Loliondo na Uuzwaji wanyama Hai, Waziri Maliasili/Utalii amepwaya

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,550
11,879
Kwanza alionekana kuingia Bungeni ukiwa umechelewa na kukaa nyuma ya waziri mkuu.

Wakati huo yeye Waziri mkuu akiwa amesimama akitoa taarifa serikali Bungeni,juuya hali halisi ya kilichokuwa kikiendelea huko Loliondo.

Kama waziri husika wa sekta hiyo,baada ya tamko la serikali Bungeni,kupitia waziri mkuu.

Tulitarajia Waziri au naibu waziri wa Maliasili na utalii, aelekee site Loliondo na kusimamia zoezi husika kwa ukaribu.

Tulitarajia waziri wa maliasili na utalii uwe mtu sahihi wa kuliambia taifa juu ya ukweli halisi wa kile kilichotokea na kinachoendelea kutokea kwa uhalisia na ukweli wake sahihi.

Jambo hili lingetuwezesha kujua ni nani na nani ndio wapotoshaji wa kile kinachoendelea baina ya jamii ya wamaasai na serikali kwa upande wake.

Lakini Pia lingeiwezesha Dunia nzima ikiwa pamoja na wadau wa utalii wanaofanya kazi na Tanzania.

Kuweza kuujua ukweli.
Na hivyo kuzipuuza baadhi ya taarifa zinazoendela kuleta sintofahamu mitandaoni,ambazo zingine zina lenga upotoshaji ambao sio mzuri kwa serikali na sekta ya utalii nchini kwa ujumla.

Badala yake tunamuona mkuu wa mkoa ambaye anatoa taarifa ambayo kiuhalisia ni kwamba haikujitosheleza na badala yake imeongeza maswali mengi kuliko majibu.

Suala la Loliondo ni la kitaifa zaidi kuliko wanavyotaka lionekane.
Suala hilo hakupaswa kuachiwa mkuu wa mkoa peke yake.

Ni hivi majuzi tu waziri wa maliasili na utalii, alituachia sintofahamu nyingine,pale alipojitokeza kusitisha amri au tamko la serikali.

Kuhusu kuruhusu vibali vya uuzwaji wa wanyama hai kupelekwa nje ya nchi.

Altoa taarifa ya serikali ikikanusha na kusitisha taarifa nyingine ya serikali hiyohiyo.

Jambo hilo mpaka sasa bado lina Utata mwingi mbele ya jamii ya kitanzania,lakini pia hata nje ya Tanzania.

Sasa waziri na Naibu waziri wa wizara ya maliasili na utalii,ni kama vile wamekaa pembeni na kumuachia sakata lote Mheshimiwa waziri mkuu.

Wote wameng'ang'ania kukaa Dodoma kuliko kwenda Site kutimiza wajibu wao.

Je!
Tukisema wamepwaya Loliondo,tutakuwa tunawakosea?
 
Usisahau wakati PM anasema Waziri wa Maliasili anaongoza kikosi kazi huko Ngorongoro,Waziri mwenyewe alionekana nyuma yake PM.

Serikali ya uongo uongo ni serikali ya kishetani kwani baba wa uongo ni shetani.
 
Huyu waziri naona Kama anapwaya. Wizara aliyopewa imemzidi uzito. Nadhan tatizo lipo kwenye teuzi kuonekana wizara zote nyeti wanazo wanawake bila kujali uwezo wa huyo mwanamke.
 
Ni wazi kabisa
 
Wabunge wamchongo wametengeneza mawaziri wa hovyo uozo huu unaanzia serikali. Za mitaa vyote vya mchongo
Mwendazake katuachia matatizo makubwa kwa kunajisi chaguzi na kusababisha viongozi Wa hovyo mpyuuuuu
 
Usisahau wakati PM anasema Waziri wa Maliasili anaongoza kikosi kazi huko Ngorongoro,Waziri mwenyewe alionekana nyuma yake PM.
Serikali ya uongo uongo ni serikali ya kishetani kwani baba wa uongo ni shetani.
Kuongoza co lazima uwepo site
 
Back
Top Bottom