Live Updates: Vodacom Premier League Simba SC Vs Ndanda FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Dimba la Taifa jijini Dar es salaam liko shwari kabisa kuelekea mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara VPL.

Simba SC vinara wa ligi hiyo wakiwakaribisha Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara.
IMG_20180506_160334_236.jpg
FB_IMG_1525611889602.jpg

0'1 mpira umekwisha anza uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Naona timu zote zikianza kwa kusoma mchezo wa mpinzani wake

07' Mpira sasa ni mashambulizi kwa pande zote.. Huku Simba SC wakijaribu kupata bao la mapema

10 ' Ndanda wanapanga shambulizi. Lakini mchezaji anachezewa madhambi. Inapigwa faulo lakini wanakaa vema mabeki wa Simba SC

Katikati ya uwanja Simba SC wanakwenda kwa kasi. Kwake Kotei anapasia Mkude.

14' Ni faulo kuelekea lango la Simba SC

15' Ndanda FC wanacheza eneo lao la kujidai..wanacheza kwa kujiamini sana.

Anachukua Kichuyaaa kwake Gyan.. Kwake huku Kotei.. Lakini Asante Kwasi anatoa mpira nje

Ndanda FC wanakwenda lakini inakuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Bocco anakwenda na Mpiraaaa lakini inakuwa faulo kuelekea Ndanda. Eneo hatari sana

Wakati huo huo mchezaji wa Ndanda anapewa kadi ya njano. Inapigwa faulo kuelekea lango la Ndanda FC

20' Kichuyaaa anapiga lakini golikipa anapangua na kuwa kona ambayo golikipa anapangua na mabeki wanaokoa

24 ' uwanja wa Taifa Simba SC 0-0 Ndanda FC

Kichuyaaa anaingiza pale kwake Asante Kwasi.. Lakini ni Offside

29' mchezaji wa Ndanda ameunawa mpira na kuwa faulo.. Maeneo ya hatari tusubiri yatakayojiri

Inapigwa.. Kichuyaaa lakini golikipa anaweka katika himaya yake

Ndanda awanatengezea nafasi. Lakini mabeki wa Simba wanakaa sawa na kuondosha hatari zote.

Asante Kwasi anapiga shuti mbele. Lakini unamkuta mchezaji wa Ndanda

Mpira unakwenda kwenye lango la Simba.. Lakini Golikipa Manula anadaka mpira ule na kupiga mbele kwake Asante Kwasiiii kwa Nyoni.. Lakini wanapoteza

Mponda anakwenda.. Anapiga mbele lakini unatoka nje na kuwa Goal Kick

Mpira unapigwa mbele kwake Okwi na mabeki wanaokoa.

Simba SC wanacheza kwa kasi lango la Ndanda FC.. Huku wakiwa nyuma wakipanga mashambulizi.

38' ni kona kuelekea lango la Ndanda.. Anapiga Kapombe lakini golikipa anadaka bila wasiwasi

Kwake Masawe mbele kule lakini anawahi Mlipili na kupiga mbele

40' Simba SC 0-0 Ndanda FC

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Mbele kabisa apiga kwake Mrisho Ngasa lakini anatokea golikipa Manula anadaka.

Ndanda wanajaribu kupenya lango la Simba lakini Ulinzi uko imara chini ya Mlipili na Erasto

43' Goooooaaal Goooooaaal Goooooaaal.. Emmanuel Okwi anaindikia Simba SC bao la kwanza kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Kapombe

Simba SC 1-0 Ndanda FC

Unapigwa mpira kuelekea lango la Simba.. Ikiwa ni faulo

45+3 Anapiga moja ndefu na kuwa Goal Kick

Mpira unapigwa mbele kwake Erasto kwake Kotei. Lakini mpira ni mapumziko

Naam mpira ni mapumziko uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.. Ambapo Simba SC wapo mbele ya goli moja dhidi ya Ndanda FC

Kuelekea Kipindi cha pili. Mpira Umeanza Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ligi kuu Tanzania Bara VPL

46' Simba SC 1-0 Ndanda FC

48' Omar Mponda anakwenda mbeleee anapiga shuti golikipa Manula anapangua na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Simba wanakwenda lakini inakuwa faulo kuelekea Ndanda. Inapigwa faulo lakini ni goal kick

Ndanda sasa wanasogea lango la Simba kwake William.. Wanapoteza Ndanda

54' Katikati ya uwanja Simba SC wanapiga pasi mbili tatu.. Mkude anapiga kwa golikipa Aishi Manula

Masawe kwake Ngasa.. Mpira unaambaa na kuuwahi mchezaji wa Simba SC

Jacob anakwenda mbeleee pembeni anapiga shuti lakini anatoa nje Mlipili na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Kapombe... Kwake Asante Kwasi lakini mpira unakosa mmaliziaji na kutoka nje

60' Simba SC 1-0 Ndanda FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Wanachukua Simba SC.. Kwasi lakini golikipa wa Ndanda anatokea na kudaka

Ngasa anapiga shuti lakini mpira unatoka nje lango la Simba na kuwa Goal Kick

63' Kida Rashid Juma anaingia kuchukua nafasi ya Nicholas Gyan

Kapombe lakini beki masoud anaokoa. Na Mpiraaaa unakwenda mbele lango la Simba

John wa Ndanda anakwenda na Mpiraaaa lakini Erasto anatoa nje na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Okwiiii.. Lakini anawekwa chini na kuwa faulo.. Maeneo ya hatari tusubiri. Inapigwa lakini ni Offside

69' Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ligi kuu Tanzania Bara VPL

Simba SC 1-0 Ndanda FC

Kwake Kichuyaaa.. Rashid Juma sasa. Lakini Asante anachelewa kuwahi mpira

Mpira umesimama baada ya mchezaji wa Ndanda kupata rabsha. Ameinuka na Mpira umeanza

Kona kuelekea lango la Ndanda FC.. Inapigwa lakini inakolewa na kuwa kona tena. Ambayo haikuzaa matunda

Bocco anakwenda anapiga shuti la juu juu na kuwa Goal Kick

76' Asante Kwasi anakwenda kwenye benchi na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Hussein

Ibrahim ametoka na nafasi yake inachukuliwa mchezaji ambaye nitakutajia

83' Ni free kick kuelekea lango la Ndanda FC. Inapigwaaaa mpira unagonga mwamba na kumkuta Boccoooo goo laaa ni Offside. Aliweka mpira kimiani tayari

87' Kwake Rashid. Lakini anapiga shuti lakini anaokoa beki wa Ndanda

90+4

Kuelekea kumalizika kipindi cha pili uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

90+2 Okwiiii anakwenda kwenye benchi na nafasi yake inachukuliwa na Mavugo Laudt

Mavugo anakotroo lakini ananyang'anya na mchezaji wa Ndanda

90+3 pembeni mwa uwanja Kapombe anarusha. Lakini Wanachukua Ndanda FC hata hivyo wanapoteza

Naam dakika 90 za mchezo wa VPL kati ya Simba SC dhidi ya Ndanda FC zimekamilika ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa goli moja bila majibu liliowekwa kimiani na Emmanuel Okwiiii na kufikisha magoli yake 20 kwenye ligi kuu Tanzania Bara..

Asanteni.. Ghazwat
 
10' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam bado milango ni migumu

Simba SC 0-0 Ndanda FC
 
Boccoooo anakwenda... Laa kona. Ibrahim analala na kuwa kona
 
Kichuya anapiga ndefu na Mpira unagonga mwamba
 
Dimba la Taifa jijini Dar es salaam liko shwari kabisa kuelekea mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara VPL.

Simba SC vinara wa ligi hiyo wakiwakaribisha Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara.View attachment 767918View attachment 767919

0'1 mpira umekwisha anza uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

14' Ni faulo kuelekea lango la Simba SC

15' Ndanda FC wanacheza eneo lao la kujidai..wanacheza kwa kujiamini sana.

Anachukua Kichuyaaa kwake Gyan.. Kwake huku Kotei.. Lakini Asante Kwasi anatoa mpira nje

Ndanda FC wanakwenda lakini inakuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Bocco anakwenda na Mpiraaaa lakini inakuwa faulo kuelekea Ndanda. Eneo hatari sana

Wakati huo huo mchezaji wa Ndanda anapewa kadi ya ngano

20' Kichuyaaa anapiga lakini golikipa anapangua na kuwa kona ambayo golikipa anapangua na mabeki wanaokoa

24 ' uwanja wa Taifa Simba SC 0-0 Ndanda FC
We mleta Uzi ni mbaguzi sana.. Mbona hujaweka na kikosi cha Ndanda wazee wa kuchele...
 
Okwi la la golikipa anacheza mpira.. Heko golikipa ilikuwa ni hatari sana
 
Itapendeza zaidi tukishinda hii game..itakua imebaki sehemu ndogo sana..
Simba nguvu moja!
 
Dimba la Taifa jijini Dar es salaam liko shwari kabisa kuelekea mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara VPL.

Simba SC vinara wa ligi hiyo wakiwakaribisha Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara.View attachment 767918View attachment 767919

0'1 mpira umekwisha anza uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

14' Ni faulo kuelekea lango la Simba SC

15' Ndanda FC wanacheza eneo lao la kujidai..wanacheza kwa kujiamini sana.

Anachukua Kichuyaaa kwake Gyan.. Kwake huku Kotei.. Lakini Asante Kwasi anatoa mpira nje

Ndanda FC wanakwenda lakini inakuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Bocco anakwenda na Mpiraaaa lakini inakuwa faulo kuelekea Ndanda. Eneo hatari sana

Wakati huo huo mchezaji wa Ndanda anapewa kadi ya ngano

20' Kichuyaaa anapiga lakini golikipa anapangua na kuwa kona ambayo golikipa anapangua na mabeki wanaokoa

24 ' uwanja wa Taifa Simba SC 0-0 Ndanda FC

Kichuyaaa anaingiza pale kwake Asante Kwasi.. Lakini ni Offside

Kadi ya NGANO.....hahaha
 
33' Simba SC 0-0 Ndanda FC Uwanja wa Taifa. Bado milango ni bila kwa bila
 
Back
Top Bottom