Nusu Fainali Azam Sports Federation Cup: Simba 4-1 Yanga uwanja wa Taifa Dar es salaam

huyu kocha huwa ananiudhi hapo tu. natamani akishapanga kikosi sub amwachie Matola. Zile goli 2 zilizorudi ziliniuma sana hazikuwa za kurudi zile
Tukubali ukweli huyu kocha hatufai hata tukishinda kocha wa yanga anajua kabisa Simba itakujaje kitajachombeba ni uwezo binafsi hii ya kuacha mshambuliaji mmoja sii wakati wote inafanya kazi
 
Karibuni katika Matukio mubashara (Live Updates) ya Mechi ya watani wa jadi "Kariakoo Derby" kutokea Uwanja Mkuu wa Taifa maarufu Kwa mkapa..

Kipute kinatarajia kuanza saa 11 jioni...

Simba ilitangulia Nusu Fainali kwa kuifunga Azam FC bao 2-0 huku Yanga ikitinga nusu Fainali kwa kuiondosha Kagera Sukari kwa mabao 2 -1

Nusu fainali ya kwanza ilichezwa jana ambapo iliwakutanisha Vijana wa Namungo Fc wakipepetuana na Wagosi wa Sahare All Stars Matokeo yalikuwa ni Namungo 1 Sahare 0

Kwa hiyo mshindi wa leo atacheza na Namungo Fc katika hatua ya Fainali ya Azam Sports Federation Cup

Shamra shamra nje na ndani ya uwanja ni kubwa na leo ndio tunasema mtoto hatumwi dukani

Kuhusu mashabiki, kwa mujibu wa maelekezo kutoka Serikalini ni kuwa wataingia 30,000 tu badala ya 60,000 na hii ni kutokana na janga la Corona COVID-19 linaloisumbua dunia kwa sasa, mashabiki pia wameambiwa wachukue tahadhari zote katika kujikinga na Ugonjwa huu.

Ukiangalia takwimu, katika misimu mitatu iliyopita, Simba wamepata ushindi dhidi ya Yanga mara mbili tu na Yanga ikishinda mchezo mmoja dhidi yao

Msimu huu Yanga imevuna alama nyingi dhidi ya Simba kwenye ligi, wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mwingine


Saikolojia ya wachezaji hubadlika kabisa pale wanapokutana kwenye derby hii, ujasiri unaongezeka na hutashangaa kuona mchezaji yeyote anayepangwa katika mchezo huo, anafanya vizuri
_
Utakuwa mchezo mzuri kwa mashabiki ku-enjoy kwani ushindani utakuwa mkubwa. Ni mchezo ambao ukanda wote wa Afrika Mashariki utatupia jicho

Wakati Simba wataingia uwanjani wakisaka taji la pili msimu huu, kwa Yanga huu ni mchezo muhimu sana kwao. Mchezo huu umeshikilia nafasi yao ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Hakika ni mchezo ambao hawatakubali wafungwe kirahisi


Kaa nami hapa kuanzia mwanzo wa mchezo, katikati ya mchezo na hadi Mwisho...

Kwa watakaoangalia kupitia Runinga, mechi itaoneshwa kupitia Azam Sports 2 kwenye Kisimbuzi cha Azam

Matarajio ya vikosi leo kwa timu zote mbili:

Simba
1. Manula Aishi
2.Haruna Shamte
3. Sergi Pascal Wawa
4. Mohamed Hussein "Tshabalala"
5. Erasto Edward Nyoni
6. Jonas Mkude
7.Francis Kahada
8.Gerson Fraga
9. John Rafael Bocco
10. Cleotus Chota Chama
11. Luis Miquissone

Yanga
1. Mnata Metacha
2. Juma Abdul
3. Adehyum Saleh
4. Said Makapu
5. Lamine Moro
6. Feisal salum "Fei Toto"
7. Deus Kaseke
8. Haruna Niyonzima 'fabregas'
9.David Molinga 'Falcao'
10.Ditram Nchimbi
11. Bernad Morrison
View attachment 1504401
View attachment 1504603
Mbona salehjembe katoa list nyingine Tshishimbi ndani ila Nyonzima hayupo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom