Wiston Mogha
Senior Member
- Feb 13, 2014
- 149
- 96
Hivyo basi kwa taarifa rasmi kesho amehitajika mapema kwa ajili ya maelezo zaidi na kusaidia na chombo hicho cha Takukuru,na hili tukio limefuata baada ya siku si nyingi kuandaa tukio kanisani na kuwaita wajumbe kwa kisingizio kuwa ni ibada ya shukrani.
Sambamba na hilo kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakikwazwa na kebehi,dharau na fedheha kutoka kwa Mbunge wao akidai ya kuwa mpinzani wake hajazaliwa, vile vile akijinasibu ya kuwa anafahamu atapita kwa fedha kwakuwa wagogo ni ombaomba na masikini, na mwishowe huwa anawapa ubwabwa kisha wagogo wanamchagua hivyo hata angekuja Kassim Majaliwa kugombea nae asingefua dafu kwake.
Vile vile amekuwa Mbungewa visasi na mara kadhaa akipishana na kiongozi yoyote aliye chini yake atamfanyia figisu na wakati mwingine kumuamisha kabisa au kumtoa kabisa kwenye nafasi yake,sambamba na hilo ni kiongozi anayetumia mabavu na lugha chafu hata kwa wapiga kura wake na kwa sasa jamii na wananchi wimbo wao ni mabadiliko hali inayopelekea Mbunge huyo kutumia nguvu Nyingi za ziada ikiwemo rushwa tena hadharani.