Loan Board; Makato yamefanyika lakini deni halijapungua hata senti!!

Cunch

Senior Member
Apr 19, 2014
162
142
Wadau mnaokatwa deni la heslb fanyeni kucheck kwenye salary slip zenu za mwez April na May mwaka huu muone kwan deni halijapungua baada ya makato.
Je,hii hutokana na nini?
Au ndo 6% yenyewe hii??
 
Lakini hili tatizo sio kwenye Board ya mikopo tu hata kwenye mikopo ya Mabenki bado makato yapo vilevile na makato yamekatwa.
 
06% ya value retention fee ni wizi unaofanywa na Mzalendo na CCM yake! Wanufaika wengi hawajui ni hivi kwawanaodaiwa na Bodi/serikali mfano unadeni la 15M ukakatwa 15% ya kila mwezi kwa mwaka utakua umelipa takriban 2M kwa mwenye mshahara wa 1.2M sasa ikifika July Mosi yani mwaka wa fedha wanakata 06% ya kile kilichobaki yani 13M toka 15M kwahiyo 13M× 06%= 1,300,000/ Hivyo hiyo Million 1.3 inajumlishwa kwenye Deni lako la 13M unakuta deni limeongezeka tena hadi 14.4M unashangaaa.,.Hii ndo serikali ya wanyange..Waambieni Bodi ni jinamizi ni wezi wakiongozwa na Mzalendo
 
06% Retention fees haikatwi separate, bali kwenye deni lako. Kwanza hii huongezeka kila siku kwa kiwango cha %6/365 na sio 06% kila July kama ulivyoandika hapa.

Sema bado ni wizi sababu imeletwa 2014 lakini hutumika hata kwa wale waliokopa kabla ya mwaka huo.

Huu Uzi uungwe na https://www.jamiiforums.com/threads...d-wamekata-panga-ila-deni-limesimama.1597280/
 
Nataka tuu kufahamu nani anayetoa sallary slip na ni system gani inayorekodi kua makato haya yamefanyika na deni au madeni yamebakia kiasi hiki.

Wakati mwingine tutamlaumu mtu au watu wasiohusika. Nadhani kinachoonekana ni kwa watumishi wa serikali ambao system inayotumika kutoa sallary slip ni moja kama sijakosea. Ila nikiangalia kwa makini naona sio loan board bali ni mwajiri au mtandao anaoutumia mwajiri anayemiliki na kutoa sallary slip hiyo.

Kumbuka loan board huwa hawaoneshi kila mwezi kua deni lako limebaki kiasi gani bila ya wewe kuomba status.

Hayo ni maoni yangu i stand to be corrected.
 
Mkuu nashukuru sana kwa kuanzisha uzi huu...
Mi nilifikiri ni mimi peke yangu.

Nilitaka ku buy time nione mwezi huu wakikata itakuaje.

Hii ni shida.

Nitaziupload slip zangu hapa mshuhudie.

Sasa swali ni ... Hela zimeenda wapi!??

Magufuli why!!??
 
Nataka tuu kufahamu nani anayetoa sallary slip na ni system gani inayorekodi kua makato haya yamefanyika na deni au madeni yamebakia kiasi hiki.
Wakati mwingine tutamlaumu mtu au watu wasiohusika. Nadhani kinachoonekana ni kwa watumishi wa serikali ambao system inayotumika kutoa sallary slip ni moja kama sijakosea. Ila nikiangalia kwa makini naona sio loan board bali ni mwajiri au mtandao anaoutumia mwajiri anayemiliki na kutoa sallary slip hiyo.
Kumbuka loan board huwa hawaoneshi kila mwezi kua deni lako limebaki kiasi gani bila ya wewe kuomba status.
Hayo ni maoni yangu i stand to be corrected.
Mkuu hayo makato ni automatic.... April hela imekatwa lakini May deni ni lilelile...

Usitumie nguvu nyingi kwa vitu vyepesi.
 
Back
Top Bottom