Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,643
- 1,786
Bajeti ya serikali inayumba, wizara na taasisi nyingi zinalalamika hazina hela, lakini hata siku moja sijasikia CCM inalalamikia bajeti yao. Huyo accountant anaewabunia miradi ya chama lazima umkubali kwa usaniiLusinde ashitushwa wagombea udiwani kulipa Sh1m
Friday, 20 August 2010 08:55
Habel Chidawali, Dodoma
Mwananchi
BALOZI mstaafu Job Lusinde amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kiwango cha Sh1.milioni, kinachotakiwa kutolewa na wagombea wa viti vya udiwani, ili kuchangia kampeni.
Wagombea udiwani katika Wilaya ya Dodoma, wamekuwa wakihaha kutafuta Sh1 milioni, kila mmoja ambazo zimeelezwa kwa kuwa ni mchango wa lazima.
Balozi Lusinde ambaye alikwenda katika ofisi za CCM za wilaya ya Dodoma mjini ili kupata ufafanuzi, alisema tayari jambo hilo limeanza kutafisiriwa vibaya na baadhi ya wagombea ambao sasa wanajutia kuomba nafasi hizo.
Mkongwe huyo wa siasa, aliingia katika ofisi hizo jana asubuhi kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wa CCM walioteuliwa kugombea udiwani katika kata za Wilaya ya Dodoma.
"Jambo hili linatia mashaka sana ndugu katibu, lazima muliangalie kwa sababu watu hao wamepitishwa na wanachama kwa kuzingatia uwezo wao katika kuongoza, lakini si matarajiri, sasa mnapowataka watoe Sh1 milioni, watazipata wapi," alihoji Balozi Lusinde.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Dodoma, David Mzuri, alisema hatua ya kuwataka wagombea kutoa kiwango hicho, inafuatia maelekezo ya CCM mkoa yaliyomtaka kila mgombea ,kutoa kiasi hicho kama mchango wake katika kampeni.
Mzuri alisema kila aliyepita kwake kuchukua fomu ya uteuzi aliaambiwa kutoa kiwango hicho.Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa kiasi hicho ni kiwango cha juu cha mgombea udiwani kutumia katika kampeni zake lakini si kiwango kamili anachotakiwa kuwa nacho.