Loriondo, Dawa ya kutibu Kansa, Kisukari na Ukim Tshs 500 au nusu kilo ya sukari

Wakuu huko kuna mmiminiko wa watu nimefika na kujionea.watu ni wengi mno.kwa wanaohitaji kwenda unapanda gari mpaka arusha ama Dar express iendayo karatu unashukia mto wa mbu,kesho yake alfajiri kuna landcruisers za tours zinaelekea huko kwa nauli ya 50,000 kwenda na kurudi..safari inachukua wastani wa masaa sita kufika,ni barabara ya vumbi,unapita Engaruka then Oldonyo lengai ule mlima wenye volcano hai then mnapita engare sero kwenye nyayo za watu wa kale na kupita ziwa la magadi..Natron.huo wote ni ukanda wa bonde la ufa nyuma ya ngorongoro crater.

ukifika hapo babu anatoa historia ya ugunduzi wake kisha anatoa sala kama dk chache then anatoa dawa ya maji ktk kikombe kimoja kwa kila mtu,yeye ni mchungaji mstaafu na ni mnyakyusa.mti wa hiyo dawa ya ajabu ameupanda nje kwake ili watu waweze kuuona

sharti la dawa ni kunywa hapohapo haitoki hapo na kwa watumia vileo hutakiwa kusitisha kwa siku moja ili dawa ya mungu ifanye kazi
ni uponyaji wa kimiujiza hivi yaani baraka na spiritual.

Ada yake ni sh 500 tu,haichukui hata robo saa unapata huduma na kuondoka kupisha wengine
sio tiba ya kisayansi kama watu wanavyodahani.watu ni wengi, sisi tulikuta magari zaidi ya hamsini hapo.

Watu kutoka mikoa yote, kenya, tumekuta waarabu wa oman na wazungu wa Denmark pia,umati unatisha na babu huyo anadai mtu mwenye magonjwa anaweza kupima after seven days..wenye sukari na pumu hupata matokeo hapohapo na wengi wanaanza kunywa fanta na vipimo vikicheza between 4 na 7.5 wakati awali iikuwa above 12 mpaka 17
 
Nimefanikiwa kupata picha zake,video clip na audio clip nikipata wasaa maana nipo safarini Dodoma nikirejea mjini nitaziupload mjionee
 
Wataala wa afya mpo kama hili kweli fuatilieni tuokoe maisha ya ndugu zetu,acheni kukaa ofisini tembeleeni hawa watu

Kaka huyo NGOS zinazo husika na HIV & AIDS zipo najua wataona hili lijamaa linataka kuwapoteza kwenye uso wa dunia kwa kukosa misaada! So kama ministry watamtangaza kuwa ana dawa ya AIDS, inabidi wamwekee ulinzi mkubwa sana!

For sure kama ni kikombe tu na ni shilingi 500, au nusu kilo ya sukari napata imani na mchungaji kwa maana hayupo kibiashara zaidi!
 
Nimesikia tetesi kuwa, jamaa mmoja aliyekuwa mchungaji baadae kuacha/kustaafu huko Loriondo amegundua dawa ambayo ni single dose (kikombe kimoja tu) ya kutibu magonjwa yanayosumbua wataalamu wa dunia hii. Bwana huyo, inasemekana kuwa hatozi gharama zaidi ya Tshs 500 au nusu kilo ya sukari kwa ajili ya matibabu hayo. haijaeleweka ni watu wangapi hadi sasa wametibiwa au kupona, lakini kwa taarifa nilizozipata watu wengi wanaenda huko kutibiwa na wengi wanaendelea vizuri lakini bado hawajaenda kupimwa, kwani inahitajika kupima baada ya siku 90 baada ya kunywa hiyo dawa. wanahabari, mlioko Loriondo tujuzeni

Hiyo habari ni ya kweli maana marafiki zangu wengi wameenda huko kupata hayo matibabu. Gharama ni ndogo sana kama ulivyosikia na jamaa alikuwa mchungaji.

Kwenda huko gharama ni tsh. 60,000/= kwa landcruiser kutoka Arusha mjini. Unajua hivi sasa magonjwa ni mengi sana, kwa hiyo watu wako tayari kwenda popote bora wapate matibabu. Tusuburi tuone
 
Huyu mchungaji hata mie nimemsikia nina ndugu yangu ambaye ametoka Dar nipo nae hapa ametoka loliondo kwa huyo jamaa ni kwamba alivyopita kwa hali yake na alivyo sasa ni tofauti sana anachosema mawaziri na maofisa wa serikari wako wanapishana sana huko,
all in all lets wait kwa kipindi alichotoa cha siku 90 kwenda kupima but watu wanapona nadhani.. na anataka watu waende wenyewe dawa haitoki pale na wala huwezi kutibiwa tofauti na pale hata hivyo aliongeza kwa kusema kwamba mti wa dawa ule pale lakini nisipokupa mimi huwezi kupona ...akaongeza kuwa imani ni muhimu sana..
 
Kwa wingi ule wa watu nina hata mashaka na usalama wake,watu wanaweza hata kumteka wajue siri pia anapambana na nguvu za giza zinazomjaribu na kutaka kumdhoofisha,yule mgonjwa mwanamama aliyekuwa HIV positive amethibitishwa na hospitali ya wilaya kuwa amekuwa tested na kubainika sa kuwa ni negative
 
Watafiti msikae ofisini nendeni mkapime watu kabla hawajapata tiba na baada ya kupata tiba
waandishi wa magazeti,radio na Televisheni fikeni hapo mpate habari kamili na kuwajulisha watanzania wengine wasiokuwa na habari hii
 
Watafiti msikae ofisini nendeni mkapime watu kabla hawajapata tiba na baada ya kupata tiba
waandishi wa magazeti,radio na Televisheni fikeni hapo mpate habari kamili na kuwajulisha watanzania wengine wasiokuwa na habari hii

Inskoskaz, asante kwa taarifa.
Hivi huckoki kucheza?
 
ni kweli kabisa huyo mchungaji anaitwa MASAPILA alikuwa mch wa kkkt akasastaafu . anatibu kwa nguvu za mungu. sasa hivi kila mtu anaenda huko.
 
Back
Top Bottom