Loliondo Babu anachukua 500 Serikali inachukua 25000 Huu ni Wizi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Loliondo Babu anachukua 500 Serikali inachukua 25000 Huu ni Wizi!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ndallo, Apr 4, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Jamani sasa tunapokwenda sasa ni pabaya kuhusiana na hili sakata la kwenda kule Loliondo kupata kikombe cha Babu! Juzi nimeshuhudia mwenyewe hapa Arusha sasa hivi limeibuka sakata kati ya wanaojiita Sumatra/Trafick na wenye magari yanayokwenda Loliondo kupata kikombe cha Babu. kinachojiri hapa Arusha sasa hivi na nimeshuhudia kwa macho yangu wakati gari langu limekodishwa na watu waliokua wanakwenda Loliondo kwa Babu kupata kikombe, magari yamesimamishwa hadi pale tupate kibali ambacho wao wanadai kua tulipe Sumatra shilingi 9500 halafu baada ya hapo unatakiwa umuone vehicle inspecta akague gari naye anadai ni shilingi 10000 isitoshe mpaka huo mlolongo uishe iliupate hiyo Sumatra toa tena kitu kidogo kama shilingi 5000 sivyo utazungushwa ikiwezekana utalala bila kuondoka! jamani huu si wizi jamani? mwenye kutoa dawa yeye anatoza shilingi 500 yaani mia mbili za kanisa 200 za wafanyakazi wake halafu shilingi 100 ni ya Babu mwenyewe jamani tunakwenda wapi???? huu ni wizi? eti vehicle naye anakuzungusha na kukuambia gari lako halipigi honi kweli sasa imefika ule wakati wa mwananchi kujilipua kwa upuuzi kama huu na pia nahisi hata Babu kule Loliondo hajui hili jamani nawasilisha!
   
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Na kwasisi wenye magari ya utalii huwa tumeshakata hiyo Sumatra kwa kiasi cha shilingi 130000 kwa mwaka eti hawaihitaji hii Sumatra tuliyonayo sasa kinachofanyika ni kua hii Sumatra tunayolazimishwa kuwa nayo ya kiasi cha shilingi 9500 ni kwaajili ya kuendea kwa Babu tu! hii tuliyonayo tunawaachia siku unaamua kwenda kupeleka wageni porini na gari lako unarudishiwa ile Sumatra yako halufu ile uliyokata kwaajili ya kwenda kwa Babu unairudisha, ukitaka kwenda kwa Babu tena toa shilingi 9500 nyingine upewe Sumatra mpya jamani nashindwa kupata jibu naombeni msaada!
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pole ndugu yangu kwa mikasa ya serikali yako.

  Sumatra ainajaribu kuwasaidia TRA kuboresha makusanyo kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato!!

  Lazima serikali ijipatie kipato kutokana na utalii wa tiba kwa babu wa loliondo, manake wabongo wakiambiwa wafanye utalii wa ndani kwa hiari hawataki, sasa serikali imeona huu ndio wakati wa kuwapata, kwakuwa wanajua wakishawagonga wasafirishaji hizo elfu kadhaa lazima mtapandisha nauli na kwa kuwa bado "kitalu cha utalii cha babu wa loliondo" kina mvuto abiria watakubali kulipa kiasi mtakachotaka!!
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo huu ndio tuseme ndio utalii wa ndani serikali kutukandamiza kulipa hizi kodi mara mbilimbili sio mkuu?
   
 5. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  kuna baadhi ya watu wanataka kujipatia fedha ambayo itawatia lahana tuwakemeeni cha muhimu sheria ifuatwe basi.
   
 6. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ebu jaribu kuchunguza hiyo Tsh 9500 inaishia kwenye vitabu gani vya Sumatra. utachoka! Nchi ilisha uzwa.
   
 7. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Lakini si tumesikia diwani wa sehemu magari yanpokuwa amekataa wenye magari kutozwa hiyo hela au na je wanaoenda na helikopta je nao Sumatra wanawatoza?
   
 8. R

  Reasoning Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndallo, unasema tunapokwenda ni pabaya kwa sababu umetakiwa na sumatra kulipia gari yako 9000 wakati Babu anatoza 500 tu. Swali langu ni je wewe gari lako unakodisha kwa shilingi ngapi kwa kila abiria? Unaona wewe kudai 120,000 kwa kila abiria ni sawa na ni haki wakati babu anatoza 500 tu? Je mwananchi ajilipue kwa sababu umetakiwa kulipa 9000 au kwa sababu umemtoza nauli 120,000? Na mimi nikuulize Ndallo tunakwenda wapi na hizi nauli mnazotutoza? Je unaona mnawatendea watanzania maskini haki kabla wewe hujalalamikia Sumatra? au Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu!!!!
   
 9. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Duh! Ndallo, chunga sana TRA wasije kuulizia "Pay as you earn, earn as you pay" Man hiyo nauli nikubwa sana.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,138
  Trophy Points: 280
  Hao Polisi nna uhakika ni wachaga.
   
 11. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Inawezekana wakawa wachaga hao polisi kabisa
   
 12. S

  ShockStopper Senior Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ndallo usikae kimya, lazima ujibu hii.
   
 13. h

  hoyce JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jamani tuwe tunafuatilia habari. Maamuzi hayo yalifikiwa ktk kikao cha Lukuvi na ma RC wa mikoa mitano jirani na Arusha. Lengo ni kupata fedha za kuboresha barabara. Helkopta walisema itatozwa 150,000/- lakini hiyo 'kitu kidogo' hawakuipanga. Pia ni kutaka kudhibiti wingi na ubora/usalama wa magari yanayokwenda Loliondo.
   
 14. LD

  LD JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah, Loliondo gumzo Tanzania. Tumetulia na tume relax kujadili Loliondo, loliondo.......g
   
 15. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu! kuna haja gani ya kurudisha sumatra niliyokata kwenda Loliondo halafu nikiihitaji tena mnitoze shilingi 9500 huo ni usanii! tafuta gari la biashara halafu uliza kodi tunazolipia ili hilo gari liweze kutembea barabara za hapa Tanzania! zindukeni bei ya shilingi 120'000 kwaabiria wewe ulie uliza hilo swali je unajua hali ya barabara ya kwenda mpaka Loliondo ufike jinsi ilivyo? garama ya matengenezo hilo gari litakapo rudi? fungua macho au nenda kajiaonee!
   
 16. yatima

  yatima JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  RUSHWA NI ADUI WA HAKI ....................... he nilijua tu ..............lazima yaibuke ............siku za mwisho watu watakuwa wanapenda fedha kuliko kumpenda Mungu.
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135


  SUMATRA (serikali) na kina Ndallo hawana tofauti. Wote mafisadi kila mmoja kwa sehemu yake. Ndallo anapractice kufa kufaana. Hali kadhalika na serikali.
   
 18. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  ndio maana hata serikali imekaa kimya haitaki kuliongelea hili swala!
   
 19. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndallo; nakubaliana na wewe, tena hata hicho kiwango kinaweza kuwa ni kidogo ukilinganisha na risk ya kupeleka gari kule. Kwa kweli njia ni mbaya sana na gari linaweza kukaa huko siku nyingi kwa ajili ya foleni.
   
Loading...