Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Kama ambavyo huwa ninajinasibu humu kuwa, japo mimi nina chama, ila sina mtu, kwenye mazuri napongeza, na kwenye mabaya nakosoa, hili ni Bandiko la Pongezi Kwa Mbunge wa Mtera, Mhe. Livingstone Lusinde.

Naangalia hapa Clouds TV, Mbunge wa Mtera, Mh. Livingstone Lusinde anahojiwa mubashara, japo elimu yake ni darasa la saba tuu, lakini kiukweli kabisa, jamaa huyu ni kichwa mbaya!, anauwezo Mkubwa sana wa uelewa wa mambo, ufahamu, uwezo wa kujieleza, lakini kwa kumsikiliza tuu, nimebaini huyu Jamaa ana kitu kingine kikubwa cha ziada, he has powers. Ni kupitia powers hizi, ndizo zilizomfanya aweze kumngoa Mzee Malecela kule Mtera.

Kwa wenye nafasi Angalieni Clouds TV saa hii, mtakubaliana na mimi.

Ameanza kwa kuelezea chanzo cha jina la kibajaji, alipewa jina hilo na Mzee Malecela baada ya yeye kujaza fomu kuchuana naye ndani ya CCM, kwa vile yeye aliitwa Tinga Tinga, akasema huu ni mpambano wa Tinga Tinga na Kibajaji, kitasagwa hadi maiti hataonekana!. Alipombwaga ndipo jina hilo likapata umaarufu..

Kibajaji anasema tangu amezaliwa hakuwahi kumjua baba yeke hadi amefariki, wamezaliwa wengi, kilichompa usongo wa maisha, ni kusikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya umasiki uliotopea katika familia yake. Kuna wakati mama yake alishindwa kutoka nje kutoka na kuwa na Kaniki moja tuu, inafuliwa usiku na kuanikwa kisha inasubiriwa kukauka ndipo mama atoke!, akaogopa kuwa kwa hali hii, siku ikitokea shida, mama yake anaweza kutembea uchi!, na kweli walikuja kupata msiba wa kufiwa na dada yake, shauri ya umasikini, walishindwa hata kupata sanda tuu ya kumzikia, wakamzika na kumviringisha kwenye gunia!. Hili jambo lilimuumiza sana, akaamua lazima apambane na kuandoka nyumbani!. (This is very bitter reality!).

Aliombwa nyumbani kwao na mama mmoja kumbebea mizigo yake kuja naye Dar, baada ya kufika jijini na kufikisha mzigo salama, kesho yake aliporudi pale yule mama alimfukuza kama mbwa!, kuwa kazi yake ilikuwa ni kuleta tuu mzigo, sasa mzigo umefika. kazi imeisha. Akiwa hana hili wala lile, hana pa kula wala pa kulala, anasema alilala juu ya mti wa mkorosho eneo la Kinondoni Moscow kwa muda wa siku saba, ndipo akaanza kujiongeza kwa kufanya chochote!.

Baada ya pele alianza kujiongeza kwa kufanya chochote, zege amebeba, vibarua amefanya, mizigo, akawa anafanya chochote, ameuza kahawa, amekuwa machinga, amefanya kila kitu. Amewataja baadhi ya aliofanyia kazi.

Anasema alipewa kazi ya ulinzi Kiwango Security, katika kazi yake ya ulinzi, kuna siku alipangiwa kulinda kwa Capt. Komba, ndipo alipokutana na mkewe Edina aliekuwa house girl kwa Komba, akiwa kazini, alipenda kuwahi kazini na kusikiliza nyimbo za dini katika redio yake ya kanda. Hivyo Edina akamuomba kanda ya nyimbo za dini akasikilize ndani, hivyo kanda ikakwama, ndipo akaitwa ndani kurekebisha mambo, na huo ukawa ndio mwanzo!. Akawa anamletea kanda zi nyimbo za dini na huo ukawa mwanzo, hadi wameona, toka kuuza kahawa sasa ni tajiri Mkubwa mwenye mashamba, majumba na magari ya kifahari!.

Anasema yeye kaishia darasa la 3, na mkewe Edna kaishia darasa la nne, hivyo wakichanganya ndio inakuwa darasa la saba. Amesema jambo moja la muhimu sana, yeye na mkewe wana elimu kubwa sana isiyo rasmi. Kama serikali ingetumia mbinu za kuitap hii elimu isiyo rasmi ya Watanzania wasio na elimu ya darasani, wanaweza kufanya mambo makubwa, kuliko ma profesa wenye elimu za vyuo vikuu, lakini faida za elimu hizo inaishia kwenye makaratasi tuu, lakini watu wenye elimu ya maisha, hawana makaratasi lakini wanafanya mambo makubwa!.

Anasema amewahi kudharauliwa sana kutokana na umasikini, hivyo kisiasa, amedharauliwa sana, amekiri kwenye siasa, fitna zipo. Anasema usipende kujibu kila tuhuma, amesema yeye ni msomi wa hali ya juu sana ya elimu dunia, elimu ya maisha, hivyo wanaosema hajasoma, wanamtaka aonyeshe vyeti, akasema akionyesha vyeti, watasema hajatahiriwa, then ataonyesha nini?, hivyo haonyeshi vyeti ila amesoma na sio elimu ya darasani!.

Jamaa amemaliza, kiukweli huyu Jamaa ni very interesting person, ana kipaji cha juu sana cha kujieleza, pia ana powers fulani za success. Kuna watu wameacha shule, au kuishia darasa la saba kutokana na mahangaiko tuu ya maisha lakini wana I.Q kubwa. Huyu Jamaa ana I.Q kubwa sana, angesoma elimu ya darasani, angekuwa profesa!, uthibitisho wa I.Q hiyo, ni kupitia kwa Binti yake aitwae Penina, yuko kwenye top 5 ya vichwa mkoa wa mzima wa Dodoma!.

Kiukweli mimi nimeguswa na historia ya huyu jamaa, na kuna kitu nimejifunza kwake kuhusu elimu ya darasani ya ma vyeti na elimu ya maisha kutokana na usongo wa umasikini!. Hata Bakhresa aliishia elimu ya madrasa tuu!.
Hongera sana Mhe. Livingstone Lusinde, kuna kitu najifunza kwako!.

Asanteni kufuatilia.

Paskali
Profiles nyingine za watu mbalimbali na mwandishi huyu ni hizi
Steven Kanumba: Has a Very Touching Story!
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Vicky Kamata Anastahili Pongezi!, Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!
Mafuru ni Mmoja wa Mashujaa wa Taifa Hili, Kwa Kuwa Mkweli Daima, Jee Kupangiwa Kazi Muhimu Zaidi?.
Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa! Ni kweli Balozi wa Uingereza ni Jasusi. To Hell with...!
 
Kibajaji anasema tangu amezaliwa hakuwahi kumjua baba yeke hadi amefariki, wamezaliwa wengi, waliwahi kupata msiba kufiwa na dada yake, shauri ya umasikini, walimzika bila hata Sanda, bali walimzika na gunia!. Aliumia sana!.

Aliletwa Dar na mama mmoja kuja kumbebea mizigo, baada ya kufika jijini na kufikisha mzigo, kesho yake aliporudi pale yule mama alimfukuza kuwa kazi yake imeisha, ni kufikisha tuu mzigo. Hana hili wala lile, alilala juu ya mti wa mkorosho kwa siku saba eneo la Kinondoni Moscow.

Baada ya pele alianza kujiongeza kwa kufanya chochote, zege amebeba, vibarua amefanya, mizigo, akawa anafanya chochote, ameuza kahawa, amekuwa machinga, amefanya kila kitu.

Very interesting!.

Paskali
 
Anasema alipewa kazi ya ulinzi Kiwango Security, katika kazi yake ya ulinzi, kuna siku alipangiwa kulinda kwa Capt. Komba, ndipo alipokutana na mkewe Edina alikuwa house girl kwa Komba, akamletea kanda ya nyimbo za dini, akaiomba, huo ukawa mwanzo!.

P.
 
Kibajaji ni muongeaji mzuri sana kwa mambo yaliyo within uelewa wake... I mean mambo yasiyohitaji usomi!!

Na kwa kuzingatia hata hao wasomi hawana hata uwezo wa kujenga hoja kwenye mambo yaliyo kwenye usomi wao, haitashangaza kuona Kibajaji akiwazidi hata hao wasomi kwenye kujieleza!!!

Sema duh, hiyo source ya jina... kumbe ni simulizi ya mende kudondosha kabati!
 
Muongo sana huyo. Leo anasema alipelekwa dar na mama fulani kwaajili ya kubeba mizigo, kuna siku alisema alipelekwa dar na rafiki yake kuuza kahawa. Ni muongo wa kutupwa, hapo mwisho wa yote utasikia atakavyojisifu kuwa ana V8 mbili, moja anatumia yeye nyingine mkewe.
 
Mkewe Edna kaishia darasa la nne, yeye aliishia darasa la 3, hivyo wakichanganya ndio inakuwa darasa la saba. Amesema jambo moja la muhimu sana, yeye na mkewe wana elimu kubwa sana isiyo rasmi. Kama serikali ingetumia mbinu za kuitap hii elimu isiyo rasmi ya Watanzania wasio na elimu ya darasani, wanaweza kufanya mambo makubwa, kuliko ma profesa wenye elimu za kwenye makaratasi!.

P.
 
Back
Top Bottom