Nusu Fainali Azam Sports Federation Cup: Simba 4-1 Yanga uwanja wa Taifa Dar es salaam

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,987
69,380
Karibuni katika Matukio mubashara (Live Updates) ya Mechi ya watani wa jadi "Kariakoo Derby" kutokea Uwanja Mkuu wa Taifa maarufu Kwa mkapa..

Kipute kinatarajia kuanza saa 11 jioni...

Simba ilitangulia Nusu Fainali kwa kuifunga Azam FC bao 2-0 huku Yanga ikitinga nusu Fainali kwa kuiondosha Kagera Sukari kwa mabao 2 -1

Nusu fainali ya kwanza ilichezwa jana ambapo iliwakutanisha Vijana wa Namungo Fc wakipepetuana na Wagosi wa Sahare All Stars Matokeo yalikuwa ni Namungo 1 Sahare 0

Kwa hiyo mshindi wa leo atacheza na Namungo Fc katika hatua ya Fainali ya Azam Sports Federation Cup

Shamra shamra nje na ndani ya uwanja ni kubwa na leo ndio tunasema mtoto hatumwi dukani

Kuhusu mashabiki, kwa mujibu wa maelekezo kutoka Serikalini ni kuwa wataingia 30,000 tu badala ya 60,000 na hii ni kutokana na janga la Corona COVID-19 linaloisumbua dunia kwa sasa, mashabiki pia wameambiwa wachukue tahadhari zote katika kujikinga na Ugonjwa huu.

Ukiangalia takwimu, katika misimu mitatu iliyopita, Simba wamepata ushindi dhidi ya Yanga mara mbili tu na Yanga ikishinda mchezo mmoja dhidi yao

Msimu huu Yanga imevuna alama nyingi dhidi ya Simba kwenye ligi, wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mwingine


Saikolojia ya wachezaji hubadlika kabisa pale wanapokutana kwenye derby hii, ujasiri unaongezeka na hutashangaa kuona mchezaji yeyote anayepangwa katika mchezo huo, anafanya vizuri
_
Utakuwa mchezo mzuri kwa mashabiki ku-enjoy kwani ushindani utakuwa mkubwa. Ni mchezo ambao ukanda wote wa Afrika Mashariki utatupia jicho

Wakati Simba wataingia uwanjani wakisaka taji la pili msimu huu, kwa Yanga huu ni mchezo muhimu sana kwao. Mchezo huu umeshikilia nafasi yao ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Hakika ni mchezo ambao hawatakubali wafungwe kirahisi

Fainali itachezwa Nelson Mandela Stadium Rukwa ambapo Namungo ameshatangulia


Kaa nami hapa kuanzia mwanzo wa mchezo, katikati ya mchezo na hadi Mwisho...

Kwa watakaoangalia kupitia Runinga, mechi itaoneshwa kupitia Azam Sports 2 kwenye Kisimbuzi cha Azam

Matarajio ya vikosi leo kwa timu zote mbili:

Simba
1. Manula Aishi
2.Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein 'Tshabalala'
4. Kennedy Juma
5. Sergi Pascal Wawa 'Sultan'
6. Jonas Mkude
7.Louis Miquissone 'Konde Boy'
8.Gerson Fraga
9. John Rafael Bocco (Nahodha)
10. Cleotus Chota Chama 'Mwamba wa Lusaka'
11. Francis Kahata

Wachezaji wa Akiba(Substitutes/Reserve)
Beno Kakolanya, Gadiel Michael,Erasto Nyoni, Mzamiru Yasini,Hassan Dilunga,Meddie Kagere,Miraji Athuman

Yanga
1. Mnata Metacha
2. Juma Abdul
3. Jaffary Mohamed
4. Lamine Moro
5. Said Juma Makapu
6. Papy Kabamba Tshishimbi (Nahodha)
7. Deus Kaseke
8. Feisal Salum 'Fei Toto'
9.David Molinga 'Falcao'
10.Haruna Niyonzima 'Fabregas'
11. Bernad Morrison

Wachezaji wa Akiba (Substitutes/Reserve)
Faroukh Shikalo, Calvin Yondan, Adeyum Saleh,Abdulaziz Makame, Patrick Sibomana, Mrisho Ngassa, Ditram Nchimbi
azamtvtz-20200712-0001.jpg

View attachment 1504603



--‐---------------------------------____________________________________
01' Mpira umeshaaanza hapa...Timu zote zinashambuliana kwa zamu.. Simba wanapata offside

04' Yanga wanashambulia na kupata kona hapa..ilikuwa hatari lakini Kenny Juma akaokoa

08' Simba wanalisakama lango la Yanga, Luis Miquissone anapiga chenga hapa na pale na kulenga goli lakini inakwenda nje

Simba 0 Yanga 0

12' Mpira bado unaendelea Mashambulizi ya hapa na pale, timu zote zinajaribu kusomana huku wakishtukizana

18' Haruna na Fei toto wanaonana vizuri kumtafuta Molinga anachelewa pale simba wanaokoa huku wakipiga pasi za visambusa

21' Simba wanashambulia pale.... Walinzi wa Yanga wanajisahau, wanategeana ....

Goooooal Gerson Fraga anaipatia Simba Goal

Simba 1 Yanga 0

26' Yanga wanacheza nyuma kujipanga, wanasogea mbele na kurudi nyuma wanajaribu kusogea mbele kwa pasi fupi fupi na ndefu lakini wanazuiwa...

32' Molinga na Niyonzima wanacheza vizuri palee lakini wanachelewa kidogo mpira unaokolewa

34' Kahata analisakama goli la Yanga lakini mpira unatoka nje...Yanga kama wamepoteza umakini kidogo

36' Lamine Moro anaoneshwa kadi ya Njano baada ya kucheza rafu pale katikati ya uwanja

41' Simba 1 Yanga 0.. Papy Tshishimbi anajitahidi kwenda pale lakini anazuiwa... Linapigwa shuti pale lakini Aishi Manula anadaka kiulaaaiiini

42' Kennedy Juma anamdondosha Ben Morisson na inakuwa faulu kuelekea Simba.. Ben Morisson anaianza kwa Papy Shishimbi Morisson tena ila anaupoteza

44' Kona kwa Simba wameanza hapa, Miquissone analeta mbwembwe pale...
Juma Abdul anapewa Kadi ya njano...




45' Dakika moja kuelekea mapumziko Simba 1 Yanga 0

45+1' Simba wanapata kona ila wanaanza kidogo...nini palee, halftime

Saa 11:47 Jioni hapa uwanja wa Taifa

Mpira ni mapumziko Simba 1 Yanga 0 ( Gerson Fraga 21')

****************************************************************************

46' Kipindi cha pili kimeanza bado matokeo ni Simba 1 Yanga 0


Gooooooal Simba wanapata bao la pili ( Cleotus Chama)

53' Goal la 3 kwa Simba, Yanga walikuwa hawajakaa sawa walizubaa, Simba wakapiga moja moja wakaonana na Goli likafungwa na Luis Misquissone

Simba 3 Yanga 0


Sub kwa Yanga
Tshishimbi Calvin Yondani In

Niyonzima out Nchimbi In

56' Morisson anacheza kizembe pale lakini Aishi Manula anauwahi mpira

60' Mabeki wa Simba wanacheza kwa uangalifu huku wakiangalia nafasi za mbele, Ditram Nchimbi anapasiwa anachelewa mpira unatika nje unakuwa wa kurusha kuelekea Yanga
Simba 3 Yanga 0


64' Mohamed Hussein Anapata njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Deus Kaseke.. inakuwa ni faulu

65' Yanga Sub Sibomana Ndani Morison nje

69' Feisal anacheza vibaya kwa Kahata, Feitoto anapewa Kadi ya njano


71' Goooooal ... Fei Toto anaipatia Yanga Goal la Kwanza
Feisal Salum Toto anapiga block buster nzuri pale

Simba 3 Yanga 1


74' Sub kwa Simba Kahata Francis nje na dilunga Hassan ndani
John Bocco out Kagere Meddie In

Wakati huo Yanga wamechangamka, wanaonana vizuri

76' Kagere anaizonga Yanga ila anazuiwa na walinzi wa Yanga... yondani na Juma Makapu

78' Sibomana na Nchimbi wanaleta uhai pale eneo la Mbele.. Simba wanaonekana kama wamerelax

80' Chama anazidiwa mbinu na Jafary Mohamed, anadhibitiwa...Jafari anaondoa mpira eneo la hatari

81' Sub kwa Simba Fraga Gerson nje Mzamiru Yasin ndani (Simba 3 Yanga 1)

85' Juma Abdul anaingiza majalo lakini inatolewa nje inakuwa Kona... Inapigwa Aishi Manula anaiokoa..

Yanga naona wameamka wanalisakama Lango la Simba

89' Goooooaaaaal.....Mzamiru Yassin anapata goli hapa Simba 4 Yanga 1

Wakati huo Miraj Athuman kaingia katoka Luis Misquisonne

90' Dakika 3 zimeongezwa kumaliza mpambano huu... Simba wanaishambulia Yanga... Makapu anapata kadi ya njano kwa kumvuta Kagere


90+3' Mpira umeisha.....

Simba 4 Yanga 1

Simba inaenda fainali ya Azam Sports Federation Cup kucheza na Namungo Fc

Ahsanteni kwa kuwa pamoja nami tangu mwanzo wa mchezo, katikati ya mchezo na hadi Mwisho wa mchezo huu


-Maendeleo Hayana Vyama-
~Baya Lisilokudhuru ni Jema lisilo na Faida~
 
Matatizo mengine ya kujitakia km kweli Yanga watapanga kikosi hicho anakufa,Simba ana kawaida ya kujaza watu kati hupaswi kuanza na Ditram na molinga kwa pamoja aidha Ditram awe striker nyuma yake akae kiungo aidha Rafael daud au hata banka au molinga awe tisa kumi akae kiungo km kawaida huwezi cheza na viungo 3 mwenzio katia umati pale kati km Tshishimbi angewepo basi kumi angecheza fey kwa kua Balama hayupo maana ndie hucheza hapo game zote 2 alicheza yeye!
 
Mechi ya leo itaamuliwa na umakini wa mabenchi ya ufundi kwa pande zote. Tatizo la kocha wa Simba si mwepesi wa kubadili mbinu kama plan A imefeli. Ni mara chache kuona timu inaanza vibaya alafu anabadili mbinu kwa wakati.

Hakuna kinachoweza kuiangusha Simba zaidi ya hilo. Simba ina timu bora kabisa kila idara ila inategemea sana uzoefu wa wachezaji kuliko mbinu. Nategemea benchi la ufundi limegundua makosa yake ili wapange majukumu inavyopaswa na kusoma mchezo kila sekunde.
 
Nisaidien jinsi ya kuchek game ya watani online au kama kuna mtu ana access anipasie kidogo niko mbal na home tafadhali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom