Loan Board naombeni msinizungushe, shughulikieni tatizo langu

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
4,433
2,000
Wakuu jana nilibaini kuwa mdogo wangu kijijini katika application ya mkopo cheti cha kuzaliwa kilichoambatanishwa hakikuwa kile kilicho thibitishwa. Nilituma Dar es Salaam haraka cheti kilicho hakikiwa na Rita na kuomba mtu akipeleke HESLB, amepeleka wakasema eti ni lazima aliyetuma maombi ambaye yupo iringa apige simu kwao.

Kiutaratibu niliwaelewa lakini sikuona Kama limekaa kihuduma kwani hata namba ya mawasiliano nizile ambazo hazijakaa kiurafiki wengi wanaziita namba za gari.

Tumetafuta mawasiliano ya bodi ya mkopo mbeya tumewaeleza tatizo wanasema tutumie ile namba yenye 6 6. Hiyo namba haipo na hatujui tuitoe wapi.

Hivi nyie loan board ni watu gani mnao wahudumia maofisini mpo kwaajili ya Nani?

Huduma za namba hii mbona ofisi nyingi waliacha siku nyingi. Mnatuumiza sio bure
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom