Livingstone Lusinde(Mb): Muuza kahawa aliyemuoa house girl!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,604
141,421
Mbunge wa Mtera mh Lusinde ( Kibajaji ) amesema katika ujana wake alikuwa ni muuza kahawa maarufu pale Kawe ambapo alijulikana kama Stone. Lusinde amesema yeye elimu yake siyo rasmi na kwa hiyo hana cheti chochote cha taaluma ila anajivunia mafanikio makubwa aliyonayo kuwapita hata hao wenye PhD.

Amesisitiza kwamba akiwa muuza kahawa alibahatika kumuoa house girl na waliishi maisha ya kuunga unga lakini kwa sasa mke wake huyo anaendesha Prado VX, hivyo anamshukuru Mungu na kufafanua kuwa kiini cha mafamikio yake ni uaminifu, nidhamu na heshima ya hali ya juu aliyonayo.

Mh Lusinde ameyasema hayo yote katika semina ya fursa anzia sokoni iliyoandaliwa na Clouds Media na kurushwa luningani mubashara kupitia Clouds Tv jana mjini Dodoma.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Nawasilisha!
 
katiba ya kujua kusoma na kuandika kama sifa ya mbunge inaleta dharau kwa wasomi,yaani muuza kahawa anakuja sema ana maisha mazuri kuliko msomi kisa kupiga domo na kujipendekeza tu.
Kwani uongo?..... Jaribu kumlinganisha Kibajaji na Prof Lipumba nani ana mafanikio na nani anaweza " kumpiga mzinga' mwenzake? Chezea ubunge wewe!!!
 
Kibajaji alisema......
Hatokuja kusahau kazi yake ya kuuza kahawa kwa mzee Saidi na Siku alipo fukuzwa kwenye chumba kimoja alichokua amepanga, na mwenyenyumba aling'oa mabati na kisha mvua ilinyesha usiku ule......
 
katiba ya kujua kusoma na kuandika kama sifa ya mbunge inaleta dharau kwa wasomi,yaani muuza kahawa anakuja sema ana maisha mazuri kuliko msomi kisa kupiga domo na kujipendekeza tu.
Kwahiyo katiba ndio ifanye nini sasa, anyone who can organise knowledge has more/wide chances of succeeding in life. Elimu ni kitu ambacho Kipo sana na kinapatikana kiurahisi zaid. The ability and know how to organize knowledge is rare.
 
Back
Top Bottom