Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
WAMACHINGA, WAPUUZENI HAWA HAWANA SERIKALI
HOTUBA YA MGENI RASMI NDUGU.MHONGA SAID RUHANYWA(MB) VITI MAALUMU CHADEMA KATIKA MKUTANO NA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA UZINDUZI WA RIPOTI YA WAMACHINGA KIGOGO SAMBUSA.
16,MACHI 2008 DAR ES SALAAM.
Ndugu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi,
Ndugu Mkurugenzi wa Vijana wa Chadema,
Ndugu Viongozi wa SERIKALI ,
Ndugu Viongozi wa Wafanyabiashara,
Mabibi na Mabwana,
Awali ya yote Niwashukuru kwa kunipa fursa hii ya kuwa mgeni rasmi na pia Niwashukuru kwa kufika kwenu hapa kuhudhuria tukio hili muhimu la mkutano wa wafanyabiashara ndogondogo wa mkoa wa Dar Es Salaam na uzinduzi wa Ripoti hii muhimu ya Wafanyabiashara Ndogondogo iliyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Uchunguzi huu ulifanyika katika kipindi cha miezi minne Aprili hadi Julai 2007 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Daresalaam.Dar es salaam imechukuliwa kama sampuli ya wafanyabiashara ndogondogo wa Tanzania.
Nawapongeza kwa kufanya uchunguzi huu ambao ulifanyika katika masoko mbalimbali katika wilaya zote za jiji la Daresalaam,masoko hayo ni kama vile soko la Makumbusho,soko la Nyuki, soko la Tegeta, soko la Kawe, soko la Mkwamani, soko la Kinondoni, soko la Chai Bora, soko la Urafiki, soko la Shekilango soko la,Mwenge, soko la Sinza, Posta Barabarani, Tegeta barabarani, soko la Tazara, soko la Tandika, soko la Temeke mwisho, soko la Kigogo Sambusa, soko la Mbagala Sabasaba,Zakhiem na Rangi tatu soko la,Mtoni Mtongani, soko la Mtoni kwa Aziz Ally, soko la Mwembe Yanga, soko la Kituo cha Polisi Changombe na soko la Yombo.
Nawapongeza kwa Uchunguzi huu ambao ulifanywa chini ya Kurugenzi ya vijana CHADEMA kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisasa katika kupata taarifa sahihi.Mbinu hizo ni pamoja na kufanya mahojianao ya ana kwa ana na wafanyabiashra ndogondogo (Wafanyabiashara ndogondogo) na kupata maelezo mbalimbali ya tatizo la Wafanyabiashara ndogondogo toka kwao, pia kutembelea na kuona mazingira halisi ya masoko ya zamani na mapya.Kurugenzi pia ilipokea maoni na mitazamo kutoka kwa watu mbalimbali wasiofanya biashara hizo na taasisi mbalimbali hapa nchini.Kurugenzi iliwalihoji watu wapatao 500 katika kupata taarifa mbalimbali katika zoezi zima la uchunguzi huu.
Ndugu wananchi,
Mtakubaliana na mimi kwamba Tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi hii kumekuwepo na kasi kubwa ya ongezeko la vijana wengi kukimbilia mijini kwa lengo la kutafuta ajira kutokana na vijana kukabiliana na hali ngumu kimaisha huko vijijini.
Hata hivyo, katika miaka ya 70 kasi ya ongezeko la vijana kwenda mijini ilipungua kutokana na mchakato wa uimarishaji vijiji na sera nzuri za kilimo wakati huo ambapo kwa sehemu kubwa kilimo kilionekana ajira ya maana hata kwa wananchi wa kawaida kutokana na mazingira mazuri ya sera ya ushirika na masoko wakati huo,ni pamoja na msukumo mkubwa wa serikali ya wakati huo katika sekta ya kilimo ambapo serikali ilihakikisha inaingilia kwa kiasi kikubwa mfumo mzima wa soko na uzalishaji kuhakikisha mkulima analindwa badala ya kuachia nguvu za soko kuamua hatma ya mkulima duni asiyejiweza kiushindani kukabili nguvu za soko.
Katikati miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 hali ilibadilika kwani kulikuwa na mfumuko mkubwa wa vijana kutoka vijijini na kukimbilia mijini hususani Dar es salaam.Hii ilitokana na sera ya uchumi wa Tanzania kubadilika kutoka kwenye Sekta ya Umma yaani uchumi hodhi na kuingia kwenye soko huria ambayo ni sekta ya kibepari na hivyo kufanya sekta ya kilimo kuwa ngumu na vijana wengi walianza kujitosa kwenda mijini kwa lengo la kujitafutia ajira ili kujikwamua na hali duni ya maisha.Wengi wa vijana hawa walikuwa wakitoka mkoa wa Mtwara katika kijiji cha Wafanyabiashara ndogondogo na kufanya jina la wamachinga kutumika kumaanisha wafanyabiashara ndogondogo na kuwa maarufu Tanzania nzima,vijana walikuwa wakienda mijini kwa lengo la kutafuta ajira lakini waliishia kufanya biashara ndogondogo kama vile uuzaji wa nguo za mitumba,viatu ,soksi,mabegi na bidhaa nyingine ndogondogo za dukani kama vile vifaa vya urembo n.k.
Wafanyabiahsra hawa walikuwa wakipata faida sana kwa kipindi hicho na hivyo kuwatamanisha vijana wengine waliokuwa kijijini Wafanyabiashara ndogondogo na kuwafanya vijana wengi zaidi kukimblia mijini kwa lengo la kujaribu bahati zao na wao.Tatizo hili la vijana kukimbilia mijini sio tatizo la Dar es salaam peke yake hata kwenye miji mingine mikubwa ndani na nje ya Tanzania kama vile Mwanza, Arusha, Dakar(Senegal) na Durban (Afrika ya Kusini).Mwishoni mwa miaka ya 1998 idadi ya wafanyabiashara ndogondogo ilikadiriwa kuwa ni laki nane na hamsini elfu-850,000 sawa na asilimia 24.2 ya wakazi wote wa jiji la Dar es salaam.Kati ya hao asilimia 80.8 ni vijana wenye umri kati ya 20-29 na kati yao asilimia 92 walikuwa na elimu ya msingi tu.Kati yao asilimia 18.4 wanatoka Mtwara, asilimia 15.2 Morogoro, asilimia 15.2 Pwani, asilimia 14.0 Tanga, asilimia 10.8 Lindi, asilimia 8.0 Mbeya,na asilimia 3.8 Iringa na asilimia 14.6 sehemu nyingine za Tanzania.Hali hii ya vijana kutoka vijijini na kwenda mijini kwa lengo la kujitafutia chochote ili kujikwamua kimaisha imeendelea hadi katika miaka ya hivi karibuni na kusababisha mijini kuwa na idadi kubwa ya watu ukilinganisha na vijijini.
Ndugu washiriki,
Zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo katika maeneo yao limekuwa na athari kubwa kwa wafanyabiashara ndogondogo na hali ya amani katika jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo; Zoezi zima liliambatana na matumizi makubwa ya nguvu,hivyo kusababisha wafanyabiashara ndogondogo kupoteza bidhaa zao. kupoteza mitaji ,na mpaka sasa bado kuna madai mengi ya wafanyabiashara ndogondogo na bado Serikali imekuiwa ikisita kutimiza majukumu yake.
Ndugu Wananchi na Viongozi wenzangu
Mtakumbuka kuwa Baada ya agizo la waziri mkuu kuwa yaandaliwe maeneo maalumu kwa ajili ya masoko ya Wafanyabiashara ndogondogo kabla ya kuhamishwa, mamlaka ya jiji ilitenga maeneo hayo ambayo hata hivyo yalionekana kutokuwa muafaka kwani mgogoro, miutano na mapigano kati ya Wafanyabiashara ndogondogo na mamlaka ya jiji uliendelea. Kwa sehemu kubwa hali hii ilitokana na mazingira na hali ya masoko mapya kwa ujumla wake. Mfano Kwa ujumla masoko mengi ya zamani yalikuwa imara kidogo ukilinganisha na masoko mapya, Pia sehemu nyingi za masoko ya zamani zilikuwa zikifika kirahisi kwa kutumia usafiri wa kawaida yaani daladala. Katika masoko hayo huduma zifuatazo zilikuwa zikipatikana kwa urahisi Huduma za choo, Chakula safi
Usafiri wa daladala na teksi, Huduma za maji,Huduma ya sehemu ya kuhifadhia mizigo na mali za wafanyabiashara.
Hadi Julai 2007 ambapo ziara ya kuzungukia maeneo haya ilifanyika hali ilikuwa mbaya pamoja na Serikali kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya masoko mapya yale ya SOKO LA TAZARA, MBAGALA RANGI TATU, SOKO LA TANDIKA, pia nayo yalikuwa hayaridhishi kwa maana ya miundo mbinu na huduma nyingine muhimu ndani ya soko Yafuatayo ni baadhi ya mapungufu yake mengine yapo pembezoni mwa barabara Mandela upande wa kushoto kama unatokea Buguruni kwenda kiwanda cha bia ya Serengeti mkabala na soko hilo ni eneo la Tazara,Hakuna stendi ya mabasi katika eneo lililo na soko, Hakuna huduma ya choo katika soko hilo, Hakuna barabara inyoingia ndani ya soko, Soko lipo eneo linalomilikiwa na Radio Tanzania hivyo kuna mtafaruku kati ya taasisi hiyo na wafanyabiashara.Soko halina ghala la kuhifadhia mizigo (stoo) soko liko mbugani kiasi ambacho mvua zikinyesha kwa wingi eneo hilo hujaa maji,.Mabanda yaliyopo hayana ubora.Mita chache kutoka sokoni hapo kuna uwanja wa mpira wa miguu hivyo kuleta usumbufu kwa wafanyabiashara wawapo kazini,Mabanda mengi yapo wazi kwasababu soko halina wateja, pengine Hakuna choo cha soko,kilichopo ni cha mtu binafsi na mbaya zaidi kipo ndani ya mabanda ya wafanyabiashara hali ambayo ni hatari kwa afya ya wafanyabiashara hao.Hakuna barabara inayoingia sokoni hivyo kuathiri upatikanaji wa wateja Soko lipo nje sana ya mji hivyo inakuwa vigumu kwa watu kwenda kufanya manunuzi katika maeneo hayo hasa ikizingatiwa kuwa wafanyabiashara ndogondogo wanauza bidhaa ndogondogo.
Ndugu wafanyabaishara Ndogondogo,
Kama leo hii Chadema ingekuwa madarakani na kwa mujibu wa Sera zetu tungeweka mazingira mazuri kwenu na tungefanya yafuatayo
1. Tutaweka kipaumbele katika mazingira ya kuongeza fursa za ajira
2. Tutatengeneza ajira milioni moja kwa mwaka mmoja kwa kuimarisha sekta ya ujenzi, madini, kilimo, utalii, na huduma za jamii.(sawa na ajira milioni 5 katika kipindi cha miaka mitano).
3. Kuanzisha biashara na viwanda vidogovidogo
4. CHADEMA iliahidi kuongeza mitaji kwa vijana wafanyabiashara
5. Tutarasimisha na kuwezesha wafanyabiashara ndogondogo kufanya biashara zao kwa uhuru.
6. Tutaweka kipaupembele umuhimu wa kurekebisha ajira na maslahi ya wafanyakazi
Ndugu wananchi,
Nachukua fursa hii kuitaka SERIKALI iipokee ripoti hii na kueleza hatua zitakazotakiwa na kwa namna ya pekee kabisa tunatoa rai kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kueleza umma kuhusu hatua zilizofikiwa kuhusu ahadi aliyoitoa wakati wa kuwahamisha wamachinga kwamba wanapelekwa mahali kwenye anuani ili wawapatie mafunzo,ujuzi, na mitaji.
Tunasikitika sana kwamba mpaka sasa hawajawapatia mafunzo,
ujuzi, wala mitaji.Hivyo tunaitaka SERIKALI yake kuweka bayana ni lini ahadi hiyo itatitimizwa.
Nawatakia mafanikio mema katika biashara zenu,nawasihi mpendane na mshirikiane katika kutatua matatizo yanayowakumba kila siku katika biashara zenu.
Nawashukuru kwa kunisikiliza.
MHONGA SAIDI RUHWANYA(MB) 16/03/2008