Liwale, Lindi: Mgombea Ubunge wa CHADEMA arudisha fomu na imepokelewa na Msimamizi wa Uchaguzi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Liwale: Mgombea Ubunge wa CHADEMA Jimbo la Liwale, Ndugu Juma Rashid Upinde amerejesha fomu yake, ambapo imepokelewa saa 5:52 asubuhi na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo, Luiza Mlelwa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Kikao Maalum cha Kamati Kuu iliyoketi Jumatatu, Septemba 10, 2018, jijini Dar es Salaam, kimemteua Ndugu Juma Rashid Upinde kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Liwale, katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 13, mwaka huu

Ndugu Upinde ni mmoja wa wanachama waandamizi wa CHADEMA Kanda ya Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma) akiwa ameshiriki kukijenga na kukiimarisha chama katika maeneo hayo kupitia shughuli na harakati mbalimbali kwa muda mrefu.
1dd0d977-7977-45e0-8d33-4db885cba397.jpeg
03c445ef-bad1-495d-9a08-94131ac50989.jpeg

455602b2-9286-4b80-8aad-e174c64edc9f.jpeg
28480f19-80bf-41a4-8b32-85fb0732b634.jpeg


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Liwale kwa tiketi ya CHADEMA ndugu UPINDE Juma Rashid akiwasilisha fomu ya uteuzi kwa kugombea kwa Msimamizi wa Uchaguzi Bi. Luiza Oswin Mlelwa ambaye alikuwa na wasaidizi wake pia. Fomu ilipokelewa saa tano na dakika hamsini na mbili (5:52) asubuhi.


=======
Uzi wa CCM kupitisha Zuberi Kuchauka

CCM yampitisha aliyeachia ubunge Liwale Zuberi Kuchauka kugombea tena - JamiiForums
 
Back
Top Bottom