Loliondo ipo kwa manufaa ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Loliondo ipo kwa manufaa ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fredmlay, Jan 10, 2011.

 1. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hivi majuzi Januari 5 mwaka huu gazeti la Raia Mwema liliandika habari kuhusu Ripoti ya tume iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga likidodosa ripoti hiyo kuzilemea NGO's zinazojihusisha na maisha ya wafugaji, ukiisoma (bofya hapa)utagundua kwamba hata wataalamu wanaotegemewa na nchi yetu ni tatizo kwa maendeleo yetu, kwamfano tume hiyo ya Shaban Malipula inashawishika kuona kwamba kiasi cha dollar milioni 2.7 kilicho changiwa na kampuni ya uwindaji ya OBC kwa kipindi cha miaka 13 ni kikubwa sana kwa maendeleo yetu bila kutafiti kwamba kwa kipindi hicho kampuni hiyo imesafirisha wanyama wenye thamani ya dollar ngapi?? Kwa kifupi kiasi hicho ni sawa na kuachia tani moja ya karanga kuondoka nchini nasisi kupewa kopo moja la peanut butter.

  Tuzinduke waTZ, nchi inakwisha, tuliowapa dhamana wamekunja mikono kisa wameshiba kakopo kamoja ka peanut butter...
   
Loading...