LOL!....Waandishi Wabongo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LOL!....Waandishi Wabongo!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, May 19, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,641
  Likes Received: 82,289
  Trophy Points: 280
  Mradi wa EPZ muhimu kwa uchumi wa nchi Tuesday, 18 May 2010 21:46 Mwananchi

  JUZI Rais Jakaya Nyerere alifungua Ukanda Maalum wa Uwekezaji wa Viwanda kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa nje ya nchi maarufu kwa jina la EPZ jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo ambao umegharamiwa kwa fedha za wananchi ni kiasi cha Sh32 bilioni.

  Mradi huo ambayo si utasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua sekta ya viwanda nchini ulibuniwa wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Rais Benjamin Mkapa.

  Kama Rais Kikwete alivyompongeza Mkapa kwa uamuzi wa kuanzisha mradi huo mwaka 2005 na ujenzi wake kuanza katika utawala wa awamu ya nne, nasi tuwapongeza viongozi wote na hasa watendaji wa EPZ kwa kuweza kufanisha malengo waliyoweka kwa manufaa ya Watanzania.
  Tunaamini kwamba EPZ itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

  Ni mwanzo mzuri ambapo viongozi wameona wazi kwamba bila nchi kushamiri kwa viwanda vingi itakuwa ndoto kuleta maendeleo ya haraka.

  Vilevile, mpango wa EPZ ambao mbali na kujengwa hapa jijini Dar es Salaam kuna maeneo kadha kwenye mikoa yametengwa kwa ajili ya uwekezaji maalum kwa viwanda na miradi mingine kama mahoteli.

  Kwanza kabisa tunaamini kwamba maeneo ambayo yametengwa yatasaidia kuwarahisishia wawekezaji adha wanayopta katika harakati za kutafuta ardhi kwa ajili shughuli zao.

  Ni wazi kwamba ingawa Watanzania wengi wanajihusisha na kilimo, lakini tunapaswa kujua kwamba nchi hapaswi kutegemea kilimo pekee.

  Ndio maana mpango huu wa EPZ utasaidia kwa kiasi kikubwa kutumia mazao ya kilimo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuziuza nje ya nchi.
  Jambo muhimu ambalo tumejifunza katika mradi huu ni kwamba serikali imetumia fedha zake za ndani kwa ajili ya ujenzi wake hivyo kuondoa dhana iliyojengeka kwamba kila mradi lazima upatiwe fedha kutoka kwa wahisani.

  Tunaambiwa vilevile, eneo hilo litatoa ajira kwa maelfu ya vijana hivyo kuinua hali yao ya maisha
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Je wameandika ambayo hayakusemwa kwenye ufunguzi huo?
   
Loading...