Live Updates: Simba Vs Yanga - Uwanja wa Taifa, Dar (Disemba 21, 2013 - Nani Mtani JEMBE?)

Utitiri wa mashabiki wa Yanga jana
Ijumaa ulijazana kwenye Uwanja wa
Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam
kumwangalia mshambuliaji wao
mpya, Okwi ambaye alianza mazoezi
na kikosi hicho ambapo kocha mkuu
wa timu hiyo, Mholanzi Ernest
Brandts amekiri kwamba atamtumia
mchezaji huyo kwenye fowadi.
Brandts alifafanua sababu ya
kumchezesha kama straika na winga
kwa sababu ana sifa zote, ni
mwepesi ana kasi, anajua
kutengeneza nafasi za mabao na
anafunga pia.
Alisema: “Uwepo wa Okwi kikosini
mwetu ni faraja. Okwi ni mchezaji
mzuri na ninafuraha kuwa naye
kikosini kwa sababu ana kila sifa za
uchezaji. Okwi ni mwepesi ana kasi
katika uchezaji, anajua kutafuta na
kutengeneza nafasi za kufunga lakini
pia yeye ni mfungaji mzuri wa
mabao, ndiyo maana tukamtafuta na
kumleta Yanga.”
Alipofika tu, mashabiki ambao
walikuwa wamewahi na kufurika
maeneo hayo, walikuwa wanaimba
nyimbo za shangwe wakimpokea,
“Okwi, Okwi..”
Na kabla ya kuanza mazoezi, Brandts
alimtambulisha, Okwi kwa wachezaji
wenzake na benchi la ufundi:
“Tumepata ugeni wa mwenzetu
hapa, nafikiri wote mnamjua, Okwi
tutakuwa naye kwenye timu,
mumpe ushirikiano.”
Wakiwa katika mazoezi, mchezaji
ambaye alikuwa karibu sana na Okwi
ni Said Bahanuzi ambaye walikuwa
wakizungumza na kucheza ingawa
baadaye alizungumza na kucheka na
wengine.
KOCHA SIMBA
Kochawa Simba, Zdravko Logarusic
amesema amekaa na wachezaji
wake na kuwaweka sawa kisaikolojia
huku akidai mechi za wapinzani wa
jadi huwa hazimsumbui hata kidogo
na anaamini asilimia 90 kikosi chake
kitaibuka na ushindi.
Simba na Yanga zinapambana katika
mchezo utakaoanza saa kumi kamili
jioni.
“Maandalizi yetu ni mazuri wachezaji
wote wako vizuri tayari kwa mchezo
huo ambao utakuwa mgumu, mzuri
na wenye ushindani sana. Nimekaa
na wachezaji wangu na nimewaweka
sawa na kuwambia kuwa hawatakiwi
kuhofia hiyo mechi, tutaingia
uwanjani kwa kasi kuanzia mwanzo
hadi mwisho wa mchezo ili
kuhakikisha tunashinda hiyo mechi,
mimi sina presha nayo kwa sababu
nazijua mechi za wapinzani hivyo
hazinisumbui,” alisema Loga.
Aliongeza: “Kutokana na ubora wa
timu yangu na aina ya wachezaji
nilionao hiyo mechi tunashinda,
amini usiamini, hatuogopi yeyote,
tunakwenda uwanjani kuonyesha
soka la kiwango, mashabiki waje kwa
wingi kutusapoti kwani wao ni
mchezaji wa ziada uwanjani.”
Mechi ya mwisho timu hizo kukutana
ilikuwa Oktoba 20 mwaka huu na
kutoka sare ya mabao 3-3, Yanga
walikuwa wa kwanza kufunga mabao
yao lakini Simba wakaibuka kipindi
cha pili na kusawazisha yote
 
NIYONZIMA
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima
amewaambia wachezaji wenzake
kwamba wanapaswa kujituma katika
mchezo huo kwani ni moja ya mechi
kali na zisizotabirika.
“Kama wachezaji wa Yanga
tunapaswa kujituma tunapocheza na
Simba hata kama tunajiamini na
kikosi imara, huu ni mchezo wa
watani wa jadi, matokeo yoyote
yanaweza kutokea mkizembea,”
alisema Niyonzima, raia wa Rwanda.
OKWI
Straika Emmanuel Okwi anatarajiwa
kucheza mechi yake ya kwanza akiwa
Yanga na anakutana na timu yake ya
zamani ya Simba katika mchezo wa
Mtani Jembe.
Okwi alisema: “Nimekuja Yanga
kufanya kazi na wao watafurahia tu,
kikubwa namwomba Mungu
aniongoze kukamilisha malengo
yangu. Kuhusu mechi ya Simba, sina
wasiwasi niko tayari kucheza lakini
mwisho wa yote.
OWINO
Beki wa kati na tegemeo zaidi kwa
Simba, Joseph Owino amewashusha
presha wachezaji wenzake na
kusema wanapaswa kuingia
uwanjani kama siku zote na
wasitishwe na majina ya wachezaji
wa Yanga.
Owino ambaye sasa atacheza pacha
na beki Mkenya Donald Musoti
alisema; “Sisi tumejiandaa vizuri kwa
ajili ya mechi na kila kitu
kinakwenda vizuri, tupo tayari
kukabiliana na Yanga na hiyo mechi
tunashinda ingawa watu hawatupi
nafasi. Kila mtu anaiongelea Yanga
kwa sababu ya usajili wao wa majina
makubwa, lakini hatupaswi kuogopa
majina yao mpira utaonekana
uwanjani, hata wenzangu
wanatakiwa kuondoa hofu hiyo,
muhimu tuingie uwanjani tukiwa
freshi hakuna kuogopa yeyote.”
Aliongeza: “Hata mechi iliyopita
tuliyotoka sare ya 3-3 wengi
hawakutupa nafasi lakini uliona
kilichotokea ndio maana nasema
mpira hautabiriki lolote linaweza
kutokea, waache watudharau lakini
soka tutaonyesha uwanjani.”
MSHIKO
Hadi jana Ijumaa mchana kwenye
mashindano ya mashabiki wa timu
hizo, Yanga ilikuwa inaongoza kwa
Sh 96 milioni huku Simba ikiwa na Sh
3.8 milioni. Fedha hizo ambazo
mwisho wa kuzipigia kura ni leo
Jumamosi kila klabu itakabidhiwa
hundi yake ambayo ni tofauti na
mapato ya mchezo.
 
MTANI JEMBE || TWITE - SIMBA
WASITARAJIE KAMA TUTARUDIA MAKOSA
Beki wa Yanga, Mbuyu Twite
amesema Simba wasitarajie kupata
mchekea wa kusawazisha mabao
kama ilivyokuwa katika mechi ya 3-3,
licha ya Yanga kuongoza kwa mabao
3-0 mpaka mapumziko.
“Simba wasitarajie kuwa tutarudia
makosa ya mechi iliyopita ya
kuwafunga mabao matatu na
baadaye wanarudisha yote, kiukweli
wasahau hilo,” alisema.
 
MAKIPA wa Simba na Yanga ni
kitendawili kikubwa kwa makocha
wa klabu hizo kuamua ni nani
ataanza kudaka mechi ya leo
Jumamosi ya Nani Mtani Jembe
itakayochezwa kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba imewasajili, Ivo Mapunda na
Mghana Yaw Berko ingawa ina
chipukizi, Abou Hashim aliyekuwa na
kikosi hicho msimu uliopita.
Yanga nao wana makipa imara, Juma
Kaseja, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally
Mustapha ‘Barthez’.
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic
anasugua kichwa kuona ni nani
atadaka mchezo huo kulingana na
uwezo wa kila kipa kwani, Ivo
ambaye amesajiliwa kutoka Gor
Mahia ya Kenya ni mzoefu na
amefanya vizuri kwenye mashindano
ya Chalenji akiwa na kikosi cha
Kilimanjaro Stars.
Sawa na Berko ambaye aliichezea
Yanga kwa mafanikio, ni mzoefu
lakini katika mazoezi ya kikosi hicho,
yaliyokuwa yanafanyika Uwanja wa
Kinesi Dar es Salaam naye alifanya
vizuri.
Logarusic alisema: “Nitajua kikosi na
kipa atakayecheza saa mbili kabla ya
mchezo kwani naweza kusema ni
fulani ikatokea matatizo, kwa maana
hiyo yeyote anaweza kucheza.”
Kwa upande wa Yanga, Ernest
Brandts ambaye ana matumaini
makubwa ya kushinda mchezo huo,
ana kazi ya kuamua nani kati ya
Kaseja, Barthez na Dida aanze.
Kaseja ni mzoefu anafanya vizuri
mazoezini, wakati Barthez na Dida si
wazoefu sana lakini nao pia ni moto
ndani ya 18 ni hodari wa kudaka.
Brandts alisema: “Yeyote anaweza
kucheza, nakwenda kuzungumza na
wenzangu wa benchi la ufundi, kujua
ni namna gani tutafanya.”
Lakini kwa upepo ulivyo hadi jana
Alhamisi jioni Ivo na Kaseja walikuwa
na nafasi kubwa ya kucheza mechi
hiyo.
 
KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic
kwa siku mbili mfululizo amekuwa
akimpa mazoezi na mbinu mpya za
ufungaji straika wake, Amissi
Tambwe ili atishe kwenye mechi ya
Nani Mtani Jembe leo Jumamosi
dhidi ya Yanga yenye kipa Juma
Kaseja.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka
Zanzibar ilipo kambi ya Simba,
Tambwe alisema kocha amekuwa
akimpa mbinu mpya za ufungaji
dhidi ya makipa wazoefu na wajanja
kama Juma Kaseja wa Yanga.
“Naendelea vizuri na mazoezi na
kocha ananipa mazoezi mengine
mapya ya kufunga mimi na
washambuliaji wenzangu ili tuweze
kufanya vizuri katika mchezo na
Yanga, kocha anataka tufunge haraka
na ametuambia tunaweza kufanya
vizuri,” alisema Tambwe raia wa
Burundi.
Alipoulizwa na Mwanaspoti kama
anamfahamu Kaseja, Tambwe alijibu:
“Namfahamu Kaseja kama kipa
mzoefu na anayeweza kuzuia, lakini
mimi namwona wa kawaida kama
walivyo makipa wengine.”
Tambwe, ambaye anaongoza kwa
ufungaji katika Ligi Kuu Bara,
alisema: “Kwa nini nisifunge?
Naomba nipate nafasi halafu tucheze
kwa kuelewana kikosini, mimi ni
mshambuliaji ninayejiamini na kazi
yangu.”
 
KITAULO cha kipa wa Simba, Ivo
Mapunda ambacho mashabiki wa
soka Kenya wanakihusisha na imani
za kishirikina kitaonekana leo
Jumamosi ndani ya Uwanja wa Taifa
katika mechi ya Nani Mtani Jembe
dhidi ya Yanga.
Ivo amesajiliwa na Simba akitokea
Gor Mahia ya Kenya ambayo ni
watani wa jadi wa AFC Leopards pia
ya Kenya. Kipa huyo aliyesajiliwa na
Simba kwenye dirisha dogo
amekuwa maarufu Kenya kutokana
na kudaka penalti pamoja na
kutundika kitaulo cheupe langoni.
Katika mechi za Gor Mahia na AFC
kimekuwa kikiibua utata baina ya
wachezaji ambao hukihofia huku
mashabiki wa timu yake wakiamini
kwamba kinawabeba na kumpa
nguvu ya ushindi langoni.
Ivo alisema kwamba; “Hiki kitaulo ni
cha kujifuta jasho tu wala hakina
lolote.”
Mbali na AFC michezo mingine
ambayo kitaulo hicho kiliibua utata
ni dhidi ya Sofapaka na nyingine
dhidi ya Tusker FC.
Tangu asajiliwe Simba mchezaji
huyo wa zamani wa Yanga atakuwa
anaonekana kwa mara ya kwanza
akiwa amevalia jezi ya Simba
kwenye mechi dhidi ya Yanga
maarufu kama Mtani Jembe.
Mashabiki wamekuwa na hamasa ya
kuona uimara wa kipa huyo
waliyekuwa wakimuona kwenye
runinga pamoja na mbwembwe za
kitaulo chake ambacho hukitundika
golini mechi inapoanza lakini
baadaye hu
 
MTANI JEMBE || JERRY TEGETE - YANGA
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha
tunapata ushindi, kutokana na
maandalizi ya nguvu tunayofanya na
kocha wetu.”
Unadhani atatupia leo kama kawaida
yake akipewa nafasi ya kushiriki
mchezo huu?
 
NIONAVYO MIMI:KUELEKEA MTANI JEMBE SAA 10 JIONI.

Kwa mara ya tatu mfululizo,Simba wanaingia kwenye mechi ya leo kama "underdogs" dhidi ya Yanga.Hawepewi nafasi na fans nje ya uwanja but wao huwa, wanajipa nafasi wenyewe ndani ya dk 90.

Ukuta "Berlin" wa Masoud na baba Ubaya,huku Pengine Owino akicheza na ndugu yake Musoti itahitaji nguvu ya ziada kuuvunja.Natamani kumuona Berko golini badala ya Mapunda.Hii ndo simba,Taifa kubwa!

Anko Mrisho,Ninyonzima na Kavumbagu,ni attacking line up ambayo inaweza kufanya kazi ya "fasihi",kuelimisha na kuburudisha.Natamani kuona Okwi akianzia benchi na Dida akianza golini.

Yanga wanahitaji Chuji kuanza kwenye midfield na Dilunga,ili kuwapa ulinzi Beki wao wa kati.Wanahitaji more defensive minded midfileders mbele ya mabeki wao kuliko attacking.

Okwi akiingia kipindi cha pili wakati Masoud na Baba ubaya wamepungua nguvu,ile kauli ya "mbele daima nyuma mwiko" ndipo itakapo timia.

Tambwe akitumia ubovu wa beki ya kati ya Yanga,atawaliza na Anko mrisho bribling na kasi vikikubali leo,simba chali!
 
Mkuu haya maelezo yote hayana maana hapa tena saivi,nilitegemea sasa hivi saa sita kasoro utakuwa maeneo ya uwanja wa Taifa hapo kwa ajili ya kuanza kutupa Updates za mechi sasa unatoa maelezo mareefu!!

Ninavyojua kwa mechi kama hii ukijumlisha na ujio wa Okwi kwa sasa najua kuna amsha amsha nyingi sana,tupe updates ili na sisi ambao hatupo uwanja wa Taifa kwa leo tena tuko nje ya nchi tufaidi!.
 
Mechi hii itatupa jibu kamili ni washabiki wa timu gani ni walevi
 
NIONAVYO MIMI:KUELEKEA MTANI JEMBE SAA 10 JIONI.

Kwa mara ya tatu mfululizo,Simba wanaingia kwenye mechi ya leo kama "underdogs" dhidi ya Yanga.Hawepewi nafasi na fans nje ya uwanja but wao huwa, wanajipa nafasi wenyewe ndani ya dk 90.9

Ukuta "Berlin" wa Masoud na baba Ubaya,huku Pengine Owino akicheza na ndugu yake Musoti itahitaji nguvu ya ziada kuuvunja.Natamani kumuona Berko golini badala ya Mapunda.Hii ndo simba,Taifa kubwa!

Anko Mrisho,Ninyonzima na Kavumbagu,ni attacking line up ambayo inaweza kufanya kazi ya "fasihi",kuelimisha na kuburudisha.Natamani kuona Okwi akianzia benchi na Dida akianza golini.

Yanga wanahitaji Chuji kuanza kwenye midfield na Dilunga,ili kuwapa ulinzi Beki wao wa kati.Wanahitaji more defensive minded midfileders mbele ya mabeki wao kuliko attacking.

Okwi akiingia kipindi cha pili wakati Masoud na Baba ubaya wamepungua nguvu,ile kauli ya "mbele daima nyuma mwiko" ndipo itakapo timia.

Tambwe akitumia ubovu wa beki ya kati ya Yanga,atawaliza na Anko mrisho bribling na kasi vikikubali leo,simba chali!

Mkuu umetia huruma sana leo umeongea kwa adabu sana!

Naomba nikukumbushe tu kwamba mpira ni dakika 90 kwa hiyo lolote laweza kutokea!

Mechi ya simba na Yanga mara nyingi huwa haina mshindi hadi pale mpira unapomalizika ukiachilia mbali maneno ya hapa na pale ya watani!

Pia ni mechi inayoweza kutoa matokeo ya ajabu sana ambayo hakuna anayetarajia kwamba yanaweza kutokea!

Yote kwa yote nitafurahi kuona mechi ikichezwa na kila timu ikionesha mchezo mzuri,lakini nitafurahi pia kuona mcheziaji Okwi aliyetikisa kwa wiki nzima sasa hapa nchini akianza na kucheza kwa dakika 90!

Mwisho wa siku naitakia ushindi Yanga!
 
Mkuu haya maelezo yote hayana maana hapa tena saivi,nilitegemea sasa hivi saa sita kasoro utakuwa maeneo ya uwanja wa Taifa hapo kwa ajili ya kuanza kutupa Updates za mechi sasa unatoa maelezo mareefu!!

Ninavyojua kwa mechi kama hii ukijumlisha na ujio wa Okwi kwa sasa najua kuna amsha amsha nyingi sana,tupe updates ili na sisi ambao hatupo uwanja wa Taifa kwa leo tena tuko nje ya nchi tufaidi!.

Asubuhi maeneo ya Steerz Posta nimefika pale kuwasubiria wauza tiketi matokeo yake walipofika wananambia zimebaki za VIP A kwa 40,000. Sasa hivi nataka kuelekea Taifa.
 
Leo nitakua Simba kwa mkopo, lakini akifungwa sinta husika kwa lolote.
 
Asubuhi maeneo ya Steerz Posta nimefika pale kuwasubiria wauza tiketi matokeo yake walipofika wananambia zimebaki za VIP A kwa 40,000. Sasa hivi nataka kuelekea Taifa.

Mkuu uwe makini sana ukae juu kule kwa sababu ule upande wa jukwaa la Yanga network huwa inasumbua sana,sijajua ni kwa nini?!
 
Mkuu uwe makini sana ukae juu kule kwa sababu ule upande wa jukwaa la Yanga network huwa inasumbua sana,sijajua ni kwa nini?!

hivi sehemu zingine huwa Network inakubali, mimi huwa huu Uwanja ukijaa Network inasumbua sana.
 
Kila la heri Simba Sports Club, mnyama unyamani, wekundu wa Tanzania na Taifa kubwa toka mtaa maarufu wa Msimbazi katikati ya jiji, kamata hao ndala rarua, tafuna hadi wajue Simba hata akikonda vipi na kunyeshewa mvua na kujikunyata na kunyong'onyea hawezi kuwa paka ataendelea kuwa Simba tu na akiamua kukunjua makucha na kurarua madhara yake ni makubwa.
 
Back
Top Bottom