Lorenzo Insigne avamiwa na majambazi

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,998
5,150
928921b414ed93f1f13ed3d8d0f2beb5.jpg


Kwenye ligi ya Serie A ambayo inaonekana Live kupitia king’amuzi cha Startimes imeshudia mchezaji Lorenzo Insigne akifunga mara 11 kwenye mechi za msimu huu.

Mchezaji huyu wa Napoli amekutana na kisanga weekend hii akiwa kwenye gari na mke wake pamoja na marafiki wawili. Wakiwa kwenye mataa wakisubiri foleni ikaja pikipiki na mtu mwenye silaha na kuwalazimisha watoe vitu vyao vya thamani.

Kwenye tukio hilo Lorenzo alitoa saa ya mkononi aina ya Rolex na mikufu yenye thamani ambapo jumla ya vitu vyote ilikua ni Euro 800.

Baada ya kuchukua vitu hivyo mwizi huyo alimwambia Insigne afunge goli kwenye mechi yao dhidi ya Fiolentina leo na goli hilo liwe dedication kwa ajili yake yeye kibaka.

Lorenzo anahusishwa sana na tetesi za kuhamia Tottenham kwenye msimu ujao akitokea Napoli.

SOURCE: ShaffihDauda.co.tz
 
Back
Top Bottom