Livingstone Lusinde amewataka CHADEMA Wamuadhibu Joshua Nassari

Hahahaha Lusinde bhana eti JPM anabadilisha mfumo!!! Huyu mbunge anajua hata maana ya mfumo kweli?!!!! Halafu anasema wao wamemwajibisha Kitwanga! Yaani huyu babu wa akili anachowaza mle ni itikadi tu badala ya utaifa hata hajui utofauti wa serikali na chama ndani ya bunge, yeye akiwa mle ndani ya bunge anaamini ndio serikali sababu yuko ccm! Hajui hata majukumu ya kibunge na Serikali ndani bunge, kuwa na wabunge wa namna hii katika karne hii ya sayansi na teknolojia ni majanga makubwa
 
Kwani kanuni zao za Bunge zinasemaje kuhusu mbunge kuingia bungeni huku amelewa au akikutwa na chupa ya pombe? Hivi kukutwa umebeba pombe ndio kwamba umelewa au unaenda kuinywa muda huo?
 
Hivi huyu mpuuzi keshawahi kuadhibiwa kwa matusi yake wakati wa kampeni na ndani ya bunge?
 
wacha uongo. toa mifano rais ametukana au amekejeli upinzani zaidi ya kufanya utani tu unaokubalika kwenye siasa zetu. huwezi kulinganisha na matusi kwenye mitandao ambayo ina mikono ya wapinzani. mtu kama lissu na lema wamekua mfano wa lugha ya kejeli na matusi kwa rais wa jamhuri
Kilaza wewe
 
wacha uongo. toa mifano rais ametukana au amekejeli upinzani zaidi ya kufanya utani tu unaokubalika kwenye siasa zetu. huwezi kulinganisha na matusi kwenye mitandao ambayo ina mikono ya wapinzani. mtu kama lissu na lema wamekua mfano wa lugha ya kejeli na matusi kwa rais wa jamhuri
Hapo tu ndo ushabiki unaharibu...
Kwa raisi ni utani
Kwa CDM ni matusi na kejeli....
Kwa nini usiseme.kina Lema na Lissu nao wanatania kama kweli unataka kuwa fair...??
 
KIMSINGI MAMBO YANAYOFANYWA NA CCM NI YA AJABU.
LAKINI KUINGIA BUNGENI UMELEWA, TENA NA CHUPA MKONONI, NI AJABU ZAIDI.
Hivi bungeni hakuna wapiga picha na waandishi wa habari?
Nassari hicho kitendo alifanyia bungeni au chumbani kwake tena chooni? Mbona sijasikia hata kuona hii habari toka kwa wanahabari?
 
Chadema hakuna mwenye uthubutu wa kumuonya Nasari.Wote wanywa viroba
Tunaposema chadema ni chama cha wanywa viroba tunamaanisha mambo kama haya ya Mbunge mzima kuingia bungeni na konyagi
You don't have facts...nani alimwona?
Huyo alomwona alikuwa peke yake?
Tunaomba proof hapa....
Nje ya hapo huu tunauita ni uzushi na propaganda za kitoto.
 
Kwenye suala la matusi na kuheshimiana, Kibajaji anapaswa kukaa kimya.
 
Mh Kitwanga aliondolewa kwa lengo la kupotezea kashfa ya LUGUMI na si kwa sababu ya ulevi.
 
You don't have facts...nani alimwona?
Huyo alomwona alikuwa peke yake?
Tunaomba proof hapa....
Nje ya hapo huu tunauita ni uzushi na propaganda za kitoto.
Unaniomba mie proof?!!
Akina Tundu Lissu wasingekaa kimya wakiona mbunge wao na chama chao akidhalilishwa,lazima ungesikia taarifa...muongozo...ukiona kimya ujue ni kweli kamanda
 
Ikithibitika Nassari aliingia na konyagi bungeni na alikuwa kalewa kiongozi Wa kambi ya upinzani aitishe kikao na wamwadhibu. Huyu chalii haonekani jimboni Kama alitaka kusoma full time angeenda kusoma agombee akishamaliza masomo. Toka ahongwe mashamba hapiganii Tena ardhi kubwa na nzuri inayoshikiliwa na wazungu/wawekezaji uchwara,ardhi kubwa inazungushiwa uzio bila kuendelezwa huku wenyeji wakikosa maeneo ya kulima na kujikuta wakikodisha ardhi kwa laki mbili hadi tatu sehemu zenyemaji kwa ekari moja.
Nassari ni bure kabisa na hafai kukosoa watu bungeni huku yeye hana afanyacho jimboni,inaudhi sana!! Ameshindwa kubuni masoko kinamama wauze bidhaa imebaki minada tuu,halmashauri ya Meru inaongoza nchini kwa madili(wanafunzi hewa,watumishi hewa,ufaulu duni,kilimo cha bangi nk) Niupuuzi sana kuongozwa na kakijana kasikojielewa,chadema wamwandae mtu sahihi next time maana maccm hayana nafasi huku!KAMA KUNA MBUNGE BUURE KABISA CHADEMA BASI NI NASSARI! hizi sichuki binafsi ni ukweli ambao inapasa Chadema wajifunze kukubali kuskiza na kuelewa. Hâta kwenye akaunti zake huwezi kukuta kapost miradi ama shughuli zozote zamaana jimboni Kama kina Joseph Haule ama Sugu ama Lema. Naona amefaidi pesa vyakutosha lkn alipe fadhila atajachuma chuki na malaana
 
Uongo upi? Nasari kakamatwa na walinzi wa bunge ikiwa amelewa na anachupa ya konyagi. Jamani laana hupati kwa baba na mama tu. Nasari anasumbuliwa na laana ya Mwakyembe.
Uongo aliosema Lusinde ni kuwa wao ccm wamemchukulia hatua Kitwanga!Ni hatua zipi chama imemchukulia kitwanga?Huo si uongo wa wazi!Nassari kakosea na anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu,hilo sibishi!Hayo ya laana ya makyembe ni porojo tu,unajionesha wigo wako finyu wa kujadili hoja!
 
Wagogo wa mtera mmekula hasara miaka mitano mfululizo kwa Mara ya pili.
 
Unaniomba mie proof?!!
Akina Tundu Lissu wasingekaa kimya wakiona mbunge wao na chama chao akidhalilishwa,lazima ungesikia taarifa...muongozo...ukiona kimya ujue ni kweli kamanda
Hujasikia alichosema Msigwa au unataka mpaka waombe mwongozo?
Tatizo ni kwamba,source ya jambo lenyewe ni Mwakyembe! Haaminiki hata kidogo.....
Usishangae kesho akakana kuwa hajasema Nassari alikuwa amelewa na kakamatwa na chupa ya konyagi.....
Bungeni kuna waandishi wa habari toka vyombo mbali mbali,unaamini kweli waandishi wote wasione habari hii ijulikane kwa Mwakyembe tu...!??
Kwa nini tusijiulize hata waandishi wa gazeti la Uhuru wasione?
 
Chadema hakuna mwenye uthubutu wa kumuonya Nasari.Wote wanywa viroba
Tunaposema chadema ni chama cha wanywa viroba tunamaanisha mambo kama haya ya Mbunge mzima kuingia bungeni na konyagi
Majungu na uzushi si ndio jadi yenu CCM. Chukua Zawadi yako mwambie na jingalao namletea.
IMG-20170422-WA0004.jpg
IMG-20170422-WA0004.jpg
IMG-20170422-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom