Longolongo kwisha: Slaa amaliza misunderstanding hapa jf

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
14
Akizunguzia suala lililozua mjadala la uchaguzi mkuu, Dk Slaa alisema kamati kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais kujadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete yalichezewa.Alisema kutokana na sababu hizo, Chadema imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

“Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa,” alisema Dk Slaa.

“Kisheria Tanzania ina rais na sisi Chadema tunasema nchi hii ina rais, lakini njia iliyutumika kumpata rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa Chadema kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge,” alisema Dk Slaa.

"Unajua hapa suala la kutambua au kutokumtambua rais siyo issue. Rais yupo na katiba inaelekeza kwamba rais akishachaguliwa huwezi kuhoji mahali popote na kwa maana hiyo rais yupo. Tatizo ni jinsi alivyopatikana."

MY TAKE:

Ninashauri JF tudiscuss kauli zinazotoka vinywani mwa wahusika zaidi ya "interpretations zetu wenyewe". Alichokisema Dr Slaa jana (soma mwananchi.co.tz ) ni kile kile alichokisema kabla matokeo rasmi ya TUME kutangazwa na pia siku ya ufunguzi wa bunge kule dodoma na na hata baada ya wabunge kutoka bungeni.

This is great consistent...hakuna shabra shabra...

Slaa apiga Chenga ya Mwaka. Nadhani hicho kingekuwa kichwa cha habari kizuri sana kwa hii thread.

Hiyo ndio chakachuwa orijino from Slaa.

"Watarudi".
 
Akizunguzia suala lililozua mjadala la uchaguzi mkuu, Dk Slaa alisema kamati kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais kujadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete yalichezewa.Alisema kutokana na sababu hizo, Chadema imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

"Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa," alisema Dk Slaa.

"Kisheria Tanzania ina rais na sisi Chadema tunasema nchi hii ina rais, lakini njia iliyutumika kumpata rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa Chadema kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge," alisema Dk Slaa.

Kuna mtu anaitwa MZEEMWANAKIJIJI, hajasikia hili la live, na matokeo yake amepandisha bandiko huko ambako ni la habari za magazetini, unlike this one from the horses mouth...Nimeboreka sana na ile thread, na nimesema wazi kwamba ni bora kuwa maneno ya Mwanakijiji yanakuwa MANENO TU..na practically hakuna mahali yanaweza kutumika!

Hii hapa, ni vichekesho tu
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/95110-chadema-must-apologize-unconditionally.html
 
Huwezi kukataa process halafu kukubali zao, simple as that. Either unakataa process na zao, au unakubali process na zao.
 
Sasa kama wanakataa utaratibu wa kumtangaza rais*anayeendelea*, ambaye ndie mteuzi wa huo utaratibu, kwa cheo chake na utashi wake, what hope do we have?

My fear kwamba wanasiasa wabongo ni wasanii na hawajui wanachofanya inazidi kuongezeka..next time wajameni siku ya uchaguzi na kampeni endeleeni na shughuli zenu..nchi imeshauzwa hii.
 
dk slaa kwani anakunywa bia? siamini kama anakunywa. kama anakunywa labda alipotoa kauli hiyo ilikuw a tayari ameonja

Dada MS, Uwe unajaribu angalau kusoma ujumbe kabla ya kujibu. ndiyo maana unaolewa na kuachwa kila mara. unadandia vitu pasipo kutafakari. Hata kama ni kada ccm, si kwa staili hiyo. Kauli ya Dr Slaa iko clear, ila kama umelewa unapoisoma hauwezi kuielewa.
 
Mimi naona hakuna ukweli uliopindishwa na Dr. Slaa hata kidogo. Tukumbuke kwamba katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati matokeo ndio yameanza kutangazwa na NEC alisema kabisa kuwa ameamua kusema mapema kabla ya rais kutangazwa kwa kuwa akishatangazwa rasmi huwezi kuhoji tena. Ndio kauli ileile anayoeleza hata sasa, kwamba SHERIA AU KATIBA INATAMKA KUWA RAIS AKISHATANGAZWA HUWEZI KUBADILISHA CHOCHOTE. Ila matukio yaliyofanyika bungeni na hata yanayoendelea kufanyika sasa ni kuufahamisha umma juu ya mwenendo na mfumo wa uchagguzi ulivyokuwa mbovu ili kuweza kuchukua hatua.

Watanzania inatupasa kutambua kuwa sote tunaathirika na mfumo mbovu na kwa hivyo tuna wajibu wa pamoja kubadilisha mfumo ili kuleta ahueni kwetu sote.
 
Huwezi kukataa process halafu kukubali zao, simple as that. Either unakataa process na zao, au unakubali process na zao.

Kiranga mawazo yako yanaheshimika. Maoni yako yanarepresent one school og thougt na ya Dr Slaa the other.

Tofauti yenu( wewe na Dr Slaa) ni kuwa wewe unaongea kipropaganda (kiccm ccm) wakati Dr Slaa anazungumzia facts. Je, unataka nini zaidi kama KATIBA HAIRUHUSU MATOKEO NA PROCESS KUWA CHALLENGED IN COURT?

Nadhani hupaswi kuongea tuu bali na kuweka facts.

Je wewe unakula asali, unamaanisha kuwa unakubalia na process ya nyuki kuokota kila penye uozo? Sio kuwa unakula asali kwa sababu ni tamu na unafumbia macho process?
 
Slaa apiga Chenga ya Mwaka. Nadhani hicho kingekuwa kichwa cha habari kizuri sana kwa hii thread.

Hiyo ndio chakachuwa orijino from Slaa.

"Watarudi".

Hicho ndicho ambacho kila kiongozi wa CHADEMA amekuwa akieleza toka mwanzo. All the time they have been very consistent. Ila kinachoshangaza ni hawa watu kama akina Dar Es Salaam wanaotengeneza maneno yao na kuyafanya ni ya CHADEMA wakifikiria watu wengine hawasikii wala kutafakari. Hongera Dr Slaa na CHADEMA kwa kusimama katika kauli zenu wakati wote na hiyo inawatofautisha na viongozi wa vyama vingi ikiwemo CCM.
 
Slaa apiga Chenga ya Mwaka. Nadhani hicho kingekuwa kichwa cha habari kizuri sana kwa hii thread.

Hiyo ndio chakachuwa orijino from Slaa.

"Watarudi".

Hii ndiyo kauli ambayo Dr. Slaa na CHADEMA wakati wote wamekuwa wakiitoa. They have been very consistent. Kuna magazeti ya CCM kama Uhuru na Habari Leo na watu kama akina Dar Es Salaam ambao wamekuwa wakitengeneza maneno yao wakidhani watu wengine hawasikii na hawafikiri. Hongereni Dr Slaa na CHADEMA, hii inawatofautisha sana na viongozi wa vyama vingine ikiwa ni pamoja na CCM. Inaonekana mnatoa kauli baada ya kuchunguza na kutafakari na siyo kwa kuropoka ndiyo maana hatuoni kauli zinazobadilika badilika kama zile za CCM.

Hii inatupa imani kuwa siku mkishika serikali, mtakapotuambia kuwa tatizo la umeme limekwisha au mgao umekwisha, itakuwa hivyo, siyo kama sasa ambapo Rais, waziri anatamka kuwa tatizo la umeme litakuwa historia, halafu baada ya siku 5 mgao unaanza!
 
Yaani mpaka sasaa hamuamini kuwa Slaa kachakachuwaa? Au tu haiingii akilini?
 
Slaa ameamua kula matapishi yake mwenyewe, baada ya kuona nguvu ya umma imemwacha peke yake akihangaika ameamua kujirudi kwa maneno yake mwenyewe. Huyu mzee amekuwa mtu wa kujichanganya sana haeleweki na amekosa mwelekeo. Kweli mfa maji haishi kutapatapa
 
Mheshimiwa THINK TWICE sidhani kama unafanya kadri ya ID yako hapa kwenye jamvi

Slaa kwa maneno kutoka kinywani mwake mwenyewe alisema hamtambui rais kutokana na kutotambua mchakato wa kumpata au unabisha hilo pia?

Hakuna mantiki ya kumtambua rais na kusema hutambui mchakato wa kumpata.

Wangeendelea kusema Tanzania inae rais kisheria lakini sisi hatumtambui kwa sababu hatutambui sheria zilizomuweka tungewaelewa.

Sasa wanatafuta kujisafisha wakati vidhibiti vinawasuta
 
Akizunguzia suala lililozua mjadala la uchaguzi mkuu, Dk Slaa alisema kamati kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais kujadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete yalichezewa.Alisema kutokana na sababu hizo, Chadema imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

"Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa," alisema Dk Slaa.

"Kisheria Tanzania ina rais na sisi Chadema tunasema nchi hii ina rais, lakini njia iliyutumika kumpata rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa Chadema kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge," alisema Dk Slaa.

"Unajua hapa suala la kutambua au kutokumtambua rais siyo issue. Rais yupo na katiba inaelekeza kwamba rais akishachaguliwa huwezi kuhoji mahali popote na kwa maana hiyo rais yupo. Tatizo ni jinsi alivyopatikana."

MY TAKE:

Ninashauri JF tudiscuss kauli zinazotoka vinywani mwa wahusika zaidi ya "interpretations zetu wenyewe". Alichokisema Dr Slaa jana (soma mwananchi.co.tz ) ni kile kile alichokisema kabla matokeo rasmi ya TUME kutangazwa na pia siku ya ufunguzi wa bunge kule dodoma na na hata baada ya wabunge kutoka bungeni.

This is great consistent...hakuna shabra shabra...

Amani tuko pamoja katika hili!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Naamini ndiyo msimamo wa wanaJF wa kweli????????????????????????
 
Naona bado hamjamuelewa Dr. Slaa.... Anachomaanisha Dr ni kwamba tume ya uchaguzi ikishatangaza mshindi hawezi kupingwa na mahakama au chombo chochote kile....That is to say, hata kama CHADEMA hawakuridhika na mchakato uliomwingiza JK madarakani ila kwa mujibu wa sheria hakuna ujanja bado JK atabaki kuwa rais wa TZ even without CHADEMA's recognition.

Pengine hii ndio sababu CHADEMA wameamua kuelekeza nguvu zao kwenye mabadiliko ya katiba na tume ya uchaguzi
Sasa kama wanakataa utaratibu wa kumtangaza rais*anayeendelea*, ambaye ndie mteuzi wa huo utaratibu, kwa cheo chake na utashi wake, what hope do we have?

My fear kwamba wanasiasa wabongo ni wasanii na hawajui wanachofanya inazidi kuongezeka..next time wajameni siku ya uchaguzi na kampeni endeleeni na shughuli zenu..nchi imeshauzwa hii.
 
Dr. Slaa anapoelezea yuko sahihi kabisa na ndio msimamo wake toka mwanzo; huu sina tatizo nao kwani unakubaliana na hali halisi na mtiririko wa mantiki. Je huu ndio msimamo wa uongozi mzima wa Chadema?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom