Livingstone Lusinde (Kibajaji), uligusa pabaya. Imekuwa vyema umejua na kukaa kimya!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ulipojitokeza na kuanza kujibu kuhusu Waraka wa akina Makamba na sauti zilizovuja za viongozi mbalimbali waandamizi chamani na Serikalini, nikajua kuwa mbio zako ni fupi tu. Ni mara bada ya kumtaja na kumpania Benard Membe. Ukasema ukirudi toka nje ya nchi, utakuja kumkuna Membe panapomuwasha.

Ukaenda, ukarudi. Ukabaki kimya. Ni kwakuwa ulijua kuwa uligusa sehemu mbaya. Membe, ndani ya chama na Serikali, si mtu wa mchezo. Anasikilizwa; anapendwa; anafuatiliwa; anazingatiwa; anasomwa na kusikika. Si wa kupuuzwa hata kidogo. Ni vyema uliona mbali na kuamua kuwa kimya.

Membe ni zaidi ya Karandinga uliloliangusha Mtera. Ni zaidi ya 'aliyekutuma' kujibu Waraka na sauti za viongozi. Uligusa pabaya. Kwakuwa wewe ni mjanja na unajua namna ya kutunza ugali wako, ukabaki kimya badala ya kujichanganya kwa Membe. Hata waliokushangilia wangekuacha solemba.

Ropoka kwa stepu, Membe ni mtu mzito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Urambo, Tabora)
 
Sio kweli usemacho,ni hivi,katibu mkuu alizuwia wanachama kujibu wapumbavu ,akasema wapuuzwe,hivyo wamepuuzwa,hiyo ni kauli ya Bashiru
 
Bashru ni hopeless yeye ndo amewaagiza viongozi wa ccm kuwanyanuasa, kuwatisha kuwakaripia na kuwabagaza watumishi wa umma,
 
Kuna watu wazito ambapo ambao wana mizizi ndani ya chama na serikali, ambao ukiwa kama mwanasiasa haupaswi kujiingiza ktk malumbano nao ama kujifanya unajua zaidi yao. Nafikiri ametambua wapi alipojikwaa na wala siyo kule alikoangukia.
 
Lusinde kibajaji alimwangusha Mzee Malecela kwenye kura za maoni Mtera hilo halishangazi Sana
CC ya ccm ikaridhia hili linashtua kwa kweli

Malecela enzi zake BUnge la 10 alikuwa akiongea ukumbi mzima unamsikiliza spika anainuka kuunga mkono na waziri mkuu ana idhinisha huo ndo msimamo wa chama na serikali
 
Kibajaji kokote uliko unaitwa njoo ukinukishe huku kama kweli wewe kidume vinginevyo siku nyingine kaa kimyaaaa kama unakunya vile.
 
Mpaka umemuanzishia Kibajaji Mada inaonyesha jinsi gani unavyombabaikia na kujipendekeza, Muzungu anaita huo ugonjwa wako na kibajaji ,, obsession syndrome“, una obsession aisee tafuta msaada wa kitaalamu.
 
Msukuma na kibajaji ndio think tank ya ccm. Hapo ujue chama kubwa lilivyofilisika katika kujenga hoja. Kubwabwaja sasa imekuwa kujenga hoja ndani ya ccm. Hii ni kinyume kabisa na Mwongozo wa ccm1981 unavyoelekeza kuhusu hoja ya nguvu dhidi ya nguvu ya hoja
 
Ulipojitokeza na kuanza kujibu kuhusu Waraka wa akina Makamba na sauti zilizovuja za viongozi mbalimbali waandamizi chamani na Serikalini, nikajua kuwa mbio zako ni fupi tu. Ni mara bada ya kumtaja na kumpania Benard Membe. Ukasema ukirudi toka nje ya nchi, utakuja kumkuna Membe panapomuwasha.

Ukaenda, ukarudi. Ukabaki kimya. Ni kwakuwa ulijua kuwa uligusa sehemu mbaya. Membe, ndani ya chama na Serikali, si mtu wa mchezo. Anasikilizwa; anapendwa; anafuatiliwa; anazingatiwa; anasomwa na kusikika. Si wa kupuuzwa hata kidogo. Ni vyema uliona mbali na kuamua kuwa kimya.

Membe ni zaidi ya Karandinga uliloliangusha Mtera. Ni zaidi ya 'aliyekutuma' kujibu Waraka na sauti za viongozi. Uligusa pabaya. Kwakuwa wewe ni mjanja na unajua namna ya kutunza ugali wako, ukabaki kimya badala ya kujichanganya kwa Membe. Hata waliokushangilia wangekuacha solemba.

Ropoka kwa stepu, Membe ni mtu mzito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Urambo, Tabora)
Hivi kasharudi kumbe kutoka CHINA? Hahahaaaaaa nilijua hajarudi bado maana nilikuwa nasubiri Press yake ya kuja kumkuna MEMBE.
 
Back
Top Bottom