Londa amgeukia Zitto

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
713
1,240
Nimesoma hii habari hapa:http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/6/25/habari22.php

yenye kichwa cha habari hapo juu.

Ni vyema suala hili likajadiliwa, mwenye ile habari ya awali ya nukuu ya hotuba ya Zitto ubungo atuwekee hapa.

Lakni mambo mawili yapo wazi:

Mosi, Londa ameshindwa kukanusha kwamba amesoma yeye hotuba ya bajeti. Ninayo hapa nakala ya hotuba yake ya kuwasilisha bajeti. Aliwasilisha yeye bajeti badala ya mkurugenzi wa halmashauri. Manake ni kwamba legislative arm ndiyo iliyowasilisha bajeti badala ya executive ambayo ni tofauti na dhana ya good utawala bora na uwajibikaji.

Pili; mapato aliyosema Zitto kuwa halmashauri imekusanya ya bilioni 7 na ushee kama kodi, yapo kwenye hotuba yake mwenyewe Londa. Hiyo bilioni 11 aliyoitaja amecheza na maneno kwa kuchanganya mapato yote ya halmashauri ikiwemo misaada ya kimaendeleo.

Kwa hiyo kwa ujumla Londa anaendelea kujichanganya!

Alipowasilisha bajeti vyombo kadhaa vya habari vilimnukuu, kama kuna mwenye links za magazeti ya siku iliyofuata atuwekee.

Lakini ameshindwa kabisa kujibu hoja kuhusu Jimbo la Ubungo kutokupewa kipaumbele katika bajeti ya mwaka huu ya halmashauri ya kinondoni hususani katika suala ujenzi wa barabara za lami

JJ
 
Hii issue imechukua sura mpya huko Bungeni naambiwa kuwa hata ma MP wa Dar nao wanalakwao jambo juu ya Zitto sasa hawa watajichanganya kama Mkullo ,mpaka siku ya mwisho
 
Back
Top Bottom