Ligi Kuu ya Tanzania Bara: Mbao FC yaitandika Simba SC kwa goli 1-0

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Timu ya soka ya Mbao ya Mwanza leo imefanikiwa kuwafunga mabingwa watetezi Simba ya Dar es Salaam kwa goli moja kwa bila

Katika mechi hiyo iliyofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, goli la washindi lilifungwa na Said Said kwa penalti katika dakika ya 27 ya mchezo huo.

Kwa matokeo hayo timu ya Mbao inaongoza ligi hiyo

==============

Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza liko shwari kabisa kuelekea mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara.
Leo Mbao FC toka jiji la Mwanza, anamkaribisha Bingwa Mtetezi, Simba SC.
Mechi hii inategemewa kuanza saa 10 kamili jioni.
Baki Hapa Hapa Kwa Taarifa Zaidi Juu ya Lineup, Historia, Msimamo n.k

UPDATE 1
Kikosi cha Simba SC Kinachoanza Leo;
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohammed Hussein
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Clatous Chama
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Mohammed Ibrahim
Kikosi cha Akiba ni; Deogratius Munishi; Paul Bukaba; Said Ndemla; James Kotei; Marcel Bonaventure: na 'The Man Himself', Meddie Kagere a.k.a MK14.
 
DONDOO KADHAA KUELEKEA MECHI YA LEO;
1. Matokeo ya Timu hizi kabla ya kukutana siku ya Leo:
Mbao FC 0 - 1 JKT Tanzania
Ndanda FC 0 - 0 Simba SC

2. Mara ya mwisho Timu hizi kukutana katika Ligi:
Simba SC 5 - 0 Mbao FC

3. Matokeo ya Hizi timu katika uwanja wa CCM Kirumba:
Tarehe: 10/04/2017
Mechi: Mbao FC 2 Simba SC 3

Tarehe: 21/09/2017
Mechi: Mbao FC 2 Simba SC 2
 
Msimao wa TPL mpaka hivi sasa;
IMG-20180919-WA0026.jpeg
 
Wachezaji wa Simba SC waliotayari kwa mtanange wa leo ni;

Aishi Manula na Deo Munishi Dida, Shomary Kapombe, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Clatous Chama, James Kotei, Mohammed Ibrahim, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Shiza Kichuya, Meddie Kagere, John Boko, Emanuel Okwi, Mohammed Rashid na Adam Salamba.

Katika mechi ya leo, Mfalme wa Nyika, atawakosa wachezaji wafuatao ambao ni majeruhi;
1. Asante Kwasi
2. Hassan Dilunga
3. Said Nduda
4. Muzamiru Yasin
Pia Niyonzima Haruna na Juuko Murshid, watakosekana kutokana na kutokua fiti.
 
UPDATE 1
Kikosi cha Simba SC Kinachoanza Leo;
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohammed Hussein
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Clatous Chama
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Mohammed Ibrahim
Kikosi cha Akiba ni; Deogratius Munishi; Paul Bukaba; Said Ndemla; James Kotei; Marcel Bonaventure: na 'The Man Himself', Meddie Kagere a.k.a MK14.
 
Mpaka sasa yamebaki masaa 3 mpira uanze.. Ila si ndani ya uwanja au nje, pote mashabiki wamejaa.. Na rangi za jezi zinazotamba mpaka sasa ni za Simba SC.
 
Back
Top Bottom