ya yule kijana, Muddy Mgosi kwamba asubuhi tulipogombana alikuja kuchukuliwa na gari na mwanaume ambaye huwa anamfuata kila siku pale nyumbani.

Nilijiinamia huku machozi yakianza upya kunibubujika! Acheni mapenzi yaitwe mapenzi! Najua mwingine anaweza kusema kirahisi tu, si umuache? Mapenzi hayapo hivyo, hasa kama mtu unampenda kwa dhati kutoka ndani kabisa ya moyo wako.

Licha ya yote yaliyokuwa yametokea, eti akili yangu ilikuwa inaniambia siwezi kuishi bila Joanna, tuliishi pamoja kwa mapenzi mazito sana katika hatua za mwanzo za mapenzi yetu, na hata kipindi wakati ndiyo kwanza tunaingia kwenye ndoa.

Ilikuwa ngumu sana kufuta kumbukumbu hizo ndani ya moyo wangu! Ucheshi aliokuwa ananionesha, mapenzi motomoto, uzuri wake wa kipekee aliojaaliwa na sifa nyingine kedekede alizokuwa amejaaliwa, vilikuwa ni vitu vilivyofanya niumie mno ndani ya moyo wangu.

Niseme tu ukweli kwamba Joanna alikuwa ni mwanamke wa kipekee, aliyeumbwa akaumbika haswaa! Alikuwa na weupe wa maji ya kunde, tena ule wa asili kabisa, achana na wengine wanaotumia makrimu kubadilisha rangi za ngozi zao, yeye alikuwa natural.

Alikuwa mrefu kiasi ingawa hakuwa amenizidi, huku akiwa amejaaliwa ‘mzigo’ mkubwa nyuma ya kiuno chake, hali iliyokuwa inafanya kila ninapopita naye, watu wageuke na kututazama. Alikuwa na shepu nzuri kwelikweli na yote tisa, kumi ni kwamba alikuwa mzuri sana wa sura! Mungu alimpendelea kwa kila kitu.

Alikuwa na macho meupe ya duara, ambayo akikutazama unaweza kujihisi kama unatazamana uso kwa uso na malaika! Akicheka sasa, meno yake yalikuwa yamepangika vizuri mno, huku akiwa na vishimo vya mashavuni, wengine wanaita ‘dimples’.

Mara zote sauti yake ilikuwa ya upole, akiwa na aibu fulani hivi za kikekike, vitu ambavyo vilizidi kumfanya awe na mvuto kwelikweli. Hata hivyo, tangu matatizo yaanze ndani, lile tabasamu lake pana nililozoea kuliona kwenye uso wake, halikuwepo tena.

Ule upole wake na sauti tamu yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni haikuwepo tena, alikuwa akiongea basi kama haongei kwa ukali, basi ataongea kwa dharau! Ikawa akinitazama, hanitazami tena kwa yale macho yake mazuri meupe, ambayo muda wote yalikuwa ni kama yana usingizi au kama amekula kungu, ikawa asiponitazama kwa ukali, basi atanitazama kwa dharau!

Mambo yalikuwa yamebadilika mno, nilishahangaika sana kurudisha maelewano yetu bila mafanikio, kumbe kuna kidudu mtu alikuwa ameingilia penzi langu, jini mkata kamba alikuwa ametutembea na sasa kila kitu kilikuwa kimevurugika kabisa.

Niweke wazi kwamba kabla ya kukutana na Joanna, sikuwahi kuwa kwenye uhusiano ‘serious’ wa kimapenzi, sikuwahi kumpenda mwanamke na kumkabidhi moyo wangu kama ilivyokuwa kwa Joanna.
Itaendelea hapo chini...
 
TEARS OF THE SOUL (MACHOZI YA ROHONI)- 3

Mtunzi: Aziz Hashim (Hash Power)

NB: UNAWEZA KUIPATA SIMULIZI HII TAMU KUANZIA MWANZO
MPAKA MWISHO KWA MFUMO WA e-Book (PDF)
UTAKAYOISOMA KWENYE SIMU YAKO KWA SH. 5000/= TU
NICHEKI WHATSAPP 0719401968!

ILIPOISHIA:

Niweke wazi kwamba kabla ya kukutana na Joanna, sikuwahi kuwa kwenye uhusiano ‘serious’ wa kimapenzi, sikuwahi kumpenda mwanamke na kumkabidhi moyo wangu kama ilivyokuwa kwa Joanna.

ENDELEA NAYO...

Ni kweli nilishaingia kwenye mahusiano mara kadhaa kabla ya kukutana naye lakini mara zote, mimi ndiyo nilikuwa mtu wa kuiumiza mioyo ya wanawake. Nilikuwa siwezi kudumu kwenye uhusiano na mwanamke, hata anioneshe mapenzi kiasi gani!

Mwonekano mzuri niliokuwa nimejaliwa, mwili wa mazoezi na utanashati, vilikuwa ni vitu vilivyofanya nijione kuwa bingwa wa mapenzi lakini safari hii nilikuwa nimepatikana!

Basi niliendelea kumwaga machozi pale sebuleni, kumbukumbu nyingi zikiendelea kupita ndani ya kichwa changu, mara wazo likaja la kumpigia simu ili kujua yuko wapi. Huwezi kuamini, bado nilikuwa nahisi pengine anaweza kuwa amepatwa na matatizo yaliyofanya asiwepo nyumbani mpaka wakati huo.

Niliposhika simu yangu, niligundua kwamba kulikuwa na missed calls kadhaa, harakaharaka nikaanza kuzifungua, nikiamini pengine Joanna atakuwa amenitafuta sana bila mafanikio lakini cha ajabu, hakukuwa na missed call yake hata moja, nikazidi kuchanganyikiwa.

Nilibonyeza namba yake ambayo nilikuwa nimeisevu kwa jina la ‘My Sweetheart’ kwenye simu yangu huku nikisindikizia na vikopakopa vyekundu, nikaibofya na kupeleka simu sikioni.

“Namba ya simu unayopiga, haipatikani kwa sasa! Tafadhali jaribu tena baadaye!” ilisikika sauti kwenye simu yangu kuonesha kwamba alikuwa amezima simu yake. Nikashusha pumzi ndefu huku nikiendelea kutokwa na machozi, nikagundua kwamba pia kulikuwa na meseji kwenye simu yangu, nikaanza kuzifungua, moja baada ya nyingine.

“Leo sirudi, nitalala kwa mama!” meseji fupi ilisomeka, ikionesha kutoka kwa Joanna. Nilipotazama muda aliotuma, niligundua kwamba aliituma majira ya saa tatu za usiku, nadhani baada ya hapo ndiyo akazima simu yake.

Japokuwa ilikuwa ni usiku sana, sikutaka kuamini haraka alichoniambia, ikabidi nimpigie simu mdomo wake wa kiume ambaye bado alikuwa akiishi na wazazi wake, Magomeni Mwembechai akiwa anasoma chuo.

“Samahani shem nimekupigia usiku sana! Naomba kuongea na dadaako, kuna jambo la muhimu sana nataka kuzungumza naye simu yake haipatikani.”

“Dada? Dada Joanna?”

“Ndiyo!”

“Mh! Kwani amekwambia amekuja huku?” aliniuliza swali lililonimaliza kabisa nguvu, nikashindwa nimjibu nini.

“Mama yupo wapi kwani?”

“Amelala!”

“Aah! Basi nahisi nimechanganya, aliniaga kwamba anaenda kwa mama, basi labda ameenda kwa mama wa Tabata,” nilivunga huku nikisikia uchungu mkali ndani ya moyo wangu, akaniambia ana karibu mwezi mzima hajaonana na Joanna na akaniambia pia kwamba usiku wa siku hiyohiyo, mama yao alikuwa anamuuliza mpaka ikabidi ampigie simu na kumuuliza kwa nini siku hizi haendi kumsalimia?

Ilibidi nimuage harakaharaka na kukata simu, uchungu mkali ukazidi kuniganda rohoni kiasi cha kuhisi kwamba naweza kuanguka na kupoteza maisha muda wowote.

“Joanna! Uko wapi mke wangu jamani? Rudi nyumbani, nimekusamehe mama,” nilijisemea huku machozi yakinibubujika. Eti licha ya mambo yote yaliyotokea na yaliyokuwa yanaendelea kutokea, nilikuwa tayari kumsamehe kwa kila kitu ili tuendelee na maisha yetu.

Unaweza kuniona pengine nilikuwa nimechanganyikiwa au pengine nilikuwa nimerogwa na Joanna lakini haikuwa hivyo, nguvu ya upendo wangu kwake ilikuwa kubwa mno ndani ya moyo wangu.

Hata sikuelewa nawezaje kuishi bila yeye! Nilikuwa nikimpenda kupitiliza na pengine alikuwa analijua hilo ndiyo maana akaamua kuutumia udhaifu huo kuutesa moyo wangu.

Mara kwa mara nilikuwa nikisikia maneno ya busara kutoka kwa watu walionizidi umri na uzoefu kwenye ndoa, kwamba ni makosa makubwa sana kumuonesha mwanamke kama unampenda sana kwa sababu wanawake wengi jinsi walivyoumbwa, akishajua kama unampenda na huwezi kufurukuta kwake, anatumia udhaifu huo kukuadhibu.

Siku zote nilikuwa siamini kabisa kama kuna ukweli wowote kwenye suala hilo, kwa nini nijifiche kwamba nampenda Joanna? Nilikuwa kama mwendawazimu kwake, nilifanya kila ninachoweza kufanya ili kumuaminisha kwamba nampenda sana na kamwe siwezi kuishi bila yeye na sasa alikuwa akiutumia udhaifu huo kuniadhibu.

Niliendelea kutafakari mambo mengi ndani ya kichwa changu, huwezi kuamini sikupata tena usingizi mpaka kunapambazuka. Kulipopambazuka nilikuwa natakiwa kwenda kazini, lakini sikuweza kufanya chochote, nilikuwa najiona mithili ya boksi tupu ambalo halina kitu ndani.

Roho yangu ilikuwa tupu kabisa, nilipoteza hamu ya kufanya kila kitu! Hata sikuona tena umuhimu wa kazi, namfanyia nani kazi sasa! Fedha nilizokuwa nazitafuta zilikuwa na maana gani tena maishani mwangu bila uwepo wa Joanna? Moyoni nikajiambia kwamba siwezi tena kwenda kazini, hata kama ni kufukuzwa, basi acha nifukuzwe tu.

Niliamka kichovu na kwenda bafuni, nikajimwagia maji na kuingia chumbani kwangu. Kila nilichokuwa nakiona kilikuwa kinanikumbusha kuhusu Joanna! Nikawa natokwa na machozi tu, nilipozitazama nguo zake, nilipotazama vipodozi alivyokuwa anavitumia na manukato aliyokuwa anapenda kuyatumia! Nilihisi ni kama moyo unataka kutoka.

Nilitamani kulewa tena lakini sauti fulani ndani ya moyo wangu ikaniambia ‘utaendelea kulewa mpaka lini?’ Nilichokifanya, nilichukua simu yangu na kujaribu kupiga namba yake ya simu.

Simu iliita bila kupokelewa, nikapiga kwa mara ya pili huku nikiwa najisikia vibaya mno ndani ya nafsi yangu. Nilitaka akipokea tu, nimwambie kwamba nimemsamehe na kama na yeye kuna kitu nimemkosea basi anisamehe na kurudi nyumbani tuyazungumze.

Cha ajabu, simu ilipoita sana, ilipokelewa upande wa pili, nikajiweka vizuri na kulilazimisha tabasamu kwenye uso wangu.

“Haloo Joanna baby!”

“We nani unapigapiga simu asubuhi yote hii?” sauti ya kiume ilinijibu kwa ukali, nikashtuka na kuitazama simu yangu nikihisi pengine labda nilikuwa nimekosea na kupiga namba ya mtu mwingine. Ilikuwa ni ileile namba anayoitumia siku zote, ilikuwa ni namba ya Joanna.

“Haloo! Haloo!”

“Nakuuliza wewe nani unayesumbua watu asubuhi yote hii?”

“Samahani ndugu yangu naomba kuongea na mwenye simu.”

“Mwenye simu unamjua wewe? We mpuuzi nini?” ilisema sauti hiyo kwa ukali kisha simu ikakatwa! Nikabaki nimepigwa na mshangao, nikiwa siamini kabisa kilichokuwa kinatokea.

Nikaipiga tena lakini safari hii haikupokelewa, ikaita wee mpaka ikakata! Nilipoipiga tena, haikuwa ikipatikana hewani kuonesha kwamba ilikuwa imezimwa.

“Khaaa! Yaani Joanna anafikia hatua ya kumpa mwanaume apokee simu yangu?” nilijisemea huku nikitetemeka kuliko kawaida! Walioimba kwamba maumivu ya mapenzi ni bora uunguzwe na moto hawakukosea, maumivu niliyoyasikia moyoni mwangu yalikuwa makali mno.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba kumbe Joanna hakuwa ameenda kwa mama yake wala kwa mama mkubwa! Alikuwa ameenda kwa mwanaume. Niliitupa simu pembeni na kuanza kulia, safari hii nilikuwa nalia mithili ya mtu aliyepokea taarifa za msiba.

Unaweza kuniona mjinga, ni sawa! Unaweza kuniona zezeta! Ni sawa pia! Nilikuwa mjinga na zezeta, nakubali kabisa na pengine hata mtu yeyote angekuwa kwenye nafasi yangu, angeweza kuonekana ni kama amechanganyikiwa! Acha kabisa na kitu kinachoitwa maumivu ya mapenzi.

Nilichoamua, ilikuwa ni kumpigia tena simu Clarence, rafiki yangu wa kitambo tangu tukiwa shule. Japokuwa alikuwa amenionya kuachana kabisa na mpango wangu wa kutaka ‘kui-hack’ simu ya Joanna ili niweze kufuatilia mawasiliano yake, maji yalikuwa yameshanifika shingoni kwa hiyo sikuwa na cha kufanya.

Nilimpigia simu, harakaharaka akapokea kwa uchangamfu kama kawaida yake, nikamueleza msimamo wangu kuhusu kile ambacho nilikuwa nimeshazungumza naye. Japokuwa alikuwa amenipa na mfano hai wa nini kinachoweza kutokea, nilimsisitiza kwamba nataka anisaidie kazi hiyo na hata ikibidi kumlipa nitafanya hivyo.

Alitafakari kwa muda mrefu sana, mwisho akaamua kukubali. Tukakubaliana kwamba jioni ya siku hiyo atakuja tuonane ili kuikamilisha kazi hiyo. Nilimshukuru sana na nikawa naona kama muda unaenda taratibu sana.

Nilishinda nikiwa nimejifungiandani siku hiyo, wafanyakazi wenzangu walikuwa wakinipigia simu kutaka kujua maendeleo yangu, nikawa nawajibu kwamba bado hali yangu siyo nzuri. Joel, rafiki yangu kipenzi naye alikuwa miongoni mwa watu walionipigia simu. Nilipopokea simu yake tu, aligundua wazi kwamba kuna kitu hakipo sawa.

“Tunaweza kuonana Alex tafadhali! Nikitoka kazini nitakupitia jioni, ni muhimu sana,” aliniambia, nikashindwa kumkatalia kutokana na jinsi tulivyokuwa tumeshibana. Siku hiyo sikunywa kabisa pombe kwa hiyo kwa sababu nilikuwa na akili zangu timamu, maumivu yalikuwa makali zaidi.

Nilijaribu kupiga simu ya Joanna mara kadhaa, kila nilipokuwa nikipiga, ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa, nikipiga mara ya pili nakuta haipatikani. Ikafika mahali, nikawa nikipiga inaita kidogo kisha inasikika sauti kwamba ‘namna unayopiga inatumika!’. Kwa lugha nyepesi ni kwamba Joanna alikuwa ameamua kuni-block ili nisiendelee kumsumbua.

Sikutaka kumwambia ndugu yake yeyote kuhusu kilichokuwa kinaendelea, majibu aliyonipamdogo wake jana yake usiku yalikuwa yanatosha kabisa kunipa picha ya kilichokuwa kinaendelea, nikaamua kufa na tai yangu shingoni. Sikula kitu chochote siku hiyo, sikuwa na hamu ya kula kitu chochote.

Simu ya Clarence ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye lindi la mawazo machungu. Tayari ilikuwa ni saa kumi na moja jioni, akaniambia kwamba yuko njiani anakuja lakini akaniambia kwamba anataka tukutanie nje ya nyumbani kwangu.

Kwa sababu alikuwa anapenda sana kunywa pombe, niliamua kumrahisishia kazi, nikamwambia tukutane Papi Churo, kwa wenyeji wa Kinondoni watakuwa wanakifahamu kiwanja hiki cha kijanja.

Basi niliamka na kwenda kuoga, nikarudi na kujiweka safi, nikapiga jeans na t-shirt, chini nikavaa raba kali na kujipulizia manukato vizuri. Nilipojitazama kwenye kioo, niliridhika kwamba nipo kwenye mwonekano bomba lakini tatizo lilikuwa ni uso wangu.

Macho yalikuwa yamevimba kwa sababu ya kulia na kukosa usingizi, ikabidi nichukue ‘kapelo’ na kuivaa kwa kuishusha upande wa usoni ili isiwe rahisi kwa mtu kuniona macho yangu kwa urahisi.

Nikafunga numba vizuri na kutoka, mfukoni nikiwa nimebeba fedha za kutosha kwa sababu lichaya matatizo niliyokuwa napitia na mke wangu, suala la kipato angalau naweza kumshukuru Mungu kwamba nilikuwa najimudu.

Nilisimamisha Bajaj, nikamuelekeza dereva sehemu ya kunipeleka na safari ya kuelekea Papi Churo ikaanza. Nilimpigia simu Clarence na kumweleza sehemu ya kunikuta, akacheka sana na kuniambia nimuandalie ‘vitu vyake’ kama kawaida, akimaanisha pombe, nikamtoa wasiwasi.

Muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nimewasili Papi Churo. Sikutaka kuchanganyikana na watu, kwa hiyo moja kwa moja nilipita mpaka VIP, nikaagiza maji na kutulia huku nikiwa naichezea simu yangu kupunguza mawazo.

Juu kabisa ya simu yangu nilikuwa nimesevu ‘screen saver’ ya picha ya Joanna, kwa hasira nikaamua kuitoa na kuweka picha nyingine tofauti kabisa. Muda mfupi baadaye, Clarence aliwasili, kwa kuwa tayari nilishamuona, nilimpigia simu na kumuelekeza mahali nilipokuwa.

Akaja na kama kawaida yake, tukasalimiana kwa uchangamfu huku akinipigisha stori za hapa na pale zilizofanya nisahau kwa muda matatizo yangu, tukawa tunacheka.

“Nambie mwanangu! Nakuona haupo sawa kabisa, shemu anazingua siyo!”

“We acha tu mwanangu!” nilisema huku nikianza kumsimulia kwa kifupi hali ilivyokuwa. Na yeye alionesha kuguswa sana na nilichokuwa namueleza lakini hakuchangia chochote zaidi ya kusikitika sana.

Alitoa laptop yake na kuifungua, akaanza kuibofyabofya na muda mfupi baadaye, aliniambia nimtajie namba ya simu ya Joanna. Nilifanya hivyo, akaniambia nimtajie na namba yangu, sijui alifanya nini mwenyewe, muda mfupi baadaye aliniomba simu yangu, nikampa! Akaibofyabofya kwa muda kisha akashusha pumzi ndefu.

“Mzigo tayari kaka! Lakini nakuomba sana uwe na moyo wa ustahimilivu, hawa wanawake wanaweza kukulostisha kabisa! Nakuombea kwa Mungu akupe busara ili ufanye maamuzi bora ambayo hayatakuletea matatizo.

“Kama unaona mambo yamekuwa mabaya kabisa, unaweza kumrudisha kwao kwanza wakati ukitafakari nini cha kufanya!” aliniambia, nikawa natingisha kichwa kuonesha kumuelewa, akanipa simu yangu na kunitaka nisifanye chochote kwa muda huo mpaka nitakapokuwa sehemu tulivu.

“Utakuwa na uwezo wa kusikiliza simu zake zote anazopiga na anazopigiwa, utakuwa na uwezo wa kusoma meseji anazotuma na anazopigiwa, utakuwa na uwezo wa kuingia kwenye ‘inbox’ yake na kusoma meseji hata ambazo alitumiwa siku nyingi nyuma.

“Utaweza pia kuona anachokifanya kwenye mitandao yote kuanzia WhatsApp, Instagram na Facebook, ila nakuomba sana kaka...” alisema lakini nikamkatisha na kumwambia asiwe na wasiwasi nimemuelewa na nitafanyia kazi alichoniambia.

Nikamuita mhudumu na kumwambia amsikilize, muda mfupi baadaye, akaanza kugonga vitu vyake kwa fujo kama kawaida yake. Muda mfupi baadaye, Joel alinipigia simu, harakaharaka nikapokea na kumueleza sehemu nilipo, akaniambia anakuja na kweli dakika kadhaa baadaye, alikuwa ameshafika.

Tukajumuika wote watatu, stori zikawa zinapigwa huku wenzangu wakiendelea kulewa lakini mimi nikawa nakunywa maji tu. Kwa sababu nilikuwa na njaa, nilimuita mhudumu wa jikoni na kumuagiza chakula, wenzangu nao wakaagiza. Japokuwa Clarence aliniambia nisijishughulishe na simu kwa muda huo, bado nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujionea mwenyewe kwa macho yangu.

“Una matatizo gani Alex, jana hujaja kazini na leo pia,” aliniuliza Joel, nikashusha pumzi ndefu na kiukweli, ilibidi na yeye nimueleze ukweli, akashtuka sana kusikia kilichokuwa kinaendelea.

“Sasa kwa nini unakaa na mambo moyoni mwako Alex? Hujui kama ni makosa makubwa sana?”

“Mimi ni mwanaume Joel, siyo kila kinachotokea natakiwa kukizungumza kwa watu! Hata hapa nimeamua kuwaambia rafiki zangu kwa sababu naona kama maji yamefika shingoni,” nilisema, kila mtu akashusha pumzi ndefu na kutulia.

“Alex, wewe ni rafiki yangu wa siku nyingi, naweza kusema wewe ni ndugu yangu lakini kuna mambo unatia sana hasira, lazima nikwambie ukweli.”

“Mambo gani Joel!”

“Kwa nini unakuwa mnyonge kiasi hicho kwa mwanamke?”

“Sasa ulitaka nifanye nini Joel, nimpige? Nimfukuze au nimuue kabisa? Ulitaka nifanye nini?” nilisema kwa jazba kwa sababu niliona kama ananishushia heshima katika kipindi ambacho mwenzake nilikuwa nahitaji msaada.

“Hapana! Hata ukipaniki mimi nitakwambia ukweli tu, upende usipende! Unampenda sana Joanna kiasi kwamba mpaka imefika mahali unakuwa bwege! Na yeye anajua kwamba unampenda sana ndiyo maana anakuendesha anavyotaka!

“Inatakiwa ubadilike na umuoneshe kwamba kweli wewe ni mwanaume, tena mwanaume wa shoka siyo unalialia kila kukicha kwa sababu ya mapenzi, wanaume huwa wanachukua maamuzi ya kiume, siyo kulialia,” alisema Joel, safari hii naye kwa sauti ya juu akionesha kukolea kinywaji, ikawa ni kama tunagombana hivi.

Clarence ambaye naye alishakolea ulabu kama mwenzake, naye akawa anatuamulia lakini naye akionesha kuwa upande wa Joel, wakawa wananisimanga sana kwamba nimezidi kuwa mpole ndiyo maana mke wangu ananiendesha kama gari bovu.

Nilipoona kama wanazidi kunishambulia, ilibidi na mimi niagize pombe ili sasa tuwe kwenye levo moja.

Nilimuita mhudumu na muda mfupi baadaye, akaja! Nikamuagiza chupa ya Baccardi, kinywaji nilichokuwa nakipendelea sana. Muda mfupi baadaye, aliniletea, basi nikaanza kugida kwa fujo, stori zikaendelea na sasa hivi angalau tulikuwa tunaelewana kwa sababu wote tulikuwa tumelewa.

“Nifanye nini na mimi nampenda?”

“We bwege nini? Unaacha kumpenda mama yako aliyekuleta duniani unajifanya kumpenda shangingi wa mjini ambaye hata hujui alikotoke? Unakumbuka nilikukatalia sana kipindi kile wakati unataka kumuoa mwisho ukaishia kuniona mimi kuwa mbaya?” Joel alilitoa dukuduku lililokuwa ndani ya moyo wake.

Ujue pombe ina kawaida moja, unaweza kuwa unazungumza hivyohovyo kwa sababu umelewa lakini jambo la uhakika kabisa ni kwamba miongoni mwa utakayoyazungumza ukiwa umelewa, yapo ambayo ni ya ukweli kwa asilimia mia moja ambayo pengine usingeweza kuyasema kama ungekuwa na akili zako timamu.

Ni kweli kipindi ambacho nipo kwenye mipango ya ndoa, Joel alinipinga sana suala la mimi kumuoa Joanna na nakumbuka kuna kipindi kilifika mpaka tukanuniana kabisa lakini kama nilivyowahi kusema, mapenzi ni kama upofu, yakikukolea unakuwa hujielewi kabisa.

Kwa hiyo siku hiyo Joel alikuwa ameamua kunitolea uvivu, akaendelea kunipaka sana, akaniambia nimekuwa dhaifu kiasi kwamba nawadhalilisha wanaume wenzangu.

“Sisi wanaume tumeumbwa kuwa viongozi wa familia, lakini wewe mwenzetu unaongozwa na mkeo! Umekuwa mjinga mpaka unatia hasira, unatutia aibu wanaume wenzako.”

“Sasa nyie wote mna kazi ya kunisimanga tu hapa! Nikiwauliza nichukue hatua gani hamsemi, mnataka niwaeleweje?”

“Mrudishe Joanna kwao mpaka atakapotia akili kichwani! Akileta ujinga tafuta mwanamke mwingine wa kusihi naye, kwa nini mwanamke mmoja anakusumbua kichwa wakati wazee wetu walikuwa wanaweza kuishi na wanawake kibao na wote wakatulia?” alisema Joel, safari hii akionesha kukolea vibaya kwa pombe.

Mazungumzo yaliyofuatia baada ya hapo yalikuwa hayaeleweki tena, ikawa ni fujo za kilevi kwa kwenda mbele.

Nililewa sana lakini kwa sababu tulikuwa tukilewa, kula, kunywa na kufurahi, wala sikugundua kwamba nilikuwa nimelewa kwa kiasi gani mpaka kesho yake asubuhi, nilipozinduka na kujikuta nikiwa ndani kwangu nimelala kwenye kochi.

Sikuwa nakumbuka chochote kwamba nimefikaje na nilirudi saa ngapi. Jambo moja ambalo nilikuwa na uhakika nalo ni kwamba kwa kuwa nilikuwa na Joel na Clarence, kila kitu changu kitakuwa salama.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa, niliamcka kichovu na kukimbilia bafuni, baada ya kujimwagia maji mengi ya baridi akili zangu zilirudi kwenye hali yake ya kawaida na kidogo nikawa najitambua.

Kitu cha kwanza ilikuwa ni kumpigia simu Joel na kumuuliza kilichotokea, akaniambia tulilewa sana usiku uliopita na walinifikisha mpaka nyumbani kwangu kabla ya wao kuondoka na kuendelea na safari.

“Clarence imebidi alale kwangu kwa sababu yeye ndiyo alizima kabisa! Nipo kazini tayari.”

“Vipi hawajaniulizia?”

“Wanakuulizia sana, nimewaambia jana nilikuja kukuona na hali yako bado siyo nzuri, kila mtu anakupa pole.”

“Ooh! Ahsante sana ndugu yangu!” nilisema huku nikishusha pumzi ndefu kwa sababu alikuwa amenisaidia sana kutuliza hali ya mambo kule kazini.

“Upo sehemu nzuri tunaweza kuongea?”
“Yaah! Haina shida Alex.”

“Ni kuhusu ishu ya shemeji yako! Najua jana tulilewa na kuongea mambo mengi sana! Hebu nipe msimamo wa nini cha kufanya maana naona baada ya kuzungumza na nyie angalau nimeanza kupata mwanga ndani ya kichwa changu.”

“Nenda nyumbani kwao! Kazungumze na mama yake na umweleze mambo yote anayokufanyia na mwisho, mweleze kwamba huhitaji kuendelea kukaa naye kwa sasa! Atazipata salamu hizo kutoka kwa mama yake,” aliniambia Joel, ushauri ambao uliniingia vizuri sana ndani ya kichwa changu.
 
TEARS OF THE SOUL (MACHOZI YA ROHONI)- 4

Mtunzi: Aziz Hashim (Hash Power)

NB: UNAWEZA KUIPATA SIMULIZI HII TAMU KUANZIA MWANZO
MPAKA MWISHO KWA MFUMO WA e-Book (PDF)
UTAKAYOISOMA KWENYE SIMU YAKO KWA SH. 5000/= TU
NICHEKI WHATSAPP 0719401968!

ILIPOISHIA:
“Nenda nyumbani kwao! Kazungumze na mama yake na umweleze mambo yote anayokufanyia na mwisho, mweleze kwamba huhitaji kuendelea kukaa naye kwa sasa! Atazipata salamu hizo kutoka kwa mama yake,” aliniambia Joel, ushauri ambao uliniingia vizuri sana ndani ya kichwa changu.
SASA ENDELEA...

Nilijiandaa asubuhi hiyohiyo, baada ya kumaliza, nikiwa najiandaa kutoka, nilikumbuika kwamba tayari Clarence alikuwa amenirekebishia simu yangu na kuiunganisha na simu ya Joanna ili niwe na uwezo wa kuwa naona kila kinachoendelea kwenye simu yake.

Sijui ni nini kilichokuwa kimetokea kwenye moyo wangu lakini huwezi kuamini kwamba sikutaka kushughulika nayo kwa wakati huo. Niliona kama nitazidi kujichanganya kichwa kwa hiyo nikaachana nayo na safari ya kuelekea Magomeni, nyumbani kwa akina Joanna ilianza.

Nilimkuta mama yake akiwa nyumbani, tukasalimiana kwa uchangamfu huku na yeye akinishangaa kwa sababu kwa kawaida, asubuhi hiyo nilitakiwa niwe kazini. Sikutaka kupoteza muda, moja kwa moja nilienda kwenye hoja ya msingi, nikamweleza kila kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yangu na mwanaye Joanna.

Tofauti na mwanaye, mama yake Joanna alikuwa mpole na mstaarabu sana, usingeweza kuamini kwamba huyo ndiyo mama yake aliyemzaa. Alisikitika sana na kusema anashindwa kuelewa kwa nini Joanna anamdhalilisha kiasi hicho, muda huohuo akampigia simu na kumuweka ‘loud speaker’.

“Uko wapi?”

“Nyumbani kwangu, vipi kwani mbona unaniuliza kiukali hivyo mama?”

“Nyumbani kwako wapi?”

“Kinondoni! Kwani nina makazi mengine jamani?”

“Unajua usijifanye mjanja sana Jo! Nipo na mumeo hapa na anakusikia unachokisema! Una siku ya ngapi hujalala nyumbani kwako leo? Unaweza kuniambia uko wapi?”

“Mama nakuomba achana na huyo bwege!” alisema Joanna kisha akakata simu, huwezi kuamini, wala sikujisikia vibaya kama nilivyokuwa nikijisikia vibaya mwanzo. Masimango ya Joel na Clarence yalikuwa ni kama yameniamsha usingizini, nikaishia kucheka tu.

“Unaona anavyonidharau mama? Basi haina shida, nilitaka tu mwenyewe ujionee hali halisi na kwa hiki kilichotokea, mimi siwezi kuendelea kuishi naye.

Akitoka huko aliko, itabidi arudi tu hapa nyumbani au atachagua mwenyewe sehemu ya kuishi lakini simhitaji kwa sasa,” nilisema kwa sauti ambayo ilionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.

Mama yake alishindwa kujibu chochote zaidi ya kujiinamia, akionesha kuwa na mwazo mengi ndani ya kichwa chake. Hata wakati nikimuaga na kuondoka, alionesha kuwa ni kama amechanganyikiwa kabisa. Nilitoka na kurudi mpaka nyumbani kwangu huku moyoni nikijihisi ni kama nimeshusha mzigo mzito sana.

Nilipofika nyumbani, kazi ya kwanza ilikuwa ni kuanza kuondoa alama zote ambazo zinanikumbusha kuhusu Joanna! Nilijikuta nikipata nguvu ya ajabu ndani ya moyo wangu, nikabandua picha za ukutani ambazo tulikuwa tumepiga mimi na yeye, nikazikusanya zote na kuziweka kwenye pipa la taka.

Nilitoa vitu vyote ambavyo vilikuwa vinamhusu yeye pale sebuleni, nikahamia chumbani ambako nako nilikusanya kila kitu chake na kufungiakwenye kabati lake. Sikuacha kitu na nilitaka hata mwenyewe akija ajue kwamba mimi siyo yule bwege wake tena! Nilikusanya kila kitu, nikaacha vitu vinavyinihusu tu!

Nilifanya hivyo nyumba nzima, nilitoa kila kitu ambacho kilikuwa na uhusiano naye, baada ya hapo nikaenda kuchoma moto baadhi ya vitu, zikiwemo baadhi ya nguo na zawadi za hapa na pale alizowahi kuninunulia siku za mwanzo za mapenzi yetu, nikachoma moto na zile picha na kurudi ndani nikiwa mtu mwingine tofauti kabisa.

Baada ya kurudi ndani, angalau sasa nilikuwa najihisi kuwa mtu mpya kabisa maishani mwangu, nilienda tena kuoga, nikarudi na kujiandalia chakula kisha nikakaa sebuleni nikiwa natazama runinga. Ni hapo ndipo nilipopata mawazo ya kuingia kwenye ile ‘software’ ya kunisaidia kuiona simu yake.

Nilianza kwenye meseji, nilisoma zote, kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho, nikawa ni kama nimechokoza upya stress ndani ya kichwa changu, kuna wakati nilikuwa nikitetemeka kuliko kawaida, nikawa najiapiza kwamba naweza kuja kumdhuru vibaya sana Joanna.

Nikiwa katika hali hiyo ya kuchanganyikiwa, nilianza kumfowadia mama yake meseji zote alizokuwa akichati Joanna na huyo mwanaume wake ambaye eti kwenye simu yake ndiye aliyekuwa amemsevu kwa jina la ‘My Husband’, mimi nikiwa hata sijaseviwa, yaani ni namba tu.

Joanna alionesha kuwa kwenye mahaba mazito na mwanaume huyo na kwa jinsi ilivyoonesha, uhusiano wao ulikuwa na muda mrefu kidogo, walishafanya mambo mengi pamoja.

Muda mfupi baadaye, mama yake alinipigia simu, akaniuliza kuhusu meseji hizo, nikamwambia ni meseji za mwanaye Joanna anazowasiliana na huyo mwanaume wake wa nje, akaniuliza nimezipata wapi? Nikamjibu tu kwamba nina mbinu zangu zilizoniwezesha kuzipata lakini ni meseji za kweli kabisa.

Muda mfupi baada ya kukata simu, Joanna alianza kunipigia simu mfululizo. Sikutaka kupokea, iliita mara ya kwanza mpaka ikakatika, ikaita mara ya pili, mara ya tatu, ya nne na kuendelea! Sikutaka kabisa kupokea na kadiri alivyokuwa anazidi kupiga, ndivyo hasira zilivyokuwa zinazidi kuongezeka kwenye moyo wangu.

“Unasemaje wewe mbwa!”

“We usiniite mimi mbwa! Hukunizaa wewe.”

“Wewe ni mbwa tu Joanna! Mbwa!” nilisema na kukata simu kwa hasira, akapiga tena, nikawa nakata, akipiga nakata na kwa hasira niliamua kuizima kabisa. Nilikuwa na jazba kali sana ndani ya moyo wangu.

Kuna wakati nilijuta kwa nini sikusikiliza ushauri wa Clarence na kuachana na mambo ya kufuatilia simu ya Joanna kwa sababu mambo niliyoyaona yalinichoma mno roho yangu. Sijui kama katika historia ya maisha yangu nimewahi kuumia kiasi hicho.

Kulikuwa na meseji nyingi ambazo Joanna alikuwa akimshukuru huyo bwanaake kwa penzi zuri alilompa. Kwa jinsi meseji zilivyokuwa nyingi, ilionesha kwamba kumbe karibu kila siku walikuwa wakikutana na kufanya yao.

Nilijaribu kuvuta kumbukumbu zangu nyuma, nikagundua kwamba kwa karibu kipindi cha kama miezi sita hivi iliyopita, Joanna hakuwa na mpango na mimi kabisa linapokuja suala la tendo. Kila nilipokuwa nikimhitaji faragha, alikuwa haishi visingizio.

Mara atakwambia amechoka, mara atakwambia tumbo linamuuma, siku nyingine hata hasemi kitu unamkuta amenuna tu akiwa hataki kabisa mawasiliano na mimi! Hata katika zile siku ambazo nilikuwa namfosi sana na kuamua kunipa haki yangu, haikuwa kama ilivyokuwa mwanzo.

Alikuwa ni kama anatimiza wajibu tu, yale mapenzi motomoto yaliyokuwepo mwanzo, zile ‘mbilingembilinge’ za kwenye uwanja wa fundi seremala, hazikuwepo tena! Alikuwa anafanya kutimiza wajibu tu na inaweza kupita hata wiki mbili au tatu ndiyo ananipa haki yangu mara moja.

Awali jambo hilo liliniumiza sana kichwa changu, kuna kipindi mpaka niliwaza kwamba labda nitafute ‘mchepuko’ ambaye atakuwa anakidhi haja za moyo wangu lakini kila nilipokuwa nafikiria kumsaliti, nilikuwa najiona kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wangu hivyo kuishia kuvumilia ndani kwa ndani, nikiamini ipo siku mambo yatakuwa kama zamani. Kumbe nilikuwa najidanganya, tena uongo mtakatifu. Joanna hakuwa na taimu na mimi kwa sababu alikuwepo mtu aliyekuwa anamchanganya kichwa chake.

Na hili linapaswa kuwa fundisho kwa wanaume wote, unapoona mkeo anaanza kukuletea visingizio visivyo na kichwa wala miguu kwenye suala zima la unyumba, lazima kengele ya hatari ilie ndani ya kichwa chako.

Wapo baadhi ambao huwa wanakuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa sababu mbalimbali, pengine za kiafya na kadhalika lakini kwa asilimua kubwa, mwanamke anapoanza kuchepuka, huwa anapoteza kabisa msisimko kwa mumewe na hapo ndipo visababu visivyo na kichwa wala miguu vinapoanza.

Nilijiona mjinga sana kwa kushindwa kulishtukia jambo hilo mapema na kiukweli, narudia tena kusema hakuna siku ambayo niliumia kama hiyo. Pengine Joanna angekuwa karibu yangu, ningeweza kufanya jambo ambalo lingeushangaza ulimwengu mzima.

Haiwezekani mtu namgharamia kwa kila kitu, kuanzia kula, mavazi, mahitaji ya msingi, akiumwa mimi ndiyo nahangaika naye hospitalini lakini kumbe wakati mimi nikijitoa kwa moyo wangu wote, asali anarina mtu mwingine kwenye mzinga wangu! Ilikuwa ni ukatili wa hali ya juu.

Nimwahi kusema na nasisitiza tena kwamba unapoona mwanaume anafikia hatua ya kufanya ukatili wa kutisha kwa mkewe, tusikimbilie kuhukumu tu kwamba wanaume siku hizi wamekuwa wakatili! Fuatilia nini kilichosababisha, pengine ukijua sababu, unaweza kuwa na mtazamo tofauti kwamba ukatili wa wanaume unaongezeka kwa sababu ya ukatili wa wake zao.

Niliendelea kuwaza kwa muda mrefu, kichwa changu kikiwa kimevurugika kabisa, mwili wote ukiwa umekufa ganzi. Nilijikuta nikimchukia mno Joanna na kiukweli nilijiapiza kwamba kamwe siwezi kuja kuendelea naye tena maishani mwangu.

Baada ya kukaa kwa muda mrefu pale sebuleni, nikiwa ni kama sanamu, niliichukua simu yangu na kuiwasha tena. Ukweli uliokuwa mbele yangu ulikuwa mchungu sana lakini sikuwa na namna zaidi ya kuukubali. Wanasema ni bora ukweli mchungu kuliko uongo mtamu.

Nilipowasha tu simu, meseji mfululizo zilianza kuingia kwenye simu yangu. Zote zilikuwa zinatoka kwa Joanna na huwezi kuamini, safari hii alikuwa akinivurumishia matusi ya nguoni. Alinitukana sana kwenye meseji, yaani mpaka mambo mengi unajiuliza mara mbilimbili, hivi huyu ni mke wangu au kitu gani?

Alifikia hatua ya kuanza mpaka kunidhalilisha kuhusu uanaume wangu. Akaniambia mimi si lolote si chochote na anajuta sana kuolewa na mtu kama mimi. Akaniambia ameipata furaha ya moyo wake kwa hiyo hajutii kwa chochote, hata kama nimeamua kwenda kumharibia kwa wazazi wake, hajali chochote na kamwe hatarudi nyuma.

Sikumjibu meseji hata moja, akaanza tena kupiga lakini sikutaka kupokea, nilipoona anazidi kunisumbua, niliiblock namba yake. Nilikuwa nahitaji utulivu wa akili yangu kwa sababu tulikokuwa tunaelekea, kamwe hakukuwa kuzuri hata kidogo.

Basi niliendelea kufuatilia mawasiliano yake, nikaingia WhatsApp ambako huko ndiyo nilichoka kabisa. Kulikuwa na picha nyingi za ajabuajabu, mke wangu akimtumia huyo mwanaume wake, akiwa mtupu kabisa, na huyo mwanaume naye akimtumia za kwake.

Hebu vuta picha, anajifungia ndani ya nyumba yangu, juu ya kitanda changu, anajipiga picha za utupu tena kwa kutumia simu ya gharama ambayo mimi ndiyo nimemnunulia kisha anamtumia mwanaume mwingine! Unaweza kupata picha halisi ya hali niliyokuwa nayo.

Katika kupekuapekua, nilikutana pia na picha nyingine ambazo walipiga wakiwa wawili, tena watupu kabisa. Kilichoniumiza moyo zaidi ni kwamba kuna picha nyingine zilikuwa zimepigwa humohumo chumbani kwangu. Kwa hiyo kumbe mbali na uchafu wote aliokuwa ananifanyia, alikuwa pia akimuingiza huyo mwanaume wake humohumo ndani kwangu na kufanya naye uchafu juu ya kitanda changu!

Haya mambo yasikie tu kwa mwenzako, usiombe yakukute, yanaumiza mno moyo kiasi kwamba kama una roho nyepesi, unaweza hata kuchukua kamba na kujinyonga. Katika kupitapita pia, niligundua kwamba walikuwa wakitumiana picha za nyumba ambayo ilikuwa inaendelea kujengwa.

Sikuwahi kusikia hata siku moja kwamba mke wangu alikuwa anajenga nyumba lakini huwezi kuamini, alikuwa akiwasiliana na huyo mwanaume wake eti wakawa wanapanga kwamba nyumba hiyo ikikamilika, ndiyo watakapohamia na kuyaanzisha maisha yao mapya.

Kengele ya hatari ililia tena ndani ya kichwa changu. Joanna hakuwa akifanya kazi yoyote na yale maelezo waliyokuwa wakitumiana, ilionesha kwamba yeye ndiye aliyekuwa akigharamia ujenzi huo, swali likawa ni je, anapata wapi fedha za kufanyia hayo anayoyafanya?

Mimi na yeye hatukuwa tumejenga bali tulinunua kiwanja Bunju na tulichokuwa tumekubaliana ni kwamba niombe mkopo mkubwa kazini ili mwezi Desemba ukifika, mwezi ambao kwa kawaida huwa naenda likizo, tukaanze ujenzi wa nyumba yetu.

Tulichokuwa tumepanga kabla mambo hayajaanza kwenda mrama, ni kwamba siku tutakapoanza kujenga, itakuwa ni non-stop mpaka nyumba iishe. Tayari mkopo nilishachukua kazini miezi mingi tu nyuma na nilimshirikisha kwa kila hatua, kwa hiyo tulichokuwa tunakisubiri, ilikuwa ni muda wa mimi kuchukua likizo tu ili tukamilishe malengo yetu.

Mkopo wenyewe niliochukua, haukuwa wa kitoto. Nilikopa shilingi milioni hamsini ambazo kwa mahesabu yake, kutokana na mshahara niliokuwa napata, ningekatwa kwa karibu miaka mitatu na nusu ili kuumaliza. Sikuona kama ni tatizo kwa sababu hata kama nakatwa mshahara kazini, lakini si tayari nitakuwa nimehamia kwangu na kufanya jambo kubwa?

Ni hapo ndipo nilipopata wazo la kwenda kuangalia fedha zangu benki. Niliinuka harakaharaka na kwenda chumbani kwangu, nikafungua kwenye droo ambayo kadi yangu ya benki huwa inakaa! HAIKUWEPO!

Nilipekua huku na kule, wala haikuwepo! Nilishtuka almanusra nianguke na kupoteza fahamu! Kadi yangu iko wapi? Sikuwa na majibu. Kwa bahati nzuri, nilikuwa nimejiunga na huduma ya Sim-banking, ambayo inakuwezesha kufanya miamala ya kibenki kwa kupitia simu yako.

Harakaharaka nikaingia na kuangalia salio. Lahaula, kati ya shilingi milioni hamsini nilizokuwa nimeingiziwa benki baada ya kupewa mkopo wangu miezi kadhaa nyuma, kulikuwa kumebakia shilingi milioni mbili tu. Nilijikuta nikishikwa na tumbo la kuendesha ghafla, nikakimbilia maliwatoni huku nikiwa ni kama siamini.

Nilikaa kwa muda mrefu, baadaye nilipotoka, nilijiandaa harakaharaka na lengo langu lilikuwa ni kwenda benki kuhakiki kama nilichokiona ndicho kilichokuwa kimetokea. Mwili haukuwa na nguvu kabisa lakini ilibidi nijilazimishe, ilikuwa nilazima niujue ukweli tena haraka iwezekanavyo.
 
TEARS OF THE SOUL (MACHOZI YA ROHONI)- 5

Mtunzi: Aziz Hashim (Hash Power)

NB: UNAWEZA KUIPATA SIMULIZI HII TAMU KUANZIA MWANZO
MPAKA MWISHO KWA MFUMO WA e-Book (PDF)
UTAKAYOISOMA KWENYE SIMU YAKO KWA SH. 5000/= TU
NICHEKI WHATSAPP 0719401968!

ILIPOISHIA

Nilichukua Bajaj na kumuelekeza dereva kunipeleka Mnazi Mmoja kwenye tawi kubwa la benki niliyokuwa nikiitumia. Njia nzima akili zangu zilikuwa ni kama zimepigwa na shoti ya umeme. Hatimaye nilifika, moja kwa moja nikaomba kuonana na meneja na kwa bahati nzuri ni kwamba hakukuwa na mlolongo wowote mrefu.

Nilipoingia ofisini kwake, nilitaka anieleze imekuwaje katika fedha zangu zilizokuwa benki, zibaki shilingi milioni mbili tu wakati sikuwahi hata siku moja kwenda kutoa fedha? Uzuri ni kwamba teknolojia huwa haidanganyi, alinitaka nisubiri kidogo, akaanza kubofyabofya kompyuta yake kisha nikamsikia akimpigia simu mtu wa upande wa pili na kumpa maelezo ya nini cha kufanya.

Muda mfupi baadaye, aliniita na kunitaka nitazame kwenye kompyuta yake.

“Huyu unamjua?” aliniuliza huku akinionesha picha ya video ya mtu akitoa fedha kwenye ATM, alikuwa ni Joanna.

“Ndiyo! Ni mke wangu!”

“Na huyu mwingine naye unamjua?” alisema huku akinioneshea picha nyingine, niliitambua haraka kwamba ndiyo yule mwanaume ambaye nimekuta picha zake akiwa na mke wangu kwenye simu, nikatingisha kichwa kuonesha kwamba namjua.

Akaniambia ekodi zao zinaonesha kwamba hao wawili ndiyo waliokuwa wakitoa fedha benki kwa kutumia kadi ya ATM, siyo kadi bandia, kadi yangu! Alinionesha rekodi zote kuanzia siku walipoanza kutoa kwa mara ya kwanza na kiwango walichotoa, akawa ananionesha kwa ushahidi wa picha za video kila kitu na mara ya mwisho kwenda kutoa fedha, ilikuwa ni jana yake tu.

Hata sikumbuki niliondokaje pale benki, nilikuja kujikuta nikiwa nikiwa barabarani, magari yakinipigia honi kwa nguvu, nikashtuka kugundua kwamba kumbe nilikuwa nikitembea katikati ya barabara huku nikiwa sijitambui kabisa.

“Utagongwa broo, ina maana magari huyaoni,” alisema mwanaume mmoja huku akinishika mkono na kunivusha upande wa pili wa barabara, ilibidi nikae chini kwa sababu nilikuwa hata sielewi ni nini kinachoendelea.

“Vipi kwani?”

“Nashukuru kwa msaada wako, unaweza kuniitia Bajaj tafadhali,” nilimwambia yule msamaria mwema ambaye alinikazia macho kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa chake kuonesha kusikitika. Japo alikuwa hajui chochote kinachoendelea, nadhani hali aliyoniona nayo ilimfanya aelewe kwamba nipo kwenye matatizo makubwa sana.

Machozi yalikuwa yananitoka huku mwenyewe hata nikiwa sina habari. Macho yangu yalikuwa mekundu sana na kuna donge kubwa sana lilikuwa limenikaba kooni kiasi cha kunifanya niwe kama mwendawazimu kabisa. Sijawahi kutamani kuyakatisha maisha yangu lakini huwezi kuamini, siku hiyo nilitamani kujiua! Nilitamani kuyakatisha maisha yangu ili kuepukana na aibu kubwa iliyokuwa mbele yangu.

Muda mfupi baadaye, yule msamaria mwema aliniitia Bajaj, akaniuliza ninapoelekea, nikamtajia na akanisaidia kuniinua na kunipakiza kwenye Bajaj, nikaondoka eneo hilo huku nikiwa bado hata sijielewi. Sikuwa najua hapo ni wapi na nimetokaje kule benki na nilikuwa naelekea wapi, nikaegamia kwenye siti ya Bajaj huku machozi yakizidi kunimwagika kwa wingi.

Safari iliendelea na baadaye, sauti ya yule dereva wa Bajaj ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye ile hali.

“Unashukia Kinondoni ipi broo!”

Aliposema hivyo, niliinua kichwa na kutazama nje, nikagundua kwamba tayari tulishafika Kinondoni, nikashangaaje nimefika bila mwenyewe kujielewa? Nilimuelekeza sehemu ya kuingia, kweli akanipeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwangu.

Nikateremka na kuingiza mkono mfukoni kwa lengo la kutaka kumlipa yule dereva wa Bajaj lakini akaniambia tayari alishalipwa na yule mtu aliyenipakiza. Nikamshukuru sana na kumuuliza kama anamfahamu.

“Ndiyo! Ukifika pale kijiweni ulizia tu Ustaadh, ni mtu poa sana kila mmoja anamfahamu,” aliniambia, nikamshukuru huku nikijitahidi kuliingiza kichwani jina hilo kwani alikuwa amenisaidia sana na siku zote huwa napenda sana kumshukuru mtu akinisaidia.

Niliingia ndani huku nikijihisi kuchanganyikiwa kabisa. Nilianza kukitazama kila kitu utafikiri ndiyo nilikuwa naingia kwa mara ya kwanza kwenye nyumba hiyo.

Japokuwa kufuatilia meseji za Joanna kulinisababishia maumivu makali sana yasiyoelezeka ndani ya moyo wangu, lakini nilikuwa nimejua kitu kikubwa sana ambacho pengine nisingekuja kukijua maishani mwangu kama nisingechukua uamuzi huo.

Nilienda kukaa kwenye sofa na kutoa simu yangu, kwa mara nyingine nikaamua kurudi kuanza kuchunguza kwa makini kuhusu ile nyumba. Nilifuatilia meseji moja baada ya nyingine walizokuwa wakitumiana WhatsApp kuhusu nyumba hiyo.

Nilishtuka zaidi baada ya kugundua kwamba kumbe Joanna alivyokuwa hana akili kichwani, hata hati zote zilizokuwa zinahusu kiwanja na nyumba, zilikuwa zimeandikwa kwa jina la mwanaume.

Nadhani yeye alifanya hivyo akiwa anajua kwamba ananikomoa lakini akili za haraka zilinituma kuamini kwamba kuna mchezo mwingine ulikuwa ukichezeka, yaani mchezo juu ya mchezo!

Niligundua mambo mengi sana siku hiyo na kiukweli, nilishinda nikiwa kama mgonjwa kabisa, nilikuja kuchangamka jioni baada ya Joel kunipigia simu na kuniuliza mahali nilipo. Nikamwambia kwamba nipo nyumbani, akataka eti tukajichanganye tena kwenye starehe kama jana yake, wazo ambalo nililikataa.

“Basi nakuja hapo nyumbani, si upo mwenyewe?” aliniuliza, nikamjibu kisha nikakata simu. Ile kusikia kwamba Joel anakuja, ndiyo angalau nikapata nguvu ya kuamka na kwenda bafuni kuoga, kisha nikajiweka vizuri na kuwasha runinga pale sebuleni. Sikutaka anikute nikiwa nimepooza kwa hiyo nikajitahidi kuchangamka.

Kweli muda mfupi baadaye, Joel aliwasili, nikaenda kumfungulia mlango na kama kawaida tukaanza kupiga stori za hapa na pale zilizonifanya nichangamke baada ya muda mfupi tu.

Alikuwa amekuja na pombe za kizungu kwenye mfuko, nadhani kwa sababu nilimwambia kwamba sitaki kutoka, aliamua kuja tunywee nyumbani. Basi tuliendelea kupiga stori huku tukiwa tumeweka muziki kwenye runinga, sikuwa nimepanga kulewa siku hiyo lakini nilijikuta tu na mimi nikianza kunywa.

Joel alikuwa mjanja sana, hakutaka kuniuliza chochote mwanzo kumhusu Joanna, nadhani alikuwa anataka nichangamke kwanza ndiyo aanze kuniuliza. Kwa hilo alishinda, nilipoanza kukolea kichwani, aliingizia hizo mada. Mwanzo sikutaka kumweleza chochote lakini akanisihi sana nisimfiche, ikabidi nianze kumweleza.

Nilimwambia kuhusu ile ‘software’ niliyokuwa nimepewa na Clarence na jinsi nilivyofanikiwa kudukua simu ya Joanna na yote niliyokutana nayo. Alisikitika sana na kuniambia kwamba nilikuwa nimekosea sana kufuatilia mawasiliano ya Joanna.

“Ungeweza tu kuchukua uamuzi wa kumrudisha kwao, ilikuwa inatosha kabisa! Hawa wanawake ukisema uwafuatilie utaishia kuumia tu moyo wako. Wapo watu wanajiua kwa sababu ya wake zao.”

“Ni kweli unachokisema lakini ilikuwa ni lazima nifanye hivyo ili hata nikiamua kumuacha, niwe na ushahidi wa kutosha! Mjanja wa maneno sana yule mwanamke, angeweza kuja kunigeuka baadaye,” nilimwambia Joel, akainua glasi na kupiga funda kubwa la pombe na kuirudisha glasi mezani, akanitazama bila kusema chochote, na mimi nikamtazama.

Nilijua alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua nimegundua nini baada ya kufuatilia mawasiliano yake, nikamtolea simu na kufungua picha moja ya WhatsApp ambayo ilikuwa inawaonesha mke wangu Joanna akiwa amekumbatiana na huyo mwanaume, wakiwa kama walivyozaliwa, tena chumbani kwangu.

Joel aliitazama ile picha kwa mshtuko akiwa ni kama haamini alichokuwa anakiona, akanitazama kwa mshtuko na kuendelea kuitazama ile picha.

“Huyu dogo namjua mbona! Namjua vizuri sana na hata wewe unamjua! Si Derrick huyu, huwa tunafupisha na kumuita Rick!” alisema, ikabidi nikae pale kwenye kiti vizuri na kumsikiliza kwa makini.

Alichokuwa anakisema kilikuwa kikiunga kabisa kwa sababu mara kadhaa Joanna alikuwa akimuita kwa jina la Rick, sikuwa najua kwamba kumbe ni kifupisho cha jina la Derrick, nikawa na shauku kubwa ya kutaka kumjua huyo Rick ni nani.

“Huyu dogo ni mjanja mjanja sana wa mjini! Yaani ni tapeli mzoefu sana! Shemeji yangu amekutana wapi na mhuni kama huyu?” alisema Derrick na kunifanya nimtazame kwa udadisi nikitaka kumjua vizuri huyo Derrick.

Alinieleza mambo mengi, yakiwemo matukio aliyokuwa akiyafanya kijana huyo, akaniambia kwamba anamfahamu vizuri sana kwa sababu amewahi kumtapeli rafiki yake mmoja baada ya kumuuzia gari la mtu mwingine kwa kutumia kadi bandia.

Akaendelea kunieleza matukio kibao waliyoenda kukutana nayo walipompeleka polisi ambapo ilibainika kwamba alikuwa na kesi nyingine nyingi za aina hiyo kiasi kwamba hata polisi wenyewe walikuwa wanamfahamu.

“Wala hata usiumie Alex, shem anachokitaka atakipata sasa hivi! Niamini kamwambia atarudi kwako kwa magoti, huyu anacheza na akili zake tu, yupo kimaslahi zaidi na nakuomba sana kuwa makini na mali zenu mlizochuma pamoja, huyu mwendawazimu anaweza hata kuja kuuza hii nyumba mliyopanga! Hafai hata kidogo,” alisema Joel, akawa ni kama amenitonesha donda kwenye moyo wangu.

Ilibidi nimueleze kuhusu nilichoenda kukutana nacho benki baada ya kugundua kwamba Joanna kwa kushirikiana na huyo mwanaume wake walikuwa wamekomba karibu milioni arobaini na nane, ambazo tulikuwa tumepanga na Joanna kwamba zitatumika kujenga nyumba yetu ili angalau na sisi tuwe na kwetu.

Alisikitika sana na akaniambia yeye anajua mbinu za kumkomoa ili hizo fedha zirudi lakini kikwazo ni kwamba Joanna hawezi kukubali kwa wakati huo na tutasababisha matatizo makubwa zaidi kwa sababu atahisi tunayafanya haya si kwa lengo la kumsaidia bali kwa wivu wa kimapenzi.

“Sikia Alex, najua shilingi milioni hamsini ni fedha nyingi sana usawa huu! Nyingi kwelikweli lakini hazina thamani kuzidi uhai wangu.”

“Huyu dogo kwanza ni mchafu sana kwa wanawake, anaweza kuwa hata ameathirika! Sasa utakubali upoteze maisha yako kizembe kwa sababu ya kumpigania mwanamke asiye na akili?”

Mambo aliyonieleza Joel yalikuwa mazito sana na akanisisitiza kwamba hata ikitokea kama matatizo yote yameisha, kabla sijamsamehe Joanna lazima kwanza tukapime virusi vya Ukimwi.

‘Siwezi kumsamehe hata kidogo.”

‘Usiseme hivyo Alex! Mimi ndiyo nakujua! Unakumbuka kipindi unataka kumuoa ilifika mahali mpaka ukawa unanichukia?”

“Hayo si tushayamaliza ndugu yangu?” ilibidi nimkatishe Joel kwa sababu ni kweli ule usemi wa wahenga kwamba asiyesikia la mkuu huvunjika guu, ulikuwa unajidhihirisha kabisa kwangu.

Joel alikuwa mtu wa kwanza kunigomea kabisa nilipomwambia kwamba nataka kumuoa Joanna na alichoniambia ni kwamba kama nampenda sana, abaki kuwa mpenzi wangu tu lakini siyo mke, tukasumbuana sana mpaka kufikia hatua ya kukasirikiana, baadaye akaamua kuniunga mkono kwa shingo upande.

“Ulikuwa unajua nini mwanzo mpaka ukawa mkali sana nilipokwambia kuhusu suala la mimi kutaka kumuoa Joanna?”

“Namjua vizuri Joanna! Anyway hayo tutazungumza siku nyingine, kwa sasa tushughulikie hili lililopo mbele yetu,” aliniambia Joel na kuendelea kunisisitiza kwamba sitakiwi kuumia au kulalamika sana kwa sababu siwezi kujua ni nini Mungu ameniepusha kwa Joanna.

“Fedha zinatafutwa wala usijali! Ipo siku utapata nyingi zaidi ya hizo, mbona mambo ya kawaida kabisa hayo?” aliniambia.

Kiukweli ujio wake ulikuwa wa faraja kubwa sana ndani ya moyo wangu kwa sababu kiukweli kitendo cha Joanna kuchukua fedha zote na kwenda kuzitumia na mwanaume mwingine, kilikuwa kimenichanganya sana kichwa changu.

Kilikuwa ni kiasi kikubwa sana cha fedha ambacho hata kama ningeamua kutenga robo yake tu nikaenda kubadilisha maisha ya wazazi wangu kule kijijini, pengine wangenishukuru na kunipa baraka kubwa sana maishani mwangu, lakini upofu wa penzi la Joanna ulikuwa umenipotezea mwelekeo kisawasawa.

Ni hapo nilipoanza kukumbuka suala jingine ambalo lilizidi kuniongezea uchungu kwenye moyo wangu. Wakati naanza kazi tu, nilikuwa na utaratibu kwamba kila ninapopokea mshahara, natenga robo nzima ya mshahara wangu na kuwatumia wazazi wangu kijijini.

Ukweli ni kwamba nilikuwa nimetokea kwenye familia ya kimaskini na najua mwenyewe ni kwa kiasi gani wazazi wangu walihangaika kunisomesha mpaka nikapata kazi kwa hiyo jukumu la kuwasaidia lilikuwa la kwangu. Hata hivyo, baada tu ya kuanzana na Joanna na kuanza kuwa namshirikisha mambo yangu, alianza kuonesha hali isiyokuwa ya kawaida.

Hakuwa akitaka kabisa niwatumie wazazi fedha, akawa ananiambia kwamba kama nikiendekeza kuwa natoa fedha nyingi kuwapa, itafika mahali nitashindwa hata kujijenga kimaisha na siku ikitokea nimefukuzwa kazi, ni wazazi haohao watakaokuwa mstari wa mbele kunisimanga kwa kushindwa kujipangilia vizuri kimaisha.

Maneno yake wala hayakuwa yakiniingia akilini na baadaye nikaamua kuacha kumshirikisha mambo ya wazazi wangu, ikawa hata nikipata mshahara nawatumia kimyakimya bila kumwambia lakini baadaye tulipokuja kuoana, akawa ananifuatilia kwa karibu kutaka kujua kila shilingi la mshahara wangu imefanyia nini.

Kila alipokuwa akigundua kwamba nimewatumia fedha, alikuwa akikasirika na kuninunia sana, ikafika mahali nikaona kwa nini kila siku tuwe tunagombana kwa sababu moja? Nilikuwa nampenda sana kuliko maelezo kwa hiyo nikajikuta nikianza kukata mawasiliano na wazazi na mpaka wakati huo, kiukweli sikuwa na maelewano kabisa na baba na mama.

Walikuwa wakilalamika sana kwamba starehe za mjini zimenifanya niwasahau wao pamoja na wadogo zangu na japokuwa lawama zao zilikuwa zinanichoma sana moyo wangu, niliamua kuweka pamba masikioni na kumsikiliza Joanna ambaye leo hii ndiyo alikuwa akinisababishia maumivu makali kiasi hicho.

“Unawaza nini?”

“Aah! Kuna jambo lilikuwa linapita akilini mwangu.”

“Vipi?”

“Ujue kwa muda mrefu sina mawasiliano mazuri na baba na mama huko bush, inawezekana manung’uniko yao ndiyo yanayonisababishia haya yote,” nilimwambia Joel, akanishangaa sana na kiukweli hata mimi mwenyewe nilijiona kuwa mjinga sana.

Itaendelea next issue...
Depal
yna2
moneytalk
 
Thanks mwaya
 
niko hapa mkuu,unapotea sana bana
 
SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA:
“Una matatizo gani Alex, jana hujaja kazini na leo pia,” aliniuliza Joel, nikashusha pumzi ndefu na kiukweli, ilibidi na yeye nimueleze ukweli, akashtuka sana kusikia kilichokuwa kinaendelea.
SASA ENDELEA...
“Sasa kwa nini unakaa na mambo moyoni mwako Alex? Hujui kama ni makosa makubwa sana?”
“Mimi ni mwanaume Joel, siyo kila kinachotokea natakiwa kukizungumza kwa watu! Hata hapa nimeamua kuwaambia rafiki zangu kwa sababu naona kama maji yamefika shingoni,” nilisema, kila mtu akashusha pumzi ndefu na kutulia.
“Alex, wewe ni rafiki yangu wa siku nyingi, naweza kusema wewe ni ndugu yangu lakini kuna mambo unatia sana hasira, lazima nikwambie ukweli.”
“Mambo gani Joel!”
“Kwa nini unakuwa mnyonge kiasi hicho kwa mwanamke?”
“Sasa ulitaka nifanye nini Joel, nimpige? Nimfukuze au nimuue kabisa? Ulitaka nifanye nini?” nilisema kwa jazba kwa sababu niliona kama ananishushia heshima katika kipindi ambacho mwenzake nilikuwa nahitaji msaada.
“Hapana! Hata ukipaniki mimi nitakwambia ukweli tu, upende usipende! Unampenda sana Joanna kiasi kwamba mpaka imefika mahali unakuwa bwege! Na yeye anajua kwamba unampenda sana ndiyo maana anakuendesha anavyotaka!
“Inatakiwa ubadilike na umuoneshe kwamba kweli wewe ni mwanaume, tena mwanaume wa shoka siyo unalialia kila kukicha kwa sababu ya mapenzi, wanaume huwa wanachukua maamuzi ya kiume, siyo kulialia,” alisema Joel, safari hii naye kwa sauti ya juu akionesha kukolea kinywaji, ikawa ni kama tunagombana hivi.
Clarence ambaye naye alishakolea ulabu kama mwenzake, naye akawa anatuamulia lakini naye akionesha kuwa upande wa Joel, wakawa wananisimanga sana kwamba nimezidi kuwa mpole ndiyo maana mke wangu ananiendesha kama gari bovu.
Nilipoona kama wanazidi kunishambulia, ilibidi na mimi niagize pombe ili sasa tuwe kwenye levo moja.
Nilimuita mhudumu na muda mfupi baadaye, akaja! Nikamuagiza chupa ya Baccardi, kinywaji nilichokuwa nakipendelea sana. Muda mfupi baadaye, aliniletea, basi nikaanza kugida kwa fujo, stori zikaendelea na sasa hivi angalau tulikuwa tunaelewana kwa sababu wote tulikuwa tumelewa.
“Nifanye nini na mimi nampenda?”
“We bwege nini? Unaacha kumpenda mama yako aliyekuleta duniani unajifanya kumpenda shangingi wa mjini ambaye hata hujui alikotoke? Unakumbuka nilikukatalia sana kipindi kile wakati unataka kumuoa mwisho ukaishia kuniona mimi kuwa mbaya?” Joel alilitoa dukuduku lililokuwa ndani ya moyo wake.
Ujue pombe ina kawaida moja, unaweza kuwa unazungumza hivyohovyo kwa sababu umelewa lakini jambo la uhakika kabisa ni kwamba miongoni mwa utakayoyazungumza ukiwa umelewa, yapo ambayo ni ya ukweli kwa asilimia mia moja ambayo pengine usingeweza kuyasema kama ungekuwa na akili zako timamu.
Ni kweli kipindi ambacho nipo kwenye mipango ya ndoa, Joel alinipinga sana suala la mimi kumuoa Joanna na nakumbuka kuna kipindi kilifika mpaka tukanuniana kabisa lakini kama nilivyowahi kusema, mapenzi ni kama upofu, yakikukolea unakuwa hujielewi kabisa.
Kwa hiyo siku hiyo Joel alikuwa ameamua kunitolea uvivu, akaendelea kunipaka sana, akaniambia nimekuwa dhaifu kiasi kwamba nawadhalilisha wanaume wenzangu.
“Sisi wanaume tumeumbwa kuwa viongozi wa familia, lakini wewe mwenzetu unaongozwa na mkeo! Umekuwa mjinga mpaka unatia hasira, unatutia aibu wanaume wenzako.”
“Sasa nyie wote mna kazi ya kunisimanga tu hapa! Nikiwauliza nichukue hatua gani hamsemi, mnataka niwaeleweje?”
“Mrudishe Joanna kwao mpaka atakapotia akili kichwani! Akileta ujinga tafuta mwanamke mwingine wa kusihi naye, kwa nini mwanamke mmoja anakusumbua kichwa wakati wazee wetu walikuwa wanaweza kuishi na wanawake kibao na wote wakatulia?” alisema Joel, safari hii akionesha kukolea vibaya kwa pombe.
Mazungumzo yaliyofuatia baada ya hapo yalikuwa hayaeleweki tena, ikawa ni fujo za kilevi kwa kwenda mbele.
Nililewa sana lakini kwa sababu tulikuwa tukilewa, kula, kunywa na kufurahi, wala sikugundua kwamba nilikuwa nimelewa kwa kiasi gani mpaka kesho yake asubuhi, nilipozinduka na kujikuta nikiwa ndani kwangu nimelala kwenye kochi.
Sikuwa nakumbuka chochote kwamba nimefikaje na nilirudi saa ngapi. Jambo moja ambalo nilikuwa na uhakika nalo ni kwamba kwa kuwa nilikuwa na Joel na Clarence, kila kitu changu kitakuwa salama.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, niliamcka kichovu na kukimbilia bafuni, baada ya kujimwagia maji mengi ya baridi akili zangu zilirudi kwenye hali yake ya kawaida na kidogo nikawa najitambua.
Kitu cha kwanza ilikuwa ni kumpigia simu Joel na kumuuliza kilichotokea, akaniambia tulilewa sana usiku uliopita na walinifikisha mpaka nyumbani kwangu kabla ya wao kuondoka na kuendelea na safari.
“Clarence imebidi alale kwangu kwa sababu yeye ndiyo alizima kabisa! Nipo kazini tayari.”
“Vipi hawajaniulizia?”
“Wanakuulizia sana, nimewaambia jana nilikuja kukuona na hali yako bado siyo nzuri, kila mtu anakupa pole.”
“Ooh! Ahsante sana ndugu yangu!” nilisema huku nikishusha pumzi ndefu kwa sababu alikuwa amenisaidia sana kutuliza hali ya mambo kule kazini.
“Upo sehemu nzuri tunaweza kuongea?”
“Yaah! Haina shida Alex.”
“Ni kuhusu ishu ya shemeji yako! Najua jana tulilewa na kuongea mambo mengi sana! Hebu nipe msimamo wa nini cha kufanya maana naona baada ya kuzungumza na nyie angalau nimeanza kupata mwanga ndani ya kichwa changu.”
“Nenda nyumbani kwao! Kazungumze na mama yake na umweleze mambo yote anayokufanyia na mwisho, mweleze kwamba huhitaji kuendelea kukaa naye kwa sasa! Atazipata salamu hizo kutoka kwa mama yake,” aliniambia Joel, ushauri ambao uliniingia vizuri sana ndani ya kichwa changu.
Nilijiandaa asubuhi hiyohiyo, baada ya kumaliza, nikiwa najiandaa kutoka, nilikumbuika kwamba tayari Clarence alikuwa amenirekebishia simu yangu na kuiunganisha na simu ya Joanna ili niwe na uwezo wa kuwa naona kila kinachoendelea kwenye simu yake.
Sijui ni nini kilichokuwa kimetokea kwenye moyo wangu lakini huwezi kuamini kwamba sikutaka kushughulika nayo kwa wakati huo. Niliona kama nitazidi kujichanganya kichwa kwa hiyo nikaachana nayo na safari ya kuelekea Magomeni, nyumbani kwa akina Joanna ilianza.
Nilimkuta mama yake akiwa nyumbani, tukasalimiana kwa uchangamfu huku na yeye akinishangaa kwa sababu kwa kawaida, asubuhi hiyo nilitakiwa niwe kazini. Sikutaka kupoteza muda, moja kwa moja nilienda kwenye hoja ya msingi, nikamweleza kila kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yangu na mwanaye Joanna.
Tofauti na mwanaye, mama yake Joanna alikuwa mpole na mstaarabu sana, usingeweza kuamini kwamba huyo ndiyo mama yake aliyemzaa. Alisikitika sana na kusema anashindwa kuelewa kwa nini Joanna anamdhalilisha kiasi hicho, muda huohuo akampigia simu na kumuweka ‘loud speaker’.
“Uko wapi?”
“Nyumbani kwangu, vipi kwani mbona unaniuliza kiukali hivyo mama?”
“Nyumbani kwako wapi?”
“Kinondoni! Kwani nina makazi mengine jamani?”
“Unajua usijifanye mjanja sana Jo! Nipo na mumeo hapa na anakusikia unachokisema! Una siku ya ngapi hujalala nyumbani kwako leo? Unaweza kuniambia uko wapi?”
“Mama nakuomba achana na huyo bwege!” alisema Joanna kisha akakata simu, huwezi kuamini, wala sikujisikia vibaya kama nilivyokuwa nikijisikia vibaya mwanzo. Masimango ya Joel na Clarence yalikuwa ni kama yameniamsha usingizini, nikaishia kucheka tu.
“Unaona anavyonidharau mama? Basi haina shida, nilitaka tu mwenyewe ujionee hali halisi na kwa hiki kilichotokea, mimi siwezi kuendelea kuishi naye.
Akitoka huko aliko, itabidi arudi tu hapa nyumbani au atachagua mwenyewe sehemu ya kuishi lakini simhitaji kwa sasa,” nilisema kwa sauti ambayo ilionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Mama yake alishindwa kujibu chochote zaidi ya kujiinamia, akionesha kuwa na mwazo mengi ndani ya kichwa chake. Hata wakati nikimuaga na kuondoka, alionesha kuwa ni kama amechanganyikiwa kabisa. Nilitoka na kurudi mpaka nyumbani kwangu huku moyoni nikijihisi ni kama nimeshusha mzigo mzito sana.
Nilipofika nyumbani, kazi ya kwanza ilikuwa ni kuanza kuondoa alama zote ambazo zinanikumbusha kuhusu Joanna! Nilijikuta nikipata nguvu ya ajabu ndani ya moyo wangu, nikabandua picha za ukutani ambazo tulikuwa tumepiga mimi na yeye, nikazikusanya zote na kuziweka kwenye pipa la taka.
Nilitoa vitu vyote ambavyo vilikuwa vinamhusu yeye pale sebuleni, nikahamia chumbani ambako nako nilikusanya kila kitu chake na kufungiakwenye kabati lake. Sikuacha kitu na nilitaka hata mwenyewe akija ajue kwamba mimi siyo yule bwege wake tena! Nilikusanya kila kitu, nikaacha vitu vinavyinihusu tu!
Nilifanya hivyo nyumba nzima, nilitoa kila kitu ambacho kilikuwa na uhusiano naye, baada ya hapo nikaenda kuchoma moto baadhi ya vitu, zikiwemo baadhiya nguo na zawadi za hapa na pale alizowahi kuninunulia siku za mwanzo za mapenzi yetu, nikachoma moto na zile picha na kurudi ndani nikiwa mtu mwingine tofauti kabisa.
Baada ya kurudi ndani, angalau sasa nilikuwa najihisi kuwa mtu mpya kabisa maishani mwangu, nilienda tena kuoga, nikarudi na kujiandalia chakula kisha nikakaa sebuleni nikiwa natazama runinga. Ni hapo ndipo nilipopata mawazo ya kuingia kwenye ile ‘software’ ya kunisaidia kuiona simu yake.
Nilianza kwenye meseji, nilisoma zote, kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho, nikawa ni kama nimechokoza upya stress ndani ya kichwa changu, kuna wakati nilikuwa nikitetemeka kuliko kawaida, nikawa najiapiza kwamba naweza kuja kumdhuru vibaya sana Joanna.
Nikiwa katika hali hiyo ya kuchanganyikiwa, nilianza kumfowadia mama yake meseji zote alizokuwa akichati Joanna na huyo mwanaume wake ambaye eti kwenye simu yake ndiye aliyekuwa amemsevu kwa jina la My Huzband, mimi nikiwa hata sijaseviwa, yaani ni namba tu.
Joanna alionesha kuwa kwenye mahaba mazito na mwanaume huyo na kwa jinsi ilivyoonesha, uhusiano wao ulikuwa na muda mrefu kidogo, walishafanya mambo mengi pamoja.
Muda mfupi baadaye, mama yake alinipigia simu, akaniuliza kuhusu meseji hizo, nikamwambia ni meseji za mwanaye Joanna anazowasiliana na huyo mwanaume wake wa nje, akaniuliza nimezipata wapi? Nikamjibu tu kwamba nina mbinu zangu zilizoniwezesha kuzipata lakini ni meseji za kweli kabisa.
Muda mfupi baada ya kukata simu, Joanna alianza kunipigia simu mfululizo. Sikutaka kupokea, iliita mara ya kwanza mpaka ikakatika, ikaita mara ya pili, mara ya tatu, ya nne na kuendelea! Sikutaka kabisa kupokea na kadiri alivyokuwa anazidi kupiga, ndivyo hasira zilivyokuwa zinazidi kuongezeka kwenye moyo wangu.
“Unasemaje wewe mbwa!”
“We usiniite mimi mbwa! Hukunizaa wewe.”
“Wewe ni mbwa tu Joanna! Mbwa!” nilisema na kukata simu kwa hasira, akapiga tena, nikawa nakata, akipiga nakata na kwa hasira niliamua kuizima kabisa. Nilikuwa na jazba kali sana ndani ya moyo wangu.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA:
“Unasemaje wewe mbwa!”
“We usiniite mimi mbwa! Hukunizaa wewe.”
“Wewe ni mbwa tu Joanna! Mbwa!” nilisema na kukata simu kwa hasira, akapiga tena, nikawa nakata, akipiga nakata na kwa hasira niliamua kuizima kabisa. Nilikuwa na jazba kali sana ndani ya moyo wangu.
SASA ENDELEA...
Kuna wakati nilijuta kwa nini sikusikiliza ushauri wa Clarence na kuachana na mambo ya kufuatilia simu ya Joanna kwa sababu mambo niliyoyaona yalinichoma mno roho yangu. Sijui kama katika historia ya maisha yangu nimewahi kuumia kiasi hicho.
Kulikuwa na meseji nyingi ambazo Joanna alikuwa akimshukuru huyo bwanaake kwa penzi zuri alilompa. Kwa jinsi meseji zilivyokuwa nyingi, ilionesha kwamba kumbe karibu kila siku walikuwa wakikutana na kufanya yao.
Nilijaribu kuvuta kumbukumbu zangu nyuma, nikagundua kwamba kwa karibu kipindi cha kama miezi sita hivi iliyopita, Joanna hakuwa na mpango na mimi kabisa linapokuja suala la tendo. Kila nilipokuwa nikimhitaji faragha, alikuwa haishi visingizio.
Mara atakwambia amechoka, mara atakwambia tumbo linamuuma, siku nyingine hata hasemi kitu unamkuta amenuna tu akiwa hataki kabisa mawasiliano na mimi! Hata katika zile siku ambazo nilikuwa namfosi sana na kuamua kunipa haki yangu, haikuwa kama ilivyokuwa mwanzo.
Alikuwa ni kama anatimiza wajibu tu, yale mapenzi motomoto yaliyokuwepo mwanzo, zile ‘mbilingembilinge’ za kwenye uwanja wa fundi seremala, hazikuwepo tena! Alikuwa anafanya kutimiza wajibu tu na inaweza kupita hata wiki mbili au tatu ndiyo ananipa haki yangu mara moja.
Awali jambo hilo liliniumiza sana kichwa changu, kuna kipindi mpaka niliwaza kwamba labda nitafute ‘mchepuko’ ambaye atakuwa anakidhi haja za moyo wangu lakini kila nilipokuwa nafikiria kumsaliti, nilikuwa najiona kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wangu hivyo kuishia kuvumilia ndani kwa ndani, nikiamini ipo siku mambo yatakuwa kama zamani. Kumbe nilikuwa najidanganya, tena uongo mtakatifu. Joanna hakuwa na taimu na mimi kwa sababu alikuwepo mtu aliyekuwa anamchanganya kichwa chake.
Na hili linapaswa kuwa fundisho kwa wanaume wote, unapoona mkeo anaanza kukuletea visingizio visivyo na kichwa wala miguu kwenye suala zima la unyumba, lazima kengele ya hatari ilie ndani ya kichwa chako.
Wapo baadhi ambao huwa wanakuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa sababu mbalimbali, pengine za kiafya na kadhalika lakini kwa asilimua kubwa, mwanamke anapoanza kuchepuka, huwa anapoteza kabisa msisimko kwa mumewe na hapo ndipo visababu visivyo na kichwa wala miguu vinapoanza.
Nilijiona mjinga sana kwa kushindwa kulishtukia jambo hilo mapema na kiukweli, narudia tena kusema hakuna siku ambayo niliumia kama hiyo. Pengine Joanna angekuwa karibu yangu, ningeweza kufanya jambo ambalo lingeushangaza ulimwengu mzima.
Haiwezekani mtu namgharamia kwa kila kitu, kuanzia kula, mavazi, mahitaji ya msingi, akiumwa mimi ndiyo nahangaika naye hospitalini lakini kumbe wakati mimi nikijitoa kwa moyo wangu wote, asali anarina mtu mwingine kwenye mzinga wangu! Ilikuwa ni ukatili wa hali ya juu.
Nimwahi kusema na nasisitiza tena kwamba unapoona mwanaume anafikia hatua ya kufanya ukatili wa kutisha kwa mkewe, tusikimbilie kuhukumu tu kwamba wanaume siku hizi wamekuwa wakatili! Fuatilia nini kilichosababisha, pengine ukijua sababu, unaweza kuwa na mtazamo tofauti kwamba ukatili wa wanaume unaongezeka kwa sababu ya ukatili wa wake zao.
Niliendelea kuwaza kwa muda mrefu, kichwa changu kikiwa kimevurugika kabisa, mwili wote ukiwa umekufa ganzi. Nilijikuta nikimchukia mno Joanna na kiukweli nilijiapiza kwamba kamwe siwezi kuja kuendelea naye tena maishani mwangu.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu pale sebuleni, nikiwa ni kama sanamu, niliichukua simu yangu na kuiwasha tena. Ukweli uliokuwa mbele yangu ulikuwa mchungu sana lakini sikuwa na namna zaidi ya kuukubali. Wanasema ni bora ukweli mchungu kuliko uongo mtamu.
Nilipowasha tu simu, meseji mfululizo zilianza kuingia kwenye simu yangu. Zote zilikuwa zinatoka kwa Joanna na huwezi kuamini, safari hii alikuwa akinivurumishia matusi ya nguoni. Alinitukana sana kwenye meseji, yaani mpaka mambo mengi unajiuliza mara mbilimbili, hivi huyu ni mke wangu au kitu gani?
Alifikia hatua ya kuanza mpaka kunidhalilisha kuhusu uanaume wangu. Akaniambia mimi si lolote si chochote na anajuta sana kuolewa na mtu kama mimi. Akaniambia ameipata furaha ya moyo wake kwa hiyo hajutii kwa chochote, hata kama nimeamua kwenda kumharibia kwa wazazi wake, hajali chochote na kamwe hatarudi nyuma.
Sikumjibu meseji hata moja, akaanza tena kupiga lakini sikutaka kupokea, nilipoona anazidi kunisumbua, niliiblock namba yake. Nilikuwa nahitaji utulivu wa akili yangu kwa sababu tulikokuwa tunaelekea, kamwe hakukuwa kuzuri hata kidogo.
Basi niliendelea kufuatilia mawasiliano yake, nikaingia WhatsApp ambako huko ndiyo nilichoka kabisa. Kulikuwa na picha nyingi za ajabuajabu, mke wangu akimtumia huyo mwanaume wake, akiwa mtupu kabisa, na huyo mwanaume naye akimtumia za kwake.
Hebu vuta picha, anajifungia ndani ya nyumba yangu, juu ya kitanda changu, anajipiga picha za utupu tena kwa kutumia simu ya gharama ambayo mimi ndiyo nimemnunulia kisha anamtumia mwanaume mwingine! Unaweza kupata picha halisi ya hali niliyokuwa nayo.
Katika kupekuapekua, nilikutana pia na picha nyingine ambazo walipiga wakiwa wawili, tena watupu kabisa. Kilichoniumiza moyo zaidi ni kwamba kuna picha nyingine zilikuwa zimepigwa humohumo chumbani kwangu. Kwa hiyo kumbe mbali na uchafu wote aliokuwa ananifanyia, alikuwa pia akimuingiza huyo mwanaume wake humohumo ndani kwangu na kufanya naye uchafu juu ya kitanda changu!
Haya mambo yasikie tu kwa mwenzako, usiombe yakukute, yanaumiza mno moyo kiasi kwamba kama una roho nyepesi, unaweza hata kuchukua kamba na kujinyonga. Katika kupitapita pia, niligundua kwamba walikuwa wakitumiana picha za nyumba ambayo ilikuwa inaendelea kujengwa.
Sikuwahi kusikia hata siku moja kwamba mke wangu alikuwa anajenga nyumba lakini huwezi kuamini, alikuwa akiwasiliana na huyo mwanaume wake eti wakawa wanapanga kwamba nyumba hiyo ikikamilika, ndiyo watakapohamia na kuyaanzisha maisha yao mapya.
Kengele ya hatari ililia tena ndani ya kichwa changu. Joanna hakuwa akifanya kazi yoyote na yale maelezo waliyokuwa wakitumiana, ilionesha kwamba yeye ndiye aliyekuwa akigharamia ujenzi huo, swali likawa ni je, anapata wapi fedha za kufanyia hayo anayoyafanya?
Mimi na yeye hatukuwa tumejenga bali tulinunua kiwanja Bunju na tulichokuwa tumekubaliana ni kwamba niombe mkopo mkubwa kazini ili mwezi Desemba ukifika, mwezi ambao kwa kawaida huwa naenda likizo, tukaanze ujenzi wa nyumba yetu.
Tulichokuwa tumepanga kabla mambo hayajaanza kwenda mrama, ni kwamba siku tutakapoanza kujenga, itakuwa ni non-stop mpaka nyumba iishe. Tayari mkonpo nilishachukua kazini miezi mingi tu nyuma na nilimshirikisha kwa kila hatua, kwa hiyo tulichokuwa tunakisubiri, ilikuwa ni muda wa mimi kuchukua likizo tu ili tukamilishe malengo yetu.
Mkopo wenyewe niliochukua, haukuwa wa kitoto. Nilikopa shilingi milioni hamsini ambazo kwa mahesabu yake, kutokana na mshahara niliokuwa napata, ningekatwa kwa karibu miaka mitatu na nusu ili kuumaliza. Sikuona kama ni tatizo kwa sababu hata kama nakatwa mshahara kazini, lakini si tayari nitakuwa nimehamia kwangu na kufanya jambo kubwa?
Ni hapo ndipo nilipopata wazo la kwenda kuangalia fedha zangu benki. Niliinuka harakaharaka na kwenda chumbani kwangu, nikafungua kwenye droo ambayo kadi yangu ya benki huwa inakaa! HAIKUWEPO!
Nilipekua huku na kule, wala haikuwepo! Nilishtuka almanusra nianguke na kupoteza fahamu! Kadi yangu iko wapi? Sikuwa na majibu. Kwa bahati nzuri, nilikuwa nimejiunga na huduma ya Sim-banking, ambayo inakuwezesha kufanya miamala ya kibenki kwa kupitia simu yako.
Harakaharaka nikaingia na kuangalia salio. Lahaula, kati ya shilingi milioni hamsini nilizokuwa nimeingiziwa benki baada ya kupewa mkopo wangu miezi kadhaa nyuma, kulikuwa kumebakia shilingi milioni mbili tu. Nilijikuta nikishikwa na tumbo la kuendesha ghafla, nikakimbilia maliwatoni huku nikiwa ni kama siamini.
Nilikaa kwa muda mrefu, baadaye nilipotoka, nilijiandaa harakaharaka na lengo langu lilikuwa ni kwenda benki kuhakiki kama nilichokiona ndicho kilichokuwa kimetokea. Mwili haukuwa na nguvu kabisa lakini ilibidi nijilazimishe, ilikuwa nilazima niujue ukweli tena haraka iwezekanavyo.
Nilichukua Bajaj na kumuelekeza dereva kunipeleka Mnazi Mmoja kwenye tawi kubwa la benki niliyokuwa nikiitumia. Njia nzima akili zangu zilikuwa ni kama zimepigwa na shoti ya umeme. Hatimaye nilifika, moja kwa moja nikaomba kuonana na meneja na kwa bahati nzuri ni kwamba hakukuwa na mlolongo wowote mrefu.
Nilipoingia ofisini kwake, nilitaka anieleze imekuwaje katika fedha zangu zilizokuwa benki, zibaki shilingi milioni mbili tu wakati sikuwahi hata siku moja kwenda kutoa fedha? Uzuri ni kwamba teknolojia huwa haidanganyi, alinitaka nisubiri kidogo, akaanza kubofyabofya kompyuta yake kisha nikamsikia akimpigia simu mtu wa upande wa pili na kumpa maelezo ya nini cha kufanya.
Muda mfupi baadaye, aliniita na kunitaka nitazame kwenye kompyuta yake.
“Huyu unamjua?” aliniuliza huku akinionesha picha ya video ya mtu akitoa fedha kwenye ATM, alikuwa ni Joanna.
“Ndiyo! Ni mke wangu!”
“Na huyu mwingine naye unamjua?” alisema huku akinioneshea picha nyingine, niliitambua haraka kwamba ndiyo yule mwanaume ambaye nimekuta picha zake akiwa na mke wangu kwenye simu, nikatingisha kichwa kuonesha kwamba namjua.
Akaniambia ekodi zao zinaonesha kwamba hao wawili ndiyo waliokuwa wakitoa fedha benki kwa kutumia kadi ya ATM, siyo kadi bandia, kadi yangu! Alinionesha rekodi zote kuanzia siku walipoanza kutoa kwa mara ya kwanza na kiwango walichotoa, akawa ananionesha kwa ushahidi wa picha za video kila kitu na mara ya mwisho kwenda kutoa fedha, ilikuwa ni jana yake tu.
Hata sikumbuki niliondokaje pale benki, nilikuja kujikuta nikiwa nikiwa barabarani, magari yakinipigia honi kwa nguvu, nikashtuka kugundua kwamba kumbe nilikuwa nikitembea katikati ya barabara huku nikiwa sijitambui kabisa.
“Utagongwa broo, ina maana magari huyaoni,” alisema mwanaume mmoja huku akinishika mkono na kunivusha upande wa pili wa barabara, ilibidi nikae chini kwa sababu nilikuwa hata sielewi ni nini kinachoendelea.
“Vipi kwani?”
“Nashukuru kwa msaada wako, unaweza kuniitia Bajaj tafadhali,” nilimwambia yule msamaria mwema ambaye alinikazia macho kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa chake kuonesha kusikitika. Japo alikuwa hajui chochote kinachoendelea, nadhani hali aliyoniona nayo ilimfanya aelewe kwamba nipo kwenye matatizo makubwa sana.
Machozi yalikuwa yananitoka huku mwenyewe hata nikiwa sina habari. Macho yangu yalikuwa mekundu sana na kuna donge kubwa sana lilikuwa limenikaba kooni kiasi cha kunifanya niwe kama mwendawazimu kabisa. Sijawahi kutamani kuyakatisha maisha yangu lakini huwezi kuamini, siku hiyo nilitamani kujiua! Nilitamani kuyakatisha maisha yangu ili kuepukana na aibu kubwa iliyokuwa mbele yangu.
Muda mfupi baadaye, yule msamaria mwema aliniitia Bajaj, akaniuliza ninapoelekea, nikamtajia na akanisaidia kuniinua na kunipakiza kwenye Bajaj, nikaondoka eneo hilo huku nikiwa bado hata sijielewi. Sikuwa najua hapo ni wapi na nimetokaje kule benki na nilikuwa naelekea wapi, nikaegamia kwenye siti ya Bajaj huku machozi yakizidi kunimwagika kwa wingi.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA:
“Unasemaje wewe mbwa!”
“We usiniite mimi mbwa! Hukunizaa wewe.”
“Wewe ni mbwa tu Joanna! Mbwa!” nilisema na kukata simu kwa hasira, akapiga tena, nikawa nakata, akipiga nakata na kwa hasira niliamua kuizima kabisa. Nilikuwa na jazba kali sana ndani ya moyo wangu.
SASA ENDELEA...
Kuna wakati nilijuta kwa nini sikusikiliza ushauri wa Clarence na kuachana na mambo ya kufuatilia simu ya Joanna kwa sababu mambo niliyoyaona yalinichoma mno roho yangu. Sijui kama katika historia ya maisha yangu nimewahi kuumia kiasi hicho.
Kulikuwa na meseji nyingi ambazo Joanna alikuwa akimshukuru huyo bwanaake kwa penzi zuri alilompa. Kwa jinsi meseji zilivyokuwa nyingi, ilionesha kwamba kumbe karibu kila siku walikuwa wakikutana na kufanya yao.
Nilijaribu kuvuta kumbukumbu zangu nyuma, nikagundua kwamba kwa karibu kipindi cha kama miezi sita hivi iliyopita, Joanna hakuwa na mpango na mimi kabisa linapokuja suala la tendo. Kila nilipokuwa nikimhitaji faragha, alikuwa haishi visingizio.
Mara atakwambia amechoka, mara atakwambia tumbo linamuuma, siku nyingine hata hasemi kitu unamkuta amenuna tu akiwa hataki kabisa mawasiliano na mimi! Hata katika zile siku ambazo nilikuwa namfosi sana na kuamua kunipa haki yangu, haikuwa kama ilivyokuwa mwanzo.
Alikuwa ni kama anatimiza wajibu tu, yale mapenzi motomoto yaliyokuwepo mwanzo, zile ‘mbilingembilinge’ za kwenye uwanja wa fundi seremala, hazikuwepo tena! Alikuwa anafanya kutimiza wajibu tu na inaweza kupita hata wiki mbili au tatu ndiyo ananipa haki yangu mara moja.
Awali jambo hilo liliniumiza sana kichwa changu, kuna kipindi mpaka niliwaza kwamba labda nitafute ‘mchepuko’ ambaye atakuwa anakidhi haja za moyo wangu lakini kila nilipokuwa nafikiria kumsaliti, nilikuwa najiona kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wangu hivyo kuishia kuvumilia ndani kwa ndani, nikiamini ipo siku mambo yatakuwa kama zamani. Kumbe nilikuwa najidanganya, tena uongo mtakatifu. Joanna hakuwa na taimu na mimi kwa sababu alikuwepo mtu aliyekuwa anamchanganya kichwa chake.
Na hili linapaswa kuwa fundisho kwa wanaume wote, unapoona mkeo anaanza kukuletea visingizio visivyo na kichwa wala miguu kwenye suala zima la unyumba, lazima kengele ya hatari ilie ndani ya kichwa chako.
Wapo baadhi ambao huwa wanakuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa sababu mbalimbali, pengine za kiafya na kadhalika lakini kwa asilimua kubwa, mwanamke anapoanza kuchepuka, huwa anapoteza kabisa msisimko kwa mumewe na hapo ndipo visababu visivyo na kichwa wala miguu vinapoanza.
Nilijiona mjinga sana kwa kushindwa kulishtukia jambo hilo mapema na kiukweli, narudia tena kusema hakuna siku ambayo niliumia kama hiyo. Pengine Joanna angekuwa karibu yangu, ningeweza kufanya jambo ambalo lingeushangaza ulimwengu mzima.
Haiwezekani mtu namgharamia kwa kila kitu, kuanzia kula, mavazi, mahitaji ya msingi, akiumwa mimi ndiyo nahangaika naye hospitalini lakini kumbe wakati mimi nikijitoa kwa moyo wangu wote, asali anarina mtu mwingine kwenye mzinga wangu! Ilikuwa ni ukatili wa hali ya juu.
Nimwahi kusema na nasisitiza tena kwamba unapoona mwanaume anafikia hatua ya kufanya ukatili wa kutisha kwa mkewe, tusikimbilie kuhukumu tu kwamba wanaume siku hizi wamekuwa wakatili! Fuatilia nini kilichosababisha, pengine ukijua sababu, unaweza kuwa na mtazamo tofauti kwamba ukatili wa wanaume unaongezeka kwa sababu ya ukatili wa wake zao.
Niliendelea kuwaza kwa muda mrefu, kichwa changu kikiwa kimevurugika kabisa, mwili wote ukiwa umekufa ganzi. Nilijikuta nikimchukia mno Joanna na kiukweli nilijiapiza kwamba kamwe siwezi kuja kuendelea naye tena maishani mwangu.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu pale sebuleni, nikiwa ni kama sanamu, niliichukua simu yangu na kuiwasha tena. Ukweli uliokuwa mbele yangu ulikuwa mchungu sana lakini sikuwa na namna zaidi ya kuukubali. Wanasema ni bora ukweli mchungu kuliko uongo mtamu.
Nilipowasha tu simu, meseji mfululizo zilianza kuingia kwenye simu yangu. Zote zilikuwa zinatoka kwa Joanna na huwezi kuamini, safari hii alikuwa akinivurumishia matusi ya nguoni. Alinitukana sana kwenye meseji, yaani mpaka mambo mengi unajiuliza mara mbilimbili, hivi huyu ni mke wangu au kitu gani?
Alifikia hatua ya kuanza mpaka kunidhalilisha kuhusu uanaume wangu. Akaniambia mimi si lolote si chochote na anajuta sana kuolewa na mtu kama mimi. Akaniambia ameipata furaha ya moyo wake kwa hiyo hajutii kwa chochote, hata kama nimeamua kwenda kumharibia kwa wazazi wake, hajali chochote na kamwe hatarudi nyuma.
Sikumjibu meseji hata moja, akaanza tena kupiga lakini sikutaka kupokea, nilipoona anazidi kunisumbua, niliiblock namba yake. Nilikuwa nahitaji utulivu wa akili yangu kwa sababu tulikokuwa tunaelekea, kamwe hakukuwa kuzuri hata kidogo.
Basi niliendelea kufuatilia mawasiliano yake, nikaingia WhatsApp ambako huko ndiyo nilichoka kabisa. Kulikuwa na picha nyingi za ajabuajabu, mke wangu akimtumia huyo mwanaume wake, akiwa mtupu kabisa, na huyo mwanaume naye akimtumia za kwake.
Hebu vuta picha, anajifungia ndani ya nyumba yangu, juu ya kitanda changu, anajipiga picha za utupu tena kwa kutumia simu ya gharama ambayo mimi ndiyo nimemnunulia kisha anamtumia mwanaume mwingine! Unaweza kupata picha halisi ya hali niliyokuwa nayo.
Katika kupekuapekua, nilikutana pia na picha nyingine ambazo walipiga wakiwa wawili, tena watupu kabisa. Kilichoniumiza moyo zaidi ni kwamba kuna picha nyingine zilikuwa zimepigwa humohumo chumbani kwangu. Kwa hiyo kumbe mbali na uchafu wote aliokuwa ananifanyia, alikuwa pia akimuingiza huyo mwanaume wake humohumo ndani kwangu na kufanya naye uchafu juu ya kitanda changu!
Haya mambo yasikie tu kwa mwenzako, usiombe yakukute, yanaumiza mno moyo kiasi kwamba kama una roho nyepesi, unaweza hata kuchukua kamba na kujinyonga. Katika kupitapita pia, niligundua kwamba walikuwa wakitumiana picha za nyumba ambayo ilikuwa inaendelea kujengwa.
Sikuwahi kusikia hata siku moja kwamba mke wangu alikuwa anajenga nyumba lakini huwezi kuamini, alikuwa akiwasiliana na huyo mwanaume wake eti wakawa wanapanga kwamba nyumba hiyo ikikamilika, ndiyo watakapohamia na kuyaanzisha maisha yao mapya.
Kengele ya hatari ililia tena ndani ya kichwa changu. Joanna hakuwa akifanya kazi yoyote na yale maelezo waliyokuwa wakitumiana, ilionesha kwamba yeye ndiye aliyekuwa akigharamia ujenzi huo, swali likawa ni je, anapata wapi fedha za kufanyia hayo anayoyafanya?
Mimi na yeye hatukuwa tumejenga bali tulinunua kiwanja Bunju na tulichokuwa tumekubaliana ni kwamba niombe mkopo mkubwa kazini ili mwezi Desemba ukifika, mwezi ambao kwa kawaida huwa naenda likizo, tukaanze ujenzi wa nyumba yetu.
Tulichokuwa tumepanga kabla mambo hayajaanza kwenda mrama, ni kwamba siku tutakapoanza kujenga, itakuwa ni non-stop mpaka nyumba iishe. Tayari mkonpo nilishachukua kazini miezi mingi tu nyuma na nilimshirikisha kwa kila hatua, kwa hiyo tulichokuwa tunakisubiri, ilikuwa ni muda wa mimi kuchukua likizo tu ili tukamilishe malengo yetu.
Mkopo wenyewe niliochukua, haukuwa wa kitoto. Nilikopa shilingi milioni hamsini ambazo kwa mahesabu yake, kutokana na mshahara niliokuwa napata, ningekatwa kwa karibu miaka mitatu na nusu ili kuumaliza. Sikuona kama ni tatizo kwa sababu hata kama nakatwa mshahara kazini, lakini si tayari nitakuwa nimehamia kwangu na kufanya jambo kubwa?
Ni hapo ndipo nilipopata wazo la kwenda kuangalia fedha zangu benki. Niliinuka harakaharaka na kwenda chumbani kwangu, nikafungua kwenye droo ambayo kadi yangu ya benki huwa inakaa! HAIKUWEPO!
Nilipekua huku na kule, wala haikuwepo! Nilishtuka almanusra nianguke na kupoteza fahamu! Kadi yangu iko wapi? Sikuwa na majibu. Kwa bahati nzuri, nilikuwa nimejiunga na huduma ya Sim-banking, ambayo inakuwezesha kufanya miamala ya kibenki kwa kupitia simu yako.
Harakaharaka nikaingia na kuangalia salio. Lahaula, kati ya shilingi milioni hamsini nilizokuwa nimeingiziwa benki baada ya kupewa mkopo wangu miezi kadhaa nyuma, kulikuwa kumebakia shilingi milioni mbili tu. Nilijikuta nikishikwa na tumbo la kuendesha ghafla, nikakimbilia maliwatoni huku nikiwa ni kama siamini.
Nilikaa kwa muda mrefu, baadaye nilipotoka, nilijiandaa harakaharaka na lengo langu lilikuwa ni kwenda benki kuhakiki kama nilichokiona ndicho kilichokuwa kimetokea. Mwili haukuwa na nguvu kabisa lakini ilibidi nijilazimishe, ilikuwa nilazima niujue ukweli tena haraka iwezekanavyo.
Nilichukua Bajaj na kumuelekeza dereva kunipeleka Mnazi Mmoja kwenye tawi kubwa la benki niliyokuwa nikiitumia. Njia nzima akili zangu zilikuwa ni kama zimepigwa na shoti ya umeme. Hatimaye nilifika, moja kwa moja nikaomba kuonana na meneja na kwa bahati nzuri ni kwamba hakukuwa na mlolongo wowote mrefu.
Nilipoingia ofisini kwake, nilitaka anieleze imekuwaje katika fedha zangu zilizokuwa benki, zibaki shilingi milioni mbili tu wakati sikuwahi hata siku moja kwenda kutoa fedha? Uzuri ni kwamba teknolojia huwa haidanganyi, alinitaka nisubiri kidogo, akaanza kubofyabofya kompyuta yake kisha nikamsikia akimpigia simu mtu wa upande wa pili na kumpa maelezo ya nini cha kufanya.
Muda mfupi baadaye, aliniita na kunitaka nitazame kwenye kompyuta yake.
“Huyu unamjua?” aliniuliza huku akinionesha picha ya video ya mtu akitoa fedha kwenye ATM, alikuwa ni Joanna.
“Ndiyo! Ni mke wangu!”
“Na huyu mwingine naye unamjua?” alisema huku akinioneshea picha nyingine, niliitambua haraka kwamba ndiyo yule mwanaume ambaye nimekuta picha zake akiwa na mke wangu kwenye simu, nikatingisha kichwa kuonesha kwamba namjua.
Akaniambia ekodi zao zinaonesha kwamba hao wawili ndiyo waliokuwa wakitoa fedha benki kwa kutumia kadi ya ATM, siyo kadi bandia, kadi yangu! Alinionesha rekodi zote kuanzia siku walipoanza kutoa kwa mara ya kwanza na kiwango walichotoa, akawa ananionesha kwa ushahidi wa picha za video kila kitu na mara ya mwisho kwenda kutoa fedha, ilikuwa ni jana yake tu.
Hata sikumbuki niliondokaje pale benki, nilikuja kujikuta nikiwa nikiwa barabarani, magari yakinipigia honi kwa nguvu, nikashtuka kugundua kwamba kumbe nilikuwa nikitembea katikati ya barabara huku nikiwa sijitambui kabisa.
“Utagongwa broo, ina maana magari huyaoni,” alisema mwanaume mmoja huku akinishika mkono na kunivusha upande wa pili wa barabara, ilibidi nikae chini kwa sababu nilikuwa hata sielewi ni nini kinachoendelea.
“Vipi kwani?”
“Nashukuru kwa msaada wako, unaweza kuniitia Bajaj tafadhali,” nilimwambia yule msamaria mwema ambaye alinikazia macho kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa chake kuonesha kusikitika. Japo alikuwa hajui chochote kinachoendelea, nadhani hali aliyoniona nayo ilimfanya aelewe kwamba nipo kwenye matatizo makubwa sana.
Machozi yalikuwa yananitoka huku mwenyewe hata nikiwa sina habari. Macho yangu yalikuwa mekundu sana na kuna donge kubwa sana lilikuwa limenikaba kooni kiasi cha kunifanya niwe kama mwendawazimu kabisa. Sijawahi kutamani kuyakatisha maisha yangu lakini huwezi kuamini, siku hiyo nilitamani kujiua! Nilitamani kuyakatisha maisha yangu ili kuepukana na aibu kubwa iliyokuwa mbele yangu.
Muda mfupi baadaye, yule msamaria mwema aliniitia Bajaj, akaniuliza ninapoelekea, nikamtajia na akanisaidia kuniinua na kunipakiza kwenye Bajaj, nikaondoka eneo hilo huku nikiwa bado hata sijielewi. Sikuwa najua hapo ni wapi na nimetokaje kule benki na nilikuwa naelekea wapi, nikaegamia kwenye siti ya Bajaj huku machozi yakizidi kunimwagika kwa wingi.
Je, nini kitafuatia?
Oya Fanya kama una imalizia

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom