Liyumba: Kesi ya kukutwa na simu nimebambikiwa

TIQO

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Messages
13,816
Likes
76
Points
0
TIQO

TIQO

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2011
13,816 76 0
Na Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na simu gerezani, ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imfutie shtaka hilo na kumuachia huru kwa madai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kumkomoa.
Liyumba aliyaeleza hayo jana wakati akijitete mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando anayetarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, Januari 15, mwaka na kuzitaka pande zote mbili kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho kama mshtakiwa ana hatia ama la, Desemba 30, mwaka huu

"Kesi hii imepangwa kwa ajili ya kunikomoa, wakati natumikia kifungo sijawahi kuvunja sheria, kupewa adhabu wala kuonywa kwa kosa lolote, simu yenye namba 0653004662 siijui nimeiona hapa na kama imesajiliwa ni lazima mhusika atajulikana." alieleza Liyumba.
Alidai kuwa, Julai 2011 alikuwa mfungwa akitumikia kifungo cha miaka miwili na unapofikishwa huko ni lazima upekuliwe mara tatu kwa kuvuliwa nguo zote.
Kutokana na utaratibu wa ulinzi gerezani, siyo rahisi kwa mfungwa ama mahabusu kuingia na simu
Julai 27, 2011 mchana nikiwa kwenye selo yangu na mtu mmoja ambaye ni mahabusu, tukisoma magazeti ghafla askari wawili akiwamo shahidi wa pili wa upande wa mashtaka, waliingia na kuniambia kuwa hii simu umeipataje wakati wakiwa wameishika mkononi.
Aliongeza kuwa tukio hilo kwake lilikuwa ni mshtuko na aliona ni kitu kilichopangwa na kwamba, wakati huo ilikuwa bado mwezi mmoja na nusu amalize kutumikia kifungo chake.
"Naamini walikuwa wananingojea, nilitafakari mlolongo wa matukio yanayonikuta, nilishtakiwa kwa kuambiwa nimesababisha harasa ya Sh261 bilioni shtaka ambalo liliondolewa na kupewa la kutumia madaraka vibaya, madaraka ambayo sina wala sijapewa huu ni uonevu." alisema Liyumba.
Alibainisha kuwa wakati akiwa gerezani muda mfupi kabla ya kutoka watu wa Takukuru walimfuata na wakitaka kuandaa kesi dhidi yake, lakini aliwapinga kwa madai ya kutaka kuwasiliana na mwanasheria wake.
Alidai kuwa watu hao walimfuata tena na kwamba baada ya dulu hilo, akaona tukio hili la Julai 27,2011 la kubambikiwa kesi ya kukutwa na simu gerezani.
Alisisitiza kuwa simu na namba ya 0653004662 haifahamu, kama imesajiliwa mhusika atajulikana na iwapo atakuja mtaalamu ataeleza angalau ilipigwa kwa nani.
Liyumba anadaiwa kukutwa na simu ya mkononi akiwa gerezani Ukonga, Dar es Salaam, wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili.
 
E

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
1,974
Likes
914
Points
280
E

ebaeban

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
1,974 914 280
Sababu ya Liyumba kukutwa na simu inasemekana alimpigia simu mkuu wa kaya, mkuu wa kaya akashituka kwa nini mfungwa awe na simu? ndipo alipowasiliana na viongozi wa gereza , uongozi wa gereza baada ya upekuzi WA ghafula ndipo alikutwa na simu hiyo na ndiyo hapo noma ikasanuka. Katika utetezi wake mbona Liyumba hajaeleza haya? Mbona hajakanusha kwamba alimpigia simu mkuu wa kaya? LIYUMBA WACHA KUJICHANGANYA.
 
B

Bobuk

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
5,875
Likes
495
Points
180
B

Bobuk

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
5,875 495 180
Wameshakutumia kama condom sasa ngoja uipate fresh
 
don-oba

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
1,386
Likes
27
Points
145
don-oba

don-oba

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
1,386 27 145
Sababu ya Liyumba kukutwa na simu inasemekana alimpigia simu mkuu wa kaya, mkuu wa kaya akashituka kwa nini mfungwa awe na simu? ndipo alipowasiliana na viongozi wa gereza , uongozi wa gereza baada ya upekuzi WA ghafula ndipo alikutwa na simu hiyo na ndiyo hapo noma ikasanuka. Katika utetezi wake mbona Liyumba hajaeleza haya? Mbona hajakanusha kwamba alimpigia simu mkuu wa kaya? LIYUMBA WACHA KUJICHANGANYA.
Sasa kama ni hivo mbona ushahidi ni mweupe, wamwite mzee wa kaya kama shahidi muhimu. Tatizo serikali huwa inakurupuka kuandaa mashtaka.
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
202
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 202 160
Sababu ya Liyumba kukutwa na simu inasemekana alimpigia simu mkuu wa kaya, mkuu wa kaya akashituka kwa nini mfungwa awe na simu? ndipo alipowasiliana na viongozi wa gereza , uongozi wa gereza baada ya upekuzi WA ghafula ndipo alikutwa na simu hiyo na ndiyo hapo noma ikasanuka. Katika utetezi wake mbona Liyumba hajaeleza haya? Mbona hajakanusha kwamba alimpigia simu mkuu wa kaya? LIYUMBA WACHA KUJICHANGANYA.
je katika ushahidi uliowasishwa na waendesha mashitaja wali-include maneno kuwa Liyumba alimpigia simu mkuu wa nchi !? Kama hawainclude basi utetezi wake unanguvu sana mbele ya macho ya sheria. Je wataweza kuthibitisha kuwa alikutwa na simu !?
 
MUSONI

MUSONI

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Messages
781
Likes
319
Points
80
MUSONI

MUSONI

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2011
781 319 80
.zee la Red cars na kujengea malaya atapata haki yake Duniani kahsribu sana watoto na dada zetu. Na hivi hskimu ni mwanamama duuuuuu pole
 
E

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
1,974
Likes
914
Points
280
E

ebaeban

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
1,974 914 280
je katika ushahidi uliowasishwa na waendesha mashitaja wali-include maneno kuwa Liyumba alimpigia simu mkuu wa nchi !? Kama hawainclude basi utetezi wake unanguvu sana mbele ya macho ya sheria. Je wataweza kuthibitisha kuwa alikutwa na simu !?
Huenda waendesha mashitaka wameframe vibaya tu kumpa chapuo Liyumba ili ashinde kesi ila kimsingi mwanzo wa kesi yake hii ni kumpigia simu mkuu wa kaya, si unajua maPP ni corrupt.
 
Mimibaba

Mimibaba

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
4,559
Likes
8
Points
0
Mimibaba

Mimibaba

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
4,559 8 0
Sababu ya Liyumba kukutwa na simu inasemekana alimpigia simu mkuu wa kaya, mkuu wa kaya akashituka kwa nini mfungwa awe na simu? ndipo alipowasiliana na viongozi wa gereza , uongozi wa gereza baada ya upekuzi WA ghafula ndipo alikutwa na simu hiyo na ndiyo hapo noma ikasanuka. Katika utetezi wake mbona Liyumba hajaeleza haya? Mbona hajakanusha kwamba alimpigia simu mkuu wa kaya? LIYUMBA WACHA KUJICHANGANYA.
Kwa hiyo shahidi wa kwanza ni mkuu wa kaya?
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
21,030
Likes
10,394
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
21,030 10,394 280
mabazazi wafujaji hao naona wana act kusulubiwa
 
Frank Wanjiru

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
9,964
Likes
12,822
Points
280
Frank Wanjiru

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
9,964 12,822 280
Hivi ile kesi ya yule Binti yake Moureen aliekamatwa na Unga kule kusini imeishia wapi?maana naona Dola imeamua kummaliza kabisa.
 
Forum statistics

Threads 1,273,020
Members 490,242
Posts 30,467,873