johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,599
- 141,415
Mbunge wa Mtera mh Lusinde ( Kibajaji ) amesema katika ujana wake alikuwa ni muuza kahawa maarufu pale Kawe ambapo alijulikana kama Stone. Lusinde amesema yeye elimu yake siyo rasmi na kwa hiyo hana cheti chochote cha taaluma ila anajivunia mafanikio makubwa aliyonayo kuwapita hata hao wenye PhD.
Amesisitiza kwamba akiwa muuza kahawa alibahatika kumuoa house girl na waliishi maisha ya kuunga unga lakini kwa sasa mke wake huyo anaendesha Prado VX, hivyo anamshukuru Mungu na kufafanua kuwa kiini cha mafamikio yake ni uaminifu, nidhamu na heshima ya hali ya juu aliyonayo.
Mh Lusinde ameyasema hayo yote katika semina ya fursa anzia sokoni iliyoandaliwa na Clouds Media na kurushwa luningani mubashara kupitia Clouds Tv jana mjini Dodoma.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Nawasilisha!