Lo! Mwaikimba

NINAHASIRA

Member
Nov 5, 2010
58
9
Si kama nina chuki binafsi ila ctaki kukiamini hiki ambacho huyu mrithi wa maximo alichokifanya cha kumteua mwai kimba staz na kumuacha mgosi hivi kweli linaingia akilini au hiyo staz ni ya majaribio! Hebu tulijadili hili wadau.
 
Mwaikimba ni strike anayehitajika staz,umbo lake ni muhimu sana pale mbele,tatizo letu wabongo hupenda kuingilia kazi zisizotuhusu.kelele zetu zilisababisha kuondolewa kwake staz.nasisitiza mwaikimba anahitajika sana,angalia mechi ya mwisho vs morocco utaona mipira yote ya juu waliyopewa strikers wetu ilipotea
 
mpira sio umbo kijana! kumbuka maximo naye alichanganyikiwa na umbo la mwaikimba lakini baada ya mechi chache aligundua kuwa ni garasa! sasa unaponiambia umbo lake litasaidia hata sikuelewi! Pili anaonekana hafundishiki kama walivyo wachezaji wengi wa kibongo. Hivyo mm suala la kufanya majaribio katika staz kwa kuwa mechi ya moroco mipira ilikuwa inapotea sikubaliani nalo!
 
Suala c mgosi wala mwaikimba, tunahitaji kina trza mputu ,yaani wapishi wa magoli, huyo mwaikimba ukimuweka na xavi hernandezi lazima atawika tu, sisi hatuna wapishi wa magoli, ila mgosi naye si strika, ukweli tuseme, hamna kitu akiwa staz cjui ananini, ila simba anakimbiza, tatizo simba anacheza na wabovu wenzie ktk ligi akija ktk uwancha wa kimataifu ni pimbi tu
 
Mwaikimba hakuondolewa sababu ya maneno na kelele za mashabiki,aliondolewa baada ya kushindwa kuperform,licha ya kupewa muda wa kutosha na pia hata kocha kuamini kuwa alipoteza muda kuwa naye.

Anyway,issue isiwe kuachwa Mgosi,au umbo la Mwaikimba,hapa tuangalie kama baada ya kuwa nje kwa muda mrefu je amebadilika? Ni matumaini yetu kuwa huenda ana jipya,na amebadilika.

Tuitumie Challenge Cup kupima yale yaliyopo mioyoni mwetu.
 
mpira sio umbo kijana! kumbuka maximo naye alichanganyikiwa na umbo la mwaikimba lakini baada ya mechi chache aligundua kuwa ni garasa! sasa unaponiambia umbo lake litasaidia hata sikuelewi! Pili anaonekana hafundishiki kama walivyo wachezaji wengi wa kibongo. Hivyo mm suala la kufanya majaribio katika staz kwa kuwa mechi ya moroco mipira ilikuwa inapotea sikubaliani nalo!

mpira ni umbo kaka,kila position na umbo lake.huwezi kumtumia ngasa kama lone striker,mwaikimba body linaruhusu kama drogba,GUIZA,TORRES,ADRIANOhata rooney anamwili bana!Mwaikimba anafundishika ila kelele za wa2 kama nyie ndo mnaharibu.mwacheni kocha afanye kazi yake.
 
mpira ni umbo kaka,kila position na umbo lake.huwezi kumtumia ngasa kama lone striker,mwaikimba body linaruhusu kama drogba,GUIZA,TORRES,ADRIANOhata rooney anamwili bana!Mwaikimba anafundishika ila kelele za wa2 kama nyie ndo mnaharibu.mwacheni kocha afanye kazi yake.
Tutafungua thread baada ya Challenge,kwa sasa tutajadili mambo yasiyo na tija,kocha hakukaa ofisini pale Karume,katembea kafika hadi Songea akaibuka na kipa kule,hajasubiri kuletewa majina na "Jumapili"Kayuni,katafuta mwenyewe,tena kwa kufunga safari.

Tuwe na subira kidogo,ili tupate tunachokililia kwa muda mrefu
 
wadau nawapata! yote kwa yote mi nadahani tusubiri hiyo challenge! lakini tuandike maumivu.........................mimi simo
 
tatizo wachezaji kujituma sifuri, ubunifu sifuri, kufundishika nako yaleyale, ukiangalia ground ya mchezaji mmoja mmoja ameibukia ligi kuu basi upupu mtupu mlete messi mweke kwenye huo upupu kama utamsikia nini mwaikimba. chama cha mpira nacho tumbo kwanza mpaka wimbo wa taifa wanasahau ianatia mauthi aaaaaaaaaaaaah
 
mwaikimba aahh! siku tumeenda kucheza na senegal wasenegal macho yote kwa mwai tokana na umbo lake.. mpira ulivyoannza alipewa watu 3 wakumkaba lakini baada ya dk 10 walimuacha peke yake no madhara at all...
 
Tutafungua thread baada ya Challenge,kwa sasa tutajadili mambo yasiyo na tija,kocha hakukaa ofisini pale Karume,katembea kafika hadi Songea akaibuka na kipa kule,hajasubiri kuletewa majina na "Jumapili"Kayuni,katafuta mwenyewe,tena kwa kufunga safari.

Tuwe na subira kidogo,ili tupate tunachokililia kwa muda mrefu
Ni kweli kocha kangalia karibu nusu ya mechi zote za mzunguko wa kwanza ameshakaa na mgosi anamfahamu, amesha muona mwaikimba acha amjaribu....Hata hivyo mgosi kwa sasa hayuko fit kivile
 
umeona hashycool!! yani mwaikimba hakuna kitu mi nawaambia tutaona tena! subirini

huyo sijui ndo kocha nani kazimika na umbo tu lile.......very sooon atampiga chini bila maelezo......nimecheza naye maharage yule!
 
poulsen popote ulipo heshima kwako kwa kumjumuisha Mwaikimba katika kikosi chako kwani ni aina ya mchezaji anahitajika kwa sasa kulingana na aina ya mfumo uutumiao wa kuweka mastriker wengi na atacking midfielders,mpenda soka yeyote mwenye akili timamu aliyebahatika kuona mechi dhidi ya algeria na morocco atajua nini ukifanyacho ila kama bado ana akili mgando na kudhani mfumo ni uleule wa maximo wa kujaza defending midfielders na striker moja lazma akurupuke na kujitia ukocha au ushabiki maandazi...huyu mtu amerudi katika fomu yake ile ambayo ndo ilimfanya mpaka ashanti wamsajili na baadae yanga,waloibahatika kumuona kabla hajajiunga ashanti wanajua nazungumzia nini.....current form ya mwaikimba ipo vizuri so far ana goli 4 nini kingine tunahitaji??mwaikimba kati,pembeni ngassa na mrwanda...natumai tutafurahi!
 
Unajua Tatizo La watanzania wengi wanajifanya wanajua Soka Kumbe hawajui!!!!!!!!!!! Mgosi Mgosi..... Hebu tuulizane Tangu Mgosi aingie Taifa Umeshasikia anafunga Goli? Mgosi anawika tu akiwa Simba... Bora Mwaikimba...Huyu akimbizi lakini akipata...Wachezeshaji wazuri utamtambua kuwa yeye ni super Striker. Shida wakati Mwingine na Fomation ya Kocha...kwa mfano wakati wa Maximo alipendelea Mchezo wa Kujilinda zaidi kwa Mantiki hiyo ilikuwa Vigumu sana Mwaikimba Kuwika. Ila Paulsen anapendelea Kushambulia na Kujilinda...mimi Naami ni Mwaikimba akijituma atawika tena sana tu.
Kwa Upande Mwingine niwaelimishe Tanzanzania wenzangu vigezo vya Mchezaji Bora ;
>>> Lazima Awe na Umbo Kubwa
>>>Awe na Nguvu
>>> Awe na Kontroo
>>>Awe na Spidi
>>> Atumie akili
Mchezaji akiwa na hivi vyote atawika vibaya
Tumpe Mwaikimba Muda mtaona tu. Kumbuka Mwaikimba alivyozitishia Simba na Yanga wakati akiwa Ashanti. Ni kwa sababu tu alikuwa katika timu iliyokuwa inapenda kushambulia. Kumbuka pia akiwa Yanga Bado alitisha.....Sasa wandugu tuache upenzi na Mahaba yaliyopitiliza. Mgosi kawekwa Taifa Stars hajafunga Goli sasa Mshambuliaji Gani huyo.?
 
Wadau mimi sio kocha ila mada hii imezua makundi 2.
Naona tuwafananishe kiunamichezo MGOSI na MWAIKIMBA -sifa za striker.

1.Mwaikimba ni mrefu vs Mgosi
2.
3:
:
;
 
msimlaumu tusubiri tumuone katika game mbili tatu.. kabla ya kuangusha lawama
 
Kwani gemu ya algeria makosa yalikuwa kwa nani, na kama ni striker type ya mwaikimba, mbona kuna John boko pale na hakucheza, any way huyu mwaikik muombeeni awike la sivyo atarudi tukuyu staz shauri yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom