Liyumba akosekana kortini, Mramba ahaha

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
Na Kiyao Hoza
22nd September 2009

Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 221, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT, Amatus Liyumba, imekwama tena kuendelea leo baada ya mtuhumiwa kukosekana kortini.

Awali kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa jana, lakini kutokana na siku ya jana kuangukia kwenye sikukuu ya Idd El Fitr, ikaamuliwa kuwa iendelee leo.

Hata hivyo, Liyumba hakuwepo mahakamani leo kutokana na kukosekana kwa hati ya kumtoa mahabusu.

Kutokana na hali hiyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia kwa Hakimu Edson Mkasmongwa anayesikiliza shauri hilo, imeamuru kuwa hati hiyo itolewe ili Liyumba aletwe mahakamani hapo Septemba 25 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali. Wiki mbili zilizopita, Liyumba hakutokea tena mahakamani kwa maelezo kuwa alikuwa mgonjwa.

Aidha, licha ya kutokuwepo kwa mtuhumiwa, mawakili wote wa utetezi na wale wa Jamhuri walikuwepo mahakamani hapo.

Liyumba anatetewa na wakiri maarufu wa kujitegemea, Majura Magafu ilhali upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili wa Serikali Justus Mulokozi

Katika shauri hilo, Liyumba anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 221 kupitia kwenye mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo. Wakati huo huo, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, leo amekataa kutaja mashahidi wake na kusisitiza kuwa atafanya hivyo pale tu mahakama itakapomuona kuwa ana kesi ya kujibu.

Mramba aligangamala hivyo leo kupitia kwa wakili wake Hubert Nyange, wakati alipofikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu na aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha Daniel Yona na pia Katibu Mkuu wa zamani wa wizara hiyo, Gray Mgonja.

Wote wanakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 11.7.

Upande wa Mashtaka ukiwakilishwa na Wakili Boniface Stanslaus, umesema utaleta mashahidi 17, mbele ya jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo ambao ni John Utamwa, Saul Kinemela na Deo Rumanyika

Wakili huyo akawataja mashahidi hao ambao wote hao anwani zao zinapitia Makao Makuu ya ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU).

Baada ya kumaliza kuwataja mashahidi wa upande wa mashtaka wakili Stanstalaus, akaiomba mahakama kutoa nafasi kwa upande wa utetezi nao kutaja mashahidi wao.

Alipopewa nafasi hiyo na mahakama, ndipo Wakili Nyange akasema ni mapema mno kuorodhesha mashahidi wakati hata kesi yenyewe haijaanza kusikilizwa na mahakama na kuona kuwa wana kesi ya kujibu.

Nyange amedai kwa mujibu wa kifungu namba 230 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, ni wajibu wa mahakama baada ya kufunga ushahidi wa upande wa mashtaka kutoa uamuzi kwa upande wa utetezi kutaja mashahidi endapo wana kesi ya kujibu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kwa makubaliano ya pande zote mbili ambapo mahakama imetoa muda kwa upande wa utetezi kupitia baadhi ya vifungu vya sheria kuhusu umuhimu wa kutaja mashahidi wa upande wao kama wakili wa serikali alivyoomba.



CHANZO: ALASIRI
 
Jamaa anaumwa nasikiaa..bp inashuka na kupanda kila siku....ameshajuaa nini hatma yake...labda ndio maana anapata woga wa kesi na bp kushuka....pole sana baba...acha haki itendeke kama kweli au kuna walakini katika kesi yako...sababu ya uliyoyafanya huko nyuma
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom