Longolongo kwisha: Slaa amaliza misunderstanding hapa jf

Naona bado hamjamuelewa Dr. Slaa.... Anachomaanisha Dr ni kwamba tume ya uchaguzi ikishatangaza mshindi hawezi kupingwa na mahakama au chombo chochote kile....That is to say, hata kama CHADEMA hawakuridhika na mchakato uliomwingiza JK madarakani ila kwa mujibu wa sheria hakuna ujanja bado JK atabaki kuwa rais wa TZ even without CHADEMA's recognition.

Pengine hii ndio sababu CHADEMA wameamua kuelekeza nguvu zao kwenye mabadiliko ya katiba na tume ya uchaguzi

Sasa ikiwa Kikwete ataendelea kuwa rais without CHADEMA's recognition, ndo inamaanisha Chadema imrecognise?

As long as maoni ya Chadema hayaongezi wala kupunguza kitu kwa cheo cha rais, why kumtambua and not kutomtambua?
 
Hawa sio makada wa CCM...ni makada wa JK... Subiri 2015 mgombea urais wa CCM awe mkristo... Wote watahamia CUF!!!
Dada MS, Uwe unajaribu angalau kusoma ujumbe kabla ya kujibu. ndiyo maana unaolewa na kuachwa kila mara. unadandia vitu pasipo kutafakari. Hata kama ni kada ccm, si kwa staili hiyo. Kauli ya Dr Slaa iko clear, ila kama umelewa unapoisoma hauwezi kuielewa.
 
Akizunguzia suala lililozua mjadala la uchaguzi mkuu, Dk Slaa alisema kamati kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais kujadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete yalichezewa.Alisema kutokana na sababu hizo, Chadema imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

“Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa,” alisema Dk Slaa.


“Kisheria Tanzania ina rais na sisi Chadema tunasema nchi hii ina rais, lakini njia iliyutumika kumpata rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa Chadema kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge,” alisema Dk Slaa.

"Unajua hapa suala la kutambua au kutokumtambua rais siyo issue. Rais yupo na katiba inaelekeza kwamba rais akishachaguliwa huwezi kuhoji mahali popote na kwa maana hiyo rais yupo. Tatizo ni jinsi alivyopatikana."

MY TAKE:

Ninashauri JF tudiscuss kauli zinazotoka vinywani mwa wahusika zaidi ya "interpretations zetu wenyewe". Alichokisema Dr Slaa jana (soma mwananchi.co.tz ) ni kile kile alichokisema kabla matokeo rasmi ya TUME kutangazwa na pia siku ya ufunguzi wa bunge kule dodoma na na hata baada ya wabunge kutoka bungeni.

This is great consistent...hakuna shabra shabra...


[/QUOTE
Mimi nadhani swala la kumtambua au kutomtambua raisi lipo wazi ntakupa mfano mdogo kule Arusha Batilda Buriani hakukubali matokeo yaliyompatia ushindi Bw. Lema ila kutotambua kwake hakukuzuia Bw. Lema kuapishwa na kuwa Mbunge, sawa kabisa na kwa swala la Matokeo ya uraisi Dr. Slaa anachosema ni kwamba taratibu zilizopelekea kupatikana kwa raisi ndio zina matatizo (my take hapa anamaanisha swala la tume ya uchaguzi huru na ya haki) kama hauna tume huru je unaweza vipi kupata raisi (bila makelele?) hivyo mimi sioni kama kuna longolongo lolote hapa hili swala lipo christal clear na linaeleweka......
 
Sasa kama wanakataa utaratibu wa kumtangaza rais*anayeendelea*, ambaye ndie mteuzi wa huo utaratibu, kwa cheo chake na utashi wake, what hope do we have?

My fear kwamba wanasiasa wabongo ni wasanii na hawajui wanachofanya inazidi kuongezeka..next time wajameni siku ya uchaguzi na kampeni endeleeni na shughuli zenu..nchi imeshauzwa hii.





Wachache wanajua hilo!!!!!
 
Ninashauri JF tudiscuss kauli zinazotoka vinywani mwa wahusika zaidi ya "interpretations zetu wenyewe". Alichokisema Dr Slaa jana (soma mwananchi.co.tz ) ni kile kile alichokisema kabla matokeo rasmi ya TUME kutangazwa na pia siku ya ufunguzi wa bunge kule dodoma na na hata baada ya wabunge kutoka bungeni.

This is great consistent...hakuna shabra shabra...


Dr. Slaa na Chadema yake ndiyo vigeugeu..........utawala bora unatuelekeza sote endapo hukubali waenda mahakamani......na huko hawataki kwenda kwa tafsiri zao za katiba ambazo zinakinzana namaamuzi ya Mahakama kuu ya mwaka 1995...................sasa sisi kwa nini tusitoe tafsiri zeti wenyewe..........where there is a dearth of quality leadership?
 
Dr. Slaa na Chadema yake ndiyo vigeugeu..........utawala bora unatuelekeza sote endapo hukubali waenda mahakamani......na huko hawataki kwenda kwa tafsiri zao za katiba ambazo zinakinzana namaamuzi ya Mahakama kuu ya mwaka 1995...................sasa sisi kwa nini tusitoe tafsiri zeti wenyewe..........where there is a dearth of quality leadership?

Sidhani kama kwenda mahakamani kutasaidia lolote juu ya hili swala kwa kua hakuna sheria inayoweza kutengua uteuzi wa raisi au kubadilisha matokeo ya ngazi ya uraisi swala hapa ni mabadiliko ya katiba, maana katiba ndo inayompa raisi madaraka ya kuteua watu wa Tume ya uchaguzi (marefaree).
 
Mimi naona hakuna ukweli uliopindishwa na Dr. Slaa hata kidogo. Tukumbuke kwamba katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati matokeo ndio yameanza kutangazwa na NEC alisema kabisa kuwa ameamua kusema mapema kabla ya rais kutangazwa kwa kuwa akishatangazwa rasmi huwezi kuhoji tena. Ndio kauli ileile anayoeleza hata sasa, kwamba SHERIA AU KATIBA INATAMKA KUWA RAIS AKISHATANGAZWA HUWEZI KUBADILISHA CHOCHOTE. Ila matukio yaliyofanyika bungeni na hata yanayoendelea kufanyika sasa ni kuufahamisha umma juu ya mwenendo na mfumo wa uchagguzi ulivyokuwa mbovu ili kuweza kuchukua hatua.

Watanzania inatupasa kutambua kuwa sote tunaathirika na mfumo mbovu na kwa hivyo tuna wajibu wa pamoja kubadilisha mfumo ili kuleta ahueni kwetu sote.

Maralia Sugu, Dar es salaam na konokono wengine vaeni miwani msome hiyo juu hapo...
 
Hoja hapa siyo kukataa au kukubali matokeo yaliyopita bali kurekebisha mfumo mzima wa uchaguzi ili uwe na uwazi na wa kuaminika kuanzia sasa na kuendelea.
Malumbano ya kishabiki yenye mlengo wa kivyama vya kisiasa ni upuuzi katika jambo hili ambalo ni muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu. Mambo ya msingi ya kitaifa kama kuboresha mfumo wa uchaguzi na madai ya katiba mpya siyo ya kujadili kwa kuegemea itikadi za kivyama bali kuweka utaifa mbele.
 
SLAA(PhD) ya ukweli kiongozi wa nguvu ya umma sio wa katiba amekuwa wazi na amekuwa akiweka sawa msimamo wake, chadema na watanzania kabla ya kutangaza matokeo, wakati matokeo ya kidikiteta yakitangazwa na baada ya kuapishana kidikiteta. Asiyetaka kuelewa ni mnafiki na mgonjwa. Dr Slaa anafahamu sheria alikuwa na choice tatu muhim za kuchukua kujitangazia ushindi kama alivyofanya Quattara, au kuamuru nguvu ya umma idai haki au kutumia ustarabu na majadiliano kuweka sawa na kuondoa serikali za kidhalimu ambalo ndilo amelichukua -sasa asiyetaka kuelewa ana lake jambo. Kimsingi Dr.Slaaa na Chadema wanalengo kubadili mfumo huu wa kidikiteta na kinyonyaji hawana fitina na mtu wana fitina na mfumo na wale wanaokumbatia mfumo huo. KWAHIYO KWA GREAT THINKER YOYOTE ATAELEWA NINI CHADEMA WANAFANYA, KWA KATIBA YA SASA INARUHUSU UZANDIKI WOTE ULIOTOKEA NDIO MAANA TUNASEMA KATIBA MPYA NDIO KILIO CHA GREAT THINKERS. THIS IS NOT FOR CHADEMA IT IS FOR TANZANIA OR TANGANYIKA
 
Kiranga mawazo yako yanaheshimika. Maoni yako yanarepresent one school og thougt na ya Dr Slaa the other.

Tofauti yenu( wewe na Dr Slaa) ni kuwa wewe unaongea kipropaganda (kiccm ccm) wakati Dr Slaa anazungumzia facts. Je, unataka nini zaidi kama KATIBA HAIRUHUSU MATOKEO NA PROCESS KUWA CHALLENGED IN COURT?

Nadhani hupaswi kuongea tuu bali na kuweka facts.

Je wewe unakula asali, unamaanisha kuwa unakubalia na process ya nyuki kuokota kila penye uozo? Sio kuwa unakula asali kwa sababu ni tamu na unafumbia macho process?

Mkuu kwenye asali hata mie nilikuwa sijawahi kujiuliza. Kumbuka msemo wetu " ukimchunguza kuku alacho huto mla". Kweli natamani nyuki watengeneze asali kutoka sehemu nzuri tu!
 
Slaa ameamua kula matapishi yake mwenyewe, baada ya kuona nguvu ya umma imemwacha peke yake akihangaika ameamua kujirudi kwa maneno yake mwenyewe. Huyu mzee amekuwa mtu wa kujichanganya sana haeleweki na amekosa mwelekeo. Kweli mfa maji haishi kutapatapa
  1. 'ThinkTwice' - you are not thinking twice.
  2. Hivi Slaa alipaswa afanye nini ili Watanzania kama TT waone kuwa ameonyesha busara katika maamuzi yake?
  3. TT, ulitaka uone akijiapisha mwenyewe kama kule Ivory Coast? Au ulitaka aamrishe watu waingie mitaani kudai yeye kuwa rais? Kama angefanya lolote kati ya hayo mawili ni dhahiri hoja ya JK kuhusu damu kumwagika ungekuwa ni unabii uliotimia.
Mimi naamini Dr. Slaa ameangalia mbali sana na kukubali kuweka kando maslahi binafsi na kujali utaifa zaidi. Hii haina tofauti na kilichotokea Zanzibar katika uchaguzi huu huu. Si kuna tetesi kuwa Maalim Seif alishinda na kwamba Dr. Shein alikuwa tayari kukubali ila system ikazuia na Seif akakubali akijua mambo yatarekebishwa ndani kwa ndani!!!
AMANI NI UFUNGUO WA YOTE!
 
Dr. Slaa anapoelezea yuko sahihi kabisa na ndio msimamo wake toka mwanzo; huu sina tatizo nao kwani unakubaliana na hali halisi na mtiririko wa mantiki. Je huu ndio msimamo wa uongozi mzima wa Chadema?

Yes, Kwa sababu Dr Slaa alikuwa anatoa tamko ra Chama kupitia kamati kuu, yale mengine yote yanasosemwa ni minong'ono tu ya baadhi ya watu,
Jamani tukumbuke pia kuwa mara nyingi sio rahisi watu wote kukubaliana kwenye kila jambo, kwa tunaotumia demokrasia ya wengi wape basi tunafuata msimamo wa wengi, Kwa Chadema nataka kuamini asilimia kubwa (Majority) wanaungana mkono na kamati kuu na msimamo huu na minority wanapinga, Kwahiyo tunafuata msimamo wa wengi
 
Slaa apiga Chenga ya Mwaka. Nadhani hicho kingekuwa kichwa cha habari kizuri sana kwa hii thread.

Hiyo ndio chakachuwa orijino from Slaa.

"Watarudi".

Kachakachua? Kabla ya kufanya hicho unachokiita uchakachuzi wa mwaka ulikua unamsupport? Kama jibu ni hapana kaa kimya basi.
 
Huwezi kukataa process halafu kukubali zao, simple as that. Either unakataa process na zao, au unakubali process na zao.

wewe nawe kiranga acha kiranga,unachosema inategema unaongelea ishu gani,kama ni ishu ya production i mean uzalishaji wa chakula unao involve process mbovu ofcoz lazima na product itakua mbovu so unaweza ikataaa,bt unapoongelea swala la election na democracy ni tofauti sanaa,ss process ya kumchagua raisi iwe mbofu mbofu na ya wizi then outcome yake ni raisi asie represnet matakwa ya wananchi then unasema nikubali is that fair...so ivory cost na wizi wooote wamkubali tu yule kibaka,mhh jamani umu itabidi ifike wakati tuchuje great thinker na less thinker mana wengine wanaongea tu ili mradi wameongeaaaa..inaboa sana
 
. KWAHIYO KWA GREAT THINKER YOYOTE ATAELEWA NINI CHADEMA WANAFANYA, KWA KATIBA YA SASA INARUHUSU UZANDIKI WOTE ULIOTOKEA NDIO MAANA TUNASEMA KATIBA MPYA NDIO KILIO CHA GREAT THINKERS. THIS IS NOT FOR CHADEMA IT IS FOR TANZANIA OR TANGANYIKA
Tulipoingia uchaguzi mkuu hawakuwa wamebahatika kuisoma hiyo katiba??? Je katika mfumo wa kidiplomasia na mazungumzo bila nguvu ya umma ccm wata surrender na kuachia utamu waliokamata miaka 49 sasa??? isingekuwa vema hata kuhusisha wananchi kidiplomasia kwa njia za mikutano n.k
 
Dr. Slaa na Chadema yake ndiyo vigeugeu..........utawala bora unatuelekeza sote endapo hukubali waenda mahakamani......na huko hawataki kwenda kwa tafsiri zao za katiba ambazo zinakinzana namaamuzi ya Mahakama kuu ya mwaka 1995...................sasa sisi kwa nini tusitoe tafsiri zeti wenyewe..........where there is a dearth of quality leadership?

Asante sana kwa kulitambua hilo ndugu Rutashubanyuma.
 
Huwezi kukataa process halafu kukubali zao, simple as that. Either unakataa process na zao, au unakubali process na zao.

mkuu inafuatana ni process ipi,ukipanda mchungwa lakini ukachange kibaolojia ukazaa limau,je utavuna au utagoma kuwa haukuzaa? Inabidi ukubali kuwa ulizaa lakni sio mategemeo yako.
 
Dr. Slaa anapoelezea yuko sahihi kabisa na ndio msimamo wake toka mwanzo; huu sina tatizo nao kwani unakubaliana na hali halisi na mtiririko wa mantiki. Je huu ndio msimamo wa uongozi mzima wa Chadema?
Hilo ni tamko la CC au unataka wanaCDM wote tuwepo studio wakati Katibu anatangaza, au unataka hadi umuone nani anatangaza ndipo uwe msimamo wa uongozi wote.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom