Lockdown za Afrika ni ubabe na kutandikana viboko

mr vata

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
462
605
Afrika tunakosea wapi? Mbona tunapenda kutumia nguvu kwa kila jambo? Unamchapa viboko na kumdhalilisha baba ambae yupo na familia yake.

Mbona ulaya sijaona wakipigana mitaani kwa kisa kama hiki. Muhimu ni kuangalia nini chanzo cha watu kuendelea kutoka licha ya marufuku iliyotolewa. Hali ya uchumi ni mbaya mtu hawezi vumilia kukaa ndani na njaa yake.

Wengine wamefika mbali zaidi na kuwatandika raia risasi. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Unampiga mtu risasi kisa katoka nje au katumia usafiri wa uma. Kama angekua jambazi au muuaji ungempa adhabu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida iko hapa ni umaskini!!

Wananchi hawajiwezi kujihudumia wakiwa hawatoki kutafuta.. hii inamaanisha kuwa waafrika wengi hatuna akiba tunatafuta na kutumia!

Na serikali zetu haziwezi kutuhudumia ni maskini endapo huwa zinakusanya kodi zetu!! Ila bado hazitoshi kulisha nchi wakati wa tabu!!

So raia wanakuwa wakaidi kutokutoka watakufa na njaa!! Na serikali zisizojiweza zinaanza kulamba stiki raia zake!

Umaskini tatizo kubwa Sana.
 
Wahenga walinena punda haendi bila ya fimbo.
Karibia shithole countries zote wenye mamlaka hua wanawaona raia zao ni punda tu, mapato yenyewe ya raia ni chini ya dollar moja kwa siku halafu unamuamrisha ajifungie ndani mwezi mzima asitoke nje bila ya kumpatia msaada wowote wa mahitaji yake.
 
Sijasikia vijijini wakilia lia kama wa mjini. Chemsha mihogo tia pilipili na karanga siku ipite, shushia na ndoo ya maji.
 
Afrika tunakosea wapi? Mbona tunapenda kutumia nguvu kwa kila jambo? Unamchapa viboko na kumdhalilisha baba ambae yupo na familia yake.

Mbona ulaya sijaona wakipigana mitaani kwa kisa kama hiki. Muhimu ni kuangalia nini chanzo cha watu kuendelea kutoka licha ya marufuku iliyotolewa. Hali ya uchumi ni mbaya mtu hawezi vumilia kukaa ndani na njaa yake.

Wengine wamefika mbali zaidi na kuwatandika raia risasi. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Unampiga mtu risasi kisa katoka nje au katumia usafiri wa uma. Kama angekua jambazi au muuaji ungempa adhabu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona putin kafungulia Simba 500 huongelei Hilo??? India wanawachapa viboko mbona husemi hvyo?????

Vitu vingne Ni kuviacha vipite tu Mana dunian hakuna haki Wala usawa

kilicho akilini kitumie
 
Mbona putin kafungulia Simba 500 huongelei Hilo??? India wanawachapa viboko mbona husemi hvyo?????

Vitu vingne Ni kuviacha vipite tu Mana dunian hakuna haki Wala usawa

kilicho akilini kitumie
Hebu hiyo taarifa au video ya putin mkuu
 
Umesahau na India mwanzisha mada. Askari polisi wa India ni washenzi sana kama wa hapa kwetu. Watu ni maskini..mahitaji yao hutegemea shughuli ya siku husika wewe wataka akae ndani. Shenzi sana.
 
Akiba ni tatizo kubwa sana wa africa tunalo
Watu wengi hawafanyi kazi za kuajiriwa na miongoni mwao wengi ni wale ambao mpaka watoke ndio wapate riziki zao.
Mtu amepanga na ana familia, kipato chake ni mpaka atoke ndio familia ile. Serikali nyingi za africa haziwezi kuhudumia hizi kaya na watu hawawezi vumilia njaa. Wakitoka wanakutna na bakora.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom