Liyumba akamatwa kwa kuhusika na kuuza madawa ya kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Liyumba akamatwa kwa kuhusika na kuuza madawa ya kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by C.T.U, Mar 20, 2012.

 1. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280

  LILE sakata la msichana Morine Amatus (22), anayetajwa kuwa ni mtoto wa Amatus Liyumba, aliyekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Lindi, akiwa na wenzake watatu, wakidaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ya kilo 210 , yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.4 limeingia katika sura mpya baada ya baba yake (Morine) kutakiwa kukamatwa, hivyo kuingia kitanzini.

  Habari za uchunguzi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa Liyumba anaingia kitanzini kwa kuwa anatakiwa akamatwe na ahojiwe kuhusiana na madawa hayo kwa kuwa mtoto wake amedaiwa kuhusika na tayari katupwa gerezani akisubiri kesi yake kusikilizwa.
  Chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi kimesema kumekuwa na shinikizo kutoka serikalini kwa waziri mmoja (jina limehifadhiwa) kutaka Liyumba akamatwe na kutupwa rumande kwa kile kilichodaiwa kuwa, ili upelelezi uweze kufanyika kwa kina.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili Jumapili iliyopita, Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa hakukiri wala kukataa kuhusu kukamatwa Liyumba ili uchunguzi ufanyike.

  "Ninachoweza kusema ni kwamba uchunguzi juu ya tukio lile unaendelea. Kuhusu Liyumba ni kwamba mtoto wake ana miaka 22, hivyo ni mtu mzima kuna mambo anaweza kuyafanya bila baba yake kujua, lakini kama uchunguzi utatutaka baba yake akamatwe kuhojiwa, hatuwezi kushindwa kufanya hivyo," alisema Kamanda Nzowa.

  Alipododoswa zaidi, kamanda huyo alisema kwa kawaida polisi wanapofanya uchunguzi wao hawawezi kusema ni nani akamatwe na kuhojiwa na wala huwa hawasemi nani amewapa taarifa za mtu anayechunguzwa.

  "Hizo ni kanuni zetu, hatuwezi kusema nani atakamatwa kwa jambo fulani au kumtaja mtu ambaye ametuletea taarifa za watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya na ndiyo maana tunafanya kazi vizuri sana, nawaomba wananchi wema wazidi kutupa ushirikiano," alisema Nzowa.

  Hata hivyo, Nzowa alifafanua kuwa kutokana na wingi wa madawa waliyokamatwa nayo, mtoto huyo wa Liyumba na wenzake, kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa itapelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Morine katika Kijiji cha Mchinga Mbili, Lindi kwa mujibu wa Nzowa na kufikishwa mahakamani ni Pendo Mohamed Cheusi (67), mkazi na mkulima wa kijiji hicho na Hemedi Said (27), dereva na mkazi wa Mtoni, jijini Dar es Salaam ambaye pia ni mtoto wa mwenye nyumba hiyo.

  Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Ismail Adamu, kwa jina lingine Athuman Mohamed Nyaubi (28), mfanyabiashara wa magari nchini Afrika Kusini na mkazi wa Morocco jijini Dar es Salaam.

  Morine Amatus ni mkazi wa Mikocheni ‘B' jijini Dar es Salaam na baba yake (Liyumba) alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na aliwahi kufungwa miaka miwili, Mei 24, 2010 kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi ya umma.

  NZOWA ATAHADHARISHA
  "Niwatahadharishe wale wote wanaofanya au kufikiria kufanya biashara hii haramu ya dawa za kulevya, waache kwa sababu polisi kwa kushirikiana na raia wema tumejipanga. Maeneo yote siku hizi tunayalinda, watakaojiingiza ni lazima watakamatwa tu," alionya.

  Kamanda Nzowa amewashukuru wote waliofanikisha kutoa taarifa ya kuwepo kwa madawa nchini na amewataka kuendelea kushirikiana na jeshi lake kwani alidai wote wanaokoa taifa na kuwa na watu mazezeta.

  UCHUNGUZI WETU
  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kuwa watuhumiwa hao wanahusishwa na askofu mmoja, Moris Charles ambaye inadaiwa amekimbilia nje ya nchi.

  Tayari magari yake matatu yamedakwa na polisi wakati upelelezi ukiendelea huku kukiwa na taarifa kuwa familia yake ameitoroshea nje ya nchi.
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hii ni tetesi au amekamatwa kweli?
   
 3. Delegate

  Delegate JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 35
  labda ndio hela za hepa hizo
   
 4. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  mkuu umesoma kwa makini?
   
 5. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  udaku tu, peleka kwa shigongo
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  udaku ze great:hand::A S-frusty2:
   
 7. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  aisee simpendi huyo mtu hapo kwenye blu..yale magazeti sio kabisa walishwahi nitoa na scandal chafu sana af ndani yake etu wakani quote niki confess wakati hata sikuwahi kuongea nao..I simply hate the guy na pesa zake haramu..yye mwenyewe ana maskendo kibao..namvutia kasi tu huyu nyauba..Mpssxxyy
   
 8. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Si umpeleke kwenye sheria mkuu
  kama ni uongo unachukua hela safi kabisa!!!
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  huo mzigo wa kilo 210 si mchezo,ningekuwa polisi nakatiwa changu nawaachia,kuvuta unga ni mapenzi ya mtu mwenyewe kama kunywa pombe,..legalize it..it's legal drug money baby..
   
 10. R

  RUTARE Senior Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utakuwa umetenda dhambi kubwa ya kula rushwa ni bora kuridhika na mshahara kama hautoshi unaacha kazi unatafuta kazi nyingine

  Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa haya madawa, bhang na gongo vinawaingizia wafanyabiashara kwa sababu ya kupigwa marufuku na kama wange legalize vingekuwa kama sigara tu na visingepata soko kwani wajinga wangevifakamia na kufa kwa wingi wakabaki welevu na huo ukawa ndio mwisho wa soko la bidhaa hizo
   
 11. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  yaani unakalia pesa mkuu??? mbona sikuelewi??????? hapo ungevuta pesa yako taratiiiiibu ukala kivulini bila jasho. Unajua gazeti la Sanifu lilipo wewe??? au ulikuwa bado mtoto mdogo enzi hizo??? Tafuta wakili mpe kesi afanye mambo, hiyo Global inaweza kuwa historia na ikafutika kabisaaaaaaaaa baada ya kesi yako kuisha huku wewe ukipiga mluzi tu
   
 12. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hepa=EPA.
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,084
  Likes Received: 6,548
  Trophy Points: 280
  Hela ndefu sana hiyo,
  watakuwa wazoefu wa huu mchezo hawakuanza leo,
  inaweze kuwa ni biashara ya watu wakubwa sana hii.
   
 14. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  una chuki naye..? aliyekamatwa ni bint yake lkn ulivyoileta ni kana kwamba aliyekamatwa ni mzazi mwenyewe. maelezo yako wazi . vp......?
   
 15. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,254
  Trophy Points: 280
  Au kuna mkono wa mtu kama alivyotaka kufanyiwa mengi natazama kwa jicho la akiba!!
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kama habari hii ni kweli hapa patakuwa na chuki dhahiri, kosa afanye mtotokukamatwa akamatwe baba? Eti ataharibu uchunguzi?

  Mnyonge mnyongeni ......................................mpeni!!!!!
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Habari imeandikwa kiudakuuu! Litoto la 22 yrs babake akamatwe ili iweje?
   
 18. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Cloudssssssssssssss fmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm
   
 19. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ya siasa mpaka kwenye sheria!
   
 20. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ya siasa mpaka kwenye sheria!
   
Loading...