Live Updates YANGA SC VS MTIBWA SUGER leo tr. 16/04/016

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
LEO Kwenye uwanja wa Taifa kutakuwa na pambano kali la kufa mtu kati ya timu ya Wananchi Dar Young Africans dhidi ya timu kutoka kule mkoani Morogoro Mtibwa Suger.

Yanga wanaingia katika pambano hili huku wakizitaka points zote 3 ili kuipiku timu inayoshikiria usukani kwa vipindi vipindi kama mvua za kusi Simba SC. Mtibwa wao wanataka point 3 ili kufufua matumaini ya kugombania ubingwa kama timu za Yanga, Simba na Mtibwa Suger.

Pambano la round ya kwanza ambalo lilifanyika kule Jamhuri Morogoro Yanga waliikung'uta mtibwa goli 2-0 goli ambazo zilifungwa na Donald Ngoma na Malimi Busungu.

Kikosi cha Yanga leo kitakuwa hivi,
1. Deogratius Munish "Dida"
2.Juma Abdul
3.Oscar Joshua
4.Kelvin Yondani
5.Nadir Haroub Cannavaro
6.Vincent Bousou
7.Simon Msuva
8.Thaban Kamusoko
9.Donald Ngoma
10.Haruna Niyonzima
11.Deus Kaseke

Substitutions
Ally Mustapha
Malimi Busungu
Pato Ngonyani
Salum Telela
Paul Nonga
Antonhy Mateo

Tahadhari kwa kocha wa Mtibwa.
Waambie wachezaji wako waingie uwanjani kwa leo la kucheza mpira waache kupanic, tofaut na hapo Kadi Nyekundu au Penalti itawahusu.

Kila la kheir timu ya Wananchi Dar Young Africans.
 
Vp leo waarabu wataishangilia mtibwa au hadi waje waarabu wenzao! Maana hii mechi inawahusu. Anyway kwa mpira ule wa mtibwa nilio uona kwenye mechi yao ya mwisho na Azam tena kwenye uwanja wao wa nyumbani, bila shaka watafungwa! labda wabadilike kwa kuwa tu wanacheza na Yanga. Walikua kawaida sana!
 
Bila kadi nyekundu msingefika hapo!Mmezoea kubebwa bebwa mtakua lini?Tunajua kombe hili lenu na sioni hata umuhimu wa kuliona kama pambano kali wakati mshindi anajulikana!Unawezaje kuwa na timu ya wachezaji 12 uwanjani halafu timu pinzani inapigwa red wanabaki 10 halafu usishinde?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wewe ulitakaje!!! Wachezaji wetu wakichezewa rafu kadi wapewe wao ndio ungefurahi!!!!! Waambie baki zenu zicheze kwa nidhamu ya mpira,
Mchezo huu hautakiwi hasira
 
LEO Kwenye uwanja wa Taifa kutakuwa na pambano kali la kufa mtu kati ya timu ya Wananchi Dar Young Africans dhidi ya timu kutoka kule mkoani Morogoro Mtibwa Suger.

Yanga wanaingia katika pambano hili huku wakizitaka points zote 3 ili kuipiku timu inayoshikiria usukani kwa vipindi vipindi kama mvua za kusi Simba SC. Mtibwa wao wanataka point 3 ili kufufua matumaini ya kugombania ubingwa kama timu za Yanga, Simba na Mtibwa Suger.

Pambano la round ya kwanza ambalo lilifanyika kule Jamhuri Morogoro Yanga waliikung'uta mtibwa goli 2-0 goli ambazo zilifungwa na Donald Ngoma na Malimi Busungu.

Kikosi cha Yanga leo kitakuwa hivi,
1. Deogratius Munish "Dida"
2.Juma Abdul
3.Oscar Joshua
4.Kelvin Yondani
5.Nadir Haroub Cannavaro
6.Vincent Bousou
7.Simon Msuva
8.Thaban Kamusoko
9.Donald Ngoma
10.Haruna Niyonzima
11.Deus Kaseke

Substitutions
Ally Mustapha
Malimi Busungu
Pato Ngonyani
Salum Telela
Paul Nonga
Antonhy Mateo

Tahadhari kwa kocha wa Mtibwa.
Waambie wachezaji wako waingie uwanjani kwa leo la kucheza mpira waache kupanic, tofaut na hapo Kadi Nyekundu au Penalti itawahusu.

Kila la kheir timu ya Wananchi Dar Young Africans.
Leta news, mpira si usha anza?
 
Bila kadi nyekundu msingefika hapo!Mmezoea kubebwa bebwa mtakua lini?Tunajua kombe hili lenu na sioni hata umuhimu wa kuliona kama pambano kali wakati mshindi anajulikana!Unawezaje kuwa na timu ya wachezaji 12 uwanjani halafu timu pinzani inapigwa red wanabaki 10 halafu usishinde?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Kunya anye kuku, bata anaharisha!
Wakicheza ovyo kadi lazima. Timu mbovu hazichezewi rafu. Ndivyo mpira ulivyo!
 
Leo nataka nithibitishe sarakasi za mpira wa tz nasubiri penalt na kadi nyekundu ili mpira huu niutelekeze kabisa maana nimeona wadau wanalalamika kadi nyekundu penalt zikikosekana basi majungu
 
Subiri tu utaona
 
Back
Top Bottom