Live Updates: Press Conference CHADEMA Makao Makuu Leo tarehe 18/06/2013

Status
Not open for further replies.

notradamme

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,012
1,195
Tuko pamoja, tushikamane sana wakati huu, kwani kilichofanyika Arusha ni dalili tosha kwamba CCM sasa wamefikia karibu na Mwisho.
Iweje WAFU wameibukia dar???? Nilidhani wameenda kuwazika wafu wenzao!!!!!! By the way, la arusha ni ule mwanzo wa MWISHO WA COCKROACHES IN COMBAT WEAR. STAY TUNED
 

Bocho

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
1,489
1,195
Watanzania tunafanya siasa kama dini kufikia kiasi cha kuamini kila neno lisemwalo na viongozi wetu wa kisiasa.

Tukubali ukweli kuwa kuna uwezekano kuwa CCM walihusika kwenye tukio lile kutokana na historia ya siasa za CCM hasa kwa upande wa ZNZ.

CCM kwa kushirikiana na askari polisi walikuwa wakitia vinyesi kwenye visima vya maji vilivyokuwa vikitumiwa na raia na shuleni kule Pemba huku wakiwatupia lawama wafuasi wa CUF.

Ukweli ulikuja kugundulika siku ambayo wanakijiji usiku wa manane walipoikamata gari ya polisi wakiifanya kazi ya kuweka kunyesi katika shule moja ya msingi. Na huo ndio ulikuwa mwisho wa vtendo hivyo.

Inawezekana tukio la Arusha halikupangwa na serikali nzima au wana CCM lakini baadhi ya makada wa CCM wakawa wanahusika kwa malengo wanayoyajua wao.

Hata hivyo, CHADEMA ni lazima wathibitishe ili wananchi waone ukweli huo. Short of that itakuwa ni malalamiko na allegations ambazo zitachukuliwa kama propaganda za kisiasa tu.
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
3,377
2,000
Wakati wa tukio la bomu la OLASIT Kardinali Pengo alitueleza kuwa alipewa taarifa na mtu aliyemwamini pasipo shaka kuwa lile bomu halikuwa na uhusiano na udini wa ugaidi.wengi wetu hatukumuelewa na sasa yetu macho na masikio.Asante mnyika kwa taarifa
 

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Kwa mtu yeyote aliye na uzoefu na utendaji kazi wa serikali makini popote duniani, tamko lililotolewa na mh. Lukuvi bungeni limeiabisha serikali. Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba serikali ndiyo inayomiliki kila aina ya dhana inayoweza kuiwezesha kupata ukweli wa kila jambo linalotokea hapa nchini, na hivyo haipashwi kuendesha manbo yake kwa hisia. Kinyume na matarajio hayo, kwa mtu makini yeyote anapochunguza kauli ya serikali iliyotolewa jana bungeni ataona wazi, ilitolewa kwa jaziba bila ya kupima madhara yanayoweza kuikumba serikali kwa kuonekana mbele ya wananchi kwamba badala ya kutafuta ukweli wa maafa yanayowapata wananchi mara zote serikali imekua nyepesi kuficha ukweli wa mambo!
 

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,885
2,000
mie nashangaa Watanzania katika suhala kubwa kama ili tunaleta ushabiki wa vyama, mie ningependa hivi vyama vyenye ukweli kuhusina na tukio zima wataambia ukweli Watanzania ili tujue mbaya wetu ni nani leo wamefanyiwa CHADEMA katika mkutano wao kesho hatujui ni tukio lipi litafuhatia zingatia haya kila mwenye ukweli ajaribu kuweka adharani ili tukomeshe matukio haya tuachane na propaganda za politics opportunity.
 

Mboko

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
1,084
1,195
hapo sasa mnyika anaonyesha kuchanganyikiwa. kweli akili ndogo huwa na fikra finyu
Hivi wewe ku.....m....a....a....a ..l umetumwa na Nape au Mwigulu na wameshakulipa bei gani hadi unatoa mapovu kiasi hiki au ulishiriki kurusha bomu?wewe aliyemuona Mnyika ana akili ndogo zako zikoje?Hapa moja kwa moja unaonyesha kwamba akili zako ni sawa na za mzoga kwa kuwa ulichoandika kinaonyesha kabisa kuwa wewe ni mbulula.tatizo shule za kata zinazoongezewa Div bila hata ya kurudia mitihani ndio zinawazalisha watu kama nyie pole sana,ila nakupa akiba ya maneno ipo siku utaamka na yatakukuta na hapo ndio utakumbuka whats is going on.Remember goes around comes around!!
 

Shenkalwa

JF-Expert Member
May 3, 2011
580
170
Kuna watu hawana uchungu na Tanzania na Raia waishio Tanzania Nikianza na mfano halisi wa Ritz sijawahi kujua huyu ni mtu wa aina gani katika jamii yetu nimefatilia mabandiko yake yananichosha kabisa

Huyo na wengine walioko humu JF ni miongoni mwa wale wanaofaidika na ufisadi wa ccm. Kwa hiyo hawana lingine zaidi ya kutetea kwa nguvu zao zote uozo wa nchi hii kupitia chama chao cha mafisadi. Ni watu ambao wamekosa muelekeo wa maisha kwa hiyo wanaishi kwa viruzuku toka Lumumba. Hawana uchungu na nchi hii jinsi inavyouzwa na watawala. Wasamehe bure tu
 

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,108
2,000
Eee bhana kumbe inawezekana kuwa ignore ! Mimi ninao kama Watano hivi , on top of my List yupo huyu Ritz !
Aiseh mimi ninao watu kama akina Lukosi aka Chili Sosi,taswira,bungeni,nashukuru yule mtoto wa mzee Jumanne bila shaka mods walishamuignore cku nyingi!
 

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,087
1,195
Wakati wa tukio la bomu la OLASIT Kardinali Pengo alitueleza kuwa alipewa taarifa na mtu aliyemwamini pasipo shaka kuwa lile bomu halikuwa na uhusiano na udini wa ugaidi.wengi wetu hatukumuelewa na sasa yetu macho na masikio.Asante mnyika kwa taarifa
Kuna mtu aliwahi kusema kuwa ile milipuko ya mabomu huko Mbagala na Gongolamboto haikuwa ajali ila ilifanywa makusudi; wakati huo nilimuona kama mwehu lakini kwa haya yanayotokea sasa naona alikuwa na hoja ya msingi.
 

Bandio

Senior Member
Feb 19, 2012
101
0
unaushahidi kama CCM wanahusika???
ukiambiwa ukaisaidie police utakua umeonewa?
fikiri kabla ya kuongea bwana mdogo.
Mkuu maandishi yako yanaashiria haya:-
  1. kama vile umekuwa mkali!
  2. Kama vile umechukia!
  3. Kama vile umeguswa na comments za watu makini!
  4. Kama vile unashabikia mambo ya hatari kwa usalama wa watu wanyonge!
  5. kama vile hujui kuwa hatuna polisi ila tuna vijana walinzi wa maslahi ya watu wachache! Lakini kama vile unajua lakini uanajaribu kuwaogopesha watu wasiseme kwa kuwa na wewe ni miongoni mwa hao wachache!
  6. Kama vile hujui kuwa Tanzania ya jana tofauti na ya leo na kwamba watu wana uwezo wa ku'draw conclusion kutokana na waliyoyaona!
  7. .........
  8. .........
  9. .........
  10. Lakini kama vile unahitaji kupewa pole kwa kuwaamini sana polisi!
 

piper

JF-Expert Member
Jan 17, 2012
3,254
1,195
Kama kawaida matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa ngoja tusubiri.
Cyo cha kujivunia mkuu, matamko haya yapaswa yafanyiwe kazi, ikifika kpindi akauwawa nduguyo ndo utajuwa km matamko yana tija au la, please dont play chess na maisha ya watu.
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,492
1,225
Mh! Hata hili bado serikali inakingia kifua polic na kujaribu kuficha ukweli
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom