Lori jingine la mafuta lapata ajali Handeni, wananchi wakimbilia tena kuchota

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,832
18,826
Huku ikiwa bado majeruhi wa ajali ya Morogoro wakiwa hawajapona vizuri, lori jingine la mafuta limepata ajali leo tarehe 27 Agosti huko Handeni na wananchi kukusanyika na vyombo kwa ajili ya kuyachota

Hata hivyo polisi waliwahi eneo la tukio na kuwatawanya wananchi hao

Ikumbukwe hii ni ajali ya 2 ya lori la mafuta baada ya ile ya Morogoro kwani jana kulitokea ajali nyingine huko Ngara mkoani Kagera ambayo pia wananchi walienda kuchota mafuta

***UPDATE***
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwatawanya wakazi wa Michungwani, wilayani Handeni waliotaka kuchota mafuta kufuatia lori la mafuta kupinduka na kumwaga mafuta. Kamanda wa Usalama Barabara Mkoani Tanga aliwaambia watu hao watakamatwa, watashughulikiwa kweli kweli, na wataozea jela.

 
Mh..aisee
.! Ile ajali ya Morogoro ilivyotangazwa
Tv, Magazeti, Radio, maombolezo sijui ya siku 3

Nadhani lori la mafuta likianguka popote pale hata pale Morogoro mjini bado watu wataenda kuchota

Watu hawafuati maelekezo ambayo yapo simple na clear kabisa kuwa MAFUTA NI HATARI, hata kama wakionyeshwa mfano hai kabisa wa watu kuungua hadi kufa.!

Pengine hili linatupa majibu kwa nini watu weusi hawajaendelea kuliko wengine
Sababu hawawezi kufuata simple instructions kama ya kukaa mbali na lori la mafuta, wataweza kufuata maelekezo hata yenye details ndogo ndogo kama kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa? Achilia mbali maelekezo ya vitu complex vya ujenzi, medicine, ICT, manufacturing, n.k? Ndio tujenge viwanda?
 
Ninachoshangaa mimi ni hayo malori kwanini ajali kila siku.., au wananunua ma scraper, kuhusu wananchi ni life of betting wanaona njaa yenye uhakika ni uhakika na lorryy la mafuta kuna probability ya kutolipuka..
 
....................Hakuna duniani mwalimu mbaya kama maisha na mwenzake wakuitwa shida,hawa wawili wakijikusanya pamoja wakakuchapa kisawasawa watakufundisha ujasiri usiokuwa na kikomo ikiwa ni pamoja na kukupunguzia uwezo wako wa kufikiri sawa.

Hapo watu wameamka wengine wana wagonjwa pesa ya kuwapeleka kituo cha afya hawana wanaona hapo ndo pakutafutia,mwengine watoto nyumbani hawajala ameona fursa ya wanae kupona ni hapo.hii yote inasababishwa na kitu shida.
 
Back
Top Bottom